Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Nakumbuka wazo la udogo wa baraza lilipendekezwa na upinzani mda mrefu....
 

Ni ngumu chini ya ccm
 

Labda Magufuli akaazime mawaziri nje ya Tanzania.
Hao ni mizigo type.
 
Kikwete katika mkutano wa CCM Morogoro jana**"(NIMEWATOA MBALI,HADI KUWAFIKISHA HAPA MLIPO SIO KAZI NDOGO)."

Magufuli katika mkutano wa CCM Morogoro jana*** (MAFISADI NA MAJIZI NDIO YALIYOTUFIKISHA HAPA TULIPO.)

***Mimi sielewi hicho kilichoongelewa hapo. WanaCCM tuelewesheni.
 
Katika serikali ijayo itakua ni serikali ya kusimamia ukweli, kama ni fisadi utaitwa fisadi bila kupepesa jicho ili tuweze kuendelea katika nyanja zote za maisha. Huu ni muda wa kufanya kazi
 

Haha hiyo inaitwa lugha gongano Mkuu
 

Tatizo letu watz ni uelewa wetu ni mdogo, hasa tunapenda ushabiki, Dr.Slaa alisema hilo jambo la hawa jamaa kuusisma viongozi wa dini, lakini watu walimbeza Dr.Slaa. sasa mwenyewe kasema kanisani, hii ni hatari sana kwa watz kutumia dini na ukabila, Lowasa anajua kabisa hawezi kushinda, yeye mipango yake ilikuwa ni kuibomoa ccm, na angeshindishwa na mafuriko kutoka ccm, baada ya kushindwa kuibomoa amepata wakati ngumu sana, nakumbuka alisema atashinda asbuhi tu, baada ya kufeli sasa anasema kwamba wampe kura nyingi kwani anaamini kuwa ataibiwa kura na ccm kwa hali hiyo wampatie nyingi sana
 

Ilikuwaje kwa JK wa sasa? Hii ndiyo ile dhana ya kwenda JKT ni kuwa "mzalendo", mzalendo my foot! Hebu angalia hao wazalendo(waliokwenda JKT) walivyoifanya Nchi.
 
MAGUFULI hafai kuwa raisi, mtu ambaye ameshindwa kuheshimu Ndola yake kisasa cha kumjengea kimada hotel I ya gorofa 4 wakati mama yake anakaae kwenye kajumba Ka kawaida huyo sioni vision yake, achiae mbalie Ufisadi kwenye barabara, kutujengeahuu upuuzi. another time alikuja rafiki yangu kutoka Mozambique akaona hii barabara ya Mtwara to Dar akaniuliza kama hii ni Masada ? It is substandard ! Na nyumba za serikali alizowagawia hawara zake !! What type of a president you guys are trumpeting ? Mnataka kufanya Tanzania sodoma na Gomorrah, God forbid
 
Tuaona mnatoa ahadi bila ufafanuzi, muda mwingi mnautumia kumshamburia Lowassa, ufafanuzi ya mnayo yaahidi ni Lowassa? Kama kweli Ufidadi unawakera, kwanini wale wa Escrow wa Stanbic hamtaki kuwataja? Ununuzi wa mabehewa Feki hamsemi? Ufisadi uko mwingi kuutaja hapa nitakesha lakini hamtaki kuusema,

Tunataka ufafanuzi wa mnayo yaahidi kama CCM, na tunataka mtwabie kwanini hajatekeleza mliyo yaahidi miaka ya nyuma ya uchaguzi, Toeni maelezo Lowassa sio Mgodi wa Madini au Gesi, Lowassa sio Barabara useme inakwamisha safari zenu, Lowassa sio nguzo za umeme useme anakwamisha Umeme kusambaa, Lowassa sio msikiti au Kanisa tuseme anakwamisha Waumini kwenda Ibada zao, Lowassa sio mafuta tuseme anakwamisha magari au Treni kufanya Safari.

Tunataka mtambie, kwanini ahadi zenu za nyuma hamkutekereza? na hizi mpya mtatekerezaje?
Sio kila siku Lowassa tumechoka.
 
1.Mmekuwa madarakani kwa miaka 54,mtafanya nini cha ziada na tofauti na mlivyofanya kwa miaka 54 ili kuifikiasha nchi yetu kwenye uchumi wa kati?2.Je kwa nini mhakuyafanya miaka 20 au 10 iliyoupita?3.Kama ilishindikana miaka yote hiyo,je miaka 5 ijayo itawatosha?4.Wapinzani wamekuwa kikizo kwa miaka 23,je kuna ugumu gani mkienda likizo ya miaka 5 tu halafu mkarudi tenda 2020?
 
Kwa upande wangu siwezi kusema hawajafanya kitu, dhamira itanisuta! Tatizo langu ni kiwango na ubora wa walichokifanya katika huo muda wote ukilinganisha na mizigo wanayotwishwa wananchi wenye umasikini wa kutupwa.

Pili, mambo ya EPA ndio yananitia hasira kabisa, mnaambiwa pesa zimeibiwa, wanakamatwa washtakiwa wanaachiwa kwa kukosekana ushahidi. Kumbuka pesa ndio imeshapotea na watu wa matatizo mengi!

Hao hao ndio wameingia mikataba mibovu na kuiuza nchi kwa tamaa na maslahi yao binafsi, kiongozi wao anaposema anataka kuleta mabadiliko, anamaanisha chama hicho hicho kitarudi tena kuvunja mikataba mibovu kilicho iweka chenyewe?
 

Kwani Tanzania ya leo ni sawa na ile ya miaka 54 iliyopita? Je, vyama vingi vina umri gani? Je, unajua kwamba lowassa amekuwa waziri kwa miaka 35? Je, umejaribu kumuuliza alifanya nini?

Wapinzani wameazima viongozi. Lowassa ni zao la CCM. Sumaye Anayesemekana kuandaliwa uwaziri mkuu ni zao la CCM. Hata timu ya kampeni ni CCM. Mafuriko ya wabunge wa CCM. Unaongelea upinzani upi? Wa kwenye keyboard au huu wa jf?

Wacha kuishi kwa nadharia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…