Tunakubaliana kwa vingi nakitofautiana kwa machache katika haya...Ila it doesnt matter kama ni Chines au weatern long as tunashindwa ku bargain na kufikia winwon situation ambayo haiji bila wenye ujuzi ba taaluma kuchukua haya majukumu.
Tatizo ni sote kugeuka kuqa waimba chorus tu bila kuwa na critical and analytical mind haya kwa ile cadre inayohotajika kusimama imara dhidi ya wengi ambao hawakupata nafasi ya kujua lugha ile mataifa makubwa wanaiongea.
Infact hakuna free lunch duniani na hakuna atalaye kuletea share yako kwenye silver plate na wala si kwakyoiga makelele mengi ndiyo utawatisha wapigaji...Let us be responsible, wewe na mimi kwa faida ya nchi yetu na vizazi vyetu
Kuna story moja, sijui kama ni kweli au story tu, lakini ujumbe wake ni muhimu kuuelewa.
Inamhusu waziri mmoja mkubwa wa Nigeria, nafikiri alikuwa waziri wa fedha.
Alikuwa waziri shupavu kupinga rushwa, nchi haijawahi kuona waziri shupavu kama huyo, alikuwa anasema sana kukemea rushwa.
Ikafika wakati akaanza mpaka kwenda benki za kimataifa kunegotiate hela za Nigeria zirudishwe, alikuwa hataki mchezo.
Akaenda Uswizi, akazwa anazunguka mabenki, akafanya uchunguzi kutafuta benki yenye usiri kabisa Uswizi.
Akaipata, akaenda kuonana na CEO wa benki.
Akamwambia anataka majina ya Wanaijeria wote wenye hela kwenye hiyo benki, na vyanzo vyao vya mapato.
CEO akamwambia siwezi kukupa majina hayo.
Akasema nipe majina, ukinipa nitakutafutia deal kubwa sana na serikali ya Nigeria iweke hela zake kwenye benki yako, utapata faida sana.
CEO akawmambia siwezi kukupa majina, nafuata kanuni za faragha za kibenki.
Waziri akamwambia nitatengeneza deal na serikali ya Nigeria kwamba ukiripoti hela za wizi zilizoibiwa Nigeria tutakupa kiasi fulani katika hizo hela.
CEO akakataa, akasema hawezi kuzisaliti kanuni za faragha za kibenki.
Basi yule Waziri akamwambia CEO, huyu hapa Dr. Adebayo Adedeji wa African Development Bank, ukitupa majina tutakupa deal kubwa sana la Benki ya Maendeleo ya Africa, uweke hela za mabilioni mengi sana ya ADB.
CEO akakataa kutoa majina, akasema siwezi kusaliti kanuni za faragha za kibenki.
Waziri akasema sawa, wewe ndiye niliyekutafuta.
Nimekuja na mimi nataka kuweka mamilioni ya dola yangu kwenye benki yenu, lakini kabla ya kuweka kwanza nilikuwa nakupa mtihani nione kama watu wakija kutaka majina ya wateja wenu unaweza kutoa au hutatoa.
What's my point?
Ukiwa so caught up na habari za "mabeberu this, mabeberu that" na kushikwa na theatrics za viongozi wa Afrika wanaojinadi kupigana na mabeberu, unaweza kuchotwa kirahisi na watu wanaoshirikiana na hao mabeberu.
Mtu anaweza kujitengenezea image nzuri kuwa anapingana na mabeberu, kumbe na yeye anajipandisha bei tu apige hela kubwa zaidi.
Tunatakiwa kuwa makini sana tusiingie katika mtego wa simple narratives.
Kuna mabeberu wengine weusi wenzetu Watanzania, na kuna watu wa nchi za nje wanaoweza kutusaidia kupigana na ubeberu.
Kwa hiyo tujadili mambo kwa nuance, sio kwa a broad painting brush.