Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Britannica uraisi ni taasisi sio maamuzi binafsi kama anavyofanya Jiwe kuvunja katiba kila mara. Ukiheshimu katiba na utawala wa sheria utaweza kuwa raisi manake yote unayotekeleza yanakuwa kwenye ilani ya chama husika!

Hiyo kuwa eti urais ni taasisi ni nadharia tu. Ingekuwa urais ni taasisi, usingeona cheo cha rais kikiendeshwa kwa utashi na tabia binafsi za rais.
 
Lissu oyeeee. Sasa iko wazi njia yake ya kuwa Rais wa Tanzania iko nyeupeee. Mungu wetu akusimamie Rais wetu mpya TL [emoji120]
 
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Hii imewapiga, mnatapatapa kutaka kuipoza
 
Amani iwe nanyi Wadau.

kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.

Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020.

Lissu ameweza kuelezea kwa kifupi na kueleweka sana hoja zote zilizotikisa kwenye miaka hii Mitano ambazo sio tu Chadema ila hadi CCM na watanzania kwa ujumla zimewagusa sana.

Hakuna ambae hajui kuwa wafanyabiashara wakubwa na wakati wamenyanyaswa sana kwenye kipindi hiki cha miaka Mitano, kwenye hili Lissu kapiga mulemule, hakuna ambayo hajui kuwa awamu ya tano imeharibu sana kwenye uchumi, kilimo na diplomasia, kwenye haya tena Lissu kapiga mulemule.

Alipomaliza Lissu ni pale alipoelezea kwa jinsi gani suala la kuonea watu na kukiuka katiba limekuwa linaumiza watu na hapa tena Lissu amepiga mulemule.

Mwisho kuonesha jinsi gani amekomaa, pamoja na kupigwa risasi 16 amesema amesamehe na hatolipa kisasa. Hapa Lissu kawa sawa na Mandela aliyewasamehe makabulu na Papa John Paul 2 aliye msamehe kijana aliyempiga risasi. Lissu ameonesha amekomaa sio tu kiuongozi ila hata kihekima na busara.

Hotuba ya leo ya Lissu imegusia mambo mengi ikiwemo kurekebisha mfumo wa sheria na vyombo vya ulinzi na usalama ili vifanye kazi kwa weredi. Lissu kusema kweli kumaliza yote.

Ukweli lazima tuseme , Ingawa vyombo vya Habari vya Tanzania ikiwemo Azam , ITV na vingine vikubwa kuogopa hata kurusha Habari ya Lissu kutangaza nia leo. Ila hotuba yale imesikika na imewasisimua watu wengi nikiwemo mie. CCM wametumia mbinu ya kuvitisha vyombo hivi kwa makusudi ila Naona nguvu ya Lissu ni kubwa sana kuliko hujuma dhidi yake.

Itoshe kusema Lissu amethibitisha kuwa anatosha akiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020

Kura yangu anayo akipitishwa na Chadema.

Ushauri kwa Chadema. Isambazeni video ya leo ya Lissu kwenye mitandao mbalimbali kuanzia Insta, Facebook, Twitter na Whatsup’ watu wengi waione maana mkitegemea vyombo vya Habari vya Tanzania vilivyobanw na Ccm mtapoteza.

Jioni Njema!
Hakuna zaidi nilichokiona mapambo ya jeneza tu!
 
Wahujumu uchumi ambao hawahukumiwi! Hivi bado mnadhani tunaishi kwenye dunia ya kuamini afanyacho rais bila kupima uhalisia? Tunajua watu waliokamatwa na kuporwa fedha zao bila kupatikana na hatia, na wakalazimishwa, kutoa pesa ili waachiwe. Hata akina Ruge na Seth kama sio msimamo, wangelipa hela ili waachiwe. Lisu kaongea mengi yenye ukweli wa wazi.
Hao waliokamatwa na kuachiwa mnao ushahidi kuwa hawakufanya malosa ya uhujumu uchumi? Na kama ni hivyo mbona kuna watanzania wengi wanafanya biashara halali hawajakamatwa? Au ndio kuipaka matope serikali? Yaani huna kosa alafu usingiziwe bure?
 
Unanifurahisha kwa uwezo wako wa kuandika maneno mengi ila bahati mbaya yote ni pumba.

Hoja yako ni maendeleo ya watu na sio vitu ila unatakiwa ujue kwamba hayo maendeleo ya vitu watatumia hao hao watu.

Hivyo huyo tundu hana uwezo wa kuleta maendeleo ya watu au vitu..

Pia usiwalinganishe wakina Nyerere na Mandela kwa hoja zako mfu.
Mbona TL mnamwogopa hivo lakini? Wewe unatumwa humu kubweka wakati hata wewe mwenyewe hali yako mbaya tu, madeni kwa Mangi yanataka kukutoa roho. Mmekaririshwa ujinga tu. Ruhusu tume huru muone mazombie nyie.
 
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Awe mshauri wa rais kwa pumba na upuuzi aliongoe? Yaani kupambana na ufisadi ki kukandamiza wafanya biashara.
Habari za kukusanya kodi eti ni kukandamiza wananchi? Serikali gani itaishi bila ya kodi?
 
Hiyo kuwa eti urais ni taasisi ni nadharia tu. Ingekuwa urais ni taasisi, usingeona cheo cha rais kikiendeshwa kwa utashi na tabia binafsi za rais.
Kabla Ya vitendo huanza nadharia.Kwa kushindwa kufuata nadharia ndio inapelekea kufeli ,ndio kinachowatokea kina Jiwe!
 
Awe mshauri wa rais kwa pumba na upuuzi aliongoe? Yaani kupambana na ufisadi ki kukandamiza wafanya biashara.
Habari za kukusanya kodi eti ni kukandamiza wananchi? Serikali gani itaishi bila ya kodi?
Nani kakwambia kuna kukusanya kodi??? Kinachofanyika ni kupora watu fedha. Kila mtu anajua na anaona hili.

Wafanyabiashara wengi sana wamefunga biashara na kukimbia. Kukusaidia tu angalia kiwango cha bank zilivyofungwa kutokana na kukosa biashara, angalia makampuni ya mafuta ya Mtwara yaliyokuwa yamejazana Masaki na kuajili watanzania wengi waliokuwa wanawalipa vizuri sana walivyofunga ofisi zao na kuondoka. Kiufupis Serikali ya awamu ya Tano imefeli pa kubwa sana kwenye uchumi. Sehemu peke ambayo naweza sema wamefanikiwa ni kwenye miondombinu tu hasa barabara, reli na hiyo stigglers gorge ambazo zote zinatengenezwa kwa fedha za mikopo na misaada hasa World Bank na Mabank ya biashara.

Kwenye kilimo ndo usiseme. Kampuni nyingi sana za korosho zimefirisika na madeni makubwa kutokana na uamuzi wa serikali ya awamu ya tani kuingilia soko la korosho.

Kiufupi wamefeli sana kwenye uchumi si kidogo
 
Hao waliokamatwa na kuachiwa mnao ushahidi kuwa hawakufanya malosa ya uhujumu uchumi? Na kama ni hivyo mbona kuna watanzania wengi wanafanya biashara halali hawajakamatwa? Au ndio kuipaka matope serikali? Yaani huna kosa alafu usingiziwe bure?
Kama hujui yanayofanyika kaa kimya ndugu. Kuna machozi ya watu wengi sana waliosingiziwa makosa mbalimbali hasa ya uhujumu uchumi na wengine hadi kuuza nyumba na kufirisika kabisa ili tu wawe huru.
 
Kama hujui yanayofanyika kaa kimya ndugu. Kuna machozi ya watu wengi sana waliosingiziwa makosa mbalimbali hasa ya uhujumu uchumi na wengine hadi kuuza nyumba na kufirisika kabisa ili tu wawe huru.
Weka ushahidi namna walivyosingiziwa. Taja na majina yao vinginevyo ni uzandiki.
 
Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.
Nchi inahitaji raisi mjenga nchi sio mjenga hoja Lisu sio mjenga nchi ni mbomoa nchi kila anapokuwa kazi yake kubomoa tu nchi isipewe misaada nk hafai
 
Tundu Lisu ameamua kupima kina cha MAJI kwa kutumua miguu yake yote miwili!! Jibu atalipata na huo ndio utakuwa mwisho wa harakati zake!! Watanzania siyo watu wa kuchezewa!! Na hatakuwa na faida tena hata kwa makaburu!
 
Hotuba imewachanganya mataga hadi wameamua kumuua Mbowe,lakini wameshindwa.
 
Back
Top Bottom