Wataaibika vibaya sana.Policcm wanatia aibu yaani mtu ni mwanasiasa wanamchagulia aseme nini?
Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
MUNGU ATAAMUA.....
MUNGU ANA NAMNA PEKEE YA KUAMUA KESI KAMA HIZI......KIPANDE KIDOGO CHA ARDHI KITAWEKWA TUTA LA KUMBU KUMBU YA KUDUMU ZA BAADHI YA MASHETANI WALIOJIVISHA UBINADAMU NA KUWAFANYIA USHETANI BINADAMU........
MUNGU ATAAMUA......
Kosa hili lilitungwa kuwalenga watu wanaohudumu katika vyombo vya ulinzi na usalama.Ni nini maana ya Kiapo cha utii? Na ni nani hao wenye viapo vya utii? Samahani naomba ufafanuzi
Hapo sasa.CCM sijui huwa wanatumia nini kufikiri.Kauli za Lissu hazina Afya kivipi? Waliokata Wagombea 12,000 wa Chadema Uchaguzi wa Mitaa na Vijiji Novemba mwaka jana tuseme wao ndo wana afya kwa Taifa letu?
Ni mwanachama Malaya Malaya tu ndiye anayeogopa kukamatwa akiongea ukweli na ndio maana siasa nyingi zinakuwaga za msimu kwa kuwa wanaogopa kukamatwa. Hebu fikiria waasisi wa nchi nyingi za Afrika wangeogopa kusema ukweli tungekuwa wapi Leo? Acha kujifanya hamnazo weweUkiwa mwanasiasa inabidi uwe na akili zakukwepa mitego ya adui. Lissu anatumia mihemko ya uanaharakati kufanya siasa kitu ambacho kinamgharimu kijinga.
Mwenendo aliokuwa anaenda nao wenye akili wengi tulishaona na wengi waliandika humu kwamba atakamatwa.
Sasa kama wengine tunaona kabisa anaenda kukamatwa yeye hakuwa ana akili ya kuyaona haya? Labda chama kimemshinda akaona akitelekeze kwa kisingizio kwamba kawekwa gerezani na dikteta.
Ujumbe mzuri na wenye afya,asante.Wabongo wa siku hizi wanapeana kesi za uhaini kama kesi za nyanya vile. Nimeanza kuziona miaka mitatu au miwili iliyopita. Prosecutors wa leo, wanaleta utani na "Uhaini" sababu hawaujui, wengi wao ni watoto wa juzi tuu. Mapoti wengi wa leo, hata wale wenye vyeo vikubwa, wengi hawajapata kuushuhudia wala hawaujui uhaini wenyewe. 😁
Watu wengi wa juzi juzi hapa, hawajui uhaini ni nini, sababu hawajawahi uona wala kuushudia ukitendeka, maana ni siku nyingi uhaini wa kweli haujatokea nchi hii, toka enzi za Mchonga na akina Chipaka and Co na njama yao ile.
Ticha akajikuta Kigamboni toka hapo Soko la Samaki, nyumba kubwa, wanasema Ticha alikutwa nyumbani kwa mtu, choo cha udongo, nyumba ya makuti. akina Mahig* wakafanikiwa kuzima jaribio lile kisayansi, enzi medani ni medani kweli. Msilete utani wanasiasa. 😁
Kwamba ndo utamhukumu mtu kifo "Death Penalty" kwa uhaini upi hapo, Mtu anakulaje kitanzi kwa kuzungumza tuu upepo, bila njama, bila kitendo. Ni Hakimu/Jaji gani atamwaga wino mtu ale kitanzi kienyeji namna hiyo. Ndio maana wazungu waga wanatuona sisi "Hamnazo" 😁
Fanyeni siasa zenu zote wanasiasa, ila kuuwana, kupigana risasi na kupeana kesi za uhaini ni kama mnaleta utoto hivi, tunajua wote mnataka kula keki. Kuleni ila mtendeane vizuri. Wote mpo ili mle.
Nasikia wakwe zenu ndio watasimamia uchaguzi wenyewe huo. Kila la kheri wanasiasa, msiumizane. 😁
Alitiachia huu upuuzi
Sante sana kwa ufafanuzi mzuri.In Tanzania, treason is considered one of the most serious criminal offenses and is addressed under the Penal Code, specifically Sections 39 to 41. Conviction for treason requires proof of specific elements, and the standard of proof is very high due to the gravity of the offense.
📜 Legal Elements for Treason Conviction in Tanzania
Under the Tanzanian Penal Code (Cap. 16), the following elements must generally be proven to secure a conviction for treason:
1. Acts Against the Sovereign or Government
The accused must have committed an act that:
- Levy war against the United Republic, or
- Intends to overthrow the lawful government by use of force or violence,
- Assists enemies of Tanzania during war (whether foreign or internal enemies),
- Conspires or attempts to do any of the above.
2. Intention (Mens Rea)
The prosecution must prove that the accused had the intention to:
- Endanger the sovereignty or integrity of the United Republic,
- Undermine or overthrow the lawful government,
- Aid enemies knowingly and willfully.
→ Mere criticism of the government does not amount to treason unless it's coupled with violent or seditious acts.
3. Overt Act
There must be an overt act—a concrete step that demonstrates the treasonous intent. This can include:
- Armed rebellion,
- Espionage,
- Attempted coup,
- Providing support to enemies.
→ Under Tanzanian law, two witnesses are typically required to prove the overt act, similar to common law standards.
4. Jurisdictional Nexus
The offense must have taken place within Tanzania, or if committed abroad, it must have had direct implications for the security or sovereignty of the state.
🧑⚖️ Penalties for Treason in Tanzania:
- Treason is punishable by death under Tanzanian law (Section 39 of the Penal Code).
- This makes it one of the few offenses in Tanzania where the death penalty is mandatory upon conviction.
Waambieni polisi vilaza wasiojua hata PGO yao kwamba haya ndio mambo wanayotakiwa kuprove kuthibitisha treason!
Hakika
Za Makala zina afya ama?Watu wasijitoe ufahamu, zipo kauli ambazo lissu amezizungumza kwa mdomo wake ambazo hazina afya kwa taifa letu, let be fair!
CHAMWINO.Hivi kesi za uhaini za Mwabukusi, Dk. Slaa au Mwamba ziliishia wapi?
Hata Polisi aina ya ukamataji waliyofanya ni makusudi ili kuonyesha jinsi serikali na CCM inatumia vibaya vyombo vya dola kuukabili upinzani. Mabomu na risasi za moto zilizotumika kwenye umati mkubwa watu vile zingeweza kuleta maafa makubwa. Wananchi wale walishahamaki na kumwambia Lissu asitii amri ya Polisi, ina maana Lissu angewaambia wale wananchi waanze kukabiliana na Polisi hali ingekuwa mbaya sana maana walikuwa tayari kwa lolote. Picha za mabomu yale zimetapakaa duniani kote hivyo kuthibitisha madai ya Chadema kuwa CCM inatumia vibaya jeshi la polisi kuinufaisha nyakati za uchaguzi.Itakuwa mawakili wa serikali wamefanya makusudi ili kutoa loop holes, technicalities, indirect hawataki Lissu akutwe na hatia!!
Subiria kesi ianze kuunguruma,achana na bettingWaswahili wanasema siku ya kufa nyani miti yote uteleza.
Msemo huu unaweza kuuchukulia kawaida ila kiukweli haya ndo yanayokikumba Chama cha Mapinduzi mwaka huu
Ukisoma hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu ya upande wa Jamhuri, kama wewe ni Mwanasheria uliyesoma Sheria na kuielewa vizuri utagundua kuwa kwa Hati ya Mashtaka ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu hakuna kosa lolote lililofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria kilichotajwa.
Tuende taratibu;
Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka ya Upande wa Jamhuri, Tundu Lissu ameshtakiwa kutenda kosa kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani Penal Code.
View attachment 3299593
Ukisoma maelezo ya kosa kwenye hati hiyo yanasema tarehe 3 April, 2025 katika Jiji la Dar es Salaam Tundu Lissu akiwa chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na nia ya kuushawishi umma wa Tanzania kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 aliitisha Serikali ya Tanzania kwa kutamka maneno kuwa,
"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"
Ukiachana na maelezo ya kosa kwenye hati ya mashtaka, Kifungu cha 39(2) (d) kilichotajwa kuvunjwa cha kanuni ya Adhabu kwa tafsiri ya kiswahili cha kawaida na kisheria kinasema hivi;
Mtu yeyote aliye chini ya kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye ndani ya Jamhuri au Nje ya Jamhuri anayetengeneza nia au kusababisha kuwepo kwa nia ya kushawishi, kufanya, kushauri kuwepo kwa vitendo vya kuitisha Serikali, Bunge au Mahakama na kuonesha nia hiyo kwa kutangaza au kuprint maandishi au maneno yoyote atakuwa na hatia ya kutenda kosa la Uhaini na atahukumiwa adhabu ya Kifo.
View attachment 3299594
Je kuna Uhusiano wa Maelezo ya Kosa na Kifungu cha Sheria kinachoanzisha kosa husika?
Ukisoma Kifungu cha 39(2) (d) utagundua kosa linalosemwa hapo lazima lifanywe na mtu mwenye kiapo cha Utii na pia ni lazima nia au kosa hilo lifanywe dhidi ya Moja ya Mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (Executive), Bunge (Legislature) au Mahakama( Judiciary)
Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025
Sitaki kujadili suala la Kiapo cha utii ambalo tayari limeshaelezwa na Mawakili wengi kupitia platforms mbalimbali ambalo kiuhalisia linamuondoa Lissu kuwa liable kufanya kosa chini ya Kifungu hicho. Mimi nitajikita kwenye hoja ngumu nyingine.
Ukisoma maelezo ya kosa , the fun thing maneno anayosema Tundu Lissu kama yalivyo kwenye hati ya Mashtaka hakuna sehemu yanaonekana akivitaja Serikali, Bunge au Mahakama. Hakuna sehemu ambayo yanaonesha amezilenga Serikali au Bunge au Mahakama. Yeye ameulenga Uchaguzi.
Lissu amesema watakichafua kwenye Uchaguzi, amesema tutazuia uchaguzi. amesema tutahamasisha uasi akihusianisha na Uchaguzi, Amesema wanaenda kuuvuruga Uchaguzi.
Kama Mwanasheria niliyepikwa na kupikika kwenye vyuo bora kabisa Duniani hasa The University of Westminster ( UK) niseme tu ukweli, kwa maelezo ya kosa yanavyoonekana kwenye hati ya Mashtaka hakuna kosa la Uhaini hapo. Serikali Mtaaibika vibaya sana Mahakamani.
Ushauri wangu kwa Watawala:
Kama nia ni kumuweka Lissu gerezani sawa mtafanikiwa kumuweka tu Gerezani ila hamtafanikiwa kuondoa spirit ya Mabadiliko ya Mifumo waliyopandikiza CHADEMA kwa wananchi.
Kama nia ni kuwatisha Wananchi sidhani kama Mtafanikiwa sana maana kwa ninavyowaona Watanzania siku msiyoijua Wanaenda kukinukisha kweli.
Mwisho kama nia yenu ni kumtisha Lissu, sioni akitishika maana kwa nilivyomuona leo picha zake akiwa Mahakamani anafurahia sana kuwepo pale.
Akili kumkichwa.
Subiria kesi ianze kuunguruma,achana na betting
View: https://www.instagram.com/reel/DITCT-ngPiK/?igsh=cWxiZ2htcDdneTli
Au siyo? Bila kutolewa Kisiasa kama Mwamba ataozea jelaMnaenda kuaibika tu na kujidhalilisha Mahakamani na hiyo kesi yenu ya kubumba.