Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kiranga humuwezi bora ukae kimya
Nimemuuliza mtu.

Nimemuambia hivi.

Babu zetu waliokuwa hawajui umeme, redio, kutabiri kupatwa kwa jua etc, walipokutana na watu kutoka Ulaya, waliojua vitu hivi, waliwaona watu hawa wachawi. Waliwaona "mizungu".

Ukichukua neno "mzungu" ukiondoa herufi z unapata neno "mungu".

Waliwaona wana nguvu za kichawi.

Kwa sababu hawakuelewa sayansi na teknolojia.

Ungewachukua hawa babu zetu kutoka miaka 140 iliyopita, ukawaweka leo na kuwaonesha tunavyowasiliana kwenye internet, mpaka kwa videocalls, wangesema ni uchawi.

Sasa na hawa watu wanaosema wameona uchawi leo, wanajuaje hawajakutana na vitu wasivyovijua tu, lakini ambavyo si uchawi?

Mpaka sasa sijajibiwa.
 
Itoshe tu kusema wewe bado mtoto.
 
Wapo wanaopinga ndio lakini kusema Dunia ya kwanza hawaamini hivi vitu si kweli, mabara yote, jamii zote hivi vitu vipo
-ukienda kwa wagiriki utakutana na Hades na wafuasi wake
-ukienda Norse na Germanic mythology utaikutana na Hel
-ukienda Hinduism na Buddhism Kuna Kali, Asura na Rakshasa na wafuasi wake

Pitia hapa Kuna mamia kama sio maelfu ya Demons wakielezewa kwa jamii tofauti tofauti za watu Duniani.

 
Wenzetu nchi zilizoendelea wamegundua na kuandika kuhusu magonjwa ya akili mengi sana.

Mara schizophrenia, mara multiple personality disorder.

Huku Afrika tunajua kichaa tu, mpaka mtu aokote makopo.

Hawa wagonjwa wa magonjwa mengine haya huko Africa hawapo?

Na tunajua vipi kama wapo na wanaona mauzauza wasiyoyaelewa, na katika kutoyaelewa mauzauza hayo, na kukosa uaguzi wa magonjwa yao ya akili, wanayapa mauzauza hayo jina rahisi la "uchawi" ?
 
Kua uyaone mwanangu!

Nakumbuka huu msemo mama yangu alipenda kuniambia sana tukiwa tunaota moto jikoni.
 
Ajabu vitu huvijui una vikanisha.

Nani alikwambia ya kuwa uwepo wa kitu mpaka ukione ?
 
Hakuna ushahidi wa kisayansi na kimantiki kwamba kuna uchawi.

Kuna hadithi nyingi na habari nyingi ambazo hazijathibitishwa kuhusu uchawi.
 
Lakini wakashindwa kuandika ugonjwa wa akili walio kuwa nao kina Eisntein,au kina Stephen Hawking au kina Richard Dawkins au Wakana Mungu wote ?

Magonjwa ya akili yako mengi sana na haya yalitambulika zama na zama zilizo pita,kipindi ambacho hizo nchi zillnazosemwa zimeendelea zilikuwa hazitajiki.
 
Hakuna ushahidi wa kisayansi na kimantiki kwamba kuna uchawi.

Kuna hadithi nyingi na habari nyingi ambazo hazijathibitishwa kuhusu uchawi.
Unaujua ukomo wa Sayansi ? Sayansi ina duru katika akili ya mwanadamu,nje ya akili ya mwanadamu hakuna sayansi,yaani Sayansi haivuki hapo.

Akili ya Mwanadamu ina ukomo kama macho yalivyo na ukomo wa kuona,yaani mpaka. Mbele ya akili ya mwanadamu ndiyo hayo mengine,ambayo akilo iliyo salama haiwezi kuyakataa.

Sayansi haiwezi kuielezea nafsi kama ilivyo,au mawingu kama yalivyo au jua kama lilivyo zaidi ya dhana na "Assumptions" tu.

Sayansi dhaifu sana,sababu msingi wake ni akili za mwanadamu.

Ni hadithi zipi hizo unazo sema hazijathibitishwa ?

Uchawi upo na Majini wapo hii ni hakika isiyo kuwa na chembe ya shaka.
 
Tuwekee hayo maneno uliyo ya nukuu vizuri.
 
Sasa kama akili ya mwanadamu ina ukomo, utajuaje kilicho nje ya ukomo wa akili ya mwanadamu kwa uhakika?

Utatumia kitu kipi ambacho hakitahusisha akili ya mwanadamu ili ujue kilichopita akili ya mwanadamu?

Na mtu akitaka kuhalalisha uongo wowote kwa minajili ya "huu ni ukweli ulio nje ya akili ya binadamu", utajuaje huu ni uongo?
 
Thibitisha Mungu yupo.
 
Hakuna ushahidi wa kisayansi na kimantiki kwamba kuna uchawi.

Kuna hadithi nyingi na habari nyingi ambazo hazijathibitishwa kuhusu uchawi.
Sijamjibu kwamba huo ni ushahidi wa kisayansi. Bali hoja yake kwamba Imani za uwepo wa uchawi na majini ni za Ki Africa, nimetoa tu ushahidi zipo Dunia nzima.

1. Unaweza kuprove mapenzi yapo?
2. Unaweza kuprove aibu?

Hivyo vitu vipo ama havipo?
 
Utatumia kitu kipi ambacho hakitahusisha akili ya mwanadamu ili ujue kilichopita akili ya mwanadamu?
Akili ya mwanadamu kuna vitu haiwezi kuvi diriki kama vilivyo,ndiyo maana ikawa inasaidiwa na ufunuo.

Kilichopita akili ya mwanadamu ni ufunuo,ambao ulikuwa una jibu maswali ambayo yaliwashinda Wanafalsafa wengi na wakatofautiana. Mathalani jiulize kwanini kina Plato au Aristoto au Pythagoras au Anaksimenesi au Anaksimanda au Socrates walitofautiana katika kuelezea chanzo cha Ulimwengu au maisha,lakini mitume na manabii wote walikuwa na kauli moja katika kuelezea chanzo cha Ulimwengu na baina yao na mwingine ni dahari kwa dahari ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…