Uchawa unadumaza maendeleo ya nchi, unalinda ufisadi na kubariki kutokuwajibika. Taifa linaangamia

Uchawa unadumaza maendeleo ya nchi, unalinda ufisadi na kubariki kutokuwajibika. Taifa linaangamia

Huwez kuongoza nchi bila chawa we kilaza
 
Kuna ajira mpya ya kisiasa imezuka katika Taifa letu nayo inaitwa uchawa.

Uchawa ni kitendo cha kuwa mfuasi kindaki ndaki wa mtu kwa matendo na kauli zake bila kujali uhalali wa kile kinachofanywa.

Mtu huyo anaweza kuwa Kiongozi mkuu wa nchi au mwanasiasa yeyote mwenye ushawishi.

Kiongozi mwenye dhamana ya kuliongoza Taifa anao wajibu wa kikatiba kulinda maslahi ya watu wake hivyo inategemewa kwamba kila anachokifanya maslahi ya uma yanapewa kipaumbele.

Ila inapotokea kiongozi huyo akakengeuka katika maamuzi yake basi kwa mifumo ya kiutawala tuliyonayo wananchi wana haki ya kumkumbusha wajibu wake.

Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na nafasi za kukosoana na kushauriana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alituasa vijana tuwe na hulka ya kuhoji , kwamba pale tunapoona kuna jambo linafanyika na tunaamini linafanyika sio kwa maslahi yetu ya Taifa basi tunapaswa kuhoji.

Hali sasa ni tofauti kabisa, kizazi cha kuhoji kinapotea na ni kama hakipo kabisa kwani watu wamegeuka wabinafsi na kuangalia maslahi yao binafsi.

Kijana anaona kuliko kuhoji na kukosa fursa kwa kuonekana mtukutu bora akubaliane na kila jambo la nwanasiasa au kiongozi wa kitaifa ili akumbukwe kwa favours mbali mbali wanaita kulamba asali.

Kitendo hiki kina faida za muda mfupi ila hasara kwa muda mrefu wa vizazi vijavyo kwani kunauwezekano wa matendo ya wanasiasa kuwa ya kuliangamiza Taifa.

Kijana au mtu mwingine yeyote anapamua kuwa chawa anashiriki kuliangamiza Taifa lake kwani kiongozi husika hatakuwa na woga wa kufanya jambo lolote kwani anajua hakuna wa kumhoji kwa lolote.

Hivyo basi ni vyema tukaondoa dhana hii ya uchawa kwani inaliangamiza Taifa.
Mbona hata wewe ni chawa tu
 
Sifa zimezidi.

Ukisikiliza hotuba za wanasiasa ni kusifu tuu kila kitu.

Sijui wana mpango gani na Taifa hili??

Sijui vizazi vijavyo watatuona vipi kwa Tabia hizi za ajabu kabisa.
JPM aliabudiwa kabisa

Mwandri alisema Mungu amshukuru kwa kazi anazozifanya

Kangi akasema jpm ni Yesu

Kuna fala wa uv-ccm akasema miujiza ya jpm inaizidi ya Yesu kwa mbali sana

Kuna diwani kanda ya ziwa huko akasema jpm ni Mungu wa Tanzania

Wakati huo hamkuyaona ndio mnayaona leo!

Tz ndio nchi inaongoza kwa unafki duniani
 
Kwanini unaona uchawa wa sasa hivi ni mbaya kuliko uchawa wa kipindi cha mwendazake?.Au kwavile sio zamu yako kulamba asali.Kipindi ambacho wewe ulikua mfuasi wa mtu hukuona kama hicho kitendo ni kibaya,au kwavile aliyepo sasa huna maslahi naye ndo unaibuka na hoja yakujifanya huupendi uchawa.Siku tutakayoamua kuacha unafiki na kuamua kusimama na nchi badala ya mtu ndio siku tutakayoanza kupiga hatua yakulisaidia hili taifa.sasa hivi watu bado wanapokezana kulamba asali.
Wazalendo uchwara
 
JPM aliabudiwa kabisa

Mwandri alisema Mungu amshukuru kwa kazi anazozifanya

Kangi akasema jpm ni Yesu

Kuna fala wa uv-ccm akasema miujiza ya jpm inaizidi ya Yesu kwa mbali sana

Kuna diwani kanda ya ziwa huko akasema jpm ni Mungu wa Tanzania

Wakati huo hamkuyaona ndio mnayaona leo!

Tz ndio nchi inaongoza kwa unafki duniani
Hawa wanaolalamika uchawa, ndio hao walikuwa chawa max pro awamu ya jpm. Walimuabudu mpaka wakakufuru.

Sasa waliemuabudu hayupo, kaja bosi mwingine na chawa wake. Halaf wanalalamika chawa as if wao hawakuwa chawa miez kadhaa iliyopita?
 
Nimerudia kusoma hoja iliyoko mezani lakini sijaona mahali ambapo mtoa hoja amesema kwamba awamu hii ndiyo awamu pekee yenye chawa. Anzisha na wewe uzi wako utakaojikita kwenye uchawa uliokuwepo wakati wa awamu fulani utakayoichagua!
 
JPM aliabudiwa kabisa

Mwandri alisema Mungu amshukuru kwa kazi anazozifanya

Kangi akasema jpm ni Yesu

Kuna fala wa uv-ccm akasema miujiza ya jpm inaizidi ya Yesu kwa mbali sana

Kuna diwani kanda ya ziwa huko akasema jpm ni Mungu wa Tanzania

Wakati huo hamkuyaona ndio mnayaona leo!

Tz ndio nchi inaongoza kwa unafki duniani

Nakuona Chawa nyemelezi at work
 
Machawa kwa kisayansi tunawaita Parasites. Scientists know what I mean
 
Back
Top Bottom