Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

Siku wakikutembelea ukaanza kukojoa dagaa wakitoka kinyume nyume na kukwaruza urethra mkojo ukawa unatoka na damu ndio utatambua kuwa wapo !! Sikushangai we bado mtoto,ukikua utayaona.
 
Je wewe unaweza thibitisha sio uchawi?
 
Thibitisha Mungu yupo.
Niliwahi kukuuliza swali ambalo unalikimbia Mara kwa Mara.

Digital information zinaweza kutokea from no where? Binary ama c++ ama Java inaweza tokea sababu ya revolution?

Kama haziwezi, nani amecode DNA zetu? DNA za binadamu zina Binary like language Kitu ambacho so far ni intelligent being pekee wanaoweza kutengeneza nani ameweka hizi code kwenye DNA zetu?
 
Majini yapo Kama unabisha sema nipandishe
 
Huyo mola unamjua kwa makalio au akili?
Tamko moja limethibitisha ufedhuli wako na ugonjwa wako wa akili,tamko "makalio"' sasa nitakuomba uniambie kivipi "kalio" liweze au uliweke katika nukta hii ?

Mola wetu unamjua kwa njia zifuatazo.

1. Akili,kwa kutafakari na kuhoji.
2. Kuyatazama maumbile yaani mazingira
3. Ufunuo (Qur'aan,Zaburi,Taurati na Injili).
 
Huu ni ujinga, unakuja JamiiForums uthibitishiwe uwepo wa UCHAWI???... Kitu chochote kina njia zake za uthibitisho,,,, mfano UMEME hauonekani kwa MACHO ila kuna vitu vinaashiria uwepo wa UMEME,, sasa kama unataka kuona UCHAWI tafuta panapopatikana UCHAWI wakuonyeshe...
 
Mola aliye nje ya akili za mwanadamu unamjua kwa kutumia akili za mwanadamu?

Hujaona kwamba unaji contradict hapo?
 
Sina la kusema zaidi ya ASANTE BABA WA MBINGUNI KWA KUTUVUSHA SISI (familia) katika kipindi kigumu sana kati ya 2006 - 2010....Mambo mengine ni magumu sana kusimulika/kueleweka hasa kama anaesikiliza/kusoma hakuwahi kuexperience...

Kabla hatujalalamikia ugumu wa maisha na mambo mengine, tuwe tunakumbuka kumshukuru Mungu kwa afya anayotujaalia..Kuna watu humu duniani wanateseka sana kwa mambo ya ajabu...Naomba niishie hapa.
 
Yani ushuzi unajamba wewe, halafu lawama unampa aliyesema hapa umejamba ushuzi unanuka?

Uongo unasema wewe, ukiambiwa uthibitishe, kazi ya kuthibitisha unampa mtu uliyemdanganya?
 
Yani ushuzi unajamba wewe, halafu lawama unampa aliyesema hapa umejamba ushuzi unanuka?

Uongo unasema wewe, ukiambiwa uthibitishe, kazi ya kuthibitisha unampa mtu uliyemdanganya?

Wewe umejuaje nimesema UONGO kama huwezi kuuthibitisha?
 
Kwa nini swali lako linakuwa "nani ame code DNA yetu"?

Huoni kwamba swali lako limelenga kwenye jibu unalolitaka wewe?

Umekuta mtu kafa, hujui kafa vipi.

Unauliza, Mmasai gani kamuua huyu mtu?

Umejuaje marehemu kauawa na aliyeua ni Mmasai?
 
Uchawi ni nini na unajuaje huyo ndugu yako umempoteza kwa uchawi na si kitu kingine unachofikiri tu ni uchawi?
We hujawahi KUAMINI kwahiyo ni ngumu kukuaminisha.
We endelea kujua kua Mzungu ndio katengeneza simu inatosha.

Mtu umezaliwa mboga saba, utaujua uchawi kweli?

Ipo siku mutabisha kua hakuna chawa wala kunguni, kisa tu haujawahi kuwaona.
 
Kwa nini swali lako linakuwa "nani ame code DNA yetu"?

Huoni kwamba swali lako limelenga kwenye jibu unalolitaka wewe?

Umekuta mtu kafa, hujui kafa vipi.

Unauliza, Mmasai gani kamuua huyu mtu?

Umejuaje aliyeua ni Mmasai?
Mfano wako si sahihi

Uweke hivi, umekuta mmasai ameuliwa lakini mwilini mwake kumeandikwa neno kwa damu, hivyo Yale maandishi ya damu yanaashiria kifo chake sio natural someone did that.

Same kwa DNA sijakuuliza nani katengeneza DNA Bali nani ameacha Code, Digital information kwenye DNA zetu,

Hili swali Atheist na Scientist wengi wasioamini Mungu mpaka Leo hawajatupa Jibu, hivyo Mkuu Kiranga tusaidie kama Hakuna Intelligence Designer nani amecode DNA zetu?
 
Mola aliye nje ya akili za mwanadamu unamjua kwa kutumia akili za mwanadamu?

Hujaona kwamba unaji contradict hapo?
Ukiwa unasoma nachokiandika unatakiwa usome kwa umakini.

Hakuna "contradiction" hapo. Kuna kujua kwa kutafakari kulingana na ishara zilizopo na kujua kwa hakika ya jambo kwa msaada wa ufunuo. Mathalani,leo hii mtu ambaye akili yake iko salama hakatai uwepo wa Mola muumba,ila kujua sifa na nini anacho taka Mola,akili haiwezi kujua hilo mpaka ipate msaada wa ufunuo.

Yaani kama ilivyo akili pekee haiwezi kumuongoza Mwanadamu katika kujua hakika ya kila jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…