Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ulitaka ushahidi gani mkuu?

Mohamed Said amesema katika kitabu chake kuwa katika hotuba ya kuaga taifa Mwalimu Nyerere alitamka kuwa
"hakumbukii Abdul Sykes alikuwa na cheo gani",

Lakini nimempa hotuba halisi inayosomeka wazi na Mwalimu amesema wazi kuwa Abdul Sykes alikuwa Katibu wa TAA,

Sasa unataka ushahidi upu kuwa Mohamed Said ni mchochezi na Mzushi?

Kwanza nakuomba kasome kitabu cha Mohamed Said kisha njoo usome madai yangu na njoo tena tujadiliane mkuu!
 

hapa ni picha,na nyerere alimtaja tu kama katibu na sio mmoja wa watu waliostahiki kuingia katika kumbukumbu muhimu za mashujaa waliokuwa mbele katika kuhakikisha uhuru wa tanganyika, na hasa hiki ndicho kaelezea mohamed said katoka kitabu chake, kwamba watu hawa pamoja na kutoa kila kitu choa kwa ajili ya kuhakikisha uhuru unapatikana lkn hawpo katika kumbukumbu na badala yake anaonekana mtu mmoja tu ndiye alileta uhuru.
 
Asante Son of Alaska lakini mbona hicho kiti anaweza tu akakaa mtu mmoja? Nasikia kuna watu wanataka na wazee wao nao wangetengewa japo kanafasi kwenye hicho kiti! Kwa kweli kujaribu kuibadilisha historia kwa kuipindisha ni kazi isiyowezekana...naona ndugu yetu Mohamed Said kidogo na kwa uchungu mkubwa, anaanza kulitambua hilo, asanteni JF. Bahati mbaya ukuta anaojaribu kusukumana nao, naye, kama wazee wake, ataondoka ukuta ukiwa bado umesimama pale pale bila hata kutikisika. Kwa hizi picha ningeomba mjadala ufungwe kama hilo litakubalika...shukhrani nyingi kwa wazalendo waliosimama kidete kuhakikisha mbegu ya chuki haipati rutuba.
 

Article pekee inayomzungumzia Peter Colmore katika kitabu cha Mwaikakagile ni hiyo ambayo inamzungumzia katika first person narrative na mtu anayejiita Ally Sykes. Mwaikakagile amesema ameitoa katika gazeti la East African la tarehe fulani. Wewe ukadai kuwa hiyo obituary uliiandika wewe. Na ukaenda mbali zaidi ukituambia kuwa ulipongezwa na mhariri wa gazeti hilo kwa jinsi ulivyomjua marehemu. Nimekuwekea ushahidi kuwa hiyo obituary iliandikwa kweli na Ally Sykes na siyo kuwa mwandishi mwingine aliandika kwa niaba yake. Sasa unataka kutuambia kuwa uliandika wewe na gazeti la East African likam-credit Ally Sykes kimakosa? na kuwa hata huyo mhariri aliyekusifia alifanya hivyo hata baada ya ku-credit makala kukunyang'anya stahili yako na kumpa Ally Sykes! Lakini kwa vile hautaki kushindwa unajiwekea njia ya kutokea kwa kudai kuwa makala hiyo ( ipi?) si uliyotaarifiwa na rafiki zako kuwa imenakiliwa bila kuku-credit ambalo ni kosa kubwa katika uandishi.

Mtu mkweli angekata mzizi wa fitna kwa kusema makala unayozungumzia ni ile iliyokuwa kwenye appendix kadhaa na tanzia uliyoibiwa ilitoka kwenye gazeti la East African la tarehe kadhaa. Nje ya hivyo, unadhidi kututhibitishia kuwa ni msanii asie na hoja.

Article aliyoitumia Mwaikakagile hii hapa:

Na ukisoma appendix husika ya kitabu chake imeanza hivi hivi! Ndio maana nilisema kuwa kama ni kweli wewe ndie mwandishi, wa kuwalaumu ni The East African na mzee wako Ally Sykes na sio Mwaikakagile.
Unayekosa utulivu wa fikra ni wewe. Jibu hoja na sio ku-grandstand kwa ajili ya echo chambers wako. Sisi wengine bado haujatu-impress.

Amandla.......
 
Wanafik wanauliza kwa nini Oscar Kambona hayumo katika orodha ya waasisi wa TANU. Soma hapa chini na pamoja na mengine utaelewa kwa nini:


Uhuru wetu ulipiganiwa na wamisheni, waislamu, wahindu, mapagan n.k. Uhuru wetu ulipiganiwa na wazungu, wakenya, wanyasa, watanganyika weusi, wahindi n.k. Mawakili waliotetea wapiganaji hawa walikuwepo wajamaica, wazungu n.k. Wengi wa hawa hawakutaka kitu kingine bali tanganyika iwe huru. Wengi katika hawa walifariki katika mazingira ambayo kwa mtazamo wetu wa leo wa kutaka kibahasha kwa kulitumikia taifa lako, tunaona hawakustahili. Lakini kitu kimoja ambacho hatutakisahau na bila shaka kiliwafariji ni kuwa juhudi zao, jasho lao, michango yao na wengine hata damu zao zilipelekea nchi hii waliyoipenda kwa dhati ilikuwa huru. Tofauti na Mohamed Said anavyotaka tuelewe, sidhani kama kuna hata mmoja wao ambae aliona kuwa alipoteza muda na kujutia alichokifanya. Kuwakumbuka kwa maandishi si hoja. Kuwepo kwa taifa letu ni mafanikio tosha.

Leo hii mtu kusimama na kudai kuwa uhuru wetu umeletwa na kikundi cha waislamu waliokuwa wakiishi Gerezani ni kututakana wote na hata hao anaojifanya kuwaenzi.

Amandla.........
 
Hoja kuu ya Mohammed said ni kwamba waislamu hawajafaidi matunda ya uhuru kama wakristo ilihali wao ndio haswa waliopigania uhuru huo. Lakini wengi wa wapigania uhuru hao wa gerezani kama siyo wote na kama ilivyoainishwa na MS mwenyewe hakuna hata kumbukumbu zao kuendesha political rally hata Morogoro, leave alone Nkasi, Karagwe, Magu au Tunduru. Hiyo haimaanishi mchango wao hautambuliwi so is to others waliokuwa maeneo mbali mbali ya Tanganyika. Shukrani kwa walioleta ushahidi wa ziada katika kurekebisha historia iliyopindishwa. Anyways!

Tulishayaongea haya 2010/2011 mpaka tukafika hitimisho mbalo lilikuwa je kama kuna hilo tatizo la mfumo kristo au waislamu kubaguliwa suluhisho lake ni nini? Tukamuuliza Mohammed Said, je ianzishwe affirmative action?, MMM akamuuliza kwa nini basi wasianzishe political movement? Mpaka leo Mohammed Said hajatoa suluhisho ya nini kifanyike kuhusu hiyo anayoiita dhulma. Zaidi zaidi ni tishio kwamba wanatoa tahadhari kwamba serikali isipoliangalia hili yatakayotokea huko baadae tusijelaumiana. Na hapa ndiyo hoja ya mfumo kristo inapojikoroga. Iweje serikali ile ile inayodaiwa kuongozwa na kusimamiwa na mfumo kristo ishughulikie hicho kinachoitwa dhulma dhidi ya inaowadhulumu??

Nilimuuliza Mohammed Said wakati ule atupe japo mfano wa nchi ambayo madaraka na ajira serikalini zinatolewa kwa kufuata uwiano wa kidini ili ikibidi tukajifunze huko. Hajajibu mpaka leo.

Kuhusu Nyerere kunyima jamii fulani elimu, nilimuuliza pia ni kwa nini 1990 kulikuwa na shule nyingi binafsi wilaya ya Rungwe (Na nilizitaja) kulinganisha na mkoa mzima wa Dar es Salaam na Pwani? Hajajibu mpaka leo. Nilitoa mfano specific wa Rungwe ili kuua hoja ya ukatoliki maana wilaya ya Rungwe by then na very likely hata leo ilikuwa na waumini wa RC wasiozidi 10% ya total population.

Nilimuuliza Mohammed Said ni kwa nini Haroub Othman aliendelea kutoa lectures kuhusu intellectualism na uongozi wa mfano wa Nyerere????? Hii ni baada ya MS kutuambia HO alikasirika sana (In a sense alianza kukosa imani na Nyerere) baada ya kujua ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika kama isimuliwavyo na yeye Mohammed Said. Mfano wa lectures za HO inazozingumzia ni ile aliyoitoa October 14, University of Cape Town, South Africa – Mwalimu Julius Nyerere: An intellectual in power (Unaweza bofya juu ya hiyo title kupata ziada ya kilichosemwa). Mohammed Said hajajibu mpaka leo?

Nilimuuliza MS kuwa inadaiwa wenye mfumo Kristo chaguo lao la uraisi in 2010 elections ilikuwa Dr. Slaa, Kilichotokea wote tunafahamu. JK alishinda, je hii haimaanishi kushindwa au kutokuwepo huo unaodaiwa kuwa mfumo Kristo wenye nguvu za ajabu wa kuamua nani asome nani asisome, nani awe raisi au waziri na nani asiwe, na aajiriwe serikali na nani asiwe. Mohammed Said hajajibu mpaka leo.

Kilichoniondoa mjadalani wakati ule ni pale MS (Mwenye bandiko) alipoonekana kuishiwa hoja na kudai ooh! Angalia nyie mko wangapi, mie peke yangu lakini bado hamniwezi. Mara ooh! Kama hamkubaliani na hoja ndani ya kitabu chake andikeni na nyie vitabu vyenu juu ya historia za wazee wenu. Ikawa sasa si kuelimishana bali kushindana. Nimepitia humu naona ndio huko huko mjadala ulikoelekea.

All in all ni kwamba huu mjadala hautakuwa na maana kama facts na opinions hazitenganishwi na pia mjadala kuhusu nini kifanyike kwa hiyo dhulma inayodaiwa kuwepo. Kutishana na kukebehiana hakutatufikisha kokote kama taifa. Unless kama mjadala huu ni burudani tu. Lakini pia ndugu zangu tusisahau individual responsibility, maana hapo ndio kwenye suluhisho la kudumu.
 

FM,

Huyo ni Judith Listowel ''The Making of Tanganyika,'' Chato and Windus, 1965.
Listowel hakufanikiwa sana katika utafiti wake.

Tayari ugomvi kuhusu historia ya TANU ulikuwa ushaanza.
Historia ya kwanza iliyoandikwa na Abdu Sykes na Dr Klerruu Nyerere hakuitaka.

Listowel alikuja Tanganyika 1962 na kwanza alitua Nairobi kuonana na Peter
Colmore na Colmore ndiyo alimwelekeza kwa Ally Sykes.

Msikilize hapa anasemaje:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] When Judith Listowel came to Tanganyika in 1962 to research for her book, The Making of Tanganyika, she wanted to interview Abdulwahid. However, knowing the controversy which had surrounded the first attempt to research the subject, Abdulwahid avoided her.

When Listowel finally caught up with him, Abdulwahid remained reserved and did not give any meaningful details about his own political career or that of his father.

However Listowel was able to get little information from Abdulwahid on the formation of TANU from which she wrote: Abdul Sykes, Ally's brother, said that they had to awaken the political consciousness of the people and form a political organisation'. [1]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] From this encounter with Abdulwahid, Listowel wrote to Ally Sykes giving her impression of Abdulwahid. Listowel wrote: ‘I like your brother very much and only wish we could have a longer conversation.' [2]

Back in London Listowel wrote to Ally Sykes on several occasions seeking clarifications on many points of historical importance.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1]Listowel, op. cit. p. 121.
[2]Listowel to Ally Sykes, 12 th November, 1962. Sykes' Papers.

Katika kitabu cha Listowel kuna matokeo mengi sana muhimu hakuyapata mfano historia ya
harakati za wafanyakazi ambazo ziliamsha sana hali ya siasa Dar es Salaam kufikia mapambano
kati ya serikali na wafanyakazi wa bandarini.

Hii ilikuwa kati ya 1947 - 1950 na ndiyo iliyomtia Abdu Sykes katika siasa na kumuongoza katika
kuasisi TANU 1954.

Lakini kubwa zaidi Listowel hakupata kuona nyaraka za Sykes zinazoelezea historia hii ya TAA na
TANU.

Nyaraka hizi zilikuja baadae kuleta ugomvi.

TANU wakizidai kuwa ni zao kwa hiyo wana haki ya kuzihifadhi wao na waliokuwanazo wakizizuia
kwa hoja kuwa baadhi ni za marehemu baba yao Kleist na nyingine ni za marehehemu Abdu Sykes.

Watafiti wawili tu ndiyo waliozisoma hizo nyaraka mwandishi huyu anayeandika na John Iliffe.

Iliffe amechukua baadhi ya nyaraka hizi na kwendanazo Cambridge University katika miaka ya awali ya
1970.

Hizi nyaraka alipewa na Daisy Sykes binti yake Abdu Sykes kwa kuzitazama tu na kurudisha.
Iliffe hakuzirejesha.

Kuna mengi lakini haya yanatosha kwa sasa.
 

FM,

Sikulazimishi wala si kitu kikubwa kwangu kuwa mimi ndiye niliyeandika hiyo taazia.
Nimeandika vitabu itakuwa taazia...

Ikiwa hiki kitu ni muhimu sana kwako.

Ikiwa utaweza na wataafiki waulize The East African, hundi ya malipo ya makala ile
iliandikwa jina la nani?

Hivi ndugu yangu unadhani mie nimo humu kuku-impress wewe?
Halafu iwe nini?
 

Vipi clip ya hotuba?

Hiyo ndiye msema kweli.
Imeshindikana kupatikana?
 

Unaongelea bao? Humjui champion wetu wakati wa nyerere alikuwa nani? Tafiti kidogo.

pata raha:

 

FM,

Kutoka kitabu changu:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] In response to the author's interpretation of Tanzania's political history which posits Islam as an ideology of resistance to colonial rule, Fr. Peter Smith, a Catholic priest and a resource person in Muslim-Christian relations, responded with two papers to counter the Muslim factor in the independence movement. [1]

In one of them he argues that:

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] ''There are revisionist histories being attempted today which are trying to show these early movements in support of TANU as Islamic Movements. The truth is that Muslims were involved; so, too, were Christians-the movement was mainly nationalistic and the ethos, though not anti-religious, was decidedly secular''.[2]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Father Smith of the Roman Catholic Church and the Party seem to be of the same mind on this dissension. [3] Both Kiwanuka and Fr Smith are expressing their own personal opinion, not facts.

No one denies the fact that some Christians were there.

Indeed Christian names appear in the dramatis personae of the play. But no one can deny the truth that they did not occupy centre stage.

This work has given a descriptive analysis of the role of urban Muslims in the struggle for independence; their contribution in the founding of TANU; in membership drives and composition which took strong Muslim characteristics. Dar es Salaam Province TANU Elders Council under its chairman Sheikh Suleiman Takadir had 173 members who were all Muslims. [4]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1] See Fr. Peter Smith, ‘Christian and Islam in Tanzania Development and Relationships' in Islamochristiana, 16 (1990) pp. 171-182. Also Smith, ‘Some Elements for Understanding Muslim-Christian Relations in Tanzania'. 1993 (seminar paper presented in Dakar, Senegal, ‘Islam in Africa South of Sahara').
[2] Smith, passim.
[3] For the understanding of political parties and the role of culture, groupings, ideology, etc., see Maurice Duverger, Political Parties, Their Organisation and Activity in the Modern State, (New York, 1963).
[4] See Elder Council Section File 376, Party Archives, Dodoma.
 

Unajua nini sweke 34....tangu Brother MS alipoleta ile story ya namba za mitihani wakati ule...kwenye ule mnakasha mzito kweli kweli...tena aliuanzishwa yeye....binafsi nikapata na ninapata taabu sana ya kuthamini alicho ana anacho kiandika......

Hiyo "hadith" ya mtoto wa kike kudhulumiwa nafasi yake ya masomo baada ya kufaulu....kama sikosei uliitoa wewe siku zile......kwa kweli nilicheka sana sana......naona bado watu wanasisitiza tu bila kutoa data za kueleweka..........hizo ndizo tunazoziita "gogovivu style stories"........ watu wanalishwa "wanameza"......kama wafuasi wa Kibwetere....
 

Mlitaka Mwalimu Nyerere katika Hotuba ile amfanyie nini Abdu Sykes ndipo muwe na amani moyoni mwenu?

Mmejaribu kudanganya kuwa alisema hakumbuki Abdu Sykes alikuwa na cheo gani, lakini tumewaambia acheni uzushi na uchochezi, Abdul Sykes alikuwa Katibu wa TAA.

Sasa mnasema eti hakumtaja kwa uzito???

Mlitaka hotuba nzima imtajetaje yeye tu?

Au mlitaka amrithishe uraiis ndipo muwe na amani?

Acheni akili za kuku nyie walimwengu!
 

Huyo ambaye unamuamini mpaka umelileta bandiko lake humu jamvini kama ushahdi hayo yote kaambiwa na wazee wa Kariakoo ambaye wewe unawadharau.

Vipi wale walioleta orodha ya wasisi wa TANU na uhuru wa Tanganyika wapo 17 tu. Hawa unawakubali kwa sababu hawajatajwa wazee wa Kariakoo.
 

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"] FM,
Mwisho mwisho wa kitabu changu hii ndiyo ilikuwa lugha yangu kwa wasomaji:

There is no way one can do research on TANU and fail to mention Abdulwahid.

There is no way one can mention Abdulwahid and not mention Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

There is no way one can mention Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika and leave out TANU and vice-versa; and for that matter there is no way one can credit Abdulwahid with any political achievement without first crediting his father Kleist.

There is no way any biographer can research on Nyerere's life and ignore the support of the people who were close to him and their influence on him.

Those in power think that to mention them as pioneers of the independence movement is to evoke deep sentiments from the people and the general Muslim community in Tanzania.

Much as Muslims fought for uhuru, the gains or even spillovers have been very little to them.

It is better for the powers that be that those sentiments remain buried.

And the only way to ensure this is to try to erase that important part of Tanganyika's history.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Huu ndiyo ugomvi wangu na hao walioandika historia rasmi.
 
Vipi clip ya hotuba?

Hiyo ndiye msema kweli.
Imeshindikana kupatikana?
Kimsingi mimi na wengine tunaozipinga ngano zako kuzihalalisha kuwa histori ya watanganyika hatuna shida ya video au audio ya hotuba hiyo ya Mtakafu Julius Nyerere,

Wenye hofu ni wewe na wenzio ndio mlistahili kuja na audio ama video kuipinga hiyo hotuba niliyoiweka hapo juu!

Mimi na wenzangu tumeridhika kuwa hotuba hiyo ni sahihi, na iimefuta uongo wako kuwa Mwalimu alisema hamfahamu/hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na CHEO gani, kumbe mwalimu alisema wazi kuwa alikuwa katibu wa TAA.

Kwanza lete hapa hiyo hotuba uliyoinukuu kuwa mwalimu alisema hakumbuki Abdul alikuwa na cheo gani, hiyo itasaidia kuipinga hotuba niliyoiweka pale juu, kisha nitaleta AUDIO kuthibitisha ZAIDI uongo na uchochezi wako mzee wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…