Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mzee mwenzangu; na mimi napitia taratibu hotuba nzima niisikilize; sidhani kama nitakuwa mbali sana na maoni yako. Kulikuwa na vitu nasubiri kuvisikia katika hotuba zake hizi mbili...Maoni ya rais kuhusu matumizi ya mbinu za kisasa katika Kilimo, kuna hatari kubwa ya nchi yetu kurudi kutawaliwa tena Kiuchumi kutokana na ujio wa mbegu za maabara ambazo zitaondoa kabisa rutuba ya Ardhi yetu, ubora wa mbegu zetu (Organic) na kubwa zaidi kumikilisha Mashirika ya nje nguzo za Uchumi wetu Kitaifa.
Maasalaam,
- Ramadhan Kareem
Nakubaliana na wewe kwa msingi kwamba uvutiaji wa wawekezaji uwe katika miradi ya kimkakati ambayo utatuwesha kutufungulia masoko ya nje kama kwenye utalii, na mboga mboga Matunda, na vyakula vingine ikiwezekana tuwe na sisi tuna hisa katika uwekezaji huo.Kwa rehma zake Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu sote tutaumaliza Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan salama salimin na hakika yeye ndiye mwenye kurehemu riziki zetu kubwa na ndogo na hapana mwingine apaswaye kuabudiwa. Tumuombe sote atuepushe na kila lisokuwa na kheri kwetu. Ameen.
Nina hakika siku ya leo tutasikia SIFA kemkem za mafuta ya tin na zaitun zitamiminika kupamba na kusifia hotuba ya rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu imewagusa watu wote katika mazingira tofauti katika mwelekeo mpya wa dira ya Awamu hii ya sita ikitekeleza kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.
Mimi binafsi, niseme ukweli wangu kutoka moyoni ya kuwa sii mshabiki wa rais Mama Samia Suluhu Hassan toka hotuba yake ya kwanza alipo apishwa kama rais wa Awamu ya sita. Huu ndio ukweli wangu! Na sababu zangu ni ndogo kabisa, nilimsoma toka mwanzo mwelekeo na Dira yake Kitaifa, dira ambayo Kiitikadi, mimi sii muumini wake na hupingana na nadharia zinazofungamana zaidi na UBEPARI badala ya UJAMAA wa Mwafrika.
Hivyo unaponisoma hapa ni muhimu Uzingatie kuwa mimi ni muumini wa UJAMAA wa Mwafrika na naamini Maendeleo ya Tanzania yataletwa na WATANZANIA wenyewe badala ya WAWEKEZAJI kutoka nje. Imani ya kwamba maendeleo yetu yanahitaji kuweka masharti rahisi ili kuvutia Wawekezaji ni sawa na fikra za.Kitumwa za Mababu zetu walokubali kupewa na wakoloni Shanga na vilemba ili tupendeze huku wagenu wakiondoka na madini mali ghafi na nyara zetu za Kitaifa.
Niseme wazi kwamba binafsi yangu naiona tofauti kubwa sana baina ya Hayati rais wa awamu ya Tani John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na kwamba hawa sii kitu kimoja hata kidogo. Tofauti zinazotokana na ahadi za mabadiriko makubwa ya SERA na SHERIA ambazo Chama cha Mapinduzi na Hayati Magufuli walizitumia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020. Niseme kwa nini nasema hivi?
Haina Shqka kabisa, Hayati Magufuli alikuwa rais anayepigania maslahi ya Wananchi Wanyonge kwa maana ya Watanzania Maskini dhidi ya Wawekezaji Mabeberu tofauti kabisa na Dira na Mwelekeo wa Mama Samia anayetazama zaidi viwashwishi kwa maslahi ya WAWEKEZAJI pamoja na dhana ya UKUONGEZA UZALISHAJI wa Mazao kwa WINGI zaidi (Quantity) badala ya fikra za Magufuli kudhamiria Kuanzisha viwanda vya ndani ili Kuongeza thamani ya Mazao yetu ya Asili yalokuwa BORA zaidi (Quality).
Nimalizie tu kwa kusema, rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan awe makini sana na dhana hizi, kwani hatukuanza jana wala juzi. Tulifuata mrengo ule toka wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi, akaja Mh. Benjamin Mkapa na Mwishowe mstaafu Jakaya Kikwete, na kote huko nyuma tulifanya makosa mengi sana kwa dhana ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Biashara. Matokeo yake tukaunda Matabaka ya Walionacho na wasiona nacho baina ya Wainanchi wenyewe. Ndipo Ufisadi na rushwa viliposhamiri kwani hapana alotaka kubakia katika kundi la wasionacho (Maskini)
Maoni ya rais kuhusu matumizi ya mbinu za kisasa katika Kilimo, kuna hatari kubwa ya nchi yetu kurudi kutawaliwa tena Kiuchumi kutokana na ujio wa mbegu za maabara ambazo zitaondoa kabisa rutuba ya Ardhi yetu, ubora wa mbegu zetu (Organic) na kubwa zaidi kumikilisha Mashirika ya nje nguzo za Uchumi wetu Kitaifa.
Maasalaam,
- Ramadhan Kareem
Mkuu wala.usisumbuke sana maana muda bado. Hapa panaitwa MTAKUJA iwe leo, kesho au keshokutwa. Kila nilisemalo hutokea ilivyo toka enzi za Hi5, Nyenzo, Bcstimes na Jamboforums. Yawezekana wewe ndio mgeni..Umejitahidi kuchambua japo Uchambuzi wako ni wa Masikini Jeuri, wa kua na Mawazo Makubwa bila ya Uwezo wa Kutenda.
Mama Samiah anataka tufanye tunachoweza kufanya sasa wakati tunaendelea kujenga Uwezo wa kufanya hayo unayoyaelezea.
Tunahitaji Uwekezaji wa Ndani na pia tunahitaji Uwekezaji kutoka nje ili kuendelea kujenga Uwezo wa kujenga Uchumi wa Kujitegemea.
Mkuu nimeishi na hawa watu miaka 33 leo hii halafu unanambia sijui approach ipi? Halafu watu wenyewe wanaoshindana ni Wamarekani na Wachina? Nani kamzidi mwenzake hapo mkuu..Mkuu Mkandara habari za siku nyingi?
Binafsi nimefurahi sana kuona wajenga hoja wazuri kama wewe wanaanza kurudi kwenye mijadala. Hii peke yake ni hatua nzuri inayoashiria kuwa tumepiga tena hatua na kurudi kwenye awamu ya hoja kwa hoja na si hoja kwa ngumi.
Kuhusu hotuba, kwa upande wangu nilitegemea kusikia niliyoyasikia na zaidi kidogo. Hata hivyo yaliyosemwa yamesemwa vizuri na ambayo nilitaraji yatasemwa zaidi na hayakusema naamini ipo siku yatasemwa. Kila kitu ni hatua.
Kuhusu approach za uwekezaji, mama yupo sahihi sana. Unapozungumzia habari za ujamaa na ubepari, inawezakana huelewi vyema implications ya dhana hizo katika ulimwengu wa sasa.
Suala hili la uwekezaji na nadharia za ujamaa na ubepari kama ulivyoliweka ni mjadala unaohitaji utulivu na ulivyouweka, umeuweka kijuu juu mno kiasi kwamba ni rahisi amma kutoeleweka vyema au kupotosha mambo kadhaa. Nikitulia nitarudi tujadiliane jambo hili kwa kina.
Kichwa cha habari hiyo kimerekebisha na Admin wa Jamiiforums kwa nia njema pengine. Kwa hiyo AKILI KUBWA husoma yaliyomo na kutafakari, sii ku judge by the cover or heading..huo ni Utindiga..Natilia shaka kinywaji unachotumia.
Kama tu maoni umeyaita uchambuzi... Kweli awamu ile tulipigwa!
Na inawezekana ni kwa sababu maalum!Duh....IDs zetu hatimaye zinaanza kurudi!
Kila mtawala una maana gani ? Kwani wananchi walipigia kura MTU au Dira na mwelekeo wa chama kwa miaka mitano ijayo? Labda nikuulize wewe unadhani haya mabadiriko unayosema yangetangazwa na CCM na rais Magufuli ametutoka kabla ya Uchaguzi wa 2020 unadhani CCM ingeshinda Uchaguzi?I like this one though you missed some points.
Kila mtawala huja na vipaumbele vyake, so It doesnt matter ana ideology kinachoangaliwa ni suala zima la maendeleo yatafikaje na kwa wakati gani!!!!!
Lakini pia serikali ni wananchi, unaposikiliza kero zao na kuzitafutia majibu, kwa mwanasiasa huu ni mtaji. Nadhani Mama Samia anatafuta njia fulani zitakazofanya aimbwe kwenye midomo ya watu ilihali anakamilisha ilani za chama chake.
Wewe ni miongoni mwa watu wenye upeo wa chini sana! Itakuchukua miongo mingi sana kujua anachoongea Mama Samia !
Wanyonge unaowazungumzia Rais Magufuli aliwapigania je ni pamoja na Paulo Makonda akiyekuwa akipora fedha za watu huku akitembelea Range Rover na Lamborghini?!
Rais Magufuli aliwahi kumkemea Paulo Makonda kuhusu tabia zake hizo?
Ndugu hujitambui na wala huijui Dunia tuliyonayo sasa.
Rais Magufuli alikuwa na nia nzuri ya kujenga Taifa Ila alikuwa na mawazo primitive sana ( mawazo ya kizamani) na hakuwa na "exposure" kubwa kuhusu Dunia inavyo operate!
Mama Samia inaonekana anayo "exposure" na anajua Dunia inavyo operate tunasubiri usimamizi wake.
Kama atakuwa na usimamizi mzuri atamfunika Rais Magufuli asubuhi sana!
Rais Magufuli alikuwa anajenga Nchi kwa jasho na damu la Watanzania!
Watu walikuwa wameshachoka sana,mlibaki wewe na akina Makonda mnafurahia matunda ya Nchi hii!
Naunga mkono mengi uliyoandika humo kwenye mada, kwani nami mlengo wangu ni huo huo wa "Watanzania kujiletea maendeleo yao wenyewe">Kila mtawala una maana gani ? Kwani wananchi walipigia kura MTU au Dira na mwelekeo wa chama kwa miaka mitano ijayo? Labda nikuulize wewe unadhani haya mabadiriko unayosema yangetangazwa na CCM na rais Magufuli ametutoka kabla ya Uchaguzi wa 2020 unadhani CCM ingeshinda Uchaguzi?
Umeanza vizuri umeanza kutoa boko ulipoanza kusema kuhusu mama anataka quantity hayo umesema wewe husimuekee mama maneno mdomoni, mama anachotaka production iongezeke with the best out come and best quantity ilikuuza adi nje sasa tasfiri yako sijui umeipata wapi shekh. Hivi unajua mda gani inatokea ili kuua nutrition ya land? Waulize wanaofanya kilimo mfano mdogo Hiroshima land imekufa sasa watatumia almost the same components kwenye kuzalisha?Tufike mda tukabali dunia ni kijiji tusiogope kuingia soko la dunia kama wachina wanaleta adi samaki huku nini kinatushinda kupeleka tunapotaka. Common sense brother.Kwa rehma zake Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu sote tutaumaliza Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan salama salimin na hakika yeye ndiye mwenye kurehemu riziki zetu kubwa na ndogo na hapana mwingine apaswaye kuabudiwa. Tumuombe sote atuepushe na kila lisokuwa na kheri kwetu. Ameen.
Nina hakika siku ya leo tutasikia SIFA kemkem za mafuta ya tin na zaitun zitamiminika kupamba na kusifia hotuba ya rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu imewagusa watu wote katika mazingira tofauti katika mwelekeo mpya wa dira ya Awamu hii ya sita ikitekeleza kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.
Mimi binafsi, niseme ukweli wangu kutoka moyoni ya kuwa sii mshabiki wa rais Mama Samia Suluhu Hassan toka hotuba yake ya kwanza alipo apishwa kama rais wa Awamu ya sita. Huu ndio ukweli wangu! Na sababu zangu ni ndogo kabisa, nilimsoma toka mwanzo mwelekeo na Dira yake Kitaifa, dira ambayo Kiitikadi, mimi sii muumini wake na hupingana na nadharia zinazofungamana zaidi na UBEPARI badala ya UJAMAA wa Mwafrika.
Hivyo unaponisoma hapa ni muhimu Uzingatie kuwa mimi ni muumini wa UJAMAA wa Mwafrika na naamini Maendeleo ya Tanzania yataletwa na WATANZANIA wenyewe badala ya WAWEKEZAJI kutoka nje. Imani ya kwamba maendeleo yetu yanahitaji kuweka masharti rahisi ili kuvutia Wawekezaji ni sawa na fikra za.Kitumwa za Mababu zetu walokubali kupewa na wakoloni Shanga na vilemba ili tupendeze huku wagenu wakiondoka na madini mali ghafi na nyara zetu za Kitaifa.
Niseme wazi kwamba binafsi yangu naiona tofauti kubwa sana baina ya Hayati rais wa awamu ya Tani John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na kwamba hawa sii kitu kimoja hata kidogo. Tofauti zinazotokana na ahadi za mabadiriko makubwa ya SERA na SHERIA ambazo Chama cha Mapinduzi na Hayati Magufuli walizitumia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020. Niseme kwa nini nasema hivi?
Haina Shqka kabisa, Hayati Magufuli alikuwa rais anayepigania maslahi ya Wananchi Wanyonge kwa maana ya Watanzania Maskini dhidi ya Wawekezaji Mabeberu tofauti kabisa na Dira na Mwelekeo wa Mama Samia anayetazama zaidi viwashwishi kwa maslahi ya WAWEKEZAJI pamoja na dhana ya UKUONGEZA UZALISHAJI wa Mazao kwa WINGI zaidi (Quantity) badala ya fikra za Magufuli kudhamiria Kuanzisha viwanda vya ndani ili Kuongeza thamani ya Mazao yetu ya Asili yalokuwa BORA zaidi (Quality).
Nimalizie tu kwa kusema, rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan awe makini sana na dhana hizi, kwani hatukuanza jana wala juzi. Tulifuata mrengo ule toka wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi, akaja Mh. Benjamin Mkapa na Mwishowe mstaafu Jakaya Kikwete, na kote huko nyuma tulifanya makosa mengi sana kwa dhana ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Biashara. Matokeo yake tukaunda Matabaka ya Walionacho na wasiona nacho baina ya Wainanchi wenyewe. Ndipo Ufisadi na rushwa viliposhamiri kwani hapana alotaka kubakia katika kundi la wasionacho (Maskini)
Maoni ya rais kuhusu matumizi ya mbinu za kisasa katika Kilimo, kuna hatari kubwa ya nchi yetu kurudi kutawaliwa tena Kiuchumi kutokana na ujio wa mbegu za maabara ambazo zitaondoa kabisa rutuba ya Ardhi yetu, ubora wa mbegu zetu (Organic) na kubwa zaidi kumikilisha Mashirika ya nje nguzo za Uchumi wetu Kitaifa.
Maasalaam,
- Ramadhan Kareem
Kweli; "rais wa mfano"?Nikasema Magufuli atakuwa rais wa mfano nikapigwa vita vile vile pande zote.
Toa na wewe uchambizi wako tofauti badala kukashifu bila kuonyesha wapi panakiwa kusahihishwa au kuongezewa. Mimi nimeona huo ni uchambuzi mahiri.Kwahiyo huu ndiyo uchambuzi au maoni yako
Jikite kwenye uchambuzi acha ukabila.Mkuu wewe ni yule Rufufu Mkandara mchambua mikanda ya video? Yaani hapa ndio umechambua hotuba ya Rais Samia? Haki ya nani Kanda ya Ziwa inatapatapa!! Uliposikia anasema kuongeza uzalishaji wewe ukenda kwenye GMO? Mbona mama alikuwa wazi kabisa kwamba wataiongezea uwezo (mtaji) ASA ili izalishe mbegu za kutosha kuliko kutegemea mbegu za kutoka nje! ASA haizalishi GMO mkuu! Naona mnahaha!!
Kwani mchambuzi wa hotuba mwenyewe anasemaje?Jikite kwenye uchambuzi acha ukabila.
Nakubaliana na mengi, lakini la mwisho siyo kweli. China haijaendelea kwa mitaji ya nje, ila imeendelea kwa kuwapeleka wachina wengi nje na kurudi kuendesha gurudumu la maendeleo. Wachina maelfu na malaki wamesoma USA, Ujermani, Ufaransa, Urusssi, na Ulaya yote. Wengi wao walibaki wakifanya kazi huko na baada ya miaka waliondoka na teknolojia ambayo wameitumia kwao kuirusha China kimaendeleo.Kuna mifumo ya kizamani dunia ilipokuwa ni kama inaanza na kila mtu alikuwa hana kitu, was the big struggle....kwa sasa dunia imeendelea sana kwenye mambo mengi na vitu vingi hupatikana kwa urahisi..
Tunapozungumzia uwekezaji tunazungumzia watu wenye mitaji kuanzia ya hela, akili na teknolojia...watu hawa wako mbele miaka mingi kwa kila kitu....kuwaalika na kuchangamana nao maana yake tunachangamsha uchumi wetu na watu wetu wanapata mitaji, akili, maarifa, teknolojia nk vitu hivi vikifika kwa watu wetu nao watapata uwezo wa kuwekeza hapa na kwingineko....China tunayoiona imekua kwa uwekezaji kutoka ulaya na kujifunza maarifa kutoka ulaya..
Kwa maoni yako,mpaka sasa amekosea au anakosea wapi...?Samia hana uthubutu wa kufanya maamuzi magumu, atakuwa rais wa maneno tu na mipasho.
Mzee Mkandala, huo ni uchambuzi maoni au ni maoni yako madogo kwenye hotuba...!!?Kwa rehma zake Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu sote tutaumaliza Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan salama salimin na hakika yeye ndiye mwenye kurehemu riziki zetu kubwa na ndogo na hapana mwingine apaswaye kuabudiwa. Tumuombe sote atuepushe na kila lisokuwa na kheri kwetu. Ameen.
Nina hakika siku ya leo tutasikia SIFA kemkem za mafuta ya tin na zaitun zitamiminika kupamba na kusifia hotuba ya rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu imewagusa watu wote katika mazingira tofauti katika mwelekeo mpya wa dira ya Awamu hii ya sita ikitekeleza kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.
Mimi binafsi, niseme ukweli wangu kutoka moyoni ya kuwa sii mshabiki wa rais Mama Samia Suluhu Hassan toka hotuba yake ya kwanza alipo apishwa kama rais wa Awamu ya sita. Huu ndio ukweli wangu! Na sababu zangu ni ndogo kabisa, nilimsoma toka mwanzo mwelekeo na Dira yake Kitaifa, dira ambayo Kiitikadi, mimi sii muumini wake na hupingana na nadharia zinazofungamana zaidi na UBEPARI badala ya UJAMAA wa Mwafrika.
Hivyo unaponisoma hapa ni muhimu Uzingatie kuwa mimi ni muumini wa UJAMAA wa Mwafrika na naamini Maendeleo ya Tanzania yataletwa na WATANZANIA wenyewe badala ya WAWEKEZAJI kutoka nje. Imani ya kwamba maendeleo yetu yanahitaji kuweka masharti rahisi ili kuvutia Wawekezaji ni sawa na fikra za.Kitumwa za Mababu zetu walokubali kupewa na wakoloni Shanga na vilemba ili tupendeze huku wagenu wakiondoka na madini mali ghafi na nyara zetu za Kitaifa.
Niseme wazi kwamba binafsi yangu naiona tofauti kubwa sana baina ya Hayati rais wa awamu ya Tani John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na kwamba hawa sii kitu kimoja hata kidogo. Tofauti zinazotokana na ahadi za mabadiriko makubwa ya SERA na SHERIA ambazo Chama cha Mapinduzi na Hayati Magufuli walizitumia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020. Niseme kwa nini nasema hivi?
Haina Shqka kabisa, Hayati Magufuli alikuwa rais anayepigania maslahi ya Wananchi Wanyonge kwa maana ya Watanzania Maskini dhidi ya Wawekezaji Mabeberu tofauti kabisa na Dira na Mwelekeo wa Mama Samia anayetazama zaidi viwashwishi kwa maslahi ya WAWEKEZAJI pamoja na dhana ya UKUONGEZA UZALISHAJI wa Mazao kwa WINGI zaidi (Quantity) badala ya fikra za Magufuli kudhamiria Kuanzisha viwanda vya ndani ili Kuongeza thamani ya Mazao yetu ya Asili yalokuwa BORA zaidi (Quality).
Nimalizie tu kwa kusema, rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan awe makini sana na dhana hizi, kwani hatukuanza jana wala juzi. Tulifuata mrengo ule toka wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi, akaja Mh. Benjamin Mkapa na Mwishowe mstaafu Jakaya Kikwete, na kote huko nyuma tulifanya makosa mengi sana kwa dhana ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Biashara. Matokeo yake tukaunda Matabaka ya Walionacho na wasiona nacho baina ya Wainanchi wenyewe. Ndipo Ufisadi na rushwa viliposhamiri kwani hapana alotaka kubakia katika kundi la wasionacho (Maskini)
Maoni ya rais kuhusu matumizi ya mbinu za kisasa katika Kilimo, kuna hatari kubwa ya nchi yetu kurudi kutawaliwa tena Kiuchumi kutokana na ujio wa mbegu za maabara ambazo zitaondoa kabisa rutuba ya Ardhi yetu, ubora wa mbegu zetu (Organic) na kubwa zaidi kumikilisha Mashirika ya nje nguzo za Uchumi wetu Kitaifa.
Maasalaam,
- Ramadhan Kareem
πππππSasa umechambua nini hapo mkuu?