Bwana
Mohamed Said nauliza tena, katika mijadala ya nyuma ulisema wapo wanaukombozi ambao uliweza kuwahojo akiwemo Baba yako,
Sasa ndugu, unaweza kututhibitishia sehemu ya mahojiano hayo kwa njia ya sauti ama video?Ikiwa ni ushahidi wa maandishi hauna mafaa kwetu kwakuwa wewe umeandika machapisho mengi kule Wikipedea na umekuwa uki copy na ku past hapa kama sehemu ya utetezi wa maandiko ya vitabu vyako.
Sijamhoji baba yangu.
Haya niliyoandika ni mambo ya wakati baba yangu akiishi katika zama hizo za 1920.
Mambo yanatokea anayaona kwa macho yake.
Mimi nikaja nikaishi katika nyakati hizo.
Bado unahitaji sauti na video ya umri mzima wa baba yangu na wangu?
Lakini kubwa wewe au yeyote yule hana lazima ya kuamini nilioyoandika katika kitabu changu.
Sihitaji kuthibitisha chochote kwa yeyote awaye yule.
Nithibitishe nini ili iwe nini na kutaka nini?
Kuwa baba yangu akimjua Abdu Sykes toka utoto na ujana wao walikuwa pamoja
pale Mtaa wa Kipata na walisoma darasa moja Al Jamiatul Islamiyya Muslim School?
Kuwa baba yangu alikuwa akijua kuwa Abdu alikuwa akaifanya mipango ya
kuunda TANU toka 1950 na akimdokeza mambo yalivyokuwa yanakwenda?
Kuwa baba yangu kajuana na Nyerere nyumbani kwa Abdu Mtaa wa Aggrey mwaka 1952?
Hivi vyote vilikuwa vitu vya kawaida sana.
Yote ni matokeo ya kawaida baina ya watu.
Laiti historia ingeliandikwa bila khiyana wala pasingekuwapo na haja ya kueleza historia hii.
Mimi hakika humu natoa mengi katika yale niliyoandika miaka mingi nyuma lakini sitoi katika Wikipedia.
Wikipedia hawana maandishi yangu.
Maandishi yangu yako kwenye mradi wa Dictionary of African Biographies (DAB), New York.
Huu ni mradi wa Oxford University Press, New York na Harvard.
Maandishi hayo siruhusiwi kuyachapa popote hadi mradi umekamilika.
Siko humu kutetea chochote kwani kitabu hicho kinasomwa sasa mwaka wa 15 si kitu kipya.
Bahati mbaya kwako kuwa wewe umekujakijua kitabu hiki leo.