Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

Uchawi au Majini hayapo! Nani ameshawahi kukutana na jini

Kamuulize jiwe why hakuenda fanya kampeni Mikoa ya Kusini...

Chukua ubani fukiza chumbani kwako and then tukana sana majini na mashetani kisha lala fofofo uchi
 
Sababu mfano wako haushabihiani na swali langu, unatunga mfano wa uongo ili update urahisi wa kujibu.

Swali lipo pale pale nani ka code DNA zetu? Kama hauna jibu usipotoshe watu humu wakati mwenyewe huna majibu.
Nimekuuliza hivi, kwa nini swali liwe nani?

Swali linaweza kuwa nini, kipi, etc, kwa nini liwe nani?

Huoni kwamba unakuja na jibu lako mfukoni halafu unauliza swali linalolenga kwenye jibu lako?

Au unafanya hivyo kwa ufinyu wa mawazo tu, huelewi kwamba swali la "nini" ni pana na zuri zaidi ya swali la "nani"?

Unaelewa kwamba "nani" ipo katika "nini" lakini nini haipo katika "nani"?

Unaelewa kwamba "nani" ni subset ya "nini"?

Kwa nini unauliza swali la subset wakati unaweza kuuliza swali la full set?
 
kuna DADA moja nilikutana nae bar flani hiv hapa mjini..nikamuita tujuike pamoja...duh akaanza kusema ana njaa nimpe 10000 ya chakula,mara aseme mama ake ni mgonjwa anahitaji 100000 ya operation,...sijakaa vizuri ktkt ya maongezi mara anasema tena nimpe 35000 anataka kwenda saloon kesho ..eh hata sijamjibu kitu akapita machinga kabeba viatu flan vya kimasai hivi...akaniambia tena Baby ninulie hiki tsh 30000 tu...
Dah Nilivoondoka ondoka pale hata sielewi nilijikuta tu nimefika home..

MAJINI yapo jamani WANAUME wenzangu
Wewe ulikuwa umelewa balimi
 
Majini,uchawi ni drama tuu,kama vipo aje mtu hapa adhibitishe atuwekee na picha kabisa.kwa sisi wenye imani kubwa hatuamini hizo drama.
 
Yani wewe huwezi elewa sababu Shetani ameshakuwin na huwezi pata jaribu lolote lile.

Funny thing na shetani, akishakuweka kwenye 18 na ukaishi kwenye kambi yake huwezi ona mauza uza hata siku moja kwa sababu wewe ndo ushaolewa tayari

Hayo yote utayaona kwenye vita ya kiroho, otherwise tutabishana miaka 1000 na tusikubaliane.

Mie nimeshapambana na nguvu za kishetani mara kibao na kila ninaposali sana lazima siku hiyo nijaribiwe.
Sawa mkuu ila tunaomba utudhibitishie.
 
Upo na upo linked na imani fulani ambao jinsi mtu anavyoyamiliki mengi ndipo anapoogopewa na kuheshimiwa kuwa ni mzito. Imani hiyo huamini kuwa kuna majini mazuri na yanaabudu kwenye nyumba za ibada kama binaadamu tofauti na imani zingine wanaoamini jini hata lijifanye lizuri ni shetani tuu na hakuna kiumbe Mungu alimusudia kukiumba kiitwacho jini bali ni kundi la malaika waliomkosea Mungu na kulaaniwa
 
Nazan umeamua tuh kubishana upoteze cku atleast yule jamaa anajiita kiranga anayepinga uwepo wa mungu kwa kua hakuna aliemuona mungu (cjasema yupo sahihi hapo )but suala la wachawi na majini czani kma kuna mtu mzima hajawai shuhudia hayo .kuna case kibao mpaka kwenye vyombo vya habar zinahusu imani za kishirikina kuna clip nyingi watu wamenaswa wakipaa na ungo .kama vyote hivo ujaona basi hakuna wa kukuonesha unabishana kupata atention tuh
 
Kwanza kabisa nimeuliza uchawi ni nini.

Ngoja nikusaidie jambo moja. Nilicho kiona kwako ni kuwa, huujui Uchawi ni nini lakini ajabu unaupinga. Hapa ndipo huwa nawaona akili zenu hazifanyi kazi.

Nanukuu :

Katika kamusi maarufu ya Kiarabu iitwayo "Lisanul Arab", muandishi anafasiri tamko "Uchawi" kama ifuatavyo "Neno Uchawi kwa kiarabu "As-Sihr", maana yake ni kitendo cha kujikurubisha kwa Shetani (wa kijini) na kwa msaada wake. Akasema tena "Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake,nalo ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli"

Ama Swahaba mtukufu Ibn Abbas (Allah amridhi),anasema " Ni kuidhihirisha batili katika sura ya haki"

Ama katika Kamusi ya dini,Uchawi kama alivyo fasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhrudinn ar-Razi anasema "Ni kila jambo lililo fichika sababu zake,linalo tokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake kuna hadaa (udanganyifu)"
Na utajuaje huu ni uchawi na si kitu kingine ambacho si uchawi ila hujakielewa tu.
Uchawi unajulikana kwa sababu nyingi sana,hasa kwa masharti ambayo ukiyapima huoni uhusiano wa moja kwa moja na huwa ni magumu. Mathalani ukiambiwa uende njia panda upasue nazi kisha usigeuke nyuma na mfano wa hayo.
Muandishi wa riwaya za kisayansi wa Kiingereza Arthur C. Clarke alikuwa na usemi wake mmoja naupenda sana.

Alisema " Any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".
Huyu muongo na alikuwa hajui nini UCHAWI.

Uchawi unajulikana na unatofautishwa kabisa bila shida yoyote.
Yani hata watu kutoka Ulaya walivyokuja na mambo ya gramophone inayopiga muziki, mababu zetu wakaona muziki na sauti za watu zinatoka katika hiki kibox cha gramophone, waliona uchawi.

Hawa mababu zetu wangekuwepo leo wakaona ndege zinaruka, wangeona tunawasilianankwa simu kutoka oande zote za dunia, wangeita huu ni uchawi.

Kumbe ni sayansi tu
Wazee wetu mambo mengi sana walikuwa wanayafanya pasi na elimu ya hakika kabisa,sababu laiti kama wangejua historia ya Uchawi basi hayo ya Wazungu wasingeona uchawi. Uchawi umegawanyika sehemu mbili,na wa mwanzo kuwa na elimu ya Uchawi ni majini,na majini walikuwa wanawafundisha watu,rejea habari za Mfalme Suleyman,aina ya pili ya uchawi ni ule uchawi ambao walikuja nao Malaika wawili wakashuka nao kule Baabil (Babeli),wanazuoni wanasema Uchawi huu ni ule wa kuwafarakanisha wapenda nao yaani mke na mume,na ule wanao fundisha Mashetani ndiyo unao husu mambo mengine kama vile mauaji na mfano wake.
Kumbe ni sayansi tu.
Kwa anaye jua Sayansi na misingi yake hawezi kudai Uchawi ni Sayansi au kulinganisha viwili hivi.
Hawa watu wa kutoka Ulaya walivyoweza kutabiri lini jua litapatwa (solar eclipse), kwa kujua sayansi tu, walionekana wachawi.
Suala jua kupatwa au mwezi kupatwa,sisi wengine tunajua pasi na kutegemea tabiri za Kisayansi,ambazo zimemili katika ubahatishaji,mimi najua kabisa ya kupatwa kwa jua hakutoi nje ya tarehe fulani miaka yote kadhalika kupatwa kwa mwezi.

Kwahiyo hizi elimu zilikuwepo tangu na tangu na Mtume wetu aliwafundisha maswahaba na nini cha kufanya pindi jua linapo patwa au mwezi na nini maana ya viwili hivyo.
 
Nimekuuliza hivi, kwa nini swali liwe nani?

Swali linaweza kuwa nini, kipi, etc, kwa nini liwe nani?

Huoni kwamba unakuja na jibu lako mfukoni halafu unauliza swali linalolenga kwenye jibu lako?

Au unafanya hivyo kwa ufinyu wa mawazo tu, huelewi kwamba swali la "nini" ni pana na zuri zaidi ya swali la "nani"?

Unaelewa kwamba "nani" ipo katika "nini" lakini nini haipo katika "nani"?

Unaelewa kwamba "nani" ni subset ya "nini"?

Kwa nini unauliza swali la subset wakati unaweza kuuliza swali la full set?
Haya jibu nini/kipi/nani aliecode/kilichocode DNA zetu?
 
Kuna kipindi shuleni walikua wanakuja wanamazingaumbwe tunatoa ela wanafanya show ...ebu niambie kile kiini macho kinachotufanya tuone yale mauza uza ni nini.alafu unasema ety uchawi ni africa tuh ebu google uone huyo mtu anayesemekana ni mchawi kuliko wote kuwai kuishi ni mzungu au muafrica
 
Unaelewa kwamba "nani" ni subset ya "nini"?
Hii si kweli sababu tamko "nani ?" ni kiulizi kwa kile chenye ufahamu na nini ni kinyume chake (au tunasema kwa Hayawani).

Sasa jifunze kutumia maneno vizuri.
 
Hawa watu wa kutoka Ulaya walivyoweza kutabiri lini jua litapatwa (solar eclipse), kwa kujua sayansi tu, walionekana wachawi.
Ngoja nikupe faida,kuhusu kupatwa kwa jua na mwezi.

Jua halipatwi kamwe nje ya tarehe 28 au 29 baada ya mwezi kuandama, na hupatwa baada ya mwezi kutoweka katika uso wa ardhi. Tarehe hii ni kwa mujibu wa tarehe ya Hijiriya (Kiislamu). Mathalani lile tukio la kupatwa kwa jua kule Rujewa mkoani Mbeya,lilikuwa ni tarehe 29 "Dhul qa'adah" yaani mwezi wa 11 kwa kalenda ya Kiislamu.

Na kuhusu mwezi haupatwi isipokuwa katika tarehe 13 au 14 au 15. Hii siku zote iko hivyo. Sasa Sayansi haina uwezo wa kujua haya.
 
Hivi mbona maneno yamekuwa meengi lakini hakuna anayeweka picha ya JINI au ushahidi rasmi ili tumalize huu ubishi?

Kusema tu Majini yapo ilihali hata picha ya jini angalau mmoja haiwekwi hapa ni kupoteza muda na kubishana pasipo mwisho

Kama wenzetu Waislam mnaswali nao si mtusaidie angalau tuone picha hata ya Maimuna tu?
 
Nimekuuliza hivi, kwa nini swali liwe nani?

Swali linaweza kuwa nini, kipi, etc, kwa nini liwe nani?

Huoni kwamba unakuja na jibu lako mfukoni halafu unauliza swali linalolenga kwenye jibu lako?
Unajua kilugha tamko "nini" ni kwa vile ambavyo havina akili yaani hayawani. Sasa kwanini iwe nini ? Na nini inaweza kufanya nini ? Yaani unaijua mipaka ya tamko "nini ?" ? Usitake kulazimisha Uongo uwe ukweli,jambo ambalo ni Muhali.
 
Back
Top Bottom