Unajua mkuu habari za.kusimuliwa na kina Zitto zinaweza kabisa kukupotosha kwa sababu wanachukua figure na kukulisha wakati hawazingatii viashiria vya Ukuaji wa deni la Taifa na matumizi yake.
Hivi wewe kama unakaa nyumba ya kupanga unalipa kodi kwa mwezi unatumia mathlan laki 5. Lakini ukaamua unataka.kujenga nyumba. Ukakopa Benki mil. 1 ya Ujenzi. Je, utasema kwamba nimefanya kosa kubwa sana maana sasa hivi nadaiwa mil. 1 pamoja na zile laki 5? Hivi nikuulize ile mikopo ya JK alijenga kitu gani haswa? Lile Daraja la Kigamboni maana nasikia wastaafu wa NSSF wanalia mpaka leo! Au mikopo ilitokana na dawa sio dawa za Ukimwi pamoja na vile vyandarua vya Malaria?!!
Kama hujui miradi aliyoifanya Kikwete basi utakuwa hufuatilii nchi hii inatoka wapi inakwenda wapi!
Ni ajabu kuuliza swali eti Kikwete alijenga kitu gani haswa? —Ina maana kuunganisha nguvu ya umma kujenga shule za kata na maabara nchi nzima unaona ni kitu kidogo?, Kuunganisha mikoa ya nchi hii kwa mtandao wa barabara za lami unaona siyo kitu?, Kutandaza mkongo wa Taifa kwa ajili ya Internet unaona ni kitu kidogo?, Kujenga Hospitali ya Mloganzila, Benjamin Mkapa huko Dodoma unaona siyo kitu?, Madaraja ya Malagarasi, Uwanja wa Ndege Terminal 3, Kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara unaona siyo kitu?, Barabara za Mwendokasi Dar unaona siyo kitu?, Ukarabati wa viwanja vikubwa vya ndege almost nchi nzima unaona siyo kitu? , Ujenzi wa Zahanati za Kata nchi nzima unaona siyo kitu?, Kusambaza umeme vijijini kupitia mpango wa REA unaona siyo kitu?, au Unadhani REA ilianza na Magufuli?, Ujenzi wa Nyumba za Maaskari nchi nzima huoni kuwa ni kitu?, Ujenzi wa Kituo cha kisasa cha kutibu moyo (JK Heart Institute) siyo kitu?, Vivuko vingi alivyonunua mfano kivuko cha MV Magogoni, na vibgine vingi tu unaona siyo kitu?, Miradi ya Maji kama vile kutoka Ruvu kupitia Bunju unaona siyo kitu?, Mieadi ya Umeme ya Kinyerezi 1 na 2 unaona siyo kitu?, Ujenzi wa chuo kikuu cha UDOM unaona siyo kitu?, Kutoa ajira kwa wingi, kupandisha kima cha chini, kupandisha watu madaraja kila mwaka kwa mujibu wa mikataba ya kazi wewe unaona hiyo siyo kitu?
Na miradi mingine mingi mingi tu ambayo siwezi kuiorodhesha hapa!
Kikwete alifanya miradi mikubwa sana lakini hakututia deni kubwa kama ambalo Magufuli katuingiza.
Unamletaje Zitto katika huu mjadala? —Kuhusu deni la Taifa kuwa kubwa sana kipindi cha Magufuli siyo habari ya Zitto baki ni fact!