Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Yaseme Mzee wetu Mohamed. Nataka sana kuyasikia. Waislam wengi siku hizi ni waelewa. Wana akili zao pia za kuchanganya na hizo za kwako. Usirudie yale ya kitabu chako na Padre Sivalon, M.M. Hayo tunayajua sana.
 
Ninafurahi kuona idadi kubwa ya watanzania na walimwengu kwaujumla imefunguka na imejua ukweli kuwa Mohamed Said ni mchochezi na mzushi wakuogopwa kama ukoma.

Idadi ya watu wamataifa waliowasiliana na mimi ilikujua ukweli inanipa matumaini zaidi, mungu ibariki jf idumu zaidi na zaidi.
 
Yericko,

Sahib yangu karibu jamvini.
Nimekuwekea halua ya lozi.

Karibu sahib wangu nakutandikia kashda yangu ukalie.
 
Yericko,

Sahib yangu karibu jamvini.
Nimekuwekea halua ya lozi.

Karibu sahib wangu nakutandikia kashda yangu ukalie.
Hahaaa asante sana, nilikuwa bize kidogo na mahangaiko ya kusaka mkate wa kila siku, naaam sasa twaweza kunena pamoja ndugu msomi pekee unayewakilisha kilio cha wajiitao waislamu wanaodhulumiwa na Nyerere hadi leo hii.
 
Yaseme Mzee wetu Mohamed. Nataka sana kuyasikia. Waislam wengi siku hizi ni waelewa. Wana akili zao pia za kuchanganya na hizo za kwako. Usirudie yale ya kitabu chako na Padre Sivalon, M.M. Hayo tunayajua sana.

WC,

Nashukuru kuwa wewe yangu na ya Sivalon unayajua.
Kuna wenzako ndiyo leo wanayasikia.

Hawa ndiyo wananifanya nilale JF, niamke JF, nile JF.
Hakika Waislam wengi sasa wameelewa.

Nani alijua itafika siku vijana watataka kujenga msikiti
wauite ''Masjid Sheikh Hassan bin Amir,'' na wala hawakupata
kumuona Sheikh Hassan.

Wamemjua kwa kumsoma katika kitabu changu na kumsikia katika
mihadhara.

Leo kuna ''Sheikh Hassan bin Amir Award'' kwa wanafunzi bora
katika shule za Kiislam.

Fedha za award hii wanachanga Waislam wa nchi nzima.

Haya yote baada ya Sheikh Hassan kufariki miaka mingi.
Alhamdulilah.

Hii ni faraja kubwa.

Nimepata kuhudhuria mchezo wa kuigiza wa Maisha ya Sheikh Hassan..
vijana wanaigiza sheikh yuko darasani anasomesha...
wanaingia Abdu, Dossa na Nyerere...

Anawapokea...

Waikela anamsomea Nyerere ile khutba maarufu ya mwaka 1963
''Moto wa Waislam Ukiwaka.''

Machozi yalinitiririka...
na ni vitoto vidogo hivi...
 
Idadi inayoujuwa ukweli leo hii ni kubwa sana kuliko unavyofikiria, na hao unaojidai "wakimataifa waliowasiliana" na wewe leo hii wanasoma na kupata mapya, kaa na wewe uyasome.

Nakukumbushia;

  1. Ile hotuba uliyotuahidi (kumbuka tumekupa na ofa ya kukusaidia kuununuwa kwani ulidai zimehitajika pesa.)
  2. Habari za Mkwawa ulizodai utazipata kwa Chifu. Unakumbuka? au ilikuwa "knockout" imekutia kizunguzungu ukawa unaweweseka?
  3. Historia ya Abushiri.
Ritz mkumbushe mengine aliyoahidi kama sikuyaweka.
 
Mwalimu nyerere alidhan ukweli hautajulikana,
Dunian hapa hakuna siri isiyofichuka..
 
Hahaaa asante sana, nilikuwa bize kidogo na mahangaiko ya kusaka mkate wa kila siku, naaam sasa twaweza kunena pamoja ndugu msomi pekee unayewakilisha kilio cha wajiitao waislamu wanaodhulumiwa na Nyerere hadi leo hii.

Yericko,

Hebu kuwa mstaarabu mdogo wangu.

Nimekukaribisha jamvini kwa kikombe cha kahawa na
halua ya lozi kisha nimekutandikia kashda yangu ukalie..

Ijaza yangu ni kejeli na kunibeza!

Nitakusamehe tu ikiwa utanambia, ''Kaka mie hiyo halua ya
lozi siijui wala hiyo taadhima ''kashda'' sijua ni kitu gani.''

Hapo nitakusamehe vinginevyo nitakuona bado sana...

Hebu fikiri unamkirimu rafiki yako kwa kumfungulia chupa ya
pombe kisha badala ya kukupa ahsante anakukejeli ungejihisi
vipi?
 
Maalim Mohamed Said anaijuwa lozi na kashda huyo?

Zomba,

Madam anaishi kwetu tuna wajib wa kumkirimu kikwetu.
Katika hii takrima ndipo atajifunza mpaka adabu.

Lakini kanifedhehesha sahib wangu.

Nilikuwa na mpango wa kumtunza kofia ya mkono lakini
hakika kanivunja moyo.
 
Maalim Mohamed Said,

Kadri unvyoendelea kutupa vitu humu, mleta mada Yericko Nyerere anatamani asingeufunguwa huu uzi.

MashAllah tunapata darsa murwa kabisa.

Allah anafanya mambo yake kwa njia za ajabu kabisa.

Ahmed Rashad Ali akimwambia Abdu Sykes kuwa akifungua mdomo
kuhusu TANU Nyerere atakaa kimya na hii TAA kilikuwa chama cha
starehe kejeli ile itakwisha.

Abdu siku zote alikuwa akisema hapana haja.
Huu ndiyo ukawa msimamo wake hadi alipokufa.

Hebu shuhudia leo nini kimetokea kuhusu historia ya Abdu na Nyerere.
Leo inazungumzwa wenyewe wote hawapo.

Waliokuwa hawajapata kumsikia Abdu Sykes sasa wanamjua na yake
mengi alofanya katika maisha ya Nyerere na kuasisi TANU.

Nani alitegemea haya?
 
Haya mambo hayawafai watoto wadogo. Unapandikiza sumu ya ajabu kama hawatasoma na kuelimika vizuri. Watakapoanza kuitapika sumu hii Tanzania hapatatosha. Umewambia pia kwamba huyo Sheikh Amir hakuwa MTANGANYIKA?
 
Yaseme Mzee wetu Mohamed. Nataka sana kuyasikia. Waislam wengi siku hizi ni waelewa. Wana akili zao pia za kuchanganya na hizo za kwako. Usirudie yale ya kitabu chako na Padre Sivalon, M.M. Hayo tunayajua sana.

Napenda sana michango yako dhidi ya Waislam unawaamsha.
 
zomba,

1) Alisema atatuletea majina ya waasi wa mwaka 1982 waliosamehewa na Nyerere na wengi kupewa vyeo wengine mabalozi.

2) Alisema ataleta picha ya gari ya kwanza ya Nyerere aliopewa na Mariale.

3) Alisema ataleta audio na video clip ya Nyerere ataenda kuchukuwa TBC baadae akasema wanaiuza lakini hataki kusema kiasi gani.
 
Last edited by a moderator:
Haya mambo hayawafai watoto wadogo. Unapandikiza sumu ya ajabu kama hawatasoma na kuelimika vizuri. Watakapoanza kuitapika sumu hii Tanzania hapatatosha. Umewambia pia kwamba huyo Sheikh Amir hakuwa MTANGANYIKA?

WC,

Uislam hauna ubaguzi.
 
Alisema kuna urasimu asiouelewa hivo atakwenda kesho yake.

Sasa mpaka sasa hivi kesho yake haijawasili. Indeed tomorrow never comes!!!
 
Last edited by a moderator:
Nina mashaka huyu si mwanafamilia na nyerere hata kidogo,anashindwaje kuwa na hata hotuba za marehem mzee wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…