Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Umeme shida maji tabu kula kwa tabu maisha magumu twiga kapanda ndege mm sijawai kapanda Ata fast jet kwenda znz yaani CCM ni shida elimu mbovu barabara mbovu hospital hakuna madawa yaani CCM ni shidaaaa toka CCM
Mkuu, ndg.mwema hivo vyote vya msingi na vya kimaisha na hata vya anasa waLibya na waIraqi, waTunisia walikuwa navyo na walikuwa wameshiba maisha mataamu...

VIJANA na vibaraka wa mashetwani wakaanza kuchocheana kuomba unachokiomba wewe!! Yakatokea yaliyotokea....tija yao sasa Leo hii wanatamani AMANI irudi ... hola !! wana tamani usalama urudi.. hola !! wanatamani waweze kuwa huru...hola !!

Jamani AMANI ktk maisha huwezi kufananisha na chochote !!

nichukulieni kadri ya akili yangu na fikra zangu !! kama mnazo zenu tafakarini...!! kanjibai Gochavez


 
Nnacho kiona kutoka kwa babu magufuli ni ahadi hewa za ccm ambazo hazitekelezeki kwa sababu viongozi kuanzia ngazi za juu wanaliibia taifa kwa ufisadi.
HAMNA NAMNA NIYNGINE ZAIDI YAKUWAPIGA CHINI
 
Kuna mtu anaitwa Mr Chin nahisi na yeye alihusika kupandisha twiga ndege!! Bila kusahau magamba mengine ambayo yapo humu!!
aseme wazi kikwete na waliomtangulia wameharibu nchi na yeye atafanya tofauti kabisa nao ili pawepo mabadiliko. Huwezi kuhubir mabadiliko huku ukiwasifia watangulizi wako. Kikwete anasema ccm imetimiza ahadi kwa asilimia 90. Magufuli anasema ataibadilusha ccm kwa sababu ilishindwa kuisimamia serikali. Anashangaa kwa nini mambo mengi hayajafanyika. Hizi ni hadaa au wanadhani watz wajinga?
 
Last edited by a moderator:
Naomba wana ccm wazee wa lumumba mnijibu hili swali.

Ndugu yenu mpendwa wenu magufuli amekuwa akimwaga ahadi kemkem kila aendako ukijumlisha na za yule mama nadhani zitakuwa zimefika mia mpaka sasa hivi.

Lakini tukumbuke pia mtangulizi wake ambaye anatamani ampe kijiti alitoa zaidi ya mia na nyingi alizotoa zinafanana na hizi anazotoa magufuli. Na nakumbuka mlitoa sana povu kumtetea kikwete kwammba ahadi zake ni nyingi but zinatekelzeka, and now ndio naona comments zile zile kwamba ahadi za magufuli zinatekelzeka na kwamba atazitimiza.

kikwete aliahidi kuwa ikifika 2015-
1.kilimo cha jembe kitafika kikomo
2.kula sahani moja na mafisadi na hatacheka nao
3.atakuwa rais wa mwisho wa tanzania masikini.
Plus ahadi kedekede za kununua meli sehemu amabzo hata watu hawahitaji meli.

mwisho wa siku alicheka nao weeeee!! Mpaka leo akawaona mramba na yona ndio mafisadi miaka 10 ya utawala wake

magufuli mpaka sasa na yeye ameshaahidi
1.milioni 50 kila kijiji-
2.kufuta kilimo cha mkono
3.kula sahani moja na mafisadi hatacheka nao na atawaundia mahakama yao
4.kufufua viwanda-hii ni ishu ya zaidi ya miaka 10 kulifanikisha

sasa nijibuni swali hili

je nini tofauti kati ya ahadi za kikwete na magufuli? Maana mi naona kama anamdesea kikwete kile kijitabu chake cha ahadi!!!!
Mkikubali magufuli atatizimiza mnakubali kikwete kafeli!! So msitudanganye kuwa ataweza yote ndani ya miaka 5 wakati mwenzake kashindwa ndani ya miaka 10.
 
Tofauti ni negligible..ni kama vile hakuna tofauti kabisa
 
Kikwete mwenyekiti wa CCM na raisi wa Tanzania aliyeshindwa kutekeleza ahadi zake hata kwa asilimia 25
Maghufuli ajigeuza mchizi anajifanya yeye sio mwanaCCM wala hatokani na serikali ya CCM na wala si waziri wa serikali inayotawala sasa kwi kwi wmechanganyikiwa had I basi maghuli the confused candidate
 
Kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu, mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya CCM ndugu John Pombe Magufuli amesikika akijinadi kwa wananchi kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ataanzisha mahakama maalumu kushughulikia kesi za ufisadi na wezi. Hilo ni jambo jema, lakini je ni kweli hayo anayosema majukwaani, si kwa ajili ya kutafuta kura tu? Nina sababu za kuhoji hivyo:

1. Mahakama zilizopo naamini hazijashindwa kufanya kazi hiyo na ndio maana kuna baadhi ya viongozi wamefunguliwa
kesi za ufisadi (Basil Mramba, Daniel yona, Grey Mgonja n.k). Mahakama zetu hazijasema hazina uwezo wa kuendesha
hizo kesi.

2. Tatizo la ufisadi hapa nchini halitokani na kutokuwepo kwa mahakama maalumu ya ufisadi bali inatokana na mfumo
wa viongozi wa serikali na CCM kulindana na hivyo kutowajibishana.

3. Magufuli anajua wazi kuwa asilimia kubwa (kama siyo zote) ya mafisadi anaowazungumzia wapo ndani ya CCM na
serikalini hasa iliyopo madarakani na wengine ni viongozi wandamizi serikalini na katika chama. Kuthibitisha hilo,
katibu mkuu wa CCM ndugu kinana hivi karibuni akiwa Moshi alikiri kuwa CCM imejaa wezi. Sasa je Magufuli yupo
tayari kukibomoa chama chake kwa kuwafungulia kesi mahakamani viongozi wa chama caheke waliomweka katika
nafasi hiyo ya kugombea urais? Maana mafisadi na wezi wengi wa hela za umma wapo huko (CCM na serikalini -
Escrow, richmond, Epa, IPTL n.k).

4. Je magufuli yupo tayari yeye mwenyewe kufikishwa katika mahakama hiyo atakayoianzisha? Maana ni mmoja wa
viongozi wa serikali (waziri) anayetuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi!

Kwa kweli katika hili binafsi naona hapa anapiga porojo tu.
 
Dr. John Pombe Joseph Magufuli;
Natambua Tanga ulikuwa Mji wa Viwanda, bahati mbaya viwanda hivyo vimebaki kuwa magofu - serikali yangu itavifufua.
Serikali ya nani iliviua baba... ?
 
HUYU NDIYE DR JOHN POMBE MAGUFULI

Mgombea wa urais kupitia CCM, DR JOHN POMBE MAGUFULI,KTKA UONGOZI WAKE,

Asema atafumua mfumo wa utendaji ndani ya Chama

Akerwa na vigogo kuwabeba watoto wao katika nafasi za uongozi

Zikiwa ni takribani siku 20 zimepita toka pazia la kampeni za uchaguzi mkuu zianze mgombea urais wa CCM Dkt. John Magufuli akutana na katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kampeni za chama hicho na kumpa mambo anayotaraji kufanyika.

Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu. Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi. Nataka nikapambane kufuta hili lililojengeka kwa watoto wa vigogo kubebwa kwenye nafasi za uongozi hata ajira na kuwaacha watoto wa watanzania maskini wakiwa mitaani eti kwa sababu hawana wa kuwashika mikono haki ya Mungu hili nitapambana nalo ili chama hiki kiwe cha wote na nchi hii iwe ya wote.

Hivyo mke wangu naomba aachwe akafundishe, wanangu waendelee na mambo yao na hata ndugu zangu. Jukumu lao kubwa ni kuniombea kwa Mungu ili nikawatumikie watanzania kwa moyo wa dhati bila kiburi na majivuno.

Asema kabla hajaapishwa anataka Chama chake kiandae utaratibu wa kuwabana wabunge wake hususani kupata ripoti za kila mwezi za kila mbunge juu ya utendaji wake kwa wananchi na mchango wake anapokuwa bungeni. Hii itasaidia kuwa na wabunge wanaochapakazi na kuwatumikia wananchi kuliki ilivyo sasa.

Amesema akiingia Oktoba utaratibu wa kuwapa misamaha ya kodi wabunge imewafanya wasahau majukumu yao na kujiingiza kwenye biashara wakati wanalipwa vizuri na wanapata posho kubwa sasa amesema atafuta misamaha hiyo ili wajikite kuwatumikia wananchi.

Asema atafumua utendaji wa chama kwa kukijengea chama uwezo zaidi kiuchumi ili watendaji wake na jumuiya zake walipwe vizuri na kuondoa michango ya gharama za kura za maoni na hata kuchangia gharama za uchaguzi kwenye majimbo ili kutoa fursa kwa vijana wanaotoka familia maskini kushiriki nafasi ya kuitumikia nchi yao kuanzia nafasi za mtaa, udiwani na ubunge hata urais. Pamoja na kufuta utendaji kazi wa mazoea.

Asema siku 100 za mwanzo zitakuwa za kufanya mageuzi makubwa ndani ya serikali yake na Chama. Asema kama kuna kiongozi aliyeshiriki ufisadi wowote ajiandae maana atakula nao sahani moja ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo chetu cha habari kinasema hata hivyo Kanali Kinana na Philip Mangula wamemuleza kumuunga mekono kwani ni mtazamo mzuri na watampa ushirikiano japo hautawapendeza wengi.

KWELI MAGUFULI NI JEMBE,KATAPILA: HAPA NI KAZI TU.
 
Kuna mgombea mmoja mkubwa hapa Namanyere mkoa wa Rukwa Mkojo ulimponyoka akawahishwa kwenye ndege
 
Hiyo jeuri hana magufuli atafukuza karibu watendaji wote na Chama chake hakitabaki na kiongozi aanze na kinana nape na mangula walitoa siku 90 kwa mafisadi wako wapi? Ccm ni kama panya
 
Back
Top Bottom