Uchambuzi kuhusu athari za vita inayoendelea baina ya Marekani, Israel dhidi ya Iran na hali ya mafuta nchini

Uchambuzi kuhusu athari za vita inayoendelea baina ya Marekani, Israel dhidi ya Iran na hali ya mafuta nchini

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
160
Reaction score
172
Vita baina ya Marekani, Israel dhidi ya Irani ilianza tarehe 28 Februari, 2026. Vita hiyo imeongezeka wigo kutokana na mashambulizi ya Irani kwa nchi za Saudi Arabia, Bahrain na Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) ambazo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani.

UTARATIBU WA UAGIZAJI WA MAFUTA TANZANIA
Mafuta yanayotumika nchini huagizwa kupitia Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Bulk Petroleum System – BPS) ambapo Kampuni za Mafuta nchini (Oil Marketing Companies - OMCs) huwasilisha kwa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pampja - PBPA mahitaji ya mafuta kila mwezi. Mahitaji hayo hugawanya katika zabuni ambapo kila zabuni ni meli moja na kisha hushindanisha kwa waleta mafuta ambayo walishafanyiwa tathmini na kuwa vigezo vya kuleta mafuta nchini (suppliers).

Waleta mafuta hushindania premiums (gharama za uletaji wa mafuta) ambazo zinajumuisha gharama za meli, bima na faida kwa bei za mafuta zinakuwa zinajulikana katika soko la dunia. Supplier mwenye premium ndogo zaidi hushinda zabuni husika. Kwa wastani kila mwezi kuna jumla ya zabuni 4 za mafuta ya dizeli, 4 za petroli na 1 ya mafuta ya ndege zenye jumla ya tani laki 6. Mafuta haya pia yanajumuisha mahitaji ya nchi jirani ambazo hazina bandari na zinapenda kupitishia mafuta yao katika bandari za Tanzania. Mafuta yanayotumika katika soko la ndani ni asilimia 60 ya mafuta yote yanayoingia nchini kupitia mfumo wa BPS.

Utaratibu wa uagizaji wa mafuta nchini ni wa mfumo wa M+2 mafuta yanayoagizwa mwezi huu hutumika miezi miwili baadaye. Utaratibu huu unawezesha Tanzania kuwa na usalama wa mafuta kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu ijayo kutokana na akiba iliyopo nchini na meli zinazoleta mafuta. Katika zabuni zilizofanyika mwishoni mwa mwezi Februari 2026 ambapo mgogoro wa Mashariki ya Kati ulianza zimeihakikishia Tanzania kuendelea kuwa na usalama wa mafuta kwa bei himilivu hadi kufikia mwezi Mei 2026.

Takwimu zinaonesha kuwa kiasi cha asilimia 60 ya yanayoagizwa kuja Tanzania yanatoka katika nchi za Mashariki ya Kati. Kwa kipindi cha miezi sita iliyopita Tanzania imeagiza mafuta yake kutoka Nchi za Falme za Kiarabu (37%), India (40%), Saudi Arabia (8%), Oman (8%), Kuwait (4%) na Bahrain (2%).

Kwa wastani, Tanzania hutumia takribani lita milioni 6 za petroli, milioni 8 za dizeli na laki 6 za mafuta ya ndege kwa siku.

MADHARA YA MGOGORO WA MASHARIKI YA KATI KATIKA UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI
Mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa mlango wa Hormuz (strait of hormuz) unaotumika kusafirisha takribani asilimia 20 ya mafuta ghafi duniani, unatarajiwa kuathiri uwezo wa nchi hizo kusafirisha mafuta kutokana na tahadhari ya vita, kushambuliwa kwa miundombinu, na changamoto za usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka maeneo ya uzalishaji hadi kwenye viwanda vya kusafisha (refinery). Kama vita hivyo vitaendelea kwa muda mrefu, kupungua kwa uzalishaji wa mafuta kutoka katika nchi hizo kunaweza kuleta madhara duniani kote ikiwemo Tanzania kutokana mahitaji kuwa makubwa ikilinganishwa na uwezo wa uzalishaji na hivyo bei za mafuta kupanda.

Hadi sasa nchi mbalimbali duniani zikiwemo Bangladesh, Pakistan, Korea ya Kusini zimeanza kukumbana na changamoto za upatikanaji wa mafuta. Baadhi ya nchi hizo zimejiwekea mikakati ya kupunguza matumizi ya mafuta ikiwemo kufunga shule, kufanya kazi kwa kutumia mtandao na kupunguza siku za kwenda maofisini.

Zaidi ya uwezekano wa kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta, vita inayoendelea inatarajiwa kuongeza bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta. Taarifa zinaonesha kuwa, kuanzia tarehe 28 Februari 2026, bei ya mafuta ghafi imeongezeka kwa takribani asilimia 9 ikilinganishwa na bei ya soko iliyofungwa tarehe 27 Februari 2026. Changamoto kama hii ilitokea mwaka 2022 wakati wa vita baina ya Urusi na Ukrain, japo vita hiyo haikusababisha athari sana katika bei na upatikanaji wa mafuta kama ilivyo sasa.

MIKAKATI ILIYOWEKWA KUHAKIKISHA USALAMA WA UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA MAFUTA NCHINI
Kama ilivyo nchi nyingine, Tanzania inaendelea kujiwekea mikakati kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha wakati wote. Mojawapo ya mikakati hiyo ni PBPA na TPDC na Kamati za Ulinzi kuhakikisha mafuta yote yaliyoagizwa kwa mikataba (shipping and supply contract) yanafika Tanzania kwa wakati na EWURA kuhakikisha OMCs wanauza mafuta yaliyopo pasipo kuyaficha kwa kusubiri bei ya mafuta kupanda.

MFUMO WA UNUNUZI WA MAFUTA
Kwa upande wa ununuzi, mfumo wa PBPA unafanya kazi kwa mtazamo wa mbele (M+2), ambapo zabuni hutangazwa kwa ajili ya shehena zitakazowasili takribani miezi miwili ijayo. Hii ina maana kuwa maamuzi ya ununuzi hufanywa kabla ya kujua kwa uhakika mwelekeo wa bei za soko (tunajua premiums, hatujui FOB Prices za product).

Tofauti kuu kati ya mifumo hii miwili ni kwamba M-1 ni inategemea gharama halisi ya meli zilizo fika na zitakazo uzwa mwezi husika, wakati BPS/M-2 ni ya procurement ya suppliers 2 months in advance kwa mafuta yatakayo letwa at least a month in advance ambapo EWURA ndio huchukua bei hizo za mwezi mmoja kabla kwa ajili ya kupanga bei.

Hivyo mafuta yatakayoauzwa nchini mwezi Aprili ni yale ambayo mzabuni alipatikana february, bei ya mafuta inakokotolewa kwa zingatia mwezi ambao mafuta hayo yamewasili nchini ambapo kwa mwezi wa nne kuna meli zilikuwa zina FOB ya february na nyingine zina FOB ya march. So bei ya mwezi huu april itapanda kwa kias fulan lakin zina balanciana, (march ndio vita zilipo anza) ndio maana bei imepanda.

MFUMO WA BEI
Mfumo wa bei za mafuta nchini unafuata utaratibu wa M-1 (Mwezi wa kutangaza bei), ambapo bei za mwezi husika hupangwa kwa kuzingatia gharama halisi za mafuta yaliyoagizwa mwezi uliotangulia. Hapa EWURA hukusanya na kuchambua vipengele vyote vya gharama ikiwemo bei za soko la dunia, premium, gharama za usafirishaji na thamani ya fedha za kigeni, kisha kutangaza bei za ndani kwa mwezi unaofuata. Mfumo huu una faida ya kuleta uwazi na kuakisi gharama halisi (cost-reflective pricing).

Hivyo bei za mwezi Aprli zitapangwa kwa kutegemea bei ya mafuta katika soko la Dunia kwa kipindi cha mwezi machi 2026 & Aprili,2026.

NB: Tender zetu ni cargo by cargo (ship by ship) so kwa mpangilio wa meli kuna meli zina pricing ya february (zina nafuu) na pricing ya march muda wa vita ni expensive.

7. HALI YA MAFUTA NCHINI

Taarifa ya Serikali iliyotolewa tarehe 27 Machi,2026 na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. James Mataragio ni kuwa:

MAFUTA YA PETROLI
  • Mafuta yaliyopo nchini kwenye matenki, Petrol tuna lita 95,256,342;
Mafuta ya petrol yaliyowasili nchini ni lita 146,683,337
Mafuta yaliyopo njiani kwenye meli ni lita 138,737,332.
Jumla ya mafuta ya Petrol yatakayokuwepo ni lita 380,677,011 na yanatosha kwa matumizi ya siku 61.”

MIKATABA
Mikataba ya mafuta iliyoingiwa na mzabuni ni jumla ya lita 183,500,450 ambayo yatafika nchini mwezi wa nne, hivyo jumla ya mafuta ya Petrol yaliyopo kwenye matenki, yatakayowasili nchini kwa meli pamoja na yaliyopo kwenye mikataba ni lita 563,682,461 kiasi ambacho kinatosheleza kwa siku 91.

MAFUTA YA DISELI
  • Mafuta ya Diseli yaliyopo kwenye matenki ni lita 55,744,397;
Yaliyowasili nchini ni lita 122,893,285;

Yaliyopo njiani kwenye meli ni lita 184,662,480.

Hivyo, jumla ya mafuta ya Diesel ni lita 362,433,845, yanayotosha kwa matumizi ya siku 44.

MIKATABA
Mafuta ya Diesel yaliyopo kwenye mikataba na wazabuni ni lita 167,321,343

Kwa ujumla, mafuta yaliyopo nchini yanayokuja kwa meli na yaliyopo kwenye mikataba ni lita 530,621,505, kiasi kitakachotosheleza kwa siku 64.

MAFUTA YA NDEGE
Kwa upande wa mafuta ya ndege yaliyopo kwenye matenki ni lita 35,241,028 Mafuta ya Ndege yaliyopo kwenye mikataba ni lita 23,779,725.

Jumla yake ni lita 59,020,753, zitakazotosheleza kwa siku 97.

TPDC YASIMAMIA UAGIZAJI WA MAFUTA, SERIKALI YALENGA BEI TULIVU SOKONI
Serikali imechukua hatua za dharura kwa kulielekeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuagiza mafuta mengi kwa pamoja, ili kuhakikisha usalama na upatikanaji wa mafuta ya kutosha nchini kwa bei himilivu kuanzia mwezi Mei hadi Julai 2026.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mafuta katika soko la kimataifa, zilizochangiwa na vita vinavyoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Imebainika kuwa TPDC ikinunua mafuta kwa pamoja, hatua hiyo itakayosaidia kupata bei nafuu zaidi ikilinganishwa na utaratibu wa awali uliokuwa ukitumika kupitia Wakala wa Ununuzi wa Pamoja wa Mafuta (PBPA), ambapo waagizaji wanakuwa wengi na wanaagiza kwa kiwango kidogo kidogo (Cargo by Cargo).

Uamuzi huo umekuja wakati bei za mafuta duniani zikiongezeka kwa kasi zaidi ya mara mbili katika miezi ya hivi karibuni kutoka kati ya dola 50 hadi 60 kwa pipa mwezi Februari hadi takribani dola 114 kwa hivi sasa hali inayoongeza wasiwasi wa kupanda kwa bei ndani ya nchi.

Waziri mwenye dhamana ana Mamlaka ya kutumia Sheria ya Mafuta kuweka utaratibu maalum wa upatikanaji wa mafuta nchini, ili kuhakikisha uwepo wa mafuta ya kutosha na kwa bei nafuu. Kutokana na hali ya sasa, TPDC imeelekezwa kuagiza mafuta yatakayokidhi mahitaji ya kipindi hiki cha changamoto.
 
Back
Top Bottom