The Knowledge Seeker
JF-Expert Member
- Apr 13, 2019
- 4,389
- 6,665
Pascal Mayalla ndugu tupe na wewe uchambuzi wako kama huu alafu tuangalie nani yuko sahihi nani kakosea....Wakuu,
Matokeo ya Uchaguzi mkuu yameshatoka na maisha yanaendelea na tumeapishwa. Lakini, kama mdadisi wa mambo, nimekuwa nikicheza na takwimu rasmi za INEC na Sensa yetu ya 2022. Naomba tusaidiane kuzitafakari hizi namba kwa pamoja, maana kwangu kimahesabu picha inagoma kukaa sawa.
Huu si uchambuzi wa nani alishinda, bali ni uchambuzi wa 'process' na uhalisia wa namba zenyewe.
KITENDAWILI CHA 1: Daftari vs. Sensa
Kwanza tuanze na hapa:
1.Watu wenye umri (14+ Miaka) - Sensa 2022: Milioni 35.3
2.Waliojiandikisha Kupiga Kura - INEC 2025: Milioni 37.7
Swali: Tumepata wapi watu Milioni 2.4 wa ziada waliojiandikisha (37.7M) kuliko watu waliopo wenye umri wa miaka 14+ (35.3M)?
-Au Sensa ya 2022 ilikosea na Watanzania tuko wengi kuliko walivyotuhesabu?😃
-Au, Daftari la Kudumu halijahuishwa kwa muda mrefu? Hizi Milioni 2.4 ni "majina hewa" (watu waliofariki, waliohama, waliojiandikisha mara mbili)?🤦
-Kama ni "majina hewa," je, yanaweza kupiga kura? Na kama yanaweza, yalipiga?🙂↕️
KITENDAWILI CHA 2: Kura 32.7M vs. Muda (The 540 Minute Puzzle)
Hapa ndipo mambo yanapopata utamu zaidi. Twende na namba rasmi:
1.Jumla ya Kura Zilizopigwa: Milioni 32.7
2.Jumla ya Vituo vya Kura: 99,895
3.Muda Rasmi wa Kura: Saa 1:00 Asubuhi - 10:00 Jioni (Jumla Saa 9 au Dakika 540)
Hesabu Rahisi:
-Wastani wa Kura kwa Kituo: 32.7M Kura / 99,895 Vituo = Wapiga Kura 327 (kwa kila kituo).
-Muda wa Mpiga Kura: Tukichukulia kwa uchache (optimistic) kwamba mpiga kura anatumia Dakika 2 tu (kuingia, kutambuliwa, kupewa karatasi, kupiga kura, kukunja, kutumbukiza).
HESABU SASA:
-Muda Uliohitajika Kituoni: 327 Watu × Dakika 2 = Dakika 654
-Muda Uliokuwepo Kituoni: Dakika 540 (Saa 9)
Utata Upo Hapa: Kimahesabu, kila kituo kilihitaji Wastani wa Dakika 654 (Saa 11) kumaliza wapiga kura wake 327.
- Lakini vituo vilifunguliwa kwa Dakika 540 (Saa 9).
Kila kituo kilipungukiwa na Dakika 114 (karibu Saa 2)!
KITENDAWILI CHA 3: Hoja ya Ukosefu wa Foleni (The 'No Queue' Paradox)
Hili ndilo linalonichanganya zaidi, na hapa naomba mliokuwa "ground" mshuhudie.
1.Matokeo ya Kimahesabu: Ili kura 32.7M zipigwe (86.9% Turnout), vituo vilitakiwa kuwa "busy" na kufanya kazi kwa Saa 11 bila kupumzika. Hii ingesababisha FOLENI KUBWA (misururu) kuanzia asubuhi hadi jioni, na watu wengi kuchelewa kumaliza.
2.Hali Halisi (Niliyoshuhudia na Niliyosikia): Vituo vingi vilikuwa "vimepooza". Hakukuwa na msongamano wa kutisha. Uchaguzi ulionekana kuwa na "hamasa ya kawaida," si ya 86.9% turnout.
Swali la Mwisho: Tunazipatanishaje hizi 'Option' mbili?
Option 1 (Super-Voters): Labda Watanzania walikuwa wepesi sana siku hiyo? Na walitumia Sekunde 99 tu (Dakika 1.6) kupiga kura badala ya Dakika 2 ambazo nimeashumu tu? (540 min / 327 kura = 1.65 min/voter).
Je, inawezekana mtu kumaliza mchakato wote kwa sekunde 99?🤔
Option 2: Labda kulikuwa na vituo vingi "visivyo rasmi" vilivyotumika ambavyo haviko kwenye hesabu ya 99,895? (Hii ni 'wild assumption').😱
Option 3 : Au...Hii 'turnout' ya 86.9% haikuwa ya watu halisi waliofika vituoni? Labda masanduku yalipata "msaada" ili kufikisha idadi ya kura 32.7M?
Option 4: Labda namba za INEC (kura zilizopigwa au idadi ya vituo) zina makosa ya kimahesabu?
Wadau,
Nawasilisha hoja hizi kwenu. Hizi namba na uhalisia wa vituoni ninaona vinapingana.
Hizi kura Milioni 32.7 ziliwezekanaje kupigwa ndani ya Dakika 540 bila kuacha foleni ?😎
Karibuni tujadili kwa HOJA.
Vitu kama hivi ndio husababisha mama kupandwa na hasira na kufanya hayo aliyoyafanya ....