Uchambuzi wa Mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai

Uchambuzi wa Mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kati ya Tanzania na Dubai

MAMBO YASIYOFAA KABISA MKATABA WA BANDARI.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

1. TANZANIA HAIRUHUSIWI KUJITOA KWENYE MKATABA

Ibara ya 23(4) ya mkataba huo inakataza wahusika wa mkataba ambao ni serikali ya Tanzania na Kampuni mwekezaji DPW kujitoa(Denounce) katika mkataba, Kuvunja, Kuahirisha(suspend), au Kusitisha(terminate).

Na ni masikitiko sana kuwa ibara hii imesisitiza kuwa haturuhusiwi kujitoa kwenye mkataba huu hata kama kuna ukiukwaji mkubwa wa masharti(Material Breach), hata kama kuna mabadiliko makubwa ya kimazingira katika utekelezaji wa mkataba(fundamental change of circumstances), hata kama kuna mgogoro mkubwa wa kidiplomasia(severe diplomatic/condular dispute), au sababu zo,ote zile zinazotambulika na sheria za kimataifa.

Maneno haya yameandikwa hivihivi kwenye huo mkataba. Si mlisema ule Fei toto, sasa upo huu mbele yenu.

2. MKATABA HAUNA MUDA

Ibara ya 23 ya mkataba inasema kuwa ukomo wa mkataba huu ni mpaka shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika. Maneno haya yameandikwa hivihivi.

Serikali inawajibika kutoa maelezo kuhusu hili. Katika sheria hakuna mkataba usio na muda isipokuwa mkataba wa kuuza au kununua tu.

Ukimuuzia mtu kitu haumwambii tumia mpaka muda fulani, ni moja kwa moja. Je na huu mkataba ni hivyo ??.

3. MIGOGORO KUHUSU MRADI KUTATULIWA AFRIKA KUSINI.

Ibara ya 20 ya mkataba inasema migogoro kuhusu mkataba wa mradi utatatuliwa Johannesburg Afrika Kusini na Sheria itakayotumika ni sheria za umoja wa mataifa UNICITRAL Arbitration Rules.

Kumbuka mwaka 2017 tulitunga sheria yetu kwa ajili ya kulinda rasimali zetu.

Katika sheria hii The Natural Wealth and Resources , Parmanent Sovereignty Act 2017, tuliweka wazi katika kifungu cha 11 kuwa Migogoro yoye inayohusu Rasilimali za Taifa hili itatatuliwa na vyombo vya hapa nchini kwa sheria zetu.

Na hiii ilikuja baada ya kuonekana hawa wanaojiita wawekezaji wanatunyonya kisha tukilalamika wanatuburuza kwenye vyombo vyao tena kwa sheria zao.

Unamshitaki mtu kwenye mahakama yake mwenyewe kwa kutumia sheria alizotunga yeye mwenyewe, halafu unategemea upate haki.

Tulitunga sheria hii kujikomboa na huu ukoloni. Mkataba huu sasa unataka kuturudisha huko.

4. TANZANIA HAINA MAMLAKA YA KUTAIFISHA MALI ZA MWEKEZAJI.

Ibara ya 14 ya mkataba inakataa kabisa Serikali ya Tanzania kutaifisha mali yoyote ya mwekezaji.

Yaani hakuna sababu yoyote iwe ya kimadai au kijinai itakayoifanya serikali itaifishe mali ya mwekezaji.

Mnajua kuwa suala la kutaifisha lipo kisheria hasa inapothibitika jinai. Lakini hii si kwa mwekezaji wa Bandari.

Ibara hii inasisitiza kuwa endapo itatokea mali zao kutaifishwa na serikali basi fidia na stahiki ya kuridhisha italipwa na serikali. Neno STAHIKI YA KURIDHISHA limetumika hivyohivyo kwenye mkataba.

Hatujui hiyo ya kuridhisha itakuwa ni kiasi gani lakini limeandikwa hivyohivyo.

5. KUTUNGA SHERIA MPYA.

Ibara ya 27 inasema baada ya mkataba kusainiwa Tanzania haitakuwa na mamlaka ya kutunga sheria, kanuni mpya ambayo itapingana na mkataba.

Tafsiri yake, kama mna marekebisho yenu ya kikodi, sera pengine kutokana namabadiliko na mda kupita hamtaruhusiwa.

Uchambuzi utaendelea.
 
Mnainguzwa mjenge. Na. Mleta mada aliyeleta vipande tu vya mkataba na kuwalisha maoni yake.

Aweke mkataba kamili.

Huyu ni wale wale tu, kina ndugai na bashiru.
Watu wamerukia article ya 23 kuhusu termination wakaacha articles za awali kuhusu jinsi miradi iliopo kwenye makubaliano itakavoendeshwa.

Kila mradi utakuwa agreements (Host Government Agreements) zake. Nafasi ya TPA kama muakilishi wa serikali kwa upande wa Tanzania ni kusimamia hizi agreements za kila mradi ziwe ni kwa muda gani.
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote...
Hawa wabunge "viazi ulaya vya CCM" walioko Dodoma wana akili kweli za kuweza kusoma na kuyaona au wanakwenda kesema tu " ndiyooooooo upite?"

Hii bila shaka yoyote ni deal la viongozi wa serikali na CCM kwa sababu katika hali hii hakuna namna unayoweza kuu - describe mkatba huu kama kweli hivi ndivyo ulivyo...
 
Naona Yale mapumziko ya Pasaka Dubai yamezaa matunda machungu kwa Watanzania. Dah!
 
Mnainguzwa mjenge. Na. Mleta mada aliyeleta vipande tu vya mkataba na kuwalisha maoni yake.

Aweke mkataba kamili.

Huyu ni wale wale tu, kina ndugai na bashiru.
Hata kama hajaleta vyote hivi alivyoleta tu vinafanya hata hivyo alivyoacha visiwe na maana yoyote ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

Moja , ni mkataba wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) zake hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.

Pili, mkataba huu unanguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa (Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23( 4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa (material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke (fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.


Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23( 4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea( coup de sac) .

Tatu, mawanda (scope) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa (logistic parks na trade corridors) ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

Nne, mkataba hausemi sisi tutapata nini( consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

Tano , mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari( TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.


Sita, pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye ibara 13( 2) ibara hiyo haina maana yoyote Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba threshold ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.

Pili hata procurement( manunuzi) ya vitu au items au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa ibara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) yoyote hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama( safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

Saba, mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

Nane , pamoja na kwamba ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu reservation utagundua kwa namna ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya reservation iliyopo kwenye ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya reservation kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya reservation Sasa ivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

Tisa, hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda.

Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

Kumi, kwa mujibu wa ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhu Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania.

Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata derivative rights badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa lease hold.
 
Waliokuwa wanaingia haya si wapo? Kwani Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakutoa Ushauri wa kisheria?

Hao walioingia huu mkataba walijiridhisha na Nchi zingine ndivyo mikataba Yao Iko?

Mwisho kwani hii mikataba Huwa Watzn wanaoambatana na Rais Huwa hawasomi kabla ya kumshauri Rais kusaini?
Raisi na yeye anasaini bila kusoma?
 
Acha udini we ajuza.Unamtetea mtu eti kisa Muislam na wale waarabu.Ungekuwa karibu yangu ningekuzaba vibao.
Naona umekosa hoja umekimbilia kwenye dini.

Naam, 1mimi ni Muislam na nnaupenda sana Uislam wangu, elewa kwamba Muislam ni ndugu ya Muislam.

Elewa pia kuwa Uislam ni dini pekee duniani inayofundisha kuwa hakuna kulazimishana katika dini na Uislam pekee ndiyo unafundisha haki kwa wote.

Muislam au asiye Muislam mradi yupo kwenye haki basi uislam unanifundisha niamue na nitende haki kwa wote.

Kwa kukutebdea haki thagane wapi ili uje kunizaba hilo kofi lako, hutothubutu hata kunyanyuwa kidole chako wacha mkono. kitachokukuta uje kukihadithia JF. Usijifanye u hodari nyuma ya keyboard. Hii ni open challenge.

Ficha upumbavu wako usifiche hekima zako - courtesy Max wa JF.
 
every progress made for the last 5 years all destroyed in few years, by 2025, there won't be a country no more.




Screenshot_20230608_013810_Samsung Internet.jpg
 
Raisi na yeye anasaini bila kusoma?
Acha mzaha Rais anaweza soma mavifungu yote hayo yenye lugha za kisheria ,hata akisoma ataelewa? Hata wewe hapo kama sio Mwanasheria hakuna unachoelewa,Ndio maana kuna wasaidizi..

Unless useme hivi aliambiwa ukweli na kama alijadiliana na Waarabu wakakubaliana hapo ni sawa..

Kwa sababu kama alidanganywa mda huu angeshakuwa amewaweka korokoloni wahusika ila Kwa kuwa alikuwa ndio maana Yuko kimya..

Kwa staili hii nadhani Kila mtu apiganie maslahi yake ,inakera sana
 
Huu mkataba unaiingiza rasmi Tanzania kwenye biashara za Kimataifa.

Wenye uelewa wa biashara za Kimataifa watalielewa hilo.


Mambumbumbu wa biashara mtabaki bandari imeuzwa, imeuzwa.

Imeuzwa kupelekwa wapi?
Sahihi kbs ✔️
 
Mh Rais watu hawa wamekulisha tango pori tafadhali msiuze bandari yetu ...Hata ile miaka mia ni nafuu mana mkataba unasema ukiingia hakuna kujitoa sasa ina maana ni milele tumeuza bandari...Baadae mtumie huo huo mkataba kwamba tutashitakiwa ndege zitakamatwa yaani hili ni janga
 
Halafu huyu mama siku hizi kaja na staili wa role model wake, JK...kuweka pamba masikioni.
Hili nalo litapita, mambo ya kiswahili kabisa haya
 
Hata Kama Ni mikataba iwe na xrenewvterms za miaka walau kumi
 
Back
Top Bottom