Uchawi wa wanawake ni gari, sitosahau gari yangu ya kwanza ilivyogeuka kuwa sumaku ya kuwatumia hadi kuwakinai, Gari! Gari! Gari!

Sidhani
 
kakangu ana mabinti zake wameshafika chuo, kawanunulia magari kila mmoja. na amewawekea bili ya mafuta pia. nadhani hapo ndipo tunatofautiana, wengine magari wameyapata miaka 5 baada ya kuajiriwa, wakati mwingine wamezaliwa wanayaona nyumbani, wamefika 18 wametafutiwa leseni walikuwa wanaendesha kwenda sokoni na walipoenda chuo wazazi wao wamewanunuliwa. wakati wewe alichoki toka mwanza huko unasugua barabara hadi uje uajiriwe tena ukae miaka kadhaa mshahara wako uongezeke then ukopee hakohako kamshahara ununue gari. hao ndio huyu aliyeleta mada.

kuna siku kuna mdada fulani wa ofisini hapahapa DSM aliomba tumsogeze nyumbani kwao kwasababu siku hiyo hakuja na gari. ni mtu anajishusha huwezi amini kama sio maskini, tukampakia tukaseme tumpitishe kwao, wapi? nikashangaa anatuelekeza tuelekee Masaki duh, tulienda kumshusha kwenye nyumba hiyo, naomba niishie hapa nisiendelee kusema, nilibaki mdomo wazi. familia ambayo kale kagari ka ofisi yetu wanaweza kununua hata 20 huko. sikuongea kitu ila hata nikikutana naye huwa namwangalia tu kwa kumchungulia manake sisi wengine wachaga nafikiri unajua maisha yetu ni ya kimara, sinza huko na tunajifanya tuna maisha mazuri, nilipelekwa sehemu ambao imetuliaaaaa kama maji ya mtungi. pale hadi ubongo lazima utulie aisee. vijana tutafute hela mabinti zetu wasiliwe kimasihara.
 
Aisee ni kweli hii kuna demu alikua anauliza eti ana gari gani huyo mwanaume kwanza kabla sijakubali
 
Acha uongo dada
 
Sema tumeshazeeka pengine wewe tayari upo 45 huko, mabinti wanazuzuka sana na magari tangu kitambo.

Kuna kijana mdogo kabisa ana miaka 23 ana corola, anatembeza mkongoto mpaka kwa dada zake wenye 28
Unaishi wapi Kwanza? Labda circle yako bado ina njaa za magari.
Yan kama mwanaume unaendesha ili uwazuzue mademu bado Una fikra finyu. Gari ni necessity siku hizi kama necessities zingine Tu.
 
wamekariri kwamba kumiliki gari umetoboa life
Sio kwa ubaya ila sio poa kwa jinsi hili jua tena la utosi linavyowaka, kwa sisi wasafiri kuelekea kwenye mishemishe hasa maeneo ya mijini kama Dar ni majonzi na huzuni ukiwa umeshikilia zako bomba kwenye daladala unafuta mijasho huku unavumilia makelele ya konda na masengenyo ya abiria wakorofi

Hakika ukimwona mtu kapanda gari yake anaserereka na kiyoyozi, hakika unamwona katoboa. . .
 
Akiki za kijana wa Kitanzania jumatatu ahsubuhi...

Hongera mkuu🤣
 
Kama kukosa ufalme wa Mungu sababu ya Gari bora usiwe nalo. Uzinzi ni dhambi itakayo kupeleka kuzimu 🤔
 
NI lazima kuwe na madaraja kwenye jamii, huyo Kaka yako kabarikiwa ana mafanikio yake kaweza kuwanunulia "watoto wake" magari mapema ni jambo zuri.

Wengine Tumeanza kuyajua magari tukiwa na 24, wengine miaka 7, wengine 16, wengine 30, wengine 40, wengine hawayajui kabisa.

Wengine wanaona Toyota sio magari parking zimejaa audi, Ford,.. House boy ndio kapewa bmw ya kufata watoto tuition.
 
Acha utani aisee.

Nyie wanawake wa kileo ndio kabisa.
 
Nifah bwana umenichekesha sana na ghafla umenifanya nimkumbuke jamaa angu mmoja wa high school alikua pcm anaitwa Jeremiah, yeye hakua akipenda kabisaa kuegemea upande wa walio wengi. Akiona weng mmechagua huku yeye anachagua kulee hata kama kiuhalisia alikua anapenda kule kwingine. He always wanted to be unique or favoured the minority.

Kwahiyo wewe hupend mwenye ukwasi kama magar.
Japo ni mentality nzuri though
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…