Uchambuzi huru: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya Aprili 22, 2021

Mzee Mkandala, huo ni uchambuzi maoni au ni maoni yako madogo kwenye hotuba...!!?

😁😁😁😁😁
Unapochambua hoja za kisiasa unatazama Uhalisia wa Sera zinazotazamiwa kuongoza DIRA na MWELEKEO wa Taifa Katika muda husika! Huhitaji kuandika gazeti au vipengele vya hotuba ilichukua masaa matatu kuelezea. Binafsi yangu, hotuba nzima sikuona jipya ambalo Mkapa na Kikwete hawakufanya. Kwa ujumla JK kwa nia nzuri kabisa alitoa nafuu ya kodi kwa Wawekezaji wa nje miaka mitano bila kulipa. zana na vitendea kazi za Ujenzi na Uendeshaji bure, vibali vya kazi vikatoka kama uyoga lakini matokeo yake Ufisadi ulikuwa mkubwa. Nini najaribu kujenga hapa? Ni kwamba Maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe.

Serikali zote za Ulaya na Amerika zimeweza kutokana na pato la Kodi kwa kuwezesha raia wao. Ubepari ni mfumo ulotangulia kabla ya soko huria ambao msingi wake ulikuwa CHUMA NJE leta Mafanikio yako nyumbani. Na ndio Utajiri wa nchi hizo ulipoanzia. Sisi kama Mabepari tutachuma wapi na kuleta nyumbani. Aidha mfumo ulofuata baada ya wao kujenga viwanda ni Soko huria! Yaani wamepanua sasa soko lao na mahitaji waweze kuuza bidhaa zao mahala popote Duniani. Sisi tutauza wapi ikiwa hatuna viwanda vyetu wenyewe? Atakaye jenga Kiwanda Tanzania atasaidia Ajira na huyo raia ndiye atakuwa mlipa kodi wakati Mwekezaji akipeleka mavuno yake kwao Ulaya. Tumewaona kina Acacia na Symbion, je bado hatujapata somo?
Jamani Mchina ajenge bandari ya Bagamoyo kweli? Kama tumeweza.kujenga Hydro sisi wenyewe tunashindwa kipi kujenga Bandari? Let people pay tax hili sii swala la Hiyari bali mandatory na halihitaji ku negotiate. Je, ikiwa rais ana bishara zake nani ataweza kuzungumza naye kuhusu kodi? Tuwaache TRA wafanye kazi zao kiutaalam. Hukulipa.kodi miaka 5 au 10 iliyopita, ni nafuu zipi zitamfanya aanze kulipa kodi kesho? Just common sense haihitaji digrii..
 
Ujamaa, baki nao nyumbani kwako mkuu, kenya mbona hawana mlengo huo ,na wametuzidi kila kitu, na Kama ndo ulikua msimamo wa mwendazake amefanya nini, Kama sio kaacha wananchi wanakufa njaa, Yani uje na ujamaa wakati wewe na watu WAKO mnaishi Kama mpo peponi, pelekeni ujamaa wenu huko,
 
Una waza kizamani bado, wajamaa akil zenu ni stugnant sana haziji-update kadri dunia inavyobadilika..
Stuka dunia inaenda resi sana ukikaa na akil mgando utakufa maskini.. na utaumiza wengi wanaokuzunguka
 

"China tunayoinoa imekua kwa uwekezaji kutoka ulaya na kujifunza maarifa kutoka ulaya"

hapo mwisho niliandika hivyo nikimaanisha walichota maarifa kutoka ulaya na america kwa maana ya kujifunza kama ulivyosema walipeleka watu wengi kusoma huko na kurudi china ndio maana ya maarifa..

Makampuni mengi kutoka Ulaya na America yalikwenda kuwekeza China yakifuata cheap skilled labor force, cheap raw materials na market force ya China....hapa kuna makampuni kama Apple, Nike, Cocacola, IBM, Microsoft, Siemens, Boeng, Wartsila nk....hii yote ni mitaji kutoka ulaya na America...
 

Faida kubwa za wawezaji huwa ni mbili tu: Walipe kodi serikalini, halafu watoe ajira kwa watanzania. Unapokuwa sera zinazotoa tax holiday kwa wawekezaji halafu zinawaruhusu kuleta wafanyakazi kutoka nje, ujue huna sera hapo.

Sera za China zilikuwa hivyo kuwa unawekeza lakini wafanyakazi watakuwa ni wachina, na uwafundishe kufanya kazi hizo.
 
Na mimi nadharia za kijamaa huwa sisomi kabisa maana ni kama uchuro wa kuabudu umaskini
Lakini Hayati rais Magufuli na mwelekeo mpya wa CCM tumeona mafanikio ya Ujamaa. Sisi wenyewe tuliishi Kijamaa zamani. Ukienda Ulaya unamwezesha rafiki yako naye kuondoka ama kufungua Biashara. Hivi mnadhani wazee wetu waliwezaje kujenga, kumiliki ardhi na maashamba tunayorithi leo hii? Wewe una kipi cha kumuachia mwanao kama sio kusema mwangu Soma na wewe katafuta zako!

Vijana wa Kariakoo, Ilala, Kinondoni, Magomeni, Manzese kote waliishi kama ndugu na tulisaidia na wamoja kwa shida na raha. Huwezi kumuondoa Mtanzania katika Umaskini kwa kutegemea hisani ya mzungu. Scandinavia yote, Canada, na hata China ni Wajamaa. Je wamekosa kipi ambacho wewe unadhani Ujamaa wa Mwafrika ni mbaya?

Unadhani Wachina wamejaanTanzania kwa bahati mbaya? Hapana wanashtuana na huo ndio Ujamaa. Ubepari ukiwa na mchongo lazima uwe na roho mbaya, yaani njia za mafanikii yako siri, ukivujisha hata kampuni unapofanya kazi watakufukuza.
 
Mimi sioni kama ni uchambuzi huru, ila umetoa maoni yako, na yapaswa kuheshimiwa.
Ulipochemsha ni pale uliposema: 'SERA na SHERIA ambazo Chama cha Mapinduzi na Hayati Magufuli walizitumia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020.'
 
Reactions: Pep
Duh! Mleta mada hana hoja kabisa. Ujamaa tena? Inamaana Magufuli alivyoturudisha nyuma kimaendeleo unaona kabisa haitoshi, na kwamba sasa mama Samia aturudishe nyuma zaidi ya Magufuli.
 
Mbegu za asili zipo? Kilimo cha kisasa hakiepukiki. Wawekezaji wapo sehemu zote duniani. Tunahitaji mitaji. Cha muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa sheria nzuri zinatungwa ili wote tuweze kunufaika na uwekezaji husika!
 
Jana ktk hotuba ya Mne.rais alisema haya makampuni yanapata hasara lkn wakat wakutoa gawio la serikal wana toa, sasa wannatolea wapi hawa watu
 
Mkuu huyu ni Luuufufuuuuuu!!!
 
Kwakweli Hapo umegongelea penyewe kabisa, kama ulivyosema, tuliokuwa na miongo 3 , ya haya mambo ya kuvutia wawekezaje toka wakati wa Mzee Ruksa, Akaja wa uwazi na ukweli, na Baadaye Ari na kasi mpya, na huko kote tunaona kutolipwa kwa kodi kwa njia mbali mbali na uwekezaji wa fdi foreign direct investment , ambao madhara yake. Tuliyaona, JPM hakukurupuka tu kutumia hizo hatua kuthibiti hali iliyokuwepo , hivyo kwa wengine wanaofuata bila kujua kwanini hatua hizi zilichukuliwa na mtangulizi wake na nini cha kufanya sasa tutarudi miaka 30 nyuma tena, na muda huo hatuna
 
Utawezaje kuongeza mazao ya mbegu pasipo kupitia maabara? Utawezaje kuongeza uzaliahaji wa.maziwa ya ng'ombe pasipo maabara? Hivi GMO wewe unaielewaje? Neno modified lina maana gani mkuu?
 
Para mbili zilizobeba ujumbe mzito sana. Mwekezaji aje toka nje, apewe misamaha ya kodi na kuja na manpower toka nje; sisi kama taifa tutafaidika vipi na huo uwekezaji?

Viongozi wengi wa kiafrika hufikiri wao wana akili sana kuliko wanaowaongoza. Tanzania ya leo si ile aliyoiongoza mzee Mwinyi. Watu wakiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo wataishiwa uvimilivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…