Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Tundu Lissu anaweza kumshinda Dkt. Magufuli na Maalim Seif anaweza kuibuka kidedea Zanzibar

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Tundu Lissu anaweza kumshinda Dkt. Magufuli na Maalim Seif anaweza kuibuka kidedea Zanzibar

October 28th ni JPM TUU.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Mnafurahisha mnavyoanzisha nyuzi za kujidanganya na kuendelea kuota
 
Dah kama series hivi, kuna watu mna vipaji vyenu

kama umesema wewe mimi ni nani nipinge?
 
Hizi ni ndoto za mchana. Mmejaribu kumnadi Lissu lakini watanzania wamemkataa, hawataki wakala wa mabeberu. Watanzania wameamua kwenda na JPM kwamiaka mingine mitano. Utafiti uliofanywa kisayansi juzi na Taasisi ya IBC Research International imegundua JPM anashinda kwa 89.5 na Lissu ataambulia tu 8.2% ya kura zote. Nakuhurumieni sana wana Ufipa, pengine ndoto hizi za mchana unazokuja nazo ni sehemu yenu ya kujifariji. Kila Mahali ni kura ya ndiyo kwa JPM. Hakuna mtanzania wa kumchagua Lissu . Tunakwenda na JPM .
Achana na habari za udaku, Huo uchambuzi wa kisayansi umezingatia vigezo gani?
 
Uchambuzi mzuri Ila free and fare election lissu anashinda kwa zaida ya 60%

Yaani toka mama yangu ambaye ni kada wa jumuiya ya wazazi ccm anihakikishie kumpigia kura Tundu lissu pia akawa anasema kamati yao nzima wamesema hawana Imani na Magufuli

Jinsi alivyo mfia chama halafu anamchinja mwenyekiti wake

Ndio niliona kabisa kwamba Magufuli Hana chake mwaka huu.
Mwambie bi mkubwa aje aungane na bi mkubwa wangu, waburudike mpaka siku akimaliza kuapishwa mheshimiwa lissu, bill yao nalipa
 
Kwanza nikushukuru kwa kuileta video hii nimeitizama yote. Msingi wa Lowassa kuwa na 18% ulikuwa political personality.

Kwa kigezo Cha politics personality twaweza walifanya utafiti na wakasema John Pombe Magufuli umaarufu wake umeporomoka.

Huyo sio Mimi Ni twaweza, wakaishia kufungiwa.

Kwa kigezo hicho hicho political personality Leo hii tukimsimasha Lissu na Lowassa bado atapata hiyo 18%?

Lowassa tukimsimasha na Magufuli atapata 18%?

Jibu Ni hapana, hivyo basi hoja yako dhaifu ya kwamba Lowassa ana watu au mvuto wa kisiasa inafia hapo.Pia Lowassa hakuwa Brand pekee iliyosababisha watu kuvutiwa na kujaa kwenye mkutano. Chadema yenyewe Ni Brand imara iliyojitosheleza na ndio maana hata Lissu anapata watu kwa wingi ule ule.

Kuondoa kwa Lowassa kungekuwa na athari chanya Lissu angekuwa Kama Membe angeishia watu wachache lakini ndio kwanza Gari linawaka.

"Politics is a game of dynamics" ukiyajua haya utaacha ushabiki, kwenye siasa za 2020 hakuna mahusiano na matukio ya 2015 . Ushahidi Ni kura za MAONI ndani ya CCM walioshinda wakati ule wameangukia pia na wamekuja wapya.

Karibu Tena tuchambue siasa.

kwani wakati lowasa angombania uraisi lissu hakuwepo chadema? kuna mtu alikua anafuatilia bunge na asijui tundu lissu wa chadema?
- wacha nkuchambulie, lowasa kama lowasa ndie alieleta machafuko ccm, yeye ndo aliesababisha mpasuko, yeye ndo alienda chadema na wengine ccm wakamfuata nyuma, na yeye ndo alirudi ccm na wakina sumaye wakamfuata nyuma

- sifanyi siasa ushabiki ni mahesabu ya kawaida sana, lowasa kama lowasa kwa mtu anaefuatilia siasa anajua nguvu alionayo kwenye hizi siasa ndo maaana, lowasa ndo richmond, lowasa ndo EPA!

- basi sasa kwa mafupi nliokupa uelewe kwamba lowasa kama lowasa ana asilimia 18% ya all tanzania voters,
(na hii imefanyika research na ndo maana lisu ameipresent apo, sio maneno ya vijiwe ni watu walilipwa kufanya huu uchungizi)
na ndo maaana chadema walimpigia magoti aende chadema, (kama una mabishano bado, lissu ndo amesema mwenyewe ubishane nae sasa kama unataka maaana wao ndo walitoa ela ya uchunguzi)
: sasa basi kwa kua umeshaambiwa lowasa kama lowasa ana 18% likability yeye kama yeye(kupendwa): basi ulichoandika chote ni rubbish
hapo tumamaliza

2) 2015 kura hazikua za chadema peke yake, kura zilikua za UKAWA! wacha kujiongeza sana una hali mbaya
3) chadema ina nguvu sana mikoa ya kaskazini, 2015 chadema ilibebwa sana na mikoa ya kaskazini, leo hii ukiongelea mikoa ya kaskazini unaongelea ngome kurudi ccm

kwa hayo mafupi nakusogezea kipaza sauti
 
Maneno ya watu walioshindwa haya
Kama hawa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
20201024_143655.jpg
 
Kuna mtu kanambia anauhakika Lissu atashinda nikamwambia mimi sio mwanasiasa wala mtabiri ila Magufuli atashinda.
Nikamuomba tuweke dau la milioni mojamoja ili ambae kauli yake itakua ilikua yakweli achukue milioni mbili kakataa nikajua kumbe ananiambia maneno asio na uhakika nayo kabisa na anaujua ukweli.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Weka video clip tukuamini
 
Hakuna wa kumpigia kura msaliti wa Nchi Lissu

Ila ndio mbembwe za Uchaguzi, mnaruhusiwa kuongea kila lugha

October 29 baada ya kuragazwa na lissu kurudi ubeligiji
mrudi shamba msimu wa mvua umeanza
Kibaraka wa Ninyiem
 
Wasalaaam wanabodi,

Kampeni za uchaguzi mkuu zinaelekea ukingoni siku mbili zijazo nchi nzima. Tumeona Kila mgombea akijinadi kwa style yake na upekee kulingana na malengo na mikakati thabiti waliyojiwekea...
Uchambuzi wako unaakisi kiwango cha akili na weledi ulionao bahati mbaya kwa makusudi kabisa umeamua kuvitumia vibaya, kwa sababu kwa kukusudia, umeacha mambo ya msingi kabisa

IDADI YA WANACHAMA
Hawa ni ndio nguzo ya kwanza muhimu ktk kusaka kura WANACHAMA loyal and committed hawayumbishwi hata hoja iwe kali kiasi gani. Hawa sio UNDECIDED VOTERS bali ni kinyume chake hawabadiliki kwa upepo wa nyomi au ubora wa Sera.. kwao chama ni itikadi.
Je Upinzani Wana wangapi
Je CCM Wana wangapi!?

NGOME ZA KISIASA (Political stronghold regions):
NGOME za kisiasa hutengeneza base ya kuanzia mashambulizi..
Kwamba mkoa gani au kanda gani chama fulani kinapendwa na kuwa na ufuasi na ushawishi mkubwa!?

Ukichukia ACT(CUF ya zamani) Ngome yao ni Pemba ambako Wana 100% ya kuchukua majority votes kwa Urais na Wabunge wengi kuliko CCM. Hayo nia maeneo ambayo hakuna TISS, POLISI, NEC au VIFARU vinaweza kubadili matokeo bali wao ndio wanaweza ku manipulate matokeo. Je ngome kama hizo CHADEMA, ACT na CCM wanazo ngapi Kama mtaji wa kuanzia..!?

IDADI YA WBUNGE..
Kikatiba mwenye Wabunge wengi ndio anaunda Serikali, jee Kuna matarajio ya kupata angalau nusu ya Wabunge!?
Ikumbukwe kwamba Wabunge huakisi kiwango cha uungwaji mkono wa Mgombea Uraisi. Uzoefu Unaonyesha maeneo mengi ambako Kuna washindani wenye nguvu ngazi ya Ubunge huleta changamoto upande wa Urais pia. Jiulize Kuna uwezekano wa majimbo mangap mikoani!? Usizungumzie majimbo mawili matatu katika mkoa au kanda... Kwa mfano kule kanda ya ziwa Musoma, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita na Bukoba jumla mikoa 6 majimbo zaidi ya 40 lakini Upinzani hawana hata viti 8 na hakuna matumaini ya kufikisha angalau majimbo 10 mwaka huu.

Ktk Hali hiyo. Moja katibyabSifa Mgombea mwenye uwezo wa kushinda Uraisi ni uwezo wake binafsi kuwabeba Wabunge wa chama chake. Tuna tegemea Wabunge wangapi wanaobebwa na upepo wa Tundu!? Au Wabunge Wangapi Kama kina Heche watambeba Lisu!? Unategemeaje Ushindi wa Urais ktk mazingira haya!??
UPEPO WA MAKUNDI MAALUM,
Hapa namaanisha makundi rika wazee vs vijana, jinsia wanaume vs wanawake, maeneo ya makazi, Mjini vs vijijini, kiwango cha uelewa(ELIMU) wasomi vs watu wa kawaida..
Tupime kujua kundi lipi kwenye uwezo kubadili matokeo dhidi ya mingine na liko upande Gani?

POLITICAL AGENDA
Hapa kwenye agenda bado Kuna ukakasi. Kuna kundi linalazimisha agenda yake ndio ibebe garagumu la uchaguzi na wamefanikiwa kuaminsha watu uchaguzi utaamuliwa na agenda yao bila kujiuliza jinsi wananchi walivyoikubali agenda hiyo!?

Watu tunaaminishwa ati agenda kuu ni UHURU NA HAKI. Tunasahau kwamba CCM chini ya JPM imetoa Uhuru na HAKI kwa raia ya kawaida kuliko kipindi chochote ktk Historia ya Nchi hii. Tuliimba sana kule nyuma juu ya CCM kuwa Kama kambale baba ndevu mtoto ndevu tukimaanisha kuwa hata balozi au mtendaji wa Kijiji anaweza kukunyanyasa na usipate msaada. Leo sio mtendaji tu bali hata Mkuu wa Mkoa au Waziri hawezi kukunyanyasa ukiwa na ujasiri wa kudai haki yako.

Wahanga wakubwa wa UHURU na HAKI ni wanasiasa, wanaharakati na wanahabari, Kwa kuwa Wana access na media wanataka Wananchi tuwapiganie vita vyao huku wakituaminisha eti na sisi ni wahanga watarajiwa..
Jamani kila mmoja ajifunze kupigana vita yake. Leo hii Mimi Raia wa kawaida nahudumiwa vzr zaidi, nasikilizwa vizuri zaidi, napata haki zangu kwa urahisi zaidi, nina Uhuru zaidi mbele viongozi wa ngazi yangu kuliko kipindi chochote ktk Historia ya Nchi hii kwani KAMBALE MWENYE NDEVU amebaki ni JPM pekee, makamu wake na PM Majaliwa, FULL STOP. Kwa hiyo agenda ya UHURU NA HAKI sio hitaji au agenda ya Raia wa kawaida bali Social Media Na Opposition wanatulisha maneno.

Nimalizie kwa kusema kwamba huenda uchaguzi Ukawa na matokeo tofauti sana na mtazamo wa baadhi ya watu kwani wanakimbia towards wrong direction wakiamini eti the commons watawafuata. Wakifika mwisho wa mwendo watashanga watakapogeuka nyuma na kukuta Raia walikimbia opposite direction.
Tujiandae kisaikolojia
 
tuna nguvu za ku control huu upepo, maadam ni upepo, utapita tuu.
P
Mku kwa hali ilivyo sijui kwani sio kabisa.

Nakumbuka andiko lako moja linalouliza juu ya Congress kuwaandikia baadhi Marais Barua na baadhi ya hao marais hawapo duniani tena.

Na katika hilo uliuliza swala je Congress wanamtaka Mwenyekiti wetu hapa majibu hatuna kabisa.
Hili la nguvu ya umma limekaa vibaya kwani hata Mzee wetu Bashiru aliwahi kuliongelea juu ya Sudan.

Mpenye umetukalia vibaya kwani maonye ya Tasisi za kimataifa yamekuwa mengi mno Mku
 
Back
Top Bottom