Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MAGUFULI NA HAPA KAZI TUU!!
Kauli mbiu ya CCM (Hapa kazi tu) na Uchapaji kazi wa Mgombea wake Dr. J.P.Magufuli inaonyesha dhamira ya dhati ya chama hicho katika kumkomboa Mtanzania.Ni dhahiri kwamba tutaijenga nchi yetu kwa sisi wote kuungana na kwa kila mtu kutekeleza wajibu wa kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi hii,hatuwezi kuwa tunataka maslahi yetu ya watanzania ya afya bora,maisha bora na elimu nzuri lakini eti unadhani una mtu ambaye atakuja kukuletea maslahi hayo!Watanzania tubadilike,tunahitajika kiongozi mchapakazi,kujituma na kufanya kazi ipasavyo!!
View attachment 289004View attachment 289005Mwaka huu atajidanganya mwenyewe.
Mbona mahakama ipo?
Mahakama itakayoanzishwa ni ipi tena.
Kama ipo, ina maana mgombea hajui kama ipo? Kama ndo hivo hastahili kura yangu
lengo la uzi huu ni kuchambua kwa kina ahadi kuu zinazotolewa na john pombe magufuli- mgombea wa urais kupitia ccm.
ahadi ya kuvirudisha serikalini viwanda vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi
hii ni moja ya ahadi kubwa ambayo magufuli anaitoa katika kampeni. Mafufuli anasema kuwa nasema kweli na anasisitiza nasema kweli kabisa kuwa nitarudisha viwanda vilivyobinafisishwa lakini havifanyi kazi. Ngoja tukubali kwa sasa kuwa kweli magafuli atavirudisha serikalini viwanda hivyo anavyosema vilibinafsishwa lakini wawekezaji wameshindwa kuviendeleza. Swali la kumuuliza magufuli, je anajua hali ya viwanda hivyo visivyozalisha?. Ni nini maana ya viwanda kwa magufuli? Hivi magafuli hajui kuwa viwanda ambavyo havizalishi wawekezaji walishangoa mashine na kuzipeleka wanakojua na hivyo siyo viwanda bali ni magofu tupu bila mashine? Je kwa magufuli kiwanda ni gofu? Hivi kwa nini magufuli anawafanya wananchi wote ni wapumbavu na malofa wa kuelewa?
Ukweli ni kuwa hakuna viwanda ambavyo magufuli atakavirudisha bali ni magofu. Hivyo ahadi ya magufuli kuhusu viwanda ambayo anainadi kwenye majukwaa na kwenye matangazo katika vyombo vya habari ni uwongo mtupu. Hao wanaoitwa wawekezaji walifanya uporaji wa mchana kweupe kwa kusaidiwa na serikali ya mr clean. Ndiyo maana wengi wanasema magufuli ni reflection ya mr. Clean, au tuseme serikali itakayoundwa na magafuli itakuwa ni mwendelezo wa serikali ya kiporaji ya b. Mkapaa. Ndiyo maana haishangazi kuwa magufuli ni jina lililoletwa katika vikao vya uteuzi vya ccm kutoka kwenye mfuko wa mkapaa.
tanzania ya magufuli itakuwa ya viwanda
ahadi hii inaonekana kwa juu juu kufanana na hiyo ya hapo juu lakini kuna kitu kimejificha nyuma yake. Anawaambia wananchi wa tanzania kuwa akiwa rais, tanzania itakuwa ni mali yake. Ni kauli inayoonyesha ubinafsi wake na pia udikiteta wa hali ya juu. Magufuli anaamini na kufikiri kuwa nchi nzima ni mali yake takapokuwa rais na atafanya atakalo maana ni mali yake binafsi. Lakini katiba ya nchi inasema tanzania ni mali ya wananchi siyo mali ya mtu yoyote wala kikundi chochote. Hivyo, kauli ya tanzania ya magufuli inaonyesha magufuli ni mtu wa namna gani akishika nafsi ya urais- yaani atakuwa mbinafsi na dikteta katika utawala wake.
WHY NOT MAGUFULI:
Mgombea wa Ccm Dk John Magufuli kwa sehemu kubwa ya mikutano yake na wananchi imehusu kilimo,ajira,miundo mbinu,afya,elimu,uongozi bora na umoja wa kitaifa:Kuna sababu kweli ya kutomchagua kiongozi huyu?Watanzania tushtukee