Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Iwe unakubaliana naye au la, Mohamed Said ni jeshi la mtu mmoja.
Kurasa ya 127 na hajakimbia wala nini. Hats off to you sir.
Kurasa ya 127 na hajakimbia wala nini. Hats off to you sir.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hapa ndio mzee said unapokuwa huwatendei haki wasomaji wako; umetuwekea vichwa vya habari tu. Why don't you scan these documents and make them public for anyone to see?
Nimetoa tafsiri ya mwasisi hapo juu hebu isome mkuu
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ...it was during this time that Abdulwahid, for the second time, advised Nyerere to resign from teaching so as to concentrate fully on the work of the Association.
This idea did not appeal to Nyerere, just as it had not appealed to Chief Kidaha Makwaia four years earlier.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
kama haya aliyoyafanya bado unaziita ngano na huziamini sembuse akienda kuziscan na kuzileta hapa utaamini??
Haukuamini yote haya anayokueleza hadi ukafikia hatua ya kumwita mchochezi itakuwa hizo scanned documents?bila shaka hutoweza amini,umekalia udini usio na kifani,haikusaidii,,
zaidi zaidi inakushushia heshima tuh.
Umepewa reference,nenda kachambue mwenyewe mzee.
Iwe unakubaliana naye au la, Mohamed Said ni jeshi la mtu mmoja.
Kurasa ya 127 na hajakimbia wala nini. Hats off to you sir.
he is on a mission(jihad)
Ritz,
Hivi vitu unavyoshusha si mchezo kaka.
Pembeni ya Nyerere ni Sheikh Suleiman Takadir ''Makarios.''
Siku hizo akisimama kukaribisha Nyerere katika mikutano akisema,
''Hii siyo TANU hii ni ''khamsa.''
Alikuwa akimaananisha hii TANU ni sawasawa na sala tano.
Kushoto kwake Sheikh Takadir ni Clement Mtamila na mwisho ni Bi Titi
Mohamed.
Nyuma ya Nyerere Mama Maria kajificha kidogo, pembeni yake Rajab Diwani,
John Rupia.
Hapa ni Mnazi Mmoja.
si huyo tuh,yupo pia mzee mwanakijiji,hao wote ni watu tuliokawa tunawaheshim sana,lakini tumekuja kushangazwa na chuki zao za kidini pale walipozionesha wazi wazi katika mjadala huu,sasa sijajua nia ya mjadala huu ni kutambiana kiimani au kuhoji kuhusu historia inayofichuliwa na ndugu moh said?Wanashangaza sana hao jamaa.
Nanren,
Ndugu yangu hata wewe huna sababu ya kujibizana na mjinga.
Hiki kitabu ni cha miaka mingi sasa.
Kisikushughulishe.
Aha! Kumbe tunakera? Nyani haoni nini vile?and you?
Whats your mission?
Crusade or?
Mnakera sana..
Nanren, well said makuu.
Watu wengi wana miss point kwa kudhani kuwa wapo wanaopinga kwa ujumla hisia za Mohamed Said.
Nimeshawahi kusema na narudia, tunawashukuru sana wazee wote walioshiriki kuikomboa nchi hii tunayojaribu kuibomoa.
Nani anakataa uwepo wa Mshume Kiyate na mchango wake katika Uhuru kama ulivyo wa familia ya Sykes, Boman, Rupia, Nyerere, Kawawa, Kasella Bantu, Dr Kyaruzi, Lugazia, Dosa Azizi n.k.?
Nani anakataa kuwa gari alilopewa Nyerere lipo makumbusho na alipewa na Dosa?
Nani anakataa uwepo wa AA then TAA na mwisho TANU?
Nyerere mwenyewe kakiri ushiriki wa wazee wa Dar es Salaam, kasema kuhusu wazo la TANU lililopoanzia na jinsi alivyosirikiana na wenzake kuliendeleza gurudumu.
Nyerere aliandikiwa barua kuwa hakuna haja ya chama kingine wakati tayari kipo.
Sasa sisi kizazi hiki tutakataa kitu gain?
Tunachokataa ni jinsi hisia za Mohamed zilivyoandikwa strategically kuwaondoa baadhi ya washiriki, kuwatupia tuhuma walioshiriki, kuwadhalilisha baadhi ya washiriki na kuwakweza hata wasio husika.
Mifano, Mohamed amepindisha ukweli kuhusu ushiriki wa kanisa kwa kuficha ukweli kuwa safari ya UNO ilichangiwa na mashirika ya kikristo. Badala yake ametoa tuhuma nzito kuwa hakukuwa na ushiriki kwa hofu ya kuasi kanisa.
Mohamed, ameficha ukweli kuwa Nyerere aliwahi kuwepo Dar es Salaam kabla ya yeye kuzaliwa.
Alichokisema ni kuwa aliyemwingiza katika siasa ni Abdul Sykes.
Lengo kubwa ni kuonyesha kuwa Nyerere hakuijua siasa hadi alipokutana na Sykes.
Huu ni uzushi kwani alishakuwa katika siasa miaka mingi kuanzia Makerere.
Mohamed ameficha ukweli kuwa Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi na akina Lugazia walikuwa viongozi wa chama na wapigania uhuru.
Katika kupunguza thamani ya mchango wao, Mohamed ameingiza majina hata yasiyo na uhusika mkubwa just to mask the impact of true patriots.
Huwezi kuniaminisha kuwa Tatu Said alikuwa muhimu sana kuliko Kyaruzi au Yusuf Ngozi.
Ndio, kila mtu alikuwa muhimu lakini umuhimu huo una kiwango chake.
Haiwezekani aelezee kwa uchungu kifo cha Idd Faiz Mwafongo huku akisahau kuwa kifo cha aliyekuwa rais wa TAA Dr Kyaruzi hakikupewa uzito ule ule kama cha mweka hazina Mwafongo.
Lengo lilikuwa kuonyesha waislam walivyodhalilishwa huku akificha ukweli kuhusu upande wa pili.
Mohamed ametoa shutuma za Nyerere kumfukuza sheikh Amir.
Ameelezea hukumu ya Nyerere kwa sheikh bila kuweka mashtaka au tuhuma.
Leo tunajua kuwa Sheikh Amir na radical moslems walitaka kumuondoa Nyerere katika nafasi kwa sababu ya ukristu mara mbili achilia mbali kupanga mipango haramu dhidi ya serikali baada ya uhuru.
Hapa lengo ni kuonyesha kuwa baada ya uhuru Nyerere aliwachukia waislam kwa kuanzia na mufti wao.
Mohamed amesahau kuwa udini anaousema upo kumbe ulianza kwa waislam hata kabla ya uhuru
Mohamed ametoa tuhuma za ushiriki wa kanisa katika kuua EAMWS.
Ameombwa ushahidi kwa bahati mbaya sana hana, ametuletea maandishi ya Sivalon.
Kumbuka huyu ndiye mtu aliyefanya research! Tulitegemea atumie maandishi ya Sivalon kutafuta ukweli, hakufanya hivyo kwa sababu lengo lilikuwa tuhuma dhidi ya kanisa na kuonyesha uhalifu wa kanisa hata kama si kweli au hakuna ukweli alio nao.
Orodha ya mambo ni mengi sana haya ni kwa uchache tu kwa mifano, ili watu watambue kwanini watu wengi hawakubaliani na uchochezi na hisia za Mohamed.Hakuna anayetaka historia ya kweli ipindishwe, lakini basi isiandikwe kwa kupindisha ukweli ili kukidhi chuki, hisia na hasira za mtu mmoja
Muhimu sana ni kuwa kwavile Mohamed anatuhuma na mashtaka dhidi ya watu na taasisi, basi anayo dhima ya kuthibitisha tuhuma zake. Utetezi wa kutaka watu waandike vitabu au kukata vipande vya maandiko yake ni wa kiwango dhifu sana cha uandishi.
Lakini pia anapohitaji heshima lazima awe tayari kutoa heshima.