Mohamed,
What is the point? Hata kama kuna mtu ameunga mkono hoja yako kuwa Nyerere alikuwa hajulikani wakati huo, lakini ukweli ni kwamba alipouchukua uongozi wa TANU alifanya kazi ambayo hata wazee wako hawakuweza kuifikia--kuisambaza TANU kwenye pembe au kona zote za Tanganyika. Ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu cha Judith Listowell:
" In the north of Tanganyika, Nyerere made a great impression. Lucy Lameck, the first woman to become a junior minister in Tanganyika, was present when he addressed her tribe, the Chagga:
I had met Julius in Dar-es-Salaam in 1953 [Lucy told the author]. Long before that I had felt that, in order to be effective in a hospital, or a school, or an office, I had to turn to politics. To obtain equal treatment was part of a much larger problem, the problem of existence under a colonial government... At this time we Chaggs had a paramount Chief called Tom Marealle, an arrogant man who made life very difficult for all of us who did not approve of his politics. When Twining offered me a scholarship to England, Marealle turned it down. I would rather not tell you why. I have never cried so much in my life. By then TANU was in existence and I pinned all my hope on it.
In October 1954 Julius Nyerere came to Moshi and held meetings. At one of them I enrolled my father, my mother, my aunt and my two sisters. Soon after that I was elected representative of the district. On his return from the Trusteeship Council meeting, Julius came north again and held two meetings: one in Machame and the other in Moshi. I went to both and witnessed the marvellous effect he had on my people. Now we TANU enthusiasts began to campaign in earnest.....We told people about the need for education and how little the British had done about it. We talked about the land shortage, and the injustice of having large areas not permitted to be used. We told them that Tanganyika was our country and that we were going to run it in our way. We told them that TANU, headed by Julius, would lead us to independence."
Hiyo ndiyo kazi aliyoifanya Julius Nyerere mbali na wazee wako kuanzisha TAA. Hiyo ndiyo sababu Julius Nyerere stands above the rest, including above your Gerezani TANU founders. Kesho nitawaletea kisha cha Austin Shaba na jinsi alivyomsaidia Nyerere katika Southern Highlands. Taking the baton from your Gerezani wazee, Nyerere became a trailblazer spreading the fires of independence in all corners of Tanzania.
J,
Ni kweli alivyosema Listowel lakini si kweli tupu karuka baadhi ya mambo.
Ngoja nikuonjeshe hapa siasa za TANU zilivyokuwa Kilimanjaro.
Ila napenda tu kukufahamisha wengi wakipata huwa wanapata maradhi
ya kusahau.
Mzee Yusuf Ngozi ndiye aliyemtia Lucy Lameck katika siasa.
Inasikitisha sana kuwa Mzee Yusuf Ngozi hadi leo mchango wake haujathaminiwa.
Na alifanya makubwa.
Nyerere asingeweza kazi hii peke yake kuna wengi waliomsaidia huko mikoani.
Hao wote nimekutananao na ninaweza Insha Allah kuweka taarifa zao hapa jamvini.
Inasikitisha kuwa hata yeye alipokuwa anatajika peke yake katika historia ya uhuru
wa Tanganyika hakujisikia vibaya.
Mimi nimefanya mahojianonae na nimemweleza vizuri katika kitabu changu ''Uamuzi
wa Busara,'' Abantu Publications Dar es Salaam 2007.
Mtoto wake mkubwa alinitafuta na kunishukuru sana na kunizawadia picha ya baba
yake katika ujana akiwa katika siasa.
Moja ya matatizo ya kitabu cha Listowel ni kuwa utafiti wake
ulikwenda haraka haraka na akikutana na ''high society'' kama
alivyokuwa yeye mwenyewe.
Kabla hajaolewa na Listowel ambae alikuwa kutoka ''upper class''
huyu mama alikuwa mtu wa ''show business.''
Mumewe alikuwa balozi wa Uingereza Ghana.
Nakuwekea siasa za Moshi kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'':
Joseph Kimalando na Japhet Kirilo walikuwa wajumbe toka Jimbo la Kaskazini katika ule mkutano mkuu wa 1954 wa kuunda TANU.[
Kumbukumbu za wakoloni zinamuonyesha Kimalando kama mtu aliyejihusisha na siasa za African Association alipokuwa akifanya kazi mjini Dar es Salaam katika miaka ya 1930.
Kimalando akiwa mzee mwanaharakati, aliheshimiwa sana na vijana waliokuwa makao makuu kama vile kwa John Rupia.
Kimalando alikataa kusajili TANU Moshi.
Kimalando alikuwa mwanasiasa mkongwe toka enzi ya African Association katika miaka ya 1930, akishiriki siasa za wakati ule huku akifanya kazi Tanganyika Railways.
Aliporudi Moshi sasa akiwa mtu mzima, aliajiriwa katika ofisi ya wakili mwenye asili ya Kiasia.
Inawezekana kabisa fikra za umri wake mkubwa baada ya kustaafu na kazi yake hii mpya ilimuweka katika hali ambayo haikumwezesha kukijenga TANU ili kudai uhuru wa Tanganyika.
Aliwazia hali yake ya baadaye zaidi kuliko siasa. Kwa ajili hii Kimalando alishindwa kukisajili TANU Moshi kama chama cha siasa.
Hii ilikuwa pigo kubwa kwa kuwa Kimalando alikuwa hodari wa kuandika Kiingereza na kwa wakati ule ilidhaniwa kuwa kujua lugha hiyo kwa fasaha ni muhimu katika kuendesha mambo ya siasa na serikali.
Wakati sehemu nyingine zikihamasika na harakati za kudai uhuru Moshi ilikuwa katika usingizi.
Uongozi wa TANU Arusha, chini ya Japhet Kirilo ulikuja Moshi pamoja na Rajab Chamshama na Robert Otieno kuja kuchunguza kwa nini TANU ilikuwa inachelewa kusajiliwa Moshi.
Viongozi hawa waliitisha mkutano wa uchaguzi Welfare Centre ambao ulihudhuriwa na watu takriban ishirini na wa tano, mmoja wao akiwa Yusuf Ngozi.
Mkutano ule ulimchagua Mzee Yusuf Ngozi kuwa mwenyekiti wa kwanza wa tawi la TANU Moshi mjini.
Taratibu Kimalando akawekwa pembeni.
Katika halmashauri ya kwanza ya tawi lile alikuwapo msichana mdogo wa miaka ishirini na minne, Lucy Lameck ambae baadaye alikuja kuwa waziri katika serikali ya wananchi.
Inasemekana miongoni mwa matawi yote ya TANU nchini Tanganyika, tawi pekee lililoungwa mkono na wanawake na wao kuwa ndiyo nguvu kuu ya chama, lilikuwa tawi la TANU la Moshi mjini.
Nguvu kuu ya TANU ilikuwa wanawake waliokuwa wakiuza mbege, pombe maarufu ya kienyeji huko Kilimanjaro.
Uuzaji wa pombe huko Kilimanjaro ilikuwa ni kazi ya wanawake tu, wanaume hawakujishughulisha nayo.
Mkuu wa kilabu cha pombe alikuwa mwanamke mmoja wa Kimasai, Mama Binti Maalim.
Ingawa mume wa Binti Maalim, Jumbe Mohamed, alikuwa mtumishi wa serikali, na kwa hiyo alijitenga na siasa, hili halikumzuia mke wake, Binti Maalim kuwa mwanachama na mwanaharakati wa TANU.
Binti Maalim alihakikisha kwamba kila mwanamke aliyekuwa akifanya biashara mahali pale alikuwa mwanachama wa TANU na alikuwa akitoa sehemu katika kipato chake kusaidia harakati za kudai uhuru.
Wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU walikuwa wale akina mama wauza pombe waliohamasishwa kujiunga na chama na Mama Binti Maalim.
Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari yake ya pili ya Nyerere Kilimanjaro.
Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi la TANU Moshi.
Joseph Kilamalando aliogopa kuitumikia TANU lakini alijiona amesalimika kuifanyia kazi United Tanganyika Party (UTP), chama cha Wazungu kilichoundwa kuipinga TANU.
Kimalando alikuwa katibu wa UTP Moshi, na Mohamed ''Kishikio'' Badi mwenyekiti wake.
Mzee Yusuf Ngozi aliwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTP hadi ikafa.
Wanawake wale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi ofisi ya TANU.
Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vya kisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya kadi za UTP na kumpelekea rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwa hawakitaki chama chake cha vibaraka.