Nanren, well said makuu.
Watu wengi wana miss point kwa kudhani kuwa wapo wanaopinga kwa ujumla hisia za Mohamed Said.
Nimeshawahi kusema na narudia, tunawashukuru sana wazee wote walioshiriki kuikomboa nchi hii tunayojaribu kuibomoa.
Nani anakataa uwepo wa Mshume Kiyate na mchango wake katika Uhuru kama ulivyo wa familia ya Sykes, Boman, Rupia, Nyerere, Kawawa, Kasella Bantu, Dr Kyaruzi, Lugazia, Dosa Azizi n.k.?
Nani anakataa kuwa gari alilopewa Nyerere lipo makumbusho na alipewa na Dosa?
Nani anakataa uwepo wa AA then TAA na mwisho TANU?
Nyerere mwenyewe kakiri ushiriki wa wazee wa Dar es Salaam, kasema kuhusu wazo la TANU lililopoanzia na jinsi alivyosirikiana na wenzake kuliendeleza gurudumu.
Nyerere aliandikiwa barua kuwa hakuna haja ya chama kingine wakati tayari kipo.
Sasa sisi kizazi hiki tutakataa kitu gain?
Tunachokataa ni jinsi hisia za Mohamed zilivyoandikwa strategically kuwaondoa baadhi ya washiriki, kuwatupia tuhuma walioshiriki, kuwadhalilisha baadhi ya washiriki na kuwakweza hata wasio husika.
Mifano, Mohamed amepindisha ukweli kuhusu ushiriki wa kanisa kwa kuficha ukweli kuwa safari ya UNO ilichangiwa na mashirika ya kikristo. Badala yake ametoa tuhuma nzito kuwa hakukuwa na ushiriki kwa hofu ya kuasi kanisa.
Mohamed, ameficha ukweli kuwa Nyerere aliwahi kuwepo Dar es Salaam kabla ya yeye kuzaliwa.
Alichokisema ni kuwa aliyemwingiza katika siasa ni Abdul Sykes.
Lengo kubwa ni kuonyesha kuwa Nyerere hakuijua siasa hadi alipokutana na Sykes.
Huu ni uzushi kwani alishakuwa katika siasa miaka mingi kuanzia Makerere.
Mohamed ameficha ukweli kuwa Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi na akina Lugazia walikuwa viongozi wa chama na wapigania uhuru.
Katika kupunguza thamani ya mchango wao, Mohamed ameingiza majina hata yasiyo na uhusika mkubwa just to mask the impact of true patriots.
Huwezi kuniaminisha kuwa Tatu Said alikuwa muhimu sana kuliko Kyaruzi au Yusuf Ngozi.
Ndio, kila mtu alikuwa muhimu lakini umuhimu huo una kiwango chake.
Haiwezekani aelezee kwa uchungu kifo cha Idd Faiz Mwafongo huku akisahau kuwa kifo cha aliyekuwa rais wa TAA Dr Kyaruzi hakikupewa uzito ule ule kama cha mweka hazina Mwafongo.
Lengo lilikuwa kuonyesha waislam walivyodhalilishwa huku akificha ukweli kuhusu upande wa pili.
Mohamed ametoa shutuma za Nyerere kumfukuza sheikh Amir.
Ameelezea hukumu ya Nyerere kwa sheikh bila kuweka mashtaka au tuhuma.
Leo tunajua kuwa Sheikh Amir na radical moslems walitaka kumuondoa Nyerere katika nafasi kwa sababu ya ukristu mara mbili achilia mbali kupanga mipango haramu dhidi ya serikali baada ya uhuru.
Hapa lengo ni kuonyesha kuwa baada ya uhuru Nyerere aliwachukia waislam kwa kuanzia na mufti wao.
Mohamed amesahau kuwa udini anaousema upo kumbe ulianza kwa waislam hata kabla ya uhuru
Mohamed ametoa tuhuma za ushiriki wa kanisa katika kuua EAMWS.
Ameombwa ushahidi kwa bahati mbaya sana hana, ametuletea maandishi ya Sivalon.
Kumbuka huyu ndiye mtu aliyefanya research! Tulitegemea atumie maandishi ya Sivalon kutafuta ukweli, hakufanya hivyo kwa sababu lengo lilikuwa tuhuma dhidi ya kanisa na kuonyesha uhalifu wa kanisa hata kama si kweli au hakuna ukweli alio nao.
Orodha ya mambo ni mengi sana haya ni kwa uchache tu kwa mifano, ili watu watambue kwanini watu wengi hawakubaliani na uchochezi na hisia za Mohamed.Hakuna anayetaka historia ya kweli ipindishwe, lakini basi isiandikwe kwa kupindisha ukweli ili kukidhi chuki, hisia na hasira za mtu mmoja
Muhimu sana ni kuwa kwavile Mohamed anatuhuma na mashtaka dhidi ya watu na taasisi, basi anayo dhima ya kuthibitisha tuhuma zake. Utetezi wa kutaka watu waandike vitabu au kukata vipande vya maandiko yake ni wa kiwango dhifu sana cha uandishi.
Lakini pia anapohitaji heshima lazima awe tayari kutoa heshima.