Uchambuzi: Mambo ya msingi kabisa ya kuyatambua kuhusu mgogoro wa wapiganaji wa M23 na Congo DRC na mapendekezo ya nini kifanyike

Sio kweli ndugu yangu hakukuwa na makubaliano kama hayo hiyo ni myth(maneno yakutunga) ambayo yamekuzwa na mitandao yakijamii.
Hima Empire pia ni myth nikitu hakiwezekani kwenye dunia ya sasa.
 
Sio kweli ndugu yangu hakukuwa na makubaliano kama hayo hiyo ni myth(maneno yakutunga) ambayo yamekuzwa na mitandao yakijamii.
Hima Empire pia ni myth nikitu hakiwezekani kwenye dunia ya sasa.
Hujui chochote wewe kwahiyo kabarebe alikuwa kiongoz wa jeshi nchini Congo kama nani. We kama hujui kitu kaa kimya.
 
Ila Bw. Richard
Ijapokuwa unasema wewe ni mchambuzi huru ila uchambuzi wako umeegemea upande mmoja.
Yan huyu jamaa ametumia nguvu kubwa sana kuepuka kila mahala ambapo ulitakiwa itajwe TPDF ame mute. Yan nimesoma hii habar yake nimechekaa..Na kwa wasiojua hiz mambo labda ndio wataona kimeandikwa kitu interesting ila kwa tunaojua jua kidogo , hakuna news hapa. Ni ujinga tu
 
Asante kiongozi.
 
Sawa, lkn congo isigawanywe, period
 
Ngara na kagera. Ngara ni sub set ya kagera...
 
Hujui chochote wewe kwahiyo kabarebe alikuwa kiongoz wa jeshi nchini Congo kama nani. We kama hujui kitu kaa kimya.
Ebu nipee source ya habari yako kuhusu Hima Empire, leta hayo makubaliano ya limera..Hakuna kitu kama hicho huwezi kupata source ya kuaminika. Baada ya serikali ya Rwanda kupinduliwa 1994 majeshi ya serikali yalikimbilia DRC wakati huo ikiitwa Zaire, kumbuka Mobutu alikuwa rafii mkubwa wa aliyekuwa raisi wa Rwanda Habyarimana. Majehi ya serikali iliyopinduliwa yalijikusanya nakujitayarisha kuingia Rwanda tena ili kurudisha serikali madarakani.
Rwanda chini ya Kagame akiwa waziri wa ulinzi kiindi hicho iliamua uingia Zaire kuwafuatilia maadui zake kabla hawajaanzisha vita ya kurudi Rwanda. Kabarebe ndiye aliye ongoza kikosi kilicho ingia Zaire.
Kwa kuogopa pressure ya jumuia ya kimataifa waliamua kumtumia raia wa Congo kama kiongozi wa vita, alitafutwa Desire Kabila.
Baada ya Mobutu kutolewa Kabarebe alifanywa waziri wa Ulinzi, Kabila akawa raisi. Vita ilianzishwa na Rwanda kabla hata Kabila hajajulishwa. So kabarebe aliongoza majeshi yaliyo ipinduwa serikali na sikwasababu ya makubaliano yoyote yale, kwani wangekubaliana nanani, kabila wakati waou ndio walimuweka?
Point nyingine sio watusi waliopigwa, waliopigwa ni wahutu ndio waliingia Congo.
 
Sasa

Baada ya kujua malengo ya watusi kuunda nchi mpya sasa tumejua na malengo ya wahutu, kifupi ugomvi wa wahutu na watusi hautaisha kizazi hiki labda vizazi vitano mbele
hv unajuw kuwa hata ww ni mhutu ?
 
U know nothing bro. Hujui chochote kaa kimya. Nakuuliza imekuwaje kabarebe awe mkuu wa jeshi nchi ya Congo. Na kwanini Rwanda inaongoza kwa kuuza madini ambayo hawana. Na kwanini hao viongoz wa m23 kila wakizidiwa wanakimbilia Kigali. Akina Laurent nkunda.
 
Tuache kutafuna maneno, kiini cha mgogoro wa DRC ni tamaa ya Rwanda chini ya mwamvuli wa uingereza. Kuumaliza huu mgogoro, hatua tatu zifanyike:
1. Kundi la M23 lifutwe kabisa ndani ya DRC na karibu na mipaka yake kwa mtutu wa bunduki. (Jeshi la TZ na South Afrika yanaweza kuikamilisha hii kazi kwa miezi sita tu)

2. Rwanda iwekewe vikwazo vya kiuchumi na kisiasa (inyimwe misaada, itengwe na jumuiya za kimataifa ikiwemo kutengwa na jumuiya ya Afrika mashariki, SADC)

3. Uingereza inyoshewe kidole, ishinikizwe, alaumiwe na kukosolewe (kwa aibu itabidi ijitenge na Rwanda)
 
Sio mimi, ni wao M23 wataka wasikilizwe madai yao ya msingi ambayo nimeyaeleza kwenye uchambuzi.
HUWEZ kuwasikiliza wahuni!

Kila kundi katika nchi likitaka kufanikishiwa mahitaji yake nchi haiwezi kwenda!

Congo waimalishe jeshi lao!


Hata hapa Tanzania tuliingia vita na Uganda kwasababu ya mkoa wa kagera tu.


Ukraine ameingia vita na Russia kwasababu ya Crimea.

Hao m23 sio wa kuacha ni kwenda nao kiulalo ulalo.
 
Hujayumbisha maneno
 
Basi bwana, naona hatutafikia muafaka ila tu sikila kilichopo kwenye mtandao nikweli, inahitaji credible sources, nasisitiza hakukuwa namukubaliano kama hayo nakama yalikuwepo basi yaweke hapa na source yako yakuaminika, ukifuatilia source ndio utajua kuwa nihabari za mitandaoni tu,,unajua uongo ukiongewa sana mwishowe unakuwa kama ndio ukweli i challenge you au mtu yoyote anayejua lolote kuhus hayo maelewano na Hima empire, mwenye vielelezo vya kuaminika avilete hapa. Nimeelezea jinsi gani Kabarebe aliteuliwa kuwa mkuu wajeshi la Congo, kumbuka Congo haikuwa na jeshi ni jeshi la Rwanda na Uganda vilikuwa Congo.
Laurent Nkunda hakukimbia alikamatwa mpaka sasa amefungiwa Rwanda, ndio maana humusikii kwa sasa.
Issue ya madini nadhani iko nje kidogo ya maada, hata kenya inaongoza kuuza tanzanite wakati inapatikana Tanzania tu.
I appreciate your debating maturity though.
 
Hujayumbisha maneno
Mleta mada amezunguka mnoo na blah blah nyingi kuhusu M23 wakati sote tunajua kiini ni Rwanda. Pale hakuna muasi bali kuna jeshi la Rwanda with full scale military invasion.

Hakuna mkongomani halisi anaweza kuungana na M23, lakini kila mnyarwanda amesimama na M23.

Narudia tena kusema M23=Rwanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…