Kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu, mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya CCM ndugu John Pombe Magufuli amesikika akijinadi kwa wananchi kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ataanzisha mahakama maalumu kushughulikia kesi za ufisadi na wezi. Hilo ni jambo jema, lakini je ni kweli hayo anayosema majukwaani, si kwa ajili ya kutafuta kura tu? Nina sababu za kuhoji hivyo:
1. Mahakama zilizopo naamini hazijashindwa kufanya kazi hiyo na ndio maana kuna baadhi ya viongozi wamefunguliwa
kesi za ufisadi (Basil Mramba, Daniel yona, Grey Mgonja n.k). Mahakama zetu hazijasema hazina uwezo wa kuendesha
hizo kesi.
2. Tatizo la ufisadi hapa nchini halitokani na kutokuwepo kwa mahakama maalumu ya ufisadi bali inatokana na mfumo
wa viongozi wa serikali na CCM kulindana na hivyo kutowajibishana.
3. Magufuli anajua wazi kuwa asilimia kubwa (kama siyo zote) ya mafisadi anaowazungumzia wapo ndani ya CCM na
serikalini hasa iliyopo madarakani na wengine ni viongozi wandamizi serikalini na katika chama. Kuthibitisha hilo,
katibu mkuu wa CCM ndugu kinana hivi karibuni akiwa Moshi alikiri kuwa CCM imejaa wezi. Sasa je Magufuli yupo
tayari kukibomoa chama chake kwa kuwafungulia kesi mahakamani viongozi wa chama caheke waliomweka katika
nafasi hiyo ya kugombea urais? Maana mafisadi na wezi wengi wa hela za umma wapo huko (CCM na serikalini -
Escrow, richmond, Epa, IPTL n.k).
4. Je magufuli yupo tayari yeye mwenyewe kufikishwa katika mahakama hiyo atakayoianzisha? Maana ni mmoja wa
viongozi wa serikali (waziri) anayetuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi!
Kwa kweli katika hili binafsi naona hapa anapiga porojo tu.