SHANTI
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 296
- 365
Wasalaam wanabodi,
Kampeni za uchaguzi mkuu zinaelekea ukingoni siku mbili zijazo nchi nzima. Tumeona Kila mgombea akijinadi kwa style yake na upekee kulingana na malengo na mikakati thabiti waliyojiwekea.
Chama tawala CCM walianza kwa kishindo kikubwa pale dodoma na kuonesha ukubwa wa idadi ya wafuasi wake walijipanga kutetea kiti Chao. Kadiri siku zilivyozidi kwenda utamu wa kampeni za chama tawala ulinoga kupita zilizotangulia.
Msingi wao mkubwa ulikuwa nyomi la watu na uwezo wa kufika vijijini zaidi. Tofauti na miaka yote mgombea wao amefika MAENEO mengi ya mijini zaidi kuliko vijijini ukilinganisha na 2015. Ukifanya SWOT Analysis utayaona haya:
Strength:
CCM huwezi kuitenganisha na Sola na pia huwezi kuitenganisha na serikali , na hapo ndipo utagundua kwa Nini NEC Ni watiifu Sana kwa CCM.
WEAKNESS
Kundi kubwa Lina wageni ambao sio wajuvi wa siasa za majukwaa na uwezo wa kubashiri yajayo kwa uyakinifu. Hii imewagharimu Sana kiasi hawajui kuwa mbaya wao Ni Seif sharrif Hamad au Tundu Lissu au ubovu wa kumsimamisha Mwinyi.
Si hivyo tu pia kushindwa kujua kuwa Kuivuruga CUF, CHADEMA na kununua wabunge wa upinzani ingelikuwa njia nyepesu ya wao kushinda Bila kupingwa au kushinda kwa kishindo kikubwa. Mpaka Sasa timu ya kampeni ya CCM imeshinda kuondoa udhaifu huu na unawagharimu kwenye field sababu kubwa walisahau kuwa upinzani Ni mioyo na hisia za watu na sio vyama. Hivyo mziki wa upinzani bado unagonga spika zao kwa Kasi Sana.
NGUVU YA UMMA
Inaonekana wazi LISSU na SEIF hawatanii hata kidogo jinsi walivyojipanga kutumia nguvu ya Umma. Kwa mwenye macho mapana .Umma haujawahi kushinda DHIDI ya watawala na Kama kweli basi hiki kitisho kikubwa Sana kwa CCM.
OPPORTUNITY
Fursa kubwa na ya pekee Ni kutumia Dola .
Pili mtaji wa fedha na rasilimali watu
TECHNICALLY
Hapa namaanisha MBINU za kiufundi za kushinda uchaguzi siku ya uchaguzi. MBINU ya kwanza NEC,hii imewapa wabunge zaidi ya 20
NEC na CCM ni watu wamoja wanaongea lugha Moja pia wanaweza kwa hiyari tu Kuivuruga ngome ya wapinzani na matokeo Yao kwa sababu hawana pa kushtakiwa popote kwa kuwa wao wanatoa tamko la mwisho.(namaanisha wakurugenzi) na dalili zishaonekana tayari.
CHADEMA NA ACT
Wote kwa pamoja na wajadili Bila kuwatenganisha ili nihitimishe vizuri. Ni ukweli usiopingika kuwa Zambarau wameiteka Zanzibar na CDM wameiteka Tanganyika.
Ubora wa viongozi wao wakuu wawili MBOWE & SEIF SHARRIF HAMAD umejidhihirisha wazi kwenye uchaguzi huu kwa kuruka mamii ya vihunzi na kuilaghai serikali mchana kweupeeee.
Hebu nikurudishe nyuma kidogo, siku Maalim Seif alipokwenda ikulu kumsalimia Rais huku MBOWE akipambana kesi ya Akwilina. Kila mtu alijua Maalim ameunga juhudi mkono na shughuli anayo mwamba. Sasa ndio nang'amua kwamba kumbe Ile Ni MBINU ya kimedani ya kuwalaghai watawala waamini upo pamoja nao. Ile ndio siku ya USHINDI wa SEIF Kama ikitokea atashinda Zanzibar kesho kutwa.
Hisia zinaniambia kwamba mwamba na mwalimu waliwaingiza Chaka CCM na Membe wao huku wakijua wamemficha mfukoni Lissu.
Tuachane na hayo hebu tuwafanyie SWOT na wao wapoje.
STRENGTH
NGUVU YA UMMA
Umma umewaelewa Sana ACT &CHADEMA na ushahidi wa Watanzania kuwachangia pesa wahalifu wasiende jela badala yake walipiwe faini na warudi uraiani Ni ishara Tosha upo tayari kufanya lolote lenye kuwalinda Chadema kwa upande wa bara. Jambo Hili liliwatia kiwewe IKULU na kesho yake Rais aliamua kumlipia msigwa kuonesha Kwamba Rais Ana huruma na wapinzani. Kama watu walichanga dusko dusko namaanisha kiasi Cha 1k -10k kinyume chake hizi buku buku Ni idadi ya wapiga kura wa upinzani. Sasa kazi yako chukua kikokotoo halafu tafuta majibu Ni watu wangapi wanasapoti Chadema. Zenji siongei Kila mtu ameona NGUVU ya Maalim kaondoka na wanachama wake kwenda ACT so like amevimbisha msuli kwa mamlaka.
UWEZO WA KUNUSA HATARI
Tukio la Membe kuachwa kwenye mataa na hajielewi linathibitisha uwezo wa wapinzani KUNUSA HATARI.
Waliujua mtego wa CCM na wao wakatega wa kwao kwenda ikulu na kuleta picha kwamba Seif Ni mshkaji na MBOWE mkorofi kumbe Ni mtego wa Kumlinda LISSU na kunifanya Membe aonekane punguani asiyejua anataka nn.
Membe Ni ujio hatarishi kwa upinzani na Lissu anatafutwa na watesi wake asirudi kwenye siasa. Inaonesha wazi Kuna makubaliano kwamba ACT na CDM wote waingize wagombea ili mmoja akikatwa aungwe mkono mwingine na ndicho kinachoendelea Sasa.
Wanachama 9M according to MBOWE
WEAKNESS
Hawana Dola Wala serikali na hawajahi kushinda uchaguzi ngazi ya Rais
NEC haipo upande wao
UWEZO mdogo wa ulinzi na USALAMA wa viongozi wake, Ni rahisi kumteka au kumkata au kuzuia mkutano wa upinzani.
Ukosefu wa rasilimali fedha
OPPORTUNITY
MPASUKO wa CCM baada ya kura za MAONI. Huu Ni mtaji mkubwa Sana wa upinzani na dalili zimeonekana wazi Kanda ya ziwa na Zanzibar. Maamuzi ya Dodoma huenda yakawafanya CCM kupoteza majimbo 35-50 ya uchaguzi wasipotumia utemi.
KULINDA KURA VITUONI
Wakiwekeza NGUVU imara ya KULINDA KURA CCM hawana Chao. Naamini Lissu anamaanisha na ujumbe umewafikia walengwa. Wameanza kujibu maneno
MAKUNDI MAALUM YALIYOUMIZWA NA SERIKALI
Hapa nawaweka wahanga wote wa utawala wa awamu ya tano. Wafanyakazi hewa,waliobomolewa,waliotoswa walimu, wafanyakazi wa serikali, waliokosa mshahara n.k
Hawa Ni game changers watatoa USHINDI 5%-7% kwa Lissu sababu Wana maumivu Yao.
TECHNICALLY
MAANDAMANO YASIYO KIKOMO
Ukifuatilia vizuri utagundua MBINU pekee ya wapinzani kuingia ikulu Ni MAANDAMANO YASIYO na KIKOMO. Hii ndio MBINU ya kiufundi yenye chanya na imewasaidi wapinzani wa nchi jirani kuingia na kushika serikali punde tu baada ya uchaguzi.
Hakuna serikali ya kiafrika imeyashinda MAANDAMANO YASIYO KIKOMO. Kiufundi wapinzani wako vyedi.
MATAMKO NA VITISHO VYA VIKWAZO
tangu wiki iliyopita mataifa makubwa yamekuwa na spidi ya MATAMKO na baru ya into kwa serikali ya Tanzania Ni wazi wapinzani kwenye MBINU hii wako mbali Sana. Yakitokea tusiyoyaomba wanatusua mapema.
Baaada ya mtazamo huo Sasa najikita kueleza kwa Nini Lissu 49% na Magufuli 47%.
Sympathy
Umaarufu wa Magufuli umeporomoka Sana baada ya kura za MAONI. Wakati huohuo umaarufu wa Chadema umekuwa mkubwa kupindukia sababu watu waliaminishwa kuwa upinzani umekufa na kinyume chake umekuwa zaidi kwa sababu ya huruma kuwa wanaonewa.
Kifungo Cha viongozi wa Chadema mwezi Machi kiliibua hisia za huruma kwa wananchi na kuamsha Ari ya huruma kwa wapinzani. Ujio wa Lissu umeikuza sympathy ya Chadema na ACT kwa pamoja na hivi tunavyoongea waliopewa kazi kushughulika na wapinzani wanalala na viatu.Hii itawapa kura sawa na 21%
Waislamu
Hapa Sina lengo la udini Ila hakuna asiyejua michango ya waislamu hapa bongo. Ujio wa sheikh Ponda Ni pigo kwa CCM na faida upinzani.
Sheikh ponda kashawagawa na Hili litawapa wapinzi USHINDI Zanzibar na pwani na mikoa ya kusini ambapo CCM imewakwaza kwa kiasi kikubwa kupitia korosho. Hili litapunguza 45% kwenye kura za waislam zilizotakiwa kwenda ccm
KOROSHO
sekeseke la korosho linaonekana Ni shida kubwa Sana kiasi Cha kuitikisa ngome ya CCM na hii ikikutana na impact ya ponda itawaumiza CCM zaidi na kuwanufaisha wapinzani.
Low turnover
Mwitiko mdogo wa wapiga kura siku ya uchaguzi, Ni pigo kingine kwa CCM na msaada kwa upinzani. Kuna uwezekano turn over ya wapiga kura ikawa watu 9M -11M
Hapa ndio kifo Cha CCM kinaanzia na hiili litawapunguzia 50% kura zote walizotarajia kupata kwenye uchaguzi huu.hii Ni faida kwa upinzani kwa sababu wao wanategemea sababu za hapo juu kupindua meza.
Common interest za Wazanzibar
Ikumbukwe watu wa visiwani wakitaka Lao hawashindwi licha ya utofauti wa vyama. Ni wazi CCM na ACT wote Lao Ni Moja ingawaje kwa nje wanashambuliana Jana kwamba wanapigana Vita ya 3 ya dunia. Seif anakwenda kushinda uchaguzi kwa sababu wazenji wote Wana ongozwa na common interest kuiona CCM Ni kikwazo kwao so best way Ni kumpa seif na sio Mwinyi.
Tutarajie mchuano mkali.
Karibuni kwa mjadalaa