Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Lissu ni changamsha genge tu yeye mwenyewe anajua hana sifa za kuwa Rais

Kwa Nchi nyingine lissu alivyoisaliti Nchi angekuwa gerezani
Tume huru ya uchaguzi ikiwepo hata mbunge mmoja mkipata mtaenda kutambika na kuku mwekundu ndio maana hamjiamini kwani mnaogopa nini kwa mfano kama mnaona mnapendwa
 
Kaongea mengi kweli, ila hilo la risasi 16 ndio limekukera zaidi maana unajua ni kashfa itakayosumbua kwenye masikio ya wapiga kura. Hayo ya elimu, sayansi, afya nk yako kwenye ilani, leo alikuwa anazungumza kwa ujumla. Akipewa ridhaa na chama chake atanadi kwenye ilani. Usitake aongee kwa mujibu wa mtazamo wako na kile kitakachowafurahisha. Bado unadhani kuna watu watafanya siasa kwa utashi na mwenendo wa kiccm?

Leo naona mmeongezewa nguvu na jeshi la akiba, nadhani imeonekana nyie wenyewe mtachemsha. Pambaneni mkanushe kwa hoja alichokisema, na muweke ukweli.
Kwanza, una tatizo la ufahamu na hata Lissu ana tatizo hilo. Hotuba ya kutaka kugombea kwa CHADEMA ilikuwa ya wanachama wenzake ndani ya CHADEMA. Unapotusimulia hadithi za CHADEMA unapoteza muda na hata yeye kutangaza eti analihutubia taifa ni ujinga tu! Yeye ahutubie kamati kuu ya CHADEMA iliyo na madaraka ya kumpitisha.

Pili, una imani mbovu kwamba kila asiyekubaliana na CHADEMA ni CCM. Hii nchi tuna imani tofauti. Siasa siyo ajira ya wote ndo maana mtu akilia-lia kama mtaji wa kisiasa, kwangu ni upuuzi tu! Kwani amelazimika kuwa mwanasiasa?
 
Wewe ni mtu mzima. Tambua kitu kinanchoitw government liability. Hawa viongozi watashitakiwa wajiwa wanafanya majukumu yao. Kwa hiyo kupeleka mashitaka kupitia kwa Ag kuna tatizo?

Government liability? Au unadhani ukitamka hilo neno kwa kiingereza ndio litaboresha utetezi wako? Hivi unajua unachoongea, watu wanasaka kinga ya kutoshtakiwa, na sio kuboresha mazingira ya kushitakiwa.

Najua halijakaa vizuri kwa wengi, hasa baada ya kutumika propaganda ya kuwa ni wazalendo, ndio maana nyie watetezi mnahangaika kucheza na maneno ili kuficha aibu hii.

Lakini ukweli ni kuwa watu hawa ni waovu na hilo halifichiki. Bahati mbaya kizazi hiki nacho kimeshamka, ila nafuu pekee ni uoga kidogo walionao, hivyo kushindwa kuchukua maamuzi magumu sasa.
 
Government liability? Au unadhani ukitamka hilo neno kwa kiingereza ndio litaboresha utetezi wako? Hivi unajua unachoongea, watu wanasaka kinga ya kutoshtakiwa, na sio kuboresha mazingira ya kushitakiwa. Najua halijakaa vizuri kwa wengi, hasa baada ya kutumika propaganda ya kuwa ni wazalendo, ndio maana nyie watetezi mnahangaika kucheza na maneno ili kuficha aibu hii. Lakini ukweli ni kuwa watu hawa ni waovu na hilo halifichiki. Bahati mbaya kizazi hiki nacho kimeshamka, ila nafuu pekee ni uoga kidogo walionao, hivyo kushindwa kuchukua maamuzi magumu sasa.
Kwani imezuiliwa kuwashitaki?
 
Shetani hana rafiki , hilo ulitambue
Tatizo mnaotetea upinzani mnatoa hoja za kinazi, kama kwenye tukio la sasa la Mbowe kuvamiwa, tayari hukumu imekwisha kutolewa ati kuna mkono wa Serikali! Serikali hiyo hiyo yenye vyombo vya ulinzi vitumie njia ya kihuni kama hiyo?

Mbowe hivi karibuni ameshambuliwa kwa tuhuma na viongozi wenzake. Isitoshe hata vijsna wa chama chake huko Dodoma wanamkosoa, iweje mhamishe tatizo la uongozi wake?


Kwa kauli ya hawa viongozi, inafikirisha kwa nini tukio lisiwe la ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuwa kuna kila dalili CHADEMA kufanya vibaya katika historia yake. Isije ikawa moha ya mbinu ya kuweka mpira kwapani
 
Labda kama anagombea urais wa Bend ya FM Academia na akina Joshi
 
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Umetumia kigezo kipi? Mwalimu Nyerere unamuweka kwenye kundi gani?
 
Kwanza, una tatizo la ufahamu na hata Lissu ana tatizo hilo. Hotuba ya kutaka kugombea kwa CHADEMA ilikuwa ya wanachama wenzake ndani ya CHADEMA. Unapotusimulia hadithi za CHADEMA unapoteza muda na hata yeye kutangaza eti analihutubia taifa ni ujinga tu! Yeye ahutubie kamati kuu ya CHADEMA iliyo na madaraka ya kumpitisha.

Pili, una imani mbovu kwamba kila asiyekubaliana na CHADEMA ni CCM. Hii nchi tuna imani tofauti. Siasa siyo ajira ya wote ndo maana mtu akilia-lia kama mtaji wa kisiasa, kwangu ni upuuzi tu! Kwani amelazimika kuwa mwanasiasa?

Kwamba anahutubia taifa, hizo ni tambo za kisiasa hata ww unaweza kusema hivyo ukipenda, labda kama hujui unachokataa. Isitoshe sioni tofauti na kuhutubia taifa kwani ni press ya wazi, na wala haikuwa kikao cha ndani. Press yake ilikuwa wazi kwa kila mtu kuona, hivyo kuita ni kuhutubia taifa, ni kutokana na hadhira itakayopata ujumbe wake. Kwa wale wote wanaofuatilia siasa hapa nchini, bila kujali unamkubali au humkubali, ni nani hajui alichoongea Lissu jana ikiwemo ww?

Nakubaliana kabisa na ww kuwa sio kila asiyekubaliana na cdm basi huyo ni ccm, kwa hili uko sawa kwa asilimia 100. Ila kama ww ni neutral, basi inanibidi nirudi shule nikajifunze maana halisi ya kuwa neutral. Hata yule mtoto wangu aliye class 4 akija hapa, hahitaji akili kubwa kujua upande unaolalia na huo uneutral wako. Hilo la kama siasa sio ajira, inaonyesha hata hujui unaoongea nini, kuna watu wanashabikia simba au yanga na wanalia timu zao zikivufungwa, je hao wameajiriwa na hizi timu au ni hisia zao? Huna ujualo boss.
 
Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.
Ugesindikiza na Data (Takwimu) Ingependeza sana; Kwamba watu kadha waongeaji, ni % kadhaa ya wanaotenda etc

Maana naona na wewe umeongea Maneno mengi pasipo Data. SO inawezewkana ikawa ni mawazo yako.
 
Unaelewa unachoongea chagu wa malunde?
Nacheka sababu unanisingizia mambo ambayo siyafahamu. Huyu jamaa ni nani? Alafu jibu swali kwani imezuiliwa kuwashitaki hao viongozi?
 
Kaa kimya pls.
Siwezi kaa kimya wakati unapotosha. Viongozi watashitakiwa wakiwa wakiwa wanafanya makosa wakati wnatekeleza majukumu yao. Na mashitaka yatapekekwa kwa Ag.
 
Amani iwe nanyi Wadau.

kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.

Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020.

Lissu ameweza kuelezea kwa kifupi na kueleweka sana hoja zote zilizotikisa kwenye miaka hii Mitano ambazo sio tu Chadema ila hadi CCM na watanzania kwa ujumla zimewagusa sana.

Hakuna ambae hajui kuwa wafanyabiashara wakubwa na wakati wamenyanyaswa sana kwenye kipindi hiki cha miaka Mitano, kwenye hili Lissu kapiga mulemule, hakuna ambayo hajui kuwa awamu ya tano imeharibu sana kwenye uchumi, kilimo na diplomasia, kwenye haya tena Lissu kapiga mulemule.

Alipomaliza Lissu ni pale alipoelezea kwa jinsi gani suala la kuonea watu na kukiuka katiba limekuwa linaumiza watu na hapa tena Lissu amepiga mulemule.

Mwisho kuonesha jinsi gani amekomaa, pamoja na kupigwa risasi 16 amesema amesamehe na hatolipa kisasa. Hapa Lissu kawa sawa na Mandela aliyewasamehe makabulu na Papa John Paul 2 aliye msamehe kijana aliyempiga risasi. Lissu ameonesha amekomaa sio tu kiuongozi ila hata kihekima na busara.

Hotuba ya leo ya Lissu imegusia mambo mengi ikiwemo kurekebisha mfumo wa sheria na vyombo vya ulinzi na usalama ili vifanye kazi kwa weredi. Lissu kusema kweli kumaliza yote.

Ukweli lazima tuseme , Ingawa vyombo vya Habari vya Tanzania ikiwemo Azam , ITV na vingine vikubwa kuogopa hata kurusha Habari ya Lissu kutangaza nia leo. Ila hotuba yale imesikika na imewasisimua watu wengi nikiwemo mie. CCM wametumia mbinu ya kuvitisha vyombo hivi kwa makusudi ila Naona nguvu ya Lissu ni kubwa sana kuliko hujuma dhidi yake.

Itoshe kusema Lissu amethibitisha kuwa anatosha akiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020

Kura yangu anayo akipitishwa na Chadema.

Ushauri kwa Chadema. Isambazeni video ya leo ya Lissu kwenye mitandao mbalimbali kuanzia Insta, Facebook, Twitter na Whatsup’ watu wengi waione maana mkitegemea vyombo vya Habari vya Tanzania vilivyobanw na Ccm mtapoteza.

Jioni Njema!
A written speech cannot say the suitability of a person.
 
Back
Top Bottom