Uchambuzi wa Kisheria juu ya Hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu

Uchambuzi wa Kisheria juu ya Hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu

Amani inavurugwa na CCM kwa kuengua wagombea wa upinzani na mawakala wa upinzani na kuitawala tume eti ya kwao
Wagombea ambao wamekiuka taratibu Kwa nini wasienguliwe? Sheria na kanuni ziliwekewa Kwa Ajili gani?
 
Mwananchi yoyote ana kiapo cha utii kwa nchi yake.

Hapana ,
Kiapo cha utii kinajulikana .
Mwananchi hana liapo cha utii .

Wabunge wanaapa.
Mawaziri wanaapa , wanajeshi wanaapa kutii ndio maana wanapewa amri .
Majaji wanaapa n.k.

wananchi ndio mabosi wanaowapa ajira hao wote .

Ni uharamia tu wa genge la mafisadi walioikalia nchi kimabavu ili kulinda maslahi yao lakini wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho kabisa .

Mbowe alisema Samia Must go na akaita maandamano ya kumtoa Samia ,madarakani.
Ni wazi kuwa Woga wa wananchi ndiyo nguvu yao. Lakini iko siku hawata amini .
Labda kama Mungu naye ni Mwanachama wa CCM lakini kwa dhulma na uonevu na mali wanaojilimbikizia halafu bado hawana shukrani wanaua wenzao ili waendelee kula wao tu na familia zao kuna jambo muda sio mrefu lioà
 
Waswahili wanasema siku ya kufa nyani miti yote uteleza.

Msemo huu unaweza kuuchukulia kawaida ila kiukweli haya ndo yanayokikumba Chama cha Mapinduzi mwaka huu

Ukisoma hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu ya upande wa Jamhuri, kama wewe ni Mwanasheria uliyesoma Sheria na kuielewa vizuri utagundua kuwa kwa Hati ya Mashtaka ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu hakuna kosa lolote lililofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria kilichotajwa.

Tuende taratibu;
Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka ya Upande wa Jamhuri, Tundu Lissu ameshtakiwa kutenda kosa kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani Penal Code.

View attachment 3299593

Ukisoma maelezo ya kosa kwenye hati hiyo yanasema tarehe 3 April, 2025 katika Jiji la Dar es Salaam Tundu Lissu akiwa chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na nia ya kuushawishi umma wa Tanzania kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 aliitisha Serikali ya Tanzania kwa kutamka maneno kuwa,

"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"

Ukiachana na maelezo ya kosa kwenye hati ya mashtaka, Kifungu cha 39(2) (d) kilichotajwa kuvunjwa cha kanuni ya Adhabu kwa tafsiri ya kiswahili cha kawaida na kisheria kinasema hivi;

Mtu yeyote aliye chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye ndani ya Jamhuri au Nje ya Jamhuri anayetengeneza nia au kusababisha kuwepo kwa nia ya kushawishi, kufanya, kushauri kuwepo kwa vitendo vya kuitisha Serikali, Bunge au Mahakama na kuonesha nia hiyo kwa kutangaza au kuprint maandishi au maneno yoyote atakuwa na hatia ya kutenda kosa la Uhaini na atahukumiwa adhabu ya Kifo.

View attachment 3299594


Je kuna Uhusiano wa Maelezo ya Kosa na Kifungu cha Sheria kinachoanzisha kosa husika?

Ukisoma Kifungu cha 39(2) (d) utagundua kosa linalosemwa hapo lazima lifanywe na mtu mwenye kiapo cha Utii na pia ni lazima nia au kosa hilo lifanywe dhidi ya Moja ya Mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (Executive), Bunge (Legislature) au Mahakama( Judiciary)

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Sitaki kujadili suala la Kiapo cha utii ambalo tayari limeshaelezwa na Mawakili wengi kupitia platforms mbalimbali ambalo kiuhalisia linamuondoa Lissu kuwa liable kufanya kosa chini ya Kifungu hicho. Mimi nitajikita kwenye hoja ngumu nyingine.

Ukisoma maelezo ya kosa , the fun thing maneno anayosema Tundu Lissu kama yalivyo kwenye hati ya Mashtaka hakuna sehemu yanaonekana akivitaja Serikali, Bunge au Mahakama. Hakuna sehemu ambayo yanaonesha amezilenga Serikali au Bunge au Mahakama. Yeye ameulenga Uchaguzi.

Lissu amesema watakichafua kwenye Uchaguzi, amesema tutazuia uchaguzi. amesema tutahamasisha uasi akihusianisha na Uchaguzi, Amesema wanaenda kuuvuruga Uchaguzi.

Kama Mwanasheria niliyepikwa na kupikika kwenye vyuo bora kabisa Duniani hasa The University of Westminster ( UK) niseme tu ukweli, kwa maelezo ya kosa yanavyoonekana kwenye hati ya Mashtaka hakuna kosa la Uhaini hapo. Serikali Mtaaibika vibaya sana Mahakamani.

Ushauri wangu kwa Watawala:

Kama nia ni kumuweka Lissu gerezani sawa mtafanikiwa kumuweka tu Gerezani ila hamtafanikiwa kuondoa spirit ya Mabadiliko ya Mifumo waliyopandikiza CHADEMA kwa wananchi.

Kama nia ni kuwatisha Wananchi sidhani kama Mtafanikiwa sana maana kwa ninavyowaona Watanzania siku msiyoijua Wanaenda kukinukisha kweli.

Mwisho kama nia yenu ni kumtisha Lissu, sioni akitishika maana kwa nilivyomuona leo picha zake akiwa Mahakamani anafurahia sana kuwepo pale.

Akili kumkichwa.
Sheria inasema ni Uhaini lakini alichosema Lisu na kilichoandikwa kwenye Particulars of Offense ni Uasi. Kwani Uchaguzi unaendeshwa na Nani? Government!! Nafikiri ungeeleza Uhaini na Uasi, na je hayo maelezo ya Lisu kwenye Particulars of Offense yana align wapi. Hata hivyo DPP anaweza akasahihisha Hiyo charge.
 
Sheria inasema ni Uhaini lakini alichosema Lisu na kilichoandikwa kwenye Particulars of Offense ni Uasi. Kwani Uchaguzi unaendeshwa na Nani? Government!! Nafikiri ungeeleza Uhaini na Uasi, na je hayo maelezo ya Lisu kwenye Particulars of Offense yana align wapi. Hata hivyo DPP anaweza akasahihisha Hiyo charge.
Kosa la Uasi linapatikana kwenye kifungu kipi cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu? Limetafsiriwa chini ya kifungu kipi cha Sheria hiyo?

Hakuna kesi hapo jombaa.
 
Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
Za lisu mnaziona vipi aliye sema watapoteza wapinzani?ni kauli nzuri? Na aliye leta taharuki kuhusu virusi vya ebola kauli zake zina afya ? Mmekuwa wabinafsi sana,
 
Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
Lisu ni Mwenyekiti wa Chama cha upinzani wews unataka aongee nini ukikubali kuingia kwenye maswala ya siasa tegemea kila Aina ya kebei ,vichambo navitisho hapo ndipo siasa zinaponoga na POLISI wanatakiwa wakae pembeni mtu vikimuuma aende mwenyewe mahakamani kufungua kesi ya madai.Ukisha simama kwenye jukwaa la siasa ujue umejiexpress kwa jamii watu watachuja mchele na pumba mbele ya safari.wewe maneno yanayo kuudhi wengine ndiyo wanayofurahia ndiyo maana kwenye siasa kukiwa hakuna uvumilivu kunatokea vurugu.
 
Back
Top Bottom