Uchambuzi: Huyu Amaleki anayezungumziwa na Askofu Gwajima ni nani?

Uchambuzi: Huyu Amaleki anayezungumziwa na Askofu Gwajima ni nani?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UCHAMBUZI; HUYU AMALEK ANAYEZUNGUMZIWA NA GWAJIMA NI NANI HASA?

Anaandika, Robert Heriel.

Leo ni Sabato, nitazungumza Kwa uchache Sana nisichoshe watu. Ingawaje napendelea maandiko marefu mno.

Tumesikia kuna Mfungo wa Masaa 72 yakumtoa Amalek katika Nchi, mfungo huo umehusishwa na Gwajima, yaweza kuwa kweli au Laa! Sipo hapa kuelezea ukweli au uongo wa Jambo hili bali nipo hapa kumuelezea AMALEK Kwa wale wasiomfahamu.
Nitaelezea Kwa ufupi na Kama kuna sehemu muhimu nitakuwa nimeiacha basi wengine wataongezea. Na Kama utakuwa na swali basi nitakuwa hapa kujibu Kwa siku ya leo kabla jua halijachwea Magharibi.

AMALEK NI NANI?

Kihistoria hasa historia ya kiyahudi ambayo sehemu kubwa ipo kwenye Biblia imemtaja Amalek.
Amalek ni mtu lakini pia ni Kabila/taifa.
Amalek kulingana na Biblia ni mjukuu wa Esau/Edomu ambaye alizaliwa na mtoto wa Kwanza wa Esau aitwaye Elifazi.

Kwa ambao hawamjui Esau,
Huyu ni Yule Kaka yake na Yakobo/Israel waliozaliwa na Isaka mwana wa Ibrahimu.
Hivyo Isaka alizaa watoto wawili mashuhuri ingawaje wapo wengine; Yakobo ambaye ndiye Israel Baba wa taifa la Israel mpaka hivi leo, Kaka yake Esau ambaye ni Edomu Baba WA taifa la Waedomu mpaka hivi leo.
Israel maana yake ni aliyepigana na MUNGU.
Wakati Edomu maana yake ikiwa mwekundu wa ngozi kutokana na kuwa Esau alikuwa na ngozi nyekundu yenye masharavu/vinyweleo vingi.

Esau akamzaa Elifazi, kisha katika majumbe/wajukuu akazaliwa Amalek Kama mjukuu wa Esau Kwa mtoto wa Kwanza aitwaye Elifazi.

Amalek ndiye Baba wa taifa la Waamalek Kama Biblia inavyoripoti.

Mpaka hapa sijui tunaenda Sawa?

Waamalek baada ya Karne nyingi kupita waliweka makazi Yao katika nchi ya NEGEBU ambayo kwenye Ramani ya kale IPO katikati ya nchi ya Misri na Kanaani.

Hivyo Waisrael walivyokuwa wanatoka Misri Kwa Farao kuelekea Kanaani ilikuwa lazima wapite nchi ya Waamalek naam ndiyo nchi ya Negebu. Na hapo ndipo kisa cha ugomvi baina ya Israel(watoto wa yakobo) dhidi ya Waamalek(Wajukuu wa Esau) inapoonekana kujitokeza.

Yoshua alivyowatuma wapelelezi wakaipeleleze nchi ya Kanaani, wapelelezi wanatoa ripoti Yao Kwa Joshua wakimwambia mataifa yaliyokatikati mpaka kufikia Kanaani. Waamalek, wahiti, waperezi na wengine wanatajwa katika ripoti hiyo.

Msafara wa Israel ulishambuliwa Kwa nyuma na Waamalek wakiwa wanaikaribia Kanaani kuukabili mto Yordan.

Hoja za Waisrael zinadai kuwa Waamalek waliwafanyia uhuni na ubaya kwani waliwashambulia wakiwa wamechoka na kuzimia, tena walishambulia msafara Kwa nyuma Kule walipo watu dhaifu pasipokuwa na Jeshi Imara.
Israel Kama kawaida Yao wakaliweka taifa la Amalek Kama sehemu ya mataifa adui ambayo yanapaswa yalipizwe kisasi.
Na kisasi hiki kitafanyika mara baada ya waisrael kuitawala nchi ya Kanaani na wakishapumzika vya kutosha.

Hoja ya Pili ya waisrael Kwa Waamalek ilikuwa ni kuwaona Waamalek Kama vizuizi vya kuzuia wao wasifike nchi ya Ahadi. Kumbuka Amalek IPO katikati ya Misri na Kanaani hivyo kitendo cha taifa la Amalek kupigana na Waisrael kilimaanisha hawataki watumie nchi Yao Kama njia ya kufikia Kanaani.

Kisiasa huenda Amalek walikuwa na hoja kuwa hawataki kuvunja uhusiano na taifa la Kanaani Kwa kuwaruhusu Waisrael wapite kwenye nchi Yao kwenda kuvamia taifa la Kanaani Jambo ambalo kimsingi walikuwa sahihi.

Joshua Wakristo humuona Nabii lakini kimsingi ukiangalia alibeba dhima ya kisiasa yaani Mtawala Kama alivyo Musa, na kina Daudi.
Hivyo sababu nyingi za watawala hukaa Kisiasa kuliko kiimani.

Viongozi wengi WA kiyahudi wa wakati huo walitumia zaidi propaganda hasa za kiiamani wakiziunganisha kwenye Siasa ili kuteka nyoyo za wananchi wa Israel.

Siajabu Joshua alivyotangaza kuhusu kisasi kinachotakiwa kulipwa Kwa Amalek na kum-term Amalek Kama Shetani na mtu mwenye roho ya Shetani ambaye Hana ni njema na taifa Lao ambalo wao Kwa dini zao waliliona taifa Lao Kama taifa la Mungu.
Kumbuka hata hao waamalek nao wanadini zao na Mungu wao hivyo nao walikuwa wanawa-term waisrael vivyo hivyo.

Ni kawaida kwenye Siasa kuwapa majina mabaya Wale waliokinyume na serikali iliyopo.
Majina Kama wahaini, waasi, magaidi, mashetani, makafiri na majina mengine ni kawaida sana kwenye Siasa.

Vivyo hivyo hata Waisrael katika dhima za Kisiasa waliwapa maadui zao majina hayo hayo mabaya Wale wote walioenda kinyume na taifa Lao.
Hata huyo Amalek ya taifa la Amalek ambalo Wayahudi wanamchukulia Kama Shetani na taifa Baya waliliita hivyo kutokana na tofauti zao za kimaslahi ya kisiasa.

Watu wengine walioenda kinyume na taifa la Israel ni pamoja na kina Goliath na taifa lake la Wafilisti. Huwezi muona Goliathi mbaya wakati alikuwa akilipigania taifa lake.
Goliath Kwangu au Kwa watu Kama Taikon ninamchukulia Kama mzalendo Kwa taifa lake. Hii pia niliwahi Kueleza Kwa Delilah ambaye ni shujaa Kwa taifa la Wafilisti baada ya kumshinda shujaa wa kiisrael aitwaye Samson.

Nikirejea kwenye Mada yetu!

Gwajima anataka kufunga Kwa ajili ya Amalek.
Na hapa Amalek anaweza kuwa mtu mmoja au kundi la watu kama nilivyoeleza hapo juu.

Kisa cha Israel Vs Amalek kipo Kisiasa, hakipo kiimani. Ni Ishu ya maslahi ya kisiasa.

Je Gwajima anajaribu Kueleza kuwa nchi yetu ilikuwa inaenda nchi ya ahadi ya maziwa na Asali, nchi ya Flyover, nchi ya SGR, nchi ya Mradi wa rufiji na umeme, nchi ya umeme kutokukatika, nchi ya vitu kutopanda bei, na mambo mengine mazuri na sasa yupo Amalek au waamalek wanaozuia taifa hili lisifike huko?

Je huyo ndiye amalek anayefungiwa masaa 72 ili aondolewe na kuangamizwa na Mungu?

Je Gwajima anajaribu Kueleza kuwa nchi yetu wapo watu wanaoitakia mabaya Kama vile waamalek walivyokuwa wanaitakia mabaya Waisrael?

Je Amalek au waamalek wanaozungumziwa na Gwajima ni kina Nani hasa katika nch yetu wanaopaswa kuondolewa?

Zingatia Gwajima Mimi namchukulia Kama watu wengine, sijampa nafasi ya unabii au mtume au Kuhani isipokuwa nafasi ya Ualimu tuu. Hivyo yeye Kama mwalimu Kama ninavyomchukulia anaweza akawa anahoja muhimu mbali na madhaifu yake mengine.

Ifahamike kuwa hakuna uwezekano wa kukaa majadiliano baina ya waamalek na waisrael hivyo Kwa vyovyote lazima mpambano upigwe.


Kufikia hapa sina la ziada. Kama kuna mwenye swali anaweza kuuliza. Kwa wale wajuvi zaidi wataeleza nilipoacha ikiwa kuna haja ya nyongeza.

Ni Yule Mtibeli kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo huku na Huku.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Goba, DAR ES SALAAM
 
Jibu ni kupunguza ukali wa ugonjwa unapokushambulia.

Swali lako linafanana; Kwa nini mtu avae Bulletproof wakati Kama atashambuliwa vyema pia anaweza kufa?
Jibu ni Kupunguza hatari ya kufa kirahisi.

Hiyo ndio hoja ya Madaktari.

Sasa Kama hujaelewa sio jukumu langu tena kukuelewesha wewe au watu wa jamii ya Gwajima katika hili

Jamaa Ni mwelewa Ila unamlazimisha kuelewa maelezo ya Kijinga
 
Asante kwa historia nzuri ya hao jamaa kibiblia. Nakupongeza pia kusema wewe wamchukukia Gwajima kama Mwalimu tu, huenda upo sahihi nami naamini hivyo lkn pia ni kiongozi mwenye watu.

Akisema wote humwamini 100% tofauti nawe nami pia. Hivyo nafikiri ameruhusiwa kufunga hadi sasa kwa kuwa sijasikia katazo lolote la mamlaka kumzuia asifunge.

Binafsi napata nashindwa pata tafsiri nzuri, japo nahisi habari za kuhojiwa yeye na wenzake sijui ni jana au Leo imepekea yeye kufunga ili awe kidedea.

Naamini kesho atasema matokeo ya mfungo wake pale kanisani kwake.
 
Asante kwa historia nzuri ya hao jamaa kibiblia. Nakupongeza pia kusema wewe wamchukukia Gwajima kama Mwalimu tu, huenda upo sahihi nami naamini hivyo lkn pia ni kiongozi mwenye watu. Akisema wote humwamini 100% tofauti nawe nami pia. Hivyo nafikiri ameruhusiwa kufunga hadi sasa kwa kuwa sijasikia katazo lolote la mamlaka kumzuia asifunge.
Binafsi napata nashindwa pata tafsiri nzuri, japo nahisi habari za kuhojiwa yeye na wenzake sijui ni jana au Leo imepekea yeye kufunga ili awe kidedea. Naamini kesho atasema matokeo ya mfungo wake pale kanisani kwake.


Amalek unamjua ni Nani Boss?
 
Kiufupi hawa chawa wa Magufuli wote awatorudi majimboni tena,chama kimerudi kwa wenyewe so ni lzm wabweke,hata mbwa akikaribia kufa ni lzm abweke.
Wanajua hawana chao tena 2025 watafutika kabisa, tutakuwa na sura mpya tena vijana.
Hakuna cha covid 19,waunga juhudi,sukuma gang wote wanamalizia kulamba sahani mwisho mwisho.
 
Kiufupi hawa chawa wa Magufuli wote awatorudi majimboni tena,chama kimerudi kwa wenyewe so ni lzm wabweke,hata mbwa akikaribia kufa ni lzm abweke.
Wanajua hawana chao tena 2025 watafutika kabisa, tutakuwa na sura mpya tena vijana.
Hakuna cha covid 19,waunga juhudi,sukuma gang wote wanamalizia kulamba sahani mwisho mwisho.


😀😀😀😀
 
Gwajima ni.zaid ya mwl bro. Kuhusu maombi ni jina tu ndilo.linaloleta mjadala lkn Gwaj amekuwa mstar wa mbele kwa taifa kunapokuwa na shida, shida hizo ni km vile mfumumuko wa bei, petrol kila mwez inapanda,vifaa vya ujenz, vyakula n.k
So gwaj yupo correct

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa historia nzuri ya hao jamaa kibiblia. Nakupongeza pia kusema wewe wamchukukia Gwajima kama Mwalimu tu, huenda upo sahihi nami naamini hivyo lkn pia ni kiongozi mwenye watu. Akisema wote humwamini 100% tofauti nawe nami pia. Hivyo nafikiri ameruhusiwa kufunga hadi sasa kwa kuwa sijasikia katazo lolote la mamlaka kumzuia asifunge.
Binafsi napata nashindwa pata tafsiri nzuri, japo nahisi habari za kuhojiwa yeye na wenzake sijui ni jana au Leo imepekea yeye kufunga ili awe kidedea. Naamini kesho atasema matokeo ya mfungo wake pale kanisani kwake.
Kwani kufunga nako kunahitaji ruhusa?
 
Back
Top Bottom