Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

Kwa nini swali liwe nani?

Umekuta jani la muembe mlangoni mwako

Unauliza nani kaweka jani hili hapa mlangoni.

Unajuaje swali sahihi ni "nani"?

Kama jani limepeperushwa na upepo huoni kwamba swali la "nani" ni potofu?
 
We hujawahi KUAMINI kwahiyo ni ngumu kukuaminisha.
We endelea kujua kua Mzungu ndio katengeneza simu inatosha.

Mtu umezaliwa mboga saba, utaujua uchawi kweli?

Ipo siku mutabisha kua hakuna chawa wala kunguni, kisa tu haujawahi kuwaona.
Hujaweza hata ku define uchawi ni nini.

Sitaki kuamini. Nataka kuelewa. Nataka kujua.
 
Vitu ambavyo viko nje ya uwezo wa akili zetu kuvijua tutavijuaje ikiwa kujua chochote tunatumia akili zetu?

Na pia, mtu akitaka kutunga uongo wowote na kukuambia ni ukweli ulio nje ya uwezo wa akili yako, utajuaje huu ni uongo ikiwa chochote utakachosema utaambiwa akili yako ni ndogo huwezi kuelewa, kubali tu hiki kipo nje ya akiki yako?

Nikikwambia Mimi ndiye Mungu muumba ulimwengu, na hujui tu hilo, kwa sababu liko nje ya uwezo wa akili yako kujua, utakanushaje hilo?

Chochote utakachosema kukanusha, nitakwambia una makosa, huwezi kuelewa vitu vilivyo nje yabuwezo wa akiki yako kuelewa.

Sasa hapo utawezaje kukanusha huo uongo?
 
Alikuaje? Nini kilikujuza kuwa huyo ni jini?
 
Na kama hayapo sioni sababu ya kukijadili, ambacho hakipo.
 
Hizo ni mental /brain disorders tu!

Kwa Tanzania, matatizo ya akili ni mpaka mtu aokote makopo.

Mtu mwenye auditory hallucinations watu watasema amepandwa na mashetani!

Mwenye tactile hallucinations watadai wachawi wanamtekenya!

Tatizo ni ujinga. Mambo tusiyoyajua au tusiyoyaelewa, tunayabatiza uchawi!
 
Mazee….hebu cheki hizi aina za hallucinations halafu unambie mtu bongo akiwa nazo watu watasemaje.

Pata picha mtu ana tactile hallucination au auditory hallucination [hawa si ndo huwa wanapandwa na mashetani?]

 
Vitu ambavyo viko nje ya uwezo wa akili zetu kuvijua tutavijuaje ikiwa kujua chochote tunatumia akili zetu?
Hujaona nilichokwambia au kuonyesha kisaidizi cha akili ? Jaribu kuwa unasoma ninacho koandika.
Na pia, mtu akitaka kutunga uongo wowote na kukuambia ni ukweli ulio nje ya uwezo wa akili yako, utajuaje huu ni uongo ikiwa chochote utakach9sema utaambiwa akiki yako ni ndogo huwezi kuelewa, kubali tu hiki kipo nje ya akiki yako
Naujia kwa kutumia uhalisia na kuhoji.

Kama ilivyo majini ni Uhalisia na Uchawi ni uhalisia,ndiyo maana mtoa mada ameenda kinyume na kanuni za kimjadala,kwamba yeye ambaye anakanusha uwepo wa viwili hivyo alipaswa kuweka ushahidi wa kutokuwepo kwake. Lakini hali ilivyo ni kinyume chake.
ulimwengu, na hujui tu hilo, kwa sababu liko nje ya uwezo wa akiki yako kujua, itakanushaje hilo?
Ukisema hivyo utakuwani mjinga,au akili zako hazifanyi kazi au unayo yote mawili.

Sababu Mola ana sifa anuai zake kwazo zikafanya akawa ni Mola. Wewe ni mwadamu na unaenda chooni na huna uwezo zaidi ya ubinadamu wako. Kwahiyo utathibitisha ya kuwa wewe ni mgonjwa wa akili.
Chochote utakachosema kukanusha, nitakwambia una makosa, huwezi kuelewa vitu vilivyo nje yabuwezo wa akiki yako kuelewa.
Mpaka uthibitishe hilo,kinyume na hapo utakuwa unafurahisha nafsi yako na kupoteza muda.
Sasa hapo utawezaje kukanusha huo uongo?
Uongo ni kinyume cha ukweli. Maana ya Ukweli ni kauli au kitendo kuafikiana na hali halisi. Uhalisia au hali halisi ipo.
 
Naam.

Nimeona. Nimeuliza hapo juu, watu wanajuaje kuwa hizo ripoti za uchawi si matatizo ya akili tu, hallucinations na kukubali mambo kwa mob psychology tu?

Sijaona jibu la kueleweka.
 
Hicho kisaidizi cha akili utakitumia bila kutumia akili?

Huko kuhoji utahoji bila kutumia akili?

Nikikwambia mimi ndiye Mungu, na kanusho lako lolote halitafaa kwa sababu ukweli huo, kwamba mimi ndiye Mungu, umepita uwezo wa akili yako kuelewa, utakanushaje hilo?

Chochote utakachokanusha kimepitia akili yako, na mimi nishakwambia akili yako haiwezi kuelewa ukweli huu kwamba mimi ndiye Mungu.

Utakanushaje?
 
Naam.

Nimeona. Nimeukiza hapo juu, watu wanajuaje kuwa hizo ripoti za uchawi si matatizo ya akili tu, hallucinations na kukubali mambo kwa mob psychology tu?

Sijaona jibu la kueleweka.
Mtu labda ana tactile hallucination.

Anajisikia kama vile anapandwa na madudu washa au anachomwa miba na watu.

Yeye anajisikia hivyo. Nyie mliomzunguka hamuoni chochote kwa macho yenu kinachomsibu.

Mnaona mtu anawashwa tu kujikuna kuna.

Watu watasema karogwa huyo! So simplistic!

Hatuna muda [pengine hata uwezo] wa kujifunza na kutaka kujua zaidi.

False sensory experiences zipo na ni aina tu ya matatizo ya akili/ ubongo.
 
Kwa nini swali liwe nani?

Umekuta jani la muembe mlangoni mwako

Unauliza nani kaweka jani hili hapa mlangoni.

Unajuaje swali sahihi ni "nani"?

Kama jani limepeperushwa na upepo huoni kwamba swali la "nani" ni potofu?
Again mfano sio sahihi, umekuta Jani LA muembe ndani ya Jani kumechorwa sigara,

Je ule mchoro umejichora wenyewe ama intelligent being imeuweka ule mchoro?

Nazungumzia code ndani ya DNA na Sio DNA yenyewe.

Swali linarudi pale pale kwanini DNA zetu zina Digital information? Nani ameweka Codes kwenye DNA zetu? Kuna ushahidi wowote wa Digital information kutokea sababu ya Nature ama revolution?
 
Mimi nakupa mfano wangu, wewe unauacha mfano wangu unakuja na mwingine tofauti.

Kwa nini unaanza na swali la nani?

Unajuaje jibu linaendana na nani?

Huoni kwamba swali la nani, kuuliza kitu ambacho hatujalijua jibu lake, limejikita kwenye jibu unalolitaka wewe na halijajikita kutafuta jibu la kweli?

Kwa nini swali liwe "nani"?
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Mkuu haya mambo yasikie hivi hivi tu omba sana yasikukute..
 
Jamii kuwa na imani ya uchawi sana ni dalili ya uvivu uliokithiri katika hiyo jamii.

Watu wavivu kuchunguza vyanzo vya mambo ni rahisi sana kusingizia uchawi vitu.

Hawataki kuvichunguza na wanataka kupata majibu rahisi.

Wanaishia kusema uchawi.
 
Kwa nini swali liwe nani?

Umekuta jani la muembe mlangoni mwako

Unauliza nani kaweka jani hili hapa mlangoni.

Unajuaje swali sahihi ni "nani"?

Kama jani limepeperushwa na upepo huoni kwamba swali la "nani" ni potofu?
You are good at debates!

Lakini ukitaka kujuzwa ukweli lazima ulegeze shingo kidogo!

Ukigangamara na midahalo utaishia kwenye ubishi tu.

Na wewe najua huwa hushindwi.

Kwa tuliokumbana na nguvu za giza tunatizama tu tunasema Hiiiiiiiii....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…