WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 8,437
- 8,136
Hilo tu ndilo mnaloliwezaAu siyo? Bila kutolewa Kisiasa kama Mwamba ataozea jela

Na mimi najiuliza sana hilo swaliKinachoshangaza haya yote yanatokea kuelekea Pasaka.
Kipindi Wakristo wanaadhimisha Mateso ya Bwana Yesu. Hawajui wanamtengenezea picha gani Tundu Lissu kwa Wakristo.
Kwani kuozea jela kuna shida?Au siyo? Bila kutolewa Kisiasa kama Mwamba ataozea jela
Ilikombolewa na nani? Si aliacha ujinga wake wa kuwatimua na kuchukua Mali zao ndio akaachwa?Kwani kuozea jela kuna shida?
Makabulu walimfunga jela Mandela miaka 27 vipi Afrika Kusini haikukombolewa?
Wayahudi walimuua Yesu vipi Ukristo umekufa? kilitokea kitu gani baadae?
Uzi unaongelea HATI ya mashtaka, wewe unaongelea KAULI.Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
Waswahili wanasema siku ya kufa nyani miti yote uteleza.
Msemo huu unaweza kuuchukulia kawaida ila kiukweli haya ndo yanayokikumba Chama cha Mapinduzi mwaka huu
Ukisoma hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu ya upande wa Jamhuri, kama wewe ni Mwanasheria uliyesoma Sheria na kuielewa vizuri utagundua kuwa kwa Hati ya Mashtaka ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu hakuna kosa lolote lililofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria kilichotajwa.
Tuende taratibu;
Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka ya Upande wa Jamhuri, Tundu Lissu ameshtakiwa kutenda kosa kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani Penal Code.
View attachment 3299593
Ukisoma maelezo ya kosa kwenye hati hiyo yanasema tarehe 3 April, 2025 katika Jiji la Dar es Salaam Tundu Lissu akiwa chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na nia ya kuushawishi umma wa Tanzania kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 aliitisha Serikali ya Tanzania kwa kutamka maneno kuwa,
"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"
Ukiachana na maelezo ya kosa kwenye hati ya mashtaka, Kifungu cha 39(2) (d) kilichotajwa kuvunjwa cha kanuni ya Adhabu kwa tafsiri ya kiswahili cha kawaida na kisheria kinasema hivi;
Mtu yeyote aliye chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye ndani ya Jamhuri au Nje ya Jamhuri anayetengeneza nia au kusababisha kuwepo kwa nia ya kushawishi, kufanya, kushauri kuwepo kwa vitendo vya kuitisha Serikali, Bunge au Mahakama na kuonesha nia hiyo kwa kutangaza au kuprint maandishi au maneno yoyote atakuwa na hatia ya kutenda kosa la Uhaini na atahukumiwa adhabu ya Kifo.
View attachment 3299594
Je kuna Uhusiano wa Maelezo ya Kosa na Kifungu cha Sheria kinachoanzisha kosa husika?
Ukisoma Kifungu cha 39(2) (d) utagundua kosa linalosemwa hapo lazima lifanywe na mtu mwenye kiapo cha Utii na pia ni lazima nia au kosa hilo lifanywe dhidi ya Moja ya Mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (Executive), Bunge (Legislature) au Mahakama( Judiciary)
Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025
Sitaki kujadili suala la Kiapo cha utii ambalo tayari limeshaelezwa na Mawakili wengi kupitia platforms mbalimbali ambalo kiuhalisia linamuondoa Lissu kuwa liable kufanya kosa chini ya Kifungu hicho. Mimi nitajikita kwenye hoja ngumu nyingine.
Ukisoma maelezo ya kosa , the fun thing maneno anayosema Tundu Lissu kama yalivyo kwenye hati ya Mashtaka hakuna sehemu yanaonekana akivitaja Serikali, Bunge au Mahakama. Hakuna sehemu ambayo yanaonesha amezilenga Serikali au Bunge au Mahakama. Yeye ameulenga Uchaguzi.
Lissu amesema watakichafua kwenye Uchaguzi, amesema tutazuia uchaguzi. amesema tutahamasisha uasi akihusianisha na Uchaguzi, Amesema wanaenda kuuvuruga Uchaguzi.
Kama Mwanasheria niliyepikwa na kupikika kwenye vyuo bora kabisa Duniani hasa The University of Westminster ( UK) niseme tu ukweli, kwa maelezo ya kosa yanavyoonekana kwenye hati ya Mashtaka hakuna kosa la Uhaini hapo. Serikali Mtaaibika vibaya sana Mahakamani.
Ushauri wangu kwa Watawala:
Kama nia ni kumuweka Lissu gerezani sawa mtafanikiwa kumuweka tu Gerezani ila hamtafanikiwa kuondoa spirit ya Mabadiliko ya Mifumo waliyopandikiza CHADEMA kwa wananchi.
Kama nia ni kuwatisha Wananchi sidhani kama Mtafanikiwa sana maana kwa ninavyowaona Watanzania siku msiyoijua Wanaenda kukinukisha kweli.
Mwisho kama nia yenu ni kumtisha Lissu, sioni akitishika maana kwa nilivyomuona leo picha zake akiwa Mahakamani anafurahia sana kuwepo pale.
Akili kumkichwa.
Kusema kweli Lisu anasema kama vile yeye ndiye anamiliki dolaUkiwa mwanasiasa inabidi uwe na akili zakukwepa mitego ya adui. Lissu anatumia mihemko ya uanaharakati kufanya siasa kitu ambacho kinamgharimu kijinga.
Mwenendo aliokuwa anaenda nao wenye akili wengi tulishaona na wengi waliandika humu kwamba atakamatwa.
Sasa kama wengine tunaona kabisa anaenda kukamatwa yeye hakuwa ana akili ya kuyaona haya? Labda chama kimemshinda akaona akitelekeze kwa kisingizio kwamba kawekwa gerezani na dikteta.
Tutapiga spana. Kwelikweli kuanzia alhamis kuu mpaka pasaka.Kinachoshangaza haya yote yanatokea kuelekea Pasaka.
Kipindi Wakristo wanaadhimisha Mateso ya Bwana Yesu. Hawajui wanamtengenezea picha gani Tundu Lissu kwa Wakristo.
That’s a possibility. Wananchi wamechoshwa na ccm hivyo any type of sabotage is plausible.Itakuwa mawakili wa serikali wamefanya makusudi ili kutoa loop holes, technicalities, indirect hawataki Lissu akutwe na hatia!!
Wewe upo kundi gani? Je hutamani kula keki za kisiasa??Wabongo wa siku hizi wanapeana kesi za uhaini kama kesi za nyanya vile. Nimeanza kuziona miaka mitatu au miwili iliyopita. Prosecutors wa leo, wanaleta utani na "Uhaini" sababu hawaujui, wengi wao ni watoto wa juzi tuu. Mapoti wengi wa leo, hata wale wenye vyeo vikubwa, wengi hawajapata kuushuhudia wala hawaujui uhaini wenyewe. 😁
Watu wengi wa juzi juzi hapa, hawajui uhaini ni nini, sababu hawajawahi uona wala kuushudia ukitendeka, maana ni siku nyingi uhaini wa kweli haujatokea nchi hii, toka enzi za Mchonga na akina Chipaka and Co na njama yao ile.
Ticha akajikuta Kigamboni toka hapo Soko la Samaki, nyumba kubwa, wanasema Ticha alikutwa nyumbani kwa mtu, choo cha udongo, nyumba ya makuti. akina Mahig* wakafanikiwa kuzima jaribio lile kisayansi, enzi medani ni medani kweli. Msilete utani wanasiasa. 😁
Kwamba ndo utamhukumu mtu kifo "Death Penalty" kwa uhaini upi hapo, Mtu anakulaje kitanzi kwa kuzungumza tuu upepo, bila njama, bila kitendo. Ni Hakimu/Jaji gani atamwaga wino mtu ale kitanzi kienyeji namna hiyo. Ndio maana wazungu waga wanatuona sisi "Hamnazo" 😁
Fanyeni siasa zenu zote wanasiasa, ila kuuwana, kupigana risasi na kupeana kesi za uhaini ni kama mnaleta utoto hivi, tunajua wote mnataka kula keki. Kuleni ila mtendeane vizuri. Wote mpo ili mle.
Nasikia wakwe zenu ndio watasimamia uchaguzi wenyewe huo. Kila la kheri wanasiasa, msiumizane. 😁
Wewe upo kundi gani? Je hutamani kula keki za kisiasa??
Umeelzezea vizuri sana ila kwa muktadha wa kuleta amani kwa kipindi hiki kueleka uchaguzi mkuu Lisu akae ndani atoke januari 2025Waswahili wanasema siku ya kufa nyani miti yote uteleza.
Msemo huu unaweza kuuchukulia kawaida ila kiukweli haya ndo yanayokikumba Chama cha Mapinduzi mwaka huu
Ukisoma hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu ya upande wa Jamhuri, kama wewe ni Mwanasheria uliyesoma Sheria na kuielewa vizuri utagundua kuwa kwa Hati ya Mashtaka ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu hakuna kosa lolote lililofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria kilichotajwa.
Tuende taratibu;
Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka ya Upande wa Jamhuri, Tundu Lissu ameshtakiwa kutenda kosa kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani Penal Code.
View attachment 3299593
Ukisoma maelezo ya kosa kwenye hati hiyo yanasema tarehe 3 April, 2025 katika Jiji la Dar es Salaam Tundu Lissu akiwa chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na nia ya kuushawishi umma wa Tanzania kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 aliitisha Serikali ya Tanzania kwa kutamka maneno kuwa,
"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"
Ukiachana na maelezo ya kosa kwenye hati ya mashtaka, Kifungu cha 39(2) (d) kilichotajwa kuvunjwa cha kanuni ya Adhabu kwa tafsiri ya kiswahili cha kawaida na kisheria kinasema hivi;
Mtu yeyote aliye chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye ndani ya Jamhuri au Nje ya Jamhuri anayetengeneza nia au kusababisha kuwepo kwa nia ya kushawishi, kufanya, kushauri kuwepo kwa vitendo vya kuitisha Serikali, Bunge au Mahakama na kuonesha nia hiyo kwa kutangaza au kuprint maandishi au maneno yoyote atakuwa na hatia ya kutenda kosa la Uhaini na atahukumiwa adhabu ya Kifo.
View attachment 3299594
Je kuna Uhusiano wa Maelezo ya Kosa na Kifungu cha Sheria kinachoanzisha kosa husika?
Ukisoma Kifungu cha 39(2) (d) utagundua kosa linalosemwa hapo lazima lifanywe na mtu mwenye kiapo cha Utii na pia ni lazima nia au kosa hilo lifanywe dhidi ya Moja ya Mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (Executive), Bunge (Legislature) au Mahakama( Judiciary)
Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025
Sitaki kujadili suala la Kiapo cha utii ambalo tayari limeshaelezwa na Mawakili wengi kupitia platforms mbalimbali ambalo kiuhalisia linamuondoa Lissu kuwa liable kufanya kosa chini ya Kifungu hicho. Mimi nitajikita kwenye hoja ngumu nyingine.
Ukisoma maelezo ya kosa , the fun thing maneno anayosema Tundu Lissu kama yalivyo kwenye hati ya Mashtaka hakuna sehemu yanaonekana akivitaja Serikali, Bunge au Mahakama. Hakuna sehemu ambayo yanaonesha amezilenga Serikali au Bunge au Mahakama. Yeye ameulenga Uchaguzi.
Lissu amesema watakichafua kwenye Uchaguzi, amesema tutazuia uchaguzi. amesema tutahamasisha uasi akihusianisha na Uchaguzi, Amesema wanaenda kuuvuruga Uchaguzi.
Kama Mwanasheria niliyepikwa na kupikika kwenye vyuo bora kabisa Duniani hasa The University of Westminster ( UK) niseme tu ukweli, kwa maelezo ya kosa yanavyoonekana kwenye hati ya Mashtaka hakuna kosa la Uhaini hapo. Serikali Mtaaibika vibaya sana Mahakamani.
Ushauri wangu kwa Watawala:
Kama nia ni kumuweka Lissu gerezani sawa mtafanikiwa kumuweka tu Gerezani ila hamtafanikiwa kuondoa spirit ya Mabadiliko ya Mifumo waliyopandikiza CHADEMA kwa wananchi.
Kama nia ni kuwatisha Wananchi sidhani kama Mtafanikiwa sana maana kwa ninavyowaona Watanzania siku msiyoijua Wanaenda kukinukisha kweli.
Mwisho kama nia yenu ni kumtisha Lissu, sioni akitishika maana kwa nilivyomuona leo picha zake akiwa Mahakamani anafurahia sana kuwepo pale.
Akili kumkichwa.
Hizo kauli sio uhaini we mbogamboga.Labda wangeita uchochezi.Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
atanyea ndoo hadi uchaguzi upiteKuchambua kesi za hivi kisheria au kivyovyote ni matumizi mabaya kabisa ya muda.
Haipo kesi hapa!
Au hata zile za uhaini za kina Mwabukusi Dk Slaa, Mdude au Mwamba ziliishia wapi?
Hawa ni wa kuwajuza kumwachia TAL Tena bila masharti yoyote!
Tlaatlaah, Lucas Mwashambwa na wale wengine:
Figisu zote Kwa Lissu ni kama kumpiga chura teke!
By the way: "Figisu zozote dhidi ya Lissu mbona ndiyo political mileage muhimu zaidi kwake?"
Baada ya kumsikiliza TAL usikilize MOYO wako na USISIKILIZE TUMBO lako.........Kama wewe unakula kupitia uchawa bora ukae kimya....Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
Haina SHIDA hata Mandela alikuwa hivyohivyo.................atanyea ndoo hadi uchaguzi upite
Achana nae nzi wa kijani huyu.Wat
Uzi unaongelea HATI ya mashtaka, wewe unaongelea KAULI.
Kwamba wewe matungunya una akili na kuijua sheria kumzidi Lissu? Uliona nini kama si ujinga na kujitia ujuajiUkiwa mwanasiasa inabidi uwe na akili zakukwepa mitego ya adui. Lissu anatumia mihemko ya uanaharakati kufanya siasa kitu ambacho kinamgharimu kijinga.
Mwenendo aliokuwa anaenda nao wenye akili wengi tulishaona na wengi waliandika humu kwamba atakamatwa.
Sasa kama wengine tunaona kabisa anaenda kukamatwa yeye hakuwa ana akili ya kuyaona haya? Labda chama kimemshinda akaona akitelekeze kwa kisingizio kwamba kawekwa gerezani na dikteta.
atanyea ndoo hadi uchaguzi upite
atanyea ndoo hadi uchaguzi upite
Nia ovu huwa hazitokei kwa bahati mbaya, mwizi hupanga kuiba mapema kabla ya tendo la wizi, Taifa line bahati sana,mungu ametenda!Baada ya kumsikiliza TAL usikilize MOYO wako na USISIKILIZE TUMBO lako.........Kama wewe unakula kupitia uchawa bora ukae kimya....