Uchambuzi wa Kisheria juu ya Hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu

Hicho kifungu kinawahusu majeshi ,Wabunge ,Mawaziri na wateule wote wa Rais lakini sio wanasiasa .
Maandamano sio uasi duniani kote .

Muda sio mrefu Watakaoaibika na kuondoka madarakani na kwenda Jela kwa mauaji na kutesa watu ni hao hao wanafungua kesi za uongo .

Watawala wanamuwakilisha Mungu hapa duniani.
Ukiona majeshi na watawala wanatumia hila na kushitaki watu kwa uongo basi ujue utawala huo umemwasi Mungu .
Wanasema Lisu anatangaza ûasi lakini ni uasi dhidi ya Utawala wa kishetani uliojaa rushwa ,ufisadi , wizi na dhulma katikati ya utajiri mkubwa tuliopewa na Mungu . Utajiri wa nchi wanautumia kujitajirisha wao wenyewe na familia zao. Wanasahau ajira kwa watoto wa maskini walijaa Tanganyika katikati ya rasilimali nyingi .Rasilimali zote wameuza kwa wageni .

Kwa sasa ajira ni nusu kwa nusu na Wazanzibari bila kujali uwiano wa watu .
Zanzibar matibabu ya figo ni Bure huku Tanganyika ni ghali sana mpaka Jeshi limeamua kutumia rasilimali zake kununua dialysis machine na kuhoji kwa nini watu maskini hawatibiwi kwa gharama nafuu wakati hizo mashine haziuzwi ghali kiasi hicho ?

Hakuna mtawala aliyelizungumzia hilo ?
Mwananchi yoyote ana kiapo cha utii kwa nchi yake.
 
Wewe ulikula kiapo hicho lini na wapi?

Mmachinga aliyepo Kariakoo au Tundu Lissu tu alikula kiapo hicho lini na wapi?
In a nation, allegiance is primarily owed by its citizens to the state or government. This duty of loyalty and obedience is a core aspect of citizenship, where individuals are expected to support and uphold the laws and principles of their nation.

Citizenship is the legal status of belonging to a state, which implies a reciprocal relationship – the citizen owes allegiance to the state, and the state owes protection and rights to the citizen.

Allegiance signifies a duty of fidelity, loyalty, and obedience that citizens owe to their nation.

Scope of Allegiance:
Natural-born citizens owe natural allegiance to their nation, while naturalized citizens owe allegiance to their new country. Resident aliens also owe temporary allegiance to the country they are.
 
Waswahili wanasema siku ya kufa nyani miti yote uteleza.

Msemo huu unaweza kuuchukulia kawaida ila kiukweli haya ndo yanayokikumba Chama cha Mapinduzi mwaka huu

Ukisoma hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu ya upande wa Jamhuri, kama wewe ni Mwanasheria uliyesoma Sheria na kuielewa vizuri utagundua kuwa kwa Hati ya Mashtaka ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu hakuna kosa lolote lililofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria kilichotajwa.

Tuende taratibu;
Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka ya Upande wa Jamhuri, Tundu Lissu ameshtakiwa kutenda kosa kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani Penal Code.

View attachment 3299593

Ukisoma maelezo ya kosa kwenye hati hiyo yanasema tarehe 3 April, 2025 katika Jiji la Dar es Salaam Tundu Lissu akiwa chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na nia ya kuushawishi umma wa Tanzania kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 aliitisha Serikali ya Tanzania kwa kutamka maneno kuwa,

"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"

Ukiachana na maelezo ya kosa kwenye hati ya mashtaka, Kifungu cha 39(2) (d) kilichotajwa kuvunjwa cha kanuni ya Adhabu kwa tafsiri ya kiswahili cha kawaida na kisheria kinasema hivi;

Mtu yeyote aliye chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye ndani ya Jamhuri au Nje ya Jamhuri anayetengeneza nia au kusababisha kuwepo kwa nia ya kushawishi, kufanya, kushauri kuwepo kwa vitendo vya kuitisha Serikali, Bunge au Mahakama na kuonesha nia hiyo kwa kutangaza au kuprint maandishi au maneno yoyote atakuwa na hatia ya kutenda kosa la Uhaini na atahukumiwa adhabu ya Kifo.

View attachment 3299594

Je kuna Uhusiano wa Maelezo ya Kosa na Kifungu cha Sheria kinachoanzisha kosa husika?

Ukisoma Kifungu cha 39(2) (d) utagundua kosa linalosemwa hapo lazima lifanywe na mtu mwenye kiapo cha Utii na pia ni lazima nia au kosa hilo lifanywe dhidi ya Moja ya Mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (Executive), Bunge (Legislature) au Mahakama( Judiciary)

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Sitaki kujadili suala la Kiapo cha utii ambalo tayari limeshaelezwa na Mawakili wengi kupitia platforms mbalimbali ambalo kiuhalisia linamuondoa Lissu kuwa liable kufanya kosa chini ya Kifungu hicho. Mimi nitajikita kwenye hoja ngumu nyingine.

Ukisoma maelezo ya kosa , the fun thing maneno anayosema Tundu Lissu kama yalivyo kwenye hati ya Mashtaka hakuna sehemu yanaonekana akivitaja Serikali, Bunge au Mahakama. Hakuna sehemu ambayo yanaonesha amezilenga Serikali au Bunge au Mahakama. Yeye ameulenga Uchaguzi.

Lissu amesema watakichafua kwenye Uchaguzi, amesema tutazuia uchaguzi. amesema tutahamasisha uasi akihusianisha na Uchaguzi, Amesema wanaenda kuuvuruga Uchaguzi.

Kama Mwanasheria niliyepikwa na kupikika kwenye vyuo bora kabisa Duniani hasa The University of Westminster ( UK) niseme tu ukweli, kwa maelezo ya kosa yanavyoonekana kwenye hati ya Mashtaka hakuna kosa la Uhaini hapo. Serikali Mtaaibika vibaya sana Mahakamani.

Ushauri wangu kwa Watawala:

Kama nia ni kumuweka Lissu gerezani sawa mtafanikiwa kumuweka tu Gerezani ila hamtafanikiwa kuondoa spirit ya Mabadiliko ya Mifumo waliyopandikiza CHADEMA kwa wananchi.

Kama nia ni kuwatisha Wananchi sidhani kama Mtafanikiwa sana maana kwa ninavyowaona Watanzania siku msiyoijua Wanaenda kukinukisha kweli.

Mwisho kama nia yenu ni kumtisha Lissu, sioni akitishika maana kwa nilivyomuona leo picha zake akiwa Mahakamani anafurahia sana kuwepo pale.

Akili kumkichwa.
Afadhali umetueleza mapema, tunaenda kufanya marejeo ya sheria na mashtaka yaweje
 
Nenda mahakamani kamtetee,hapa jf,utapoteza mda tu.Atatìa akili.
 
Issue ni No reforms, no election!

Lissu ameweza fikisha ujumbe kwa watu kwa njia ambayo hata lay man anaelewa.
Amezungumza ukweli mtupu!

Hii imewastua watu wasiopenda ukweli, wamempa hii kesi kumpunguza speed na kututoa kwenye hoja (No reforms,no election).

Tunapoendelea kumpambania Lissu nadhani hii hoja inahitaji kusukumwa zaidi na zaidi.

Tuungane kwenye maombi pia wa imani zote,Mungu alimuepusha TAL na risasi nyingi za moto, atampitisha na hapa salama!
 
Chukua nafasi yake,na wewe ukahutubie uwanjani,ukione cha moto.Mwenzako aliwaogopa Polisi,akaomba asikamatwe,aachwe alale uwanjani
 
Kwani kuozea jela kuna shida?

Makabulu walimfunga jela Mandela miaka 27 vipi Afrika Kusini haikukombolewa?

Wayahudi walimuua Yesu vipi Ukristo umekufa? kilitokea kitu gani baadae?
Atatia akili.Kachezea sharubu za simba
 
Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
Taifa lako na nani wewe mfia njaaa wa ushirombo ndani kabisa karibu na bukoli kuelekea segese Kuja mpaka kahama ukishukia dar!! Huna hata nyumba taifa utalitolea wapi!?
 
Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
Ni kama matendo waliotufanyia ccm na tume ya uchaguzi 2020 na 2024 hayana Afya kwa Taifa letu, mbona hii mko kimya wakati ndio kiini cha yote haya. let be fair once and for all.
 
In a nation, allegiance is primarily owed by its citizens to the state or government. This duty of loyalty and obedience is a core aspect of citizenship, where individuals are expected to support and uphold the laws and principles of their nation.

Citizenship is the legal status of belonging to a state, which implies a reciprocal relationship – the citizen owes allegiance to the state, and the state owes protection and rights to the citizen.

Allegiance signifies a duty of fidelity, loyalty, and obedience that citizens owe to their nation.

Scope of Allegiance:
Natural-born citizens owe natural allegiance to their nation, while naturalized citizens owe allegiance to their new country. Resident aliens also owe temporary allegiance to the country they are.
Hayo maneno yaliwahi kutamkwa na Mahakama ipi ya hapa Tanzania? Au chini ya kifungu kipi cha Sheria hasa Penal Code?
 
Back
Top Bottom