Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Makamanda huyu Magufuli sifa zake zimeenea sana, na inaonyesha kajipanga kuchukua nchi tayari.
 
MAGUFULI NA HAPA KAZI TUU!!
Kauli mbiu ya CCM (Hapa kazi tu) na Uchapaji kazi wa Mgombea wake Dr. J.P.Magufuli inaonyesha dhamira ya dhati ya chama hicho katika kumkomboa Mtanzania.Ni dhahiri kwamba tutaijenga nchi yetu kwa sisi wote kuungana na kwa kila mtu kutekeleza wajibu wa kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi hii,hatuwezi kuwa tunataka maslahi yetu ya watanzania ya afya bora,maisha bora na elimu nzuri lakini eti unadhani una mtu ambaye atakuja kukuletea maslahi hayo!Watanzania tubadilike,tunahitajika kiongozi mchapakazi,kujituma na kufanya kazi ipasavyo!!

Magufuli safi lakini meli iliyombeba Magufuli ina nuka harufu kali ya rushwa na ufisadi.inanuka kutowajibika inanuka uzembe inanuka uonevu inanuka upendeleo inanuka hila. Inanuka utawala usio bora.Na harufu hizo imekuwa kali mno kiasi kwamba ili waliopo wapone ni lazima meli hii ibadilishwe sio kubadili kapteni kila baada ya miaka kumi.sasa ni wakati wa kubadili meli ili hata makepten wazuri wasiendelee kutoa harufu kali iliyopo ndani ya meli.Huu si wakati wa kubadili kapten ni WAKATI WA KUBADILI MELI ILIYOPO KATIKA ARDHI NZURI YENYE RUTUBA TANZANIA. MELI INAYOHITAJIKA KUBADILI WA NI CCM.panda meli mpya hata kama kapten kachopoka kwenye inayoanguka
KUMBUKA MABADILIKO YA MWAKA HUU SIO WA KUBADILI KAPTEN TU NI MWAKA WA KUZAMISHA MELI ILIYOCHOKA INAYOTOA HARUFU KALI NA MBAYA.NA KUPANDA MELI MPYA AMBAYO HAIJAWAHI KUPATA NAFASI YA KUBEBA WATANZANIA . USIFANYE makosa.Harufu ya meli ya zamani ni kali mno
 
Magufuli wewe ndiye, wakati upo wizara ya ardhi mambo makubwa ulitufanyia sisi watanzania, kweli tunatambua thamani yako.
 
IMG-20150809-WA0100.jpgView attachment 289004View attachment 289005
Magufuli ana usafi gani?endeleeni kujitoa ufahamu muda ukifika mtakuta tanzania mpya chini ya utawala wa Lowasa.
 
Mgombea uraic kwa tiket ya ccm ana uambia uma kua ataunda mahakama yakupambana na mafisad wakat huo huo anawanyanyua mafisad hao wa escrow anasema tuwape kura je hiyo mahakama itaweza kupambana na hao mafisad wakat huko majimbon kwao anawashka mkono akisema tuwape kura? Hebu changanua
 
Mwaka huu atajidanganya mwenyewe.

Mbona mahakama ipo?
Mahakama itakayoanzishwa ni ipi tena.
 
Lengo la uzi huu ni kuchambua kwa kina ahadi kuu zinazotolewa na John Pombe Magufuli- mgombea wa urais kupitia CCM.

Ahadi ya kuvirudisha serikalini viwanda vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi
Hii ni moja ya ahadi kubwa ambayo Magufuli anaitoa katika kampeni. Mafufuli anasema kuwa nasema kweli na anasisitiza nasema kweli kabisa kuwa nitarudisha viwanda vilivyobinafisishwa lakini havifanyi kazi. Ngoja tukubali kwa sasa kuwa kweli Magafuli atavirudisha serikalini viwanda hivyo anavyosema vilibinafsishwa lakini wawekezaji wameshindwa kuviendeleza. Swali la kumuuliza Magufuli, je anajua hali ya viwanda hivyo visivyozalisha?. Ni nini maana ya viwanda kwa Magufuli? Hivi Magafuli hajui kuwa viwanda ambavyo havizalishi wawekezaji walishang'oa mashine na kuzipeleka wanakojua na hivyo siyo viwanda bali ni magofu tupu bila mashine? Je kwa Magufuli kiwanda ni gofu? Hivi kwa nini Magufuli anawafanya wananchi wote ni wapumbavu na malofa wa kuelewa?

Ukweli ni kuwa hakuna viwanda ambavyo Magufuli atakavirudisha bali ni Magofu. Hivyo ahadi ya Magufuli kuhusu viwanda ambayo anainadi kwenye majukwaa na kwenye matangazo katika vyombo vya habari ni uwongo mtupu. Hao wanaoitwa wawekezaji walifanya uporaji wa mchana kweupe kwa kusaidiwa na serikali ya "Mr Clean". Ndiyo maana wengi wanasema Magufuli ni reflection ya Mr. Clean, au tuseme serikali itakayoundwa na Magafuli itakuwa ni mwendelezo wa serikali ya kiporaji ya B. Mkapaa. Ndiyo maana haishangazi kuwa Magufuli ni jina lililoletwa katika vikao vya uteuzi vya CCM kutoka kwenye mfuko wa Mkapaa.

Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda
Ahadi hii inaonekana kwa juu juu kufanana na hiyo ya hapo juu lakini kuna kitu kimejificha nyuma yake. Anawaambia wananchi wa Tanzania kuwa akiwa rais, Tanzania itakuwa ni mali yake. Ni kauli inayoonyesha ubinafsi wake na pia udikiteta wa hali ya juu. Magufuli anaamini na kufikiri kuwa nchi nzima ni mali yake takapokuwa rais na atafanya atakalo maana ni mali yake binafsi. Lakini katiba ya nchi inasema Tanzania ni mali ya wananchi siyo mali ya mtu yoyote wala kikundi chochote. Hivyo, kauli ya "Tanzania ya Magufuli" inaonyesha Magufuli ni mtu wa namna gani akishika nafsi ya urais- yaani atakuwa mbinafsi na dikteta katika utawala wake.
 
Kiwanda cha kuchambua Pamba na kutengeneza mafuta ya kula kilichopo Chato ambako yeye anatokea na kuwahi kuwa mbunge wa miaka 20 chini ya Biharamulo Cooperative Union (BCU) kina hali gani?

Amewahi kusikika akikiongelea?
 
Huyu sasa hivi wala hajielewi anachokisema! Nimemshangaa leo anawashangaa kina Sumaye kuwa wamekaa serikalini miaka mingi wakiwa watendaji lkn sasa hivi wanalalamika kuwa serikali haijafanya kitu, sasa yeye mwenyewe amesahau kuwa kampeni zake zote amekuwa akishangaa matatizo yaliyopo kana kwamba yeye anatoka upinzani! :nono:
 
Dkt.j.p.magufuli anainyelea katiba ya jmt ya mwaka 77,kila anapopanda majukaani ni kusema"tanzania ya magufuli"
lengo la uzi huu ni kuchambua kwa kina ahadi kuu zinazotolewa na john pombe magufuli- mgombea wa urais kupitia ccm.

ahadi ya kuvirudisha serikalini viwanda vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi
hii ni moja ya ahadi kubwa ambayo magufuli anaitoa katika kampeni. Mafufuli anasema kuwa nasema kweli na anasisitiza nasema kweli kabisa kuwa nitarudisha viwanda vilivyobinafisishwa lakini havifanyi kazi. Ngoja tukubali kwa sasa kuwa kweli magafuli atavirudisha serikalini viwanda hivyo anavyosema vilibinafsishwa lakini wawekezaji wameshindwa kuviendeleza. Swali la kumuuliza magufuli, je anajua hali ya viwanda hivyo visivyozalisha?. Ni nini maana ya viwanda kwa magufuli? Hivi magafuli hajui kuwa viwanda ambavyo havizalishi wawekezaji walishang’oa mashine na kuzipeleka wanakojua na hivyo siyo viwanda bali ni magofu tupu bila mashine? Je kwa magufuli kiwanda ni gofu? Hivi kwa nini magufuli anawafanya wananchi wote ni wapumbavu na malofa wa kuelewa?

Ukweli ni kuwa hakuna viwanda ambavyo magufuli atakavirudisha bali ni magofu. Hivyo ahadi ya magufuli kuhusu viwanda ambayo anainadi kwenye majukwaa na kwenye matangazo katika vyombo vya habari ni uwongo mtupu. Hao wanaoitwa wawekezaji walifanya uporaji wa mchana kweupe kwa kusaidiwa na serikali ya “mr clean”. Ndiyo maana wengi wanasema magufuli ni reflection ya mr. Clean, au tuseme serikali itakayoundwa na magafuli itakuwa ni mwendelezo wa serikali ya kiporaji ya b. Mkapaa. Ndiyo maana haishangazi kuwa magufuli ni jina lililoletwa katika vikao vya uteuzi vya ccm kutoka kwenye mfuko wa mkapaa.

tanzania ya magufuli itakuwa ya viwanda
ahadi hii inaonekana kwa juu juu kufanana na hiyo ya hapo juu lakini kuna kitu kimejificha nyuma yake. Anawaambia wananchi wa tanzania kuwa akiwa rais, tanzania itakuwa ni mali yake. Ni kauli inayoonyesha ubinafsi wake na pia udikiteta wa hali ya juu. Magufuli anaamini na kufikiri kuwa nchi nzima ni mali yake takapokuwa rais na atafanya atakalo maana ni mali yake binafsi. Lakini katiba ya nchi inasema tanzania ni mali ya wananchi siyo mali ya mtu yoyote wala kikundi chochote. Hivyo, kauli ya “tanzania ya magufuli” inaonyesha magufuli ni mtu wa namna gani akishika nafsi ya urais- yaani atakuwa mbinafsi na dikteta katika utawala wake.
 
Kwani ukisubiri kuona kama amedanganya itakuwaje? IPO ndani ya kichwa chake?
 
WHY NOT MAGUFULI:
Mgombea wa Ccm Dk John Magufuli kwa sehemu kubwa ya mikutano yake na wananchi imehusu kilimo,ajira,miundo mbinu,afya,elimu,uongozi bora na umoja wa kitaifa:Kuna sababu kweli ya kutomchagua kiongozi huyu?Watanzania tushtukee
 
WHY NOT MAGUFULI:
Mgombea wa Ccm Dk John Magufuli kwa sehemu kubwa ya mikutano yake na wananchi imehusu kilimo,ajira,miundo mbinu,afya,elimu,uongozi bora na umoja wa kitaifa:Kuna sababu kweli ya kutomchagua kiongozi huyu?Watanzania tushtukee

Huyu ndo kura yangu mm na familia yangu
 
Back
Top Bottom