Uchambuzi wa Mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai

Wakati mwingine naumia wakati mwingine Naona Ni sawa. Maana wazawa wakipewa hawawezi endesha. Ni upigaji na fitina kwa waagiza mizigo ambao fulani anauuza. Yaani mtu akawahonga ukija mwingine na mzigo Kama unapigwa Kodi so utauza Bei ya juu mwenzako anauza ya chini so anashika soko.
Pia waafrika nadhani uchumi tuwachie hao jamaa weupe. Cheki sauzi wazungu walibaki cheki iko juu kiuchumi. Mugabe akafukuza wazungu cheki kilichotokea.
Angalia Angola huko raisi na mwanae binti wakaibia nchi utajiri wote.
Mifano Ni mingi tukianza kuchambua. Waza hata reli,tanesco ,atcl tumeshashindwa. Hii nchi ama afrika yote ilitakiwa iwe na akina jpm,Sankara,gadafi,sokoine,etc ili isonge mbele tukishakuwa na maendeleo ndio turuhusu demokrasia hata wanaotaka kuolewa waolewe wawe gay okay. Watu wanadhani maendeleo yanakuja kiulaini kwa kubembelezana. Rudi huko nyuma hata USA , German,France,Spain,Russia,China Kuna watu walikufa waliuwa so wapo walipo na ndio Mana ukienda kwao wanakucheki ulivyoshindwa kujenga kwako
 
Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.

Mamvunbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa. Imeuzwa kupelekwa wapi?

Genge la Msoga kama kawaida yenu...

Kipara hii dhambi itakutafuna Sana

Hii deal tangu last year ishakuwa matured

Kipara kama kipara... Unaupiga Mwingi Sana....
 
Genge la Msoga kama kawaida yenu

Kipara hii dhabi itakutafuna Sana

Hii deal tangu last year ishakuwa matured

Kipara kama kipara... Unaupiga Mwingi Sana....
Hilo lisikupe shida, toka mama alipoenda Dubai lilikuwa tayari.

Halihusishi Bandari ya Dar tu. Bandari zote na mifumo yake.

Nyinyi kaeni mnalalamika bandari inapoteza mapato kila kukicha. Mama kapata Mwarubaini wake.

Ndanib ya miezi mitatu toka wakiabidhiwa rasmi tutaona bandari inavyo kuza uchumi wetu.
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

Moja , ni mkataba wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) zake hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.

Pili, mkataba huu unanguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa ( Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23( 4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa ( material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke ( fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.

Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23( 4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea( coup de sac) .

Tatu , mawanda ( scope ) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa logistic parks na trade corridors ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

Nne , mkataba hausemi sisi tutapata nini( consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

Tano , mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari( TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.

Sita , pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye ibara 13( 2) ibara hiyo haina maana yoyote Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba threshold ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.

Pili hata procurement( manunuzi) ya vitu au items au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa ibara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) yoyote hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama( safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

Saba , mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

Nane , pamoja na kwamba ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu reservation utagundua kwa namna ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya reservation iliyopo kwenye ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya reservation kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya reservation Sasa ivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

Tisa , hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda.

Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

Kumi , kwa mujibu wa ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhu Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania.

Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata derivative rights badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa lease hold.
Buriani bandari, buriani TRA, buriani TPA bila kusahau usalama wa nchi yetu. Tumeuzwa mchana kweupeee
 
Kwa maana hiyo huu mkataba haupishani sana na ule kati ya Mangungu wa Msowero na Wajerumani
Historia Ina tabia ya kujirudia hasa wanaoisoma wakiiita SoMo la kike🤣🤣🤣🤣
Nchi inauzwa mbele ya macho yetu siye wasomi uchwara😭
 
Weka mkataba kamili mbona unaweka vipande vipande tu?
 
Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.

Mambumbumbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa.

Imeuzwa kupelekwa wapi?
Uzeni pote maana mmepata wasaa wakutawala wajinga watanzania. Wataandamana siku wakisikia Simba au Yanga zimeuzwa sio bandari wala mbuga za wanyama.
 
Mnaingizwa mkenge na nketa mada na nyinyi mnauvaa kichwa kichwa, Mleta mada ameleta vipande tu vya mkataba na kuwalisha maoni yake.

Aweke mkataba kamili.

Huyu ni wale wale tu, kina ndugai na bashiru.
Umesoma mkataba?
 
Back
Top Bottom