Yaseme Mzee wetu Mohamed. Nataka sana kuyasikia. Waislam wengi siku hizi ni waelewa. Wana akili zao pia za kuchanganya na hizo za kwako. Usirudie yale ya kitabu chako na Padre Sivalon, M.M. Hayo tunayajua sana.
WC,
Nashukuru kuwa wewe yangu na ya Sivalon unayajua.
Kuna wenzako ndiyo leo wanayasikia.
Hawa ndiyo wananifanya nilale JF, niamke JF, nile JF.
Hakika Waislam wengi sasa wameelewa.
Nani alijua itafika siku vijana watataka kujenga msikiti
wauite ''Masjid Sheikh Hassan bin Amir,'' na wala hawakupata
kumuona Sheikh Hassan.
Wamemjua kwa kumsoma katika kitabu changu na kumsikia katika
mihadhara.
Leo kuna ''Sheikh Hassan bin Amir Award'' kwa wanafunzi bora
katika shule za Kiislam.
Fedha za award hii wanachanga Waislam wa nchi nzima.
Haya yote baada ya Sheikh Hassan kufariki miaka mingi.
Alhamdulilah.
Hii ni faraja kubwa.
Nimepata kuhudhuria mchezo wa kuigiza wa Maisha ya Sheikh Hassan..
vijana wanaigiza sheikh yuko darasani anasomesha...
wanaingia Abdu, Dossa na Nyerere...
Anawapokea...
Waikela anamsomea Nyerere ile khutba maarufu ya mwaka 1963
''Moto wa Waislam Ukiwaka.''
Machozi yalinitiririka...
na ni vitoto vidogo hivi...