Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Tundu Lissu anaweza kumshinda Dkt. Magufuli na Maalim Seif anaweza kuibuka kidedea Zanzibar

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Tundu Lissu anaweza kumshinda Dkt. Magufuli na Maalim Seif anaweza kuibuka kidedea Zanzibar

Ninm ngumu wewe huoni hata kampeni tumepigwa mabomu lakini tumewaweza?? Ni ngumu kumshinda lakini sio kuwa haiwezekani.

Tumepigwa mabomu watu wametekwa hadi kuuawa lakini bado kampeni zetu zime hit sana. Kampeni zilikuwa ngumu sana lakini tumemaliza kwa ushindi .kubwa. hiyo ndio maana ya ngumu. Ni ngumu lakini tutashinda.
Kumbe wewe ni CHADEMA? Kwa vile wewe ni CHADEMA unataka tuseme unachotaka kusikia tu ee?
 
Jikite kwenye mada based on SWOT anal
Mkuu hakuna mada hapa ya kujikita kwayo, Ulichotuletea ni hisia zako binafsi zisizo na base ya kisayansi. Nakujibu kwa utafiti wa kisayansi inayothibitisha JPM atapata ushindi wa kura 89.5% na Lissu ataambualia tu 8.2%. Tafiti ujibiwa kwa tafiti na siyo mada za hisia.
 
Mkuu si ujielekeze kwenye SWOT analysis?? Zile akili zako unazotiaminisha unazo umezikabidhi wapi Mayalla. Unanyemelea uteuzi?
Hivi Huu ujinga SWOT umekalirishwa na KAS AU?
 
Kuna mtu kanambia anauhakika Lissu atashinda nikamwambia mimi sio mwanasiasa wala mtabiri ila Magufuli atashinda.
Nikamuomba tuweke dau la milioni mojamoja ili ambae kauli yake itakua ilikua yakweli achukue milioni mbili kakataa nikajua kumbe ananiambia maneno asio na uhakika nayo kabisa na anaujua ukweli.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app

Kwa tume hii inakuwa ngumu, lakini kwa nguvu ya umma hela yako ingeenda mchana kweupe.
 
Kazi iko pale juu kwa Kaijage. Yaani nini kitamfanya Kaijage atamke Lissu badala ya Magufuli? Na likatiba letu linasema akishatangazwa ndio basi!
Kukishinda chama dola ni ngumu sana.

Kama ulifatilia kampeni za Ccm utagundua kwamba Ccm iliendesha kampeni ya kiserikali/dola na sio kampeni ya chama cha siasa.
 
Ccm ni chama cha kisasa, na itaendelea kushinda kwa haki kwa miaka miamoja ijayo
Kwaina ya Wapinzani hawa km lissu wanaotumwa na Mabeberu waje wagombee kwa maslahi ya watu wa nje mtateseka sana

Uchaguzi utakuwa huru na haki na Ccm itashinda kwa kishindo
Jiandaeni kupora kuta tu, na muombe wananchi waendelee kuwa makondoo wasilinde ushindi wao. Tumechoka kuburuzwa na chama cha zamani. Ccm sio chama cha kizazi hiki. Lazima tutapata mabadiliko tunayoyataka, hiki sio kizazi cha kumsujudia rais.
 
Democratic election is the representation of the inner human behavior.

Therefore 40% of all eligible Tanzanians gets fully participation in political campaign and out of them nearly 35% have the fully voting qualifications, others on that will not vote (because of lack of voting qualifications), they just enjoy (benefit) what is in the campaign process.

60% of the Tanzanians usually do not get involved in political campaign and they sometime never participate in any political gathering for the whole period of campaigning but 50% are determined to voting and will surely vote. In this 50% we have business people, government employees, students, and others affiliated to the current government/presidency. These are most carefully people in voting, they never want election to affect their business and employment prospects, so they will prefer to vote for the political party of which they are aware of its ruling style in favor of them.

So the Most Challenging election will in 2025 When it will be Majaliwa K. Majaliwa (CCM) vs Tundu A.Lissu (CHADEMA)
Consider 35% effect on sharing of votes among strong contestants.
Consider 50% of votes in favor of the current president.
 
CCM ni chama cha kisasa, na itaendelea kushinda kwa haki kwa miaka miamoja ijayo
Kwaina ya Wapinzani hawa km lissu wanaotumwa na Mabeberu waje wagombee kwa maslahi ya watu wa nje mtateseka sana

Uchaguzi utakuwa huru na haki na Ccm itashinda kwa kishindo

CCM sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha dola kilichovaa koti la chama cha siasa.
 
Kwa hali ya mtaani ni wazi Lissu ni Bingwa,ila trophy pekee anaitegemea ni Umma kwa maandamano yasiyokuwa na ukomo sijajua wao watakuwa wamejipangaje-maana umma huu wa Watanzania wanataka mabadiliko lakini kutoka kwenda front ni ngumu sana upinzani wakifanikiwa kwenye hili ikijumulisha na pressure ya hivi karibuni ya matamko ya USA ikulu ni yao.
 
Asante kwa uchambuzi mzuri na mahiri, hii ya Lissu atashinda, naomba usubirie tarehe 28 October, utashangaa!.
P
Atashangaa kweli. Kwa mbinu za ushindi (soma wizi wa kura uliotukuka), CCM hawana mpinzani Africa mashariki, kusini na kaskazini. They are second to none.

I am sure hata ZANU-PF huwa wanakuja kwetu kupata uzoefu
 
Unakosea aliyesaliti nchi kwenye madini ni lissu
Onyesha alisaliti vipi. Upi mkataba alo sign mheshimiwa Lissu. Ukiweza kutuelezea hilo basi nitabadili mawazo ile tarehe 28 nimuadabishe. Mnajenga madaraja haharini wakati watu vjijini hawana maji safi na salama. Shule hazina madawati, shule hazina matundu ya vyoo tena huyo mgombea wenu ndo kajenga kituo cha mwendo kasi pale jangwani kwenye mkondo wa bahari fisadi wakubwA
 
Ukweli mchungu ni kwamba uchaguzi ukiwa huru na wa haki, Magufuli hawezi kufikisha asilimia thelathini (30%) ya kura zote zitakazopigwa. Kwanza Magufuli hapendwi ila kazungukwa na genge la wanafiki na walafi ambao kwa kujua hulka yake hawathubutu kumwambia ukweli huo.

Pili ni kwamba Magufuli mwenyewe anajua wazi ukweli huo kwamba hapendwi ila anapakwa mafuta tu na watu hao na hivyo hana imani nao kabisa. Magufuli anajua wazi kuwa alibebwa tu katika uchaguzi uliopita na kama si nguvu za dola na ubabe wa CCM hangeshinda.

Magufuli ni mwoga sana ila anajitahidi kuficha hofu yake kwa mwavuli wa ubabe katika kauli na matendo lakini moyoni anaogopa hadi kivuli chake mwenyewe. Zaidi hawaamini hadi watu aliowateua yeye mwenyewe na hii imepelekea hali ya teua na tumbua kukidhi matakwa yake.

Uchaguzi wa mwaka huu ndio unammaliza kabisa Magufuli; kwa miaka mitano amejitahidi kufagia njia kwa kung'oa visiki vyote asije akajikwaa njiani akielekea Ikulu kwa mara nyingine. Kwa bahati mbaya kwa sasa amekutana na kisiki cha mpingo alichojiaminisha ameking'oa awali!

Ghafla ujasiri wote aliojijengea anauona ukitoweka na nguvu zimemwishia, kazeeka na hatamaniki tena. Je nani sasa atampa kura? Bahati nzuri kwake wapo...watu wa aina hiyo wapo na kama kenge hawatoki nduki hadi damu zimewavuja ila bahati mbaya idadi yao haifiki asilimia 30%.

Je vyombo vya dola vitatumika tena kuwanyima wananchi uhuru wao na haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka? Hilo ndilo swali!
 
Umechambua vizuri na kila mtu anayesema Y au X atashinda aje na kitu kama hiki. Nilikuwa kijijini na hakika kuna vijana na watu wamebadilika. Kuna wengine wapenzi wa kijani wameshindwa wasimame wapi na wameona wasipige kura. So anayesema vijana hawatapiga kura na ni CCM tu watapiga anajidanganya. Kwangu mimi naona bado uchaguzi ni mgumu na fitna zometawala.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom