Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Mpuuzi wewe mfuate huko aliko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I cannot say never...Lakini tumpe mama benefit of doubt ni mapema sana kuhukumu; ila nilishajiapiza sintaondoka dunia hii kama msindikizaji ipo siku nayo yaja tena si mbali sana kama si mimi kizazi changu nchi hii haitakaa irudi kwenye ufisadi....nadhani sipo ndotoni ebu tuendelee tuone!Mkuu 'Ame'
Nimefuatilia maandishi yako kwenye mada hii, na nadhani nimeelewa vizuri unachkiandika hapa; ambacho mimi ninakubaliana nacho kabisaaaaa!
Ila, usijidanganye, ukadhani viongozi tulionao wana fikra kama ulizonazo wewe; na wala usidhani kwa hali ya wananchi wa Tanzania ilivyo, unaweza ukaitegemea kuzuia chochote.
Akitokea JK mwingine sasa hivi huko CCM, usidhani kuna mtu yeyote atakayenyanyua kidole. Utaanza kuona watu wanajipanga kwenye mstari kuimba nyimbo zake na kumwonyesha yeye ni kama malaika.
Inaumiza sana.
Iwe ni kwa bahati tu, tumpate kiongozi mwenye kuyaamini haya yanayopigiwa kifua na mkuu 'Ame' na wengine kama akina 'Mkandara' na akina 'Kalamu1' - hiyo itakuwa ni bahati yetu nzuri tu na sio kwa utashi wa waTanzania..., sijui kwa nini.
Lakini mtu huyo asiwe kama Marehemu Magufuli, kwa yale mabaya yake!
Sijui tutampataje mtu wa aina hiyo. Najua wapo..., lakini hawataki kujitokeza mbele waliokoe taifa letu.
Basi ulishindwa kutimiza wajibu wako maana CAG katuonyesha wazi, serikali ya mwendazake ilijaa ufisadi na upigaji.I cannot say never...Lakini tumpe mama benefit of doubt ni mapema sana kuhukumu; ila nilishajiapiza sintaondoka dunia hii kama msindikizaji ipo siku nayo yaja tena si mbali sana kama si mimi kizazi changu nchi hii haitakaa irudi kwenye ufisadi....nadhani sipo ndotoni ebu tuendelee tuone!
Kama nilivyosema nakubalina kabisa na wewe kwa mengi ila amini nimeishi na hawa ndugu zetu, nimefanya nao kazi tangu ni kiwa kinda kabisa age ya 25 years....Linapokuja maslahi ya jamii yao na mataifa yao imeshakuwa kama ugonjwa they never count us as beneficiaries....At personal level ni watu wazuri sana honest wenye integrity ila nadhani wamekuzwa kuamini sisi hatustahili kama wao. Hata akijitahidi vipi bado hawezi kubali kuwa sawa na sisi...Hofu hii ndiyo inayowapelekea kutoamini kutoa fursa ya sisi kujitegemea hata siku moja kwakua wanajua tukishafanikiwa pengine watapunguza heshima yao.Kuna story moja, sijui kama ni kweli au story tu, lakini ujumbe wake ni muhimu kuuelewa.
Inamhusu waziri mmoja mkubwa wa Nigeria, nafikiri alikuwa waziri wa fedha.
Alikuwa waziri shupavu kupinga rushwa, nchi haijawahi kuona waziri shupavu kama huyo, alikuwa anasema sana kukemea rushwa.
Ikafika wakati akaanza mpaka kwenda benki za kimataifa kunegotiate hela za Nigeria zirudishwe, alikuwa hataki mchezo.
Akaenda Uswizi, akazwa anazunguka mabenki, akafanya uchunguzi kutafuta benki yenye usiri kabisa Uswizi.
Akaipata, akaenda kuonana na CEO wa benki.
Akamwambia anataka majina ya Wanaijeria wote wenye hela kwenye hiyo benki, na vyanzo vyao vya mapato.
CEO akamwambia siwezi kukupa majina hayo.
Akasema nipe majina, ukinipa nitakutafutia deal kubwa sana na serikali ya Nigeria iweke hela zake kwenye benki yako, utapata faida sana.
CEO akawmambia siwezi kukupa majina, nafuata kanuni za faragha za kibenki.
Waziri akamwambia nitatengeneza deal na serikali ya Nigeria kwamba ukiripoti hela za wizi zilizoibiwa Nigeria tutakupa kiasi fulani katika hizo hela.
CEO akakataa, akasema hawezi kuzisaliti kanuni za faragha za kibenki.
Basi yule Waziri akamwambia CEO, huyu hapa Dr. Adebayo Adedeji wa African Development Bank, ukitupa majina tutakupa deal kubwa sana la Benki ya Maendeleo ya Africa, uweke hela za mabilioni mengi sana ya ADB.
CEO akakataa kutoa majina, akasema siwezi kusaliti kanuni za faragha za kibenki.
Waziri akasema sawa, wewe ndiye niliyekutafuta.
Nimekuja na mimi nataka kuweka mamilioni ya dola yangu kwenye benki yenu, lakini kabla ya kuweka kwanza nilikuwa nakupa mtihani nione kama watu wakija kutaka majina ya wateja wenu unaweza kutoa au hutatoa.
What's my point?
Ukiwa so caught up na habari za "mabeberu this, mabeberu that" na kushikwa na theatrics za viongozi wa Afrika wanaojinadi kupigana na mabeberu, unaweza kuchotwa kirahisi na watu wanaoshirikiana na hao mabeberu.
Mtu anaweza kujitengenezea image nzuri kuwa anapingana na mabeberu, kumbe na yeye anajipandisha bei tu apige hela kubwa zaidi.
Tunatakiwa kuwa makini sana tusiingie katika mtego wa simple narratives.
Kuna mabeberu wengine weusi wenzetu Watanzania, na kuna watu wa nchi za nje wanaoweza kutusaidia kupigana na ubeberu.
Kwa hiyo tujadili mambo kwa nuance, sio kwa a broad painting brush.
Pengine!Basi ulishindwa kutimiza wajibu wako maana CAG katuonyesha wazi, serikali ya mwendazake ilijaa ufisadi na upigaji.
Na upigaji aliotuonyesha CAG ni just tip of the iceberg, je angekagua mamununuzi ya hizo ndege si pangechimbika?
Well nachambua kulingana na jinsi mnavyopeleka Mjadala huu maanake nimeona watu wengi bado wanataka kulinganisha sio tu Magufuli na Samia bali hata Viongozi walotangulia kama JK .@Mkandara ,unachambua hotuba ya Mh. Rais Samia au unamuongelea mwendazake JPM!!??
Naona Magufuli nyingi zaidi ya kilichoongelewa na Mh. Rais.
Na mm pengine natafuta nafasi hiyo...Moyo wa binadamu una siri sana...I concur!Kuna story moja, sijui kama ni kweli au story tu, lakini ujumbe wake ni muhimu kuuelewa.
Inamhusu waziri mmoja mkubwa wa Nigeria, nafikiri alikuwa waziri wa fedha.
Alikuwa waziri shupavu kupinga rushwa, nchi haijawahi kuona waziri shupavu kama huyo, alikuwa anasema sana kukemea rushwa.
Ikafika wakati akaanza mpaka kwenda benki za kimataifa kunegotiate hela za Nigeria zirudishwe, alikuwa hataki mchezo.
Akaenda Uswizi, akazwa anazunguka mabenki, akafanya uchunguzi kutafuta benki yenye usiri kabisa Uswizi.
Akaipata, akaenda kuonana na CEO wa benki.
Akamwambia anataka majina ya Wanaijeria wote wenye hela kwenye hiyo benki, na vyanzo vyao vya mapato.
CEO akamwambia siwezi kukupa majina hayo.
Akasema nipe majina, ukinipa nitakutafutia deal kubwa sana na serikali ya Nigeria iweke hela zake kwenye benki yako, utapata faida sana.
CEO akawmambia siwezi kukupa majina, nafuata kanuni za faragha za kibenki.
Waziri akamwambia nitatengeneza deal na serikali ya Nigeria kwamba ukiripoti hela za wizi zilizoibiwa Nigeria tutakupa kiasi fulani katika hizo hela.
CEO akakataa, akasema hawezi kuzisaliti kanuni za faragha za kibenki.
Basi yule Waziri akamwambia CEO, huyu hapa Dr. Adebayo Adedeji wa African Development Bank, ukitupa majina tutakupa deal kubwa sana la Benki ya Maendeleo ya Africa, uweke hela za mabilioni mengi sana ya ADB.
CEO akakataa kutoa majina, akasema siwezi kusaliti kanuni za faragha za kibenki.
Waziri akasema sawa, wewe ndiye niliyekutafuta.
Nimekuja na mimi nataka kuweka mamilioni ya dola yangu kwenye benki yenu, lakini kabla ya kuweka kwanza nilikuwa nakupa mtihani nione kama watu wakija kutaka majina ya wateja wenu unaweza kutoa au hutatoa.
What's my point?
Ukiwa so caught up na habari za "mabeberu this, mabeberu that" na kushikwa na theatrics za viongozi wa Afrika wanaojinadi kupigana na mabeberu, unaweza kuchotwa kirahisi na watu wanaoshirikiana na hao mabeberu.
Mtu anaweza kujitengenezea image nzuri kuwa anapingana na mabeberu, kumbe na yeye anajipandisha bei tu apige hela kubwa zaidi.
Tunatakiwa kuwa makini sana tusiingie katika mtego wa simple narratives.
Kuna mabeberu wengine weusi wenzetu Watanzania, na kuna watu wa nchi za nje wanaoweza kutusaidia kupigana na ubeberu.
Kwa hiyo tujadili mambo kwa nuance, sio kwa a broad painting brush.
Huu ni ufupisho wa hotuba na wala si uchambuziKwa rehma zake Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu sote tutaumaliza Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan salama salimin na hakika yeye ndiye mwenye kurehemu riziki zetu kubwa na ndogo na hapana mwingine apaswaye kuabudiwa. Tumuombe sote atuepushe na kila lisokuwa na kheri kwetu. Ameen.
Nina hakika siku ya leo tutasikia SIFA kemkem za mafuta ya tin na zaitun zitamiminika kupamba na kusifia hotuba ya rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu imewagusa watu wote katika mazingira tofauti katika mwelekeo mpya wa dira ya Awamu hii ya sita ikitekeleza kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.
Mimi binafsi, niseme ukweli wangu kutoka moyoni ya kuwa sii mshabiki wa rais Mama Samia Suluhu Hassan toka hotuba yake ya kwanza alipo apishwa kama rais wa Awamu ya sita. Huu ndio ukweli wangu! Na sababu zangu ni ndogo kabisa, nilimsoma toka mwanzo mwelekeo na Dira yake Kitaifa, dira ambayo Kiitikadi, mimi sii muumini wake na hupingana na nadharia zinazofungamana zaidi na UBEPARI badala ya UJAMAA wa Mwafrika.
Hivyo unaponisoma hapa ni muhimu Uzingatie kuwa mimi ni muumini wa UJAMAA wa Mwafrika na naamini Maendeleo ya Tanzania yataletwa na WATANZANIA wenyewe badala ya WAWEKEZAJI kutoka nje. Imani ya kwamba maendeleo yetu yanahitaji kuweka masharti rahisi ili kuvutia Wawekezaji ni sawa na fikra za.Kitumwa za Mababu zetu walokubali kupewa na wakoloni Shanga na vilemba ili tupendeze huku wagenu wakiondoka na madini mali ghafi na nyara zetu za Kitaifa.
Niseme wazi kwamba binafsi yangu naiona tofauti kubwa sana baina ya Hayati rais wa awamu ya Tani John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na kwamba hawa sii kitu kimoja hata kidogo. Tofauti zinazotokana na ahadi za mabadiriko makubwa ya SERA na SHERIA ambazo Chama cha Mapinduzi na Hayati Magufuli walizitumia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020. Niseme kwa nini nasema hivi?
Haina Shqka kabisa, Hayati Magufuli alikuwa rais anayepigania maslahi ya Wananchi Wanyonge kwa maana ya Watanzania Maskini dhidi ya Wawekezaji Mabeberu tofauti kabisa na Dira na Mwelekeo wa Mama Samia anayetazama zaidi viwashwishi kwa maslahi ya WAWEKEZAJI pamoja na dhana ya UKUONGEZA UZALISHAJI wa Mazao kwa WINGI zaidi (Quantity) badala ya fikra za Magufuli kudhamiria Kuanzisha viwanda vya ndani ili Kuongeza thamani ya Mazao yetu ya Asili yalokuwa BORA zaidi (Quality).
Nimalizie tu kwa kusema, rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan awe makini sana na dhana hizi, kwani hatukuanza jana wala juzi. Tulifuata mrengo ule toka wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi, akaja Mh. Benjamin Mkapa na Mwishowe mstaafu Jakaya Kikwete, na kote huko nyuma tulifanya makosa mengi sana kwa dhana ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Biashara. Matokeo yake tukaunda Matabaka ya Walionacho na wasiona nacho baina ya Wainanchi wenyewe. Ndipo Ufisadi na rushwa viliposhamiri kwani hapana alotaka kubakia katika kundi la wasionacho (Maskini)
Maoni ya rais kuhusu matumizi ya mbinu za kisasa katika Kilimo, kuna hatari kubwa ya nchi yetu kurudi kutawaliwa tena Kiuchumi kutokana na ujio wa mbegu za maabara ambazo zitaondoa kabisa rutuba ya Ardhi yetu, ubora wa mbegu zetu (Organic) na kubwa zaidi kumikilisha Mashirika ya nje nguzo za Uchumi wetu Kitaifa.
Maasalaam,
- Ramadhan Kareem
Kama ilivyo ada sitachoka kutoa darasa kwa watu wanojadili vitu kwa sababu wamesikia kwa watu wakisema ama wamesoma pahala. ATCL haijafufuka kivipi wakati shirika.lipo, ndege zinaruklshwa na marubani Waajiriwa wa ATCL! Au kufufuka mpaka uhakiki na vidole kama Wafuasi wa Yesu? Hahahaha it's joke.Kama wewe unaamini kuwa 1984 Nyerere aliiacha nchi kwenye hali nzuri sana kiuchumi sina neno la kukuongezea.
Isipokuwa ninachofahamu ni kuwa Nyerere alikuwa amehangaika sana kutafuta misaada na mikopo nafuu akaishia kukutana na kikwazo cha IMF. Wafadhili wakubwa hata marafiki wa Tanzania hawakuwa tayari kumpa misaada mikubwa nje ya muafaka na IMF. Yeye aligoma kabisa kusaini mkataba na IMF akaamua kung’atuka.
Nilisoma kuwa AHM alipoingia madarakani kama Rais, wadau mbalimbali na media walimuuliza Mwalimu kama atakuwa radhi mrithi wake AHM asaini mkataba na IMF kama Rais wa JMT. Akasema hana tatizo kabisa na hilo ilimuradi sio yeye!
Nyerere alijua vizuri sana masharti ya IMF kwamba yangeathiri sana legacy yake hasa mashirika ya umma yaliyokuwa yameshikilia uchumi wa taifa. Lakini alijua hakuna namna. Itabidi AHM asaini mkataba na IMF na kuutekeleza. Ilikuwa dhahiri kwamba mashirika kama TRC, ATC, TANESCO, n.k. yaliyokuwa yakiendeshwa bila ufanisi, rushwa kwa wingi, nepotism, n.k. yangetetereka na mengine kufa.
Kwa taarifa yako, ATCL bado haijafufuliwa. Kilichofanyika ni serikali kujitwisha mzigo wa kununua na kumiliki ndege angalau kuweka taswira ya uhai wa ATCL. Ndege sio kigezo cha uhai wa shirika ya ndege. Kama alivyosema Rais Mh. SSH, hatua za kufufua shirika zitachukuliwa rasmi ili kulipa uhai wa kibiashara.
Miradi mingine ya umeme, reli, n.k. bado ni miradi. Tusubiri kuona hatua zitakazochukuliwa kuikamilisha na kuiendesha kwa ufanisi. Nina hakika hata Magufuli angekuwepo isingeendeshwa “KIJAMAA” kama enzi za Nyerere. Na angethubutu kufanya hivyo angekwama mapema sana. Hata North Korea yenyewe leo hii inashiriki uchumi wa kibepari kwa kuibia sana. Makampuni ya US na Ulaya yanazalisha bidhaa huko kwa kutumia mgongo wa China kukwepa vikwazo vya UN.
Kuhusu wizi wa Magufuli nakuachia ubishane na hao waliokuambia. Sina hizo siri.
Soma hiyo document niliyokuwekea hapo nchini uone jinsi nchi ilivyokuwa inatimka vumbi kwa ujenzi kipindi cha JK
Achana na hearsay
By the way ni JK ndiye aliyetuondolea aibu ya kupitia Kenya kwenda Kagerhoja hapa.ni kipanda kwa dwni la Taifa. Nimekuuliza ni vitu gani vilivyojengwa kwa fesha hizo hujanibu. Unanipa list ya vitu ambavyo hata Mkuu wa Mkoa au Halmashauri walivifanya... Wabongo bana khaaa!
Tatizo mabeberu huangalia maslahi yao tu!! Inabidi kuwa tafu sana kushughulika na mabeberu! Wakikuona ni mjanja wanakupigia hesabu ya kukuondoa!!Sioni kosa kwa huo mtazamo wa Rais, hiyo dhana ya kila Rais kuja na mtazamo wake imeasisiwa na watangulizi wake, hivyo naye sio wa kwanza, japo hii tabia kwa namna fulani inachangia kuturudisha nyuma kitaifa, binafsi ningependa pawe na kitu kama succession plan kwa hawa viongozi wetu, anapomalizia mmoja ndipo aanzie mwingine.
Kuhusu kuvutia wawekezaji yupo sawa, hawa watu tunawahitaji na dollar zao watasaidia kwa namna kupunguza tatizo la ajira nchini, na kuongeza mzunguko wa pesa kwa watanzania kama anavyojinasibisha Rais, japo anatakiwa kuwa na tahadhari ahakikishe analinda maslahi yetu kama taifa.
Mfano. Alipozungumzia uchimbwaji wa madini ya Hellium yaliyopo kwenye mbuga fulani akasema Simba hawayali yale, sawa hawayali, lakini awe makini kwenye mikataba serikali yake itakayoingia na wawekezaji coz record za mikataba na wawekezaji kwa viongozi wa awamu zilizopita ni mbovu.
Mwisho kabisa unajinasibu kwa ujamaa kwa kusema wewe unaamini maendeleo ya mwafrika yataletwa na mwafrika mwenyewe, hiyo dhana kiukweli kwangu imepitwa na wakati, huu ujamaa wa mwafrika utaleta maendeleo gani bila kuwa na teknolojia, capital, na skilled man power inayohitajika? hapa unanikumbusha ile kauli ya Nyerere aliposema madini yaachwe ardhini yatachimbwa na mtanzania akiwa tayari.
Sasa kuliko kuendelea kusubiri huo utayari kwa serikali hii ya CCM ambayo imekuwa ikipigana na maadui watatu (ujinga, umaskini, maradhi) toka tupate uhuru zaidi ya miaka sitini sasa, huo utayari wa kuchimba wenyewe tutaupata lini? naona bora tuwape wazungu wachimbe, lakini tuhakikishe tunapata faida badala ya kuwaachia wazungu waondoke na faida huku viongozi wetu wakipata 10% na sisi kuachiwa mashimo.
Lakini umeona tumejadili page ngapi? Hizi ndio hekima katika mjadala. Nisingeweza yaweka yoote haya Ukurasa mmoja...Huu ni ufupisho wa hotuba na wala si uchambuzi
Mimi ningeomba hizi taarifa za CAG siku moja zinyanyambuliwe vizuri ili zieleweke.Basi ulishindwa kutimiza wajibu wako maana CAG katuonyesha wazi, serikali ya mwendazake ilijaa ufisadi na upigaji.
Na upigaji aliotuonyesha CAG ni just tip of the iceberg, je angekagua mamununuzi ya hizo ndege si pangechimbika?
CAG hapeleki watu mahakamani.Mimi ningeomba hizi taarifa za CAG siku moja zinyanyambuliwe vizuri ili zieleweke.
Haiingii akilini hata mara moja, matarakimu yote yale anayoyatoa kila mwaka uwe ni upigaji; halafu cha kusikitisha zaidi, kila anapomaliza kuyatangaza, na watu kuyapigia mayowe kwa muda, kila kitu kinarudi pale pale kama kawaida, kana kwamba hakuna lolote lililotokea.
Huoni yeyote akiwajibishwa, na wala juhudi za serikali kurekebisha chochote.
Mwishowe, imenibidi nihitimishe kwamba huu ni aina fulani ya usanii mtupu!
Naelewa vyema, kwamba sio kazi ya CAG kupeleka watu mahakamani, lakini si kuna vyombo stahiki?CAG hapeleki watu mahakamani.
Yeye anafanya kazi na kuiachia serikali au Bunge vichukue hatua. sasa serikali isipochukua hatua au bunge kutochukua hatua, wa kulaumiwa siyo CAG
Mkuu,nakubaliana nawe.Lakini,hao wazungu hawawezi kutulazimisha.Tunahiari kukubali au kukataa.Katika diplomasia ya uchumi sisi kama nchi lazima tuzingatie "the so called win-win situation." Tunategemeana.Ndugu yangu, kwa wazungu hicho kinachoitwa "diplomasia ya uchumi" kinamaanisha wewe kutoa malighafi ziende kwao na wewe uwe mpokezi wa "finished products" kutoka kwao ikiwemo mitumba.
Tuwe makini sana na ufunguaji milango ya kukaribisha wawekezaji kwani wengi ni WAPORAJI na wajengaji wa kwao. KAMWE HATUTAENDELEZWA NA WAWEKEZAJI.
#TANZANIAISNOTFORSALE!
Kuwa exposed ina maana gani kwako na ushamba ni nini?!Nimependa hapo kwa wanyonge. Hivi huwa wanamaanisha nn hasa wanaposema wanyonge? Au ni hao mama na baba lishe wanaowalisha wananchi wetu uchafu kwa kuvunja sheria za nchi? Jpm kwangu mm ni the most divisive president ever kwa Tanzania. Kizazi cha akina makonda, sabaya etc walikuwa juu ya sheria enzi za jpm why? Jpm hajawahi kuwa rais wa wanyonge alikuwa rais wa kikundi fulani na wale brain washed aliokuwa anawagawia pesa barabarani.
Mama Samia yuko exposed na part of ipi kwa kuwa amefanya kazi kwenye NGOs kubwa Znz kwa zaidi ya 20 yrs kama sikosei. Yule mwingine im sorry ila ushamba wake umetucost sana kama nchi kwa kweli.
Nasikia uchungu sana nikisoma uzi huu...yale machozi na zile kanga watanzania walizokuwa wanazitandika barabarani walizimaanisha...hata km JPM hakuwapa shilingi....maana kupata kiongozi mzalendo km JPM nimajaliwa na sasa kaondoka what next, business as usual ama?!Unapochambua hoja za kisiasa unatazama Uhalisia wa Sera zinazotazamiwa kuongoza DIRA na MWELEKEO wa Taifa Katika muda husika! Huhitaji kuandika gazeti au vipengele vya hotuba ilichukua masaa matatu kuelezea. Binafsi yangu, hotuba nzima sikuona jipya ambalo Mkapa na Kikwete hawakufanya. Kwa ujumla JK kwa nia nzuri kabisa alitoa nafuu ya kodi kwa Wawekezaji wa nje miaka mitano bila kulipa. zana na vitendea kazi za Ujenzi na Uendeshaji bure, vibali vya kazi vikatoka kama uyoga lakini matokeo yake Ufisadi ulikuwa mkubwa. Nini najaribu kujenga hapa? Ni kwamba Maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe.
Serikali zote za Ulaya na Amerika zimeweza kutokana na pato la Kodi kwa kuwezesha raia wao. Ubepari ni mfumo ulotangulia kabla ya soko huria ambao msingi wake ulikuwa CHUMA NJE leta Mafanikio yako nyumbani. Na ndio Utajiri wa nchi hizo ulipoanzia. Sisi kama Mabepari tutachuma wapi na kuleta nyumbani. Aidha mfumo ulofuata baada ya wao kujenga viwanda ni Soko huria! Yaani wamepanua sasa soko lao na mahitaji waweze kuuza bidhaa zao mahala popote Duniani. Sisi tutauza wapi ikiwa hatuna viwanda vyetu wenyewe? Atakaye jenga Kiwanda Tanzania atasaidia Ajira na huyo raia ndiye atakuwa mlipa kodi wakati Mwekezaji akipeleka mavuno yake kwao Ulaya. Tumewaona kina Acacia na Symbion, je bado hatujapata somo?
Jamani Mchina ajenge bandari ya Bagamoyo kweli? Kama tumeweza.kujenga Hydro sisi wenyewe tunashindwa kipi kujenga Bandari? Let people pay tax hili sii swala la Hiyari bali mandatory na halihitaji ku negotiate. Je, ikiwa rais ana bishara zake nani ataweza kuzungumza naye kuhusu kodi? Tuwaache TRA wafanye kazi zao kiutaalam. Hukulipa.kodi miaka 5 au 10 iliyopita, ni nafuu zipi zitamfanya aanze kulipa kodi kesho? Just common sense haihitaji digrii..
Mkuu hili neno 'win- win situation' ni mtego tu inategemea wewe utalielewaje.Mkuu,nakubaliana nawe.Lakini,hao wazungu hawawezi kutulazimisha.Tunahiari kukubali au kukataa.Katika diplomasia ya uchumi sisi kama nchi lazima tuzingatie "the so called win-win situation." Tunategemeana.
Daaah Uzuri hiyo ni hadithi japo inafikirisha! Ukweli unabakia Ukisha umwa na nyoka kuogopa majani yakikugusa sii kosa! Tembea sehemu za wazi zaidi kulizo zenye kiza na majani..Kuna story moja, sijui kama ni kweli au story tu, lakini ujumbe wake ni muhimu kuuelewa.