Kwanza kabisa nimeuliza uchawi ni nini.
Ngoja nikusaidie jambo moja. Nilicho kiona kwako ni kuwa, huujui Uchawi ni nini lakini ajabu unaupinga. Hapa ndipo huwa nawaona akili zenu hazifanyi kazi.
Nanukuu :
Katika kamusi maarufu ya Kiarabu iitwayo "Lisanul Arab", muandishi anafasiri tamko "Uchawi" kama ifuatavyo "Neno Uchawi kwa kiarabu "As-Sihr", maana yake ni kitendo cha kujikurubisha kwa Shetani (wa kijini) na kwa msaada wake. Akasema tena "Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake,nalo ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli"
Ama Swahaba mtukufu Ibn Abbas (Allah amridhi),anasema " Ni kuidhihirisha batili katika sura ya haki"
Ama katika Kamusi ya dini,Uchawi kama alivyo fasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhrudinn ar-Razi anasema "Ni kila jambo lililo fichika sababu zake,linalo tokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake kuna hadaa (udanganyifu)"
Na utajuaje huu ni uchawi na si kitu kingine ambacho si uchawi ila hujakielewa tu.
Uchawi unajulikana kwa sababu nyingi sana,hasa kwa masharti ambayo ukiyapima huoni uhusiano wa moja kwa moja na huwa ni magumu. Mathalani ukiambiwa uende njia panda upasue nazi kisha usigeuke nyuma na mfano wa hayo.
Muandishi wa riwaya za kisayansi wa Kiingereza Arthur C. Clarke alikuwa na usemi wake mmoja naupenda sana.
Alisema " Any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".
Huyu muongo na alikuwa hajui nini UCHAWI.
Uchawi unajulikana na unatofautishwa kabisa bila shida yoyote.
Yani hata watu kutoka Ulaya walivyokuja na mambo ya gramophone inayopiga muziki, mababu zetu wakaona muziki na sauti za watu zinatoka katika hiki kibox cha gramophone, waliona uchawi.
Hawa mababu zetu wangekuwepo leo wakaona ndege zinaruka, wangeona tunawasilianankwa simu kutoka oande zote za dunia, wangeita huu ni uchawi.
Kumbe ni sayansi tu
Wazee wetu mambo mengi sana walikuwa wanayafanya pasi na elimu ya hakika kabisa,sababu laiti kama wangejua historia ya Uchawi basi hayo ya Wazungu wasingeona uchawi. Uchawi umegawanyika sehemu mbili,na wa mwanzo kuwa na elimu ya Uchawi ni majini,na majini walikuwa wanawafundisha watu,rejea habari za Mfalme Suleyman,aina ya pili ya uchawi ni ule uchawi ambao walikuja nao Malaika wawili wakashuka nao kule Baabil (Babeli),wanazuoni wanasema Uchawi huu ni ule wa kuwafarakanisha wapenda nao yaani mke na mume,na ule wanao fundisha Mashetani ndiyo unao husu mambo mengine kama vile mauaji na mfano wake.
Kwa anaye jua Sayansi na misingi yake hawezi kudai Uchawi ni Sayansi au kulinganisha viwili hivi.
Hawa watu wa kutoka Ulaya walivyoweza kutabiri lini jua litapatwa (solar eclipse), kwa kujua sayansi tu, walionekana wachawi.
Suala jua kupatwa au mwezi kupatwa,sisi wengine tunajua pasi na kutegemea tabiri za Kisayansi,ambazo zimemili katika ubahatishaji,mimi najua kabisa ya kupatwa kwa jua hakutoi nje ya tarehe fulani miaka yote kadhalika kupatwa kwa mwezi.
Kwahiyo hizi elimu zilikuwepo tangu na tangu na Mtume wetu aliwafundisha maswahaba na nini cha kufanya pindi jua linapo patwa au mwezi na nini maana ya viwili hivyo.