Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Shekh M. Said,

Hapo kwenye Red! umenikumbusha Sheikh maarufu sana huyu miaka ya 80! jee, bado yuko hai? si alikuwa Serikalini miaka ya nyuma?
 
Makoye,

Serikali ina hofu ya kumjua nani anambagua nani.
Waislam tumelieleza tatizo hili miaka mingi...

Bado tunapuuzwa.

mohamed, tuacheni ushabiki! mkuu, hawa watu wote wanabaguana kwa sasa, tujiulize, mbona hii haikutokea kabla ya miaka ya kuanzia 1980?
 
Shekh M. Said,

Hapo kwenye Red! umenikumbusha Sheikh maarufu sana huyu miaka ya 80! jee, bado yuko hai? si alikuwa Serikalini miaka ya nyuma?

Bi. Z,

Sheikh Mwilima amefariki miaka mingi sasa inazidi 15 na zaidi.

Sheikh Mwilima alipambana na Nyerere katika Halmashauri Kuu
ya CCM.

Alitaka kujua vipi Waislam wako nyuma katika nyanja zote na
akamwomba mwenyekiti alitazame tatizo hili kama alivyolitazama
tatizo la Wabarbaig, Wahadzabe na wanawake.

Amenihadithia mwenyewe.

Anasema ukumbi mzima ulikuwa kimyaaaaaa...
Wajumbe wanasikiliza mwenyekiti Nyerere atajibu nini.

Kwa kama dakika moja mbili...

Sheikh Abubakar Mwilima na Nyerere walitazamana kama majogoo
wanaotaka kupigana.

Nyerere akaahirisha kikao....
 
Mara ya mwisho nilimuona hakiwa na Huthoman Matata kwenye munakasha wa Quran and Sciance miaka mingi imepita.
 
mohamed, tuacheni ushabiki! mkuu, hawa watu wote wanabaguana kwa sasa, tujiulize, mbona hii haikutokea kabla ya miaka ya kuanzia 1980?

Makoye,

Baada ya Nyerere kuivunja EAMWS na kuundwa BAKWATA Waislam wakawa
kama wamepwelewa.

Umma ulihangaika sana na jinsi ya kuiangusha BAKWATA lakini ikawa tabu
kwa kuwa serikali iliipa BAKWATA ulinzi kamili.

Ilipofika 1980 ilifanyika semina Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam iliyotayarishwa
na wanafunzi wa Kiislam wa Mlimani (MSAUD).

Hapo ndipo ilipoamuliwa vijana wa Kiislam waingie BAKWATA kutoa uongozi.
Vilevile kulikuwa na ''underground movement'' ikiitwa Warsha.

Hii ilifanya kazi kubwa sana kuwaamsha Waislam kuhusu dhulma.

Jambo la kwanza waliofanya vijana kutoka MSAUD ilikuwa kwanza kuwaeleza
Waislam kuwa ipo dhulma nchini.

Hapo ndipo pakawa mwanzo wa Waislam kuanza kujitazama upya...

Ni kisa kirefu hapa hapatoshi lakini kuanzia hapo hali ikaanza kubadilika.
 

Mohamed hebu watendee haki watu wanaotufuatilia hapa,

Hivi Mwalimu aahirishe kikao baada ya swali hilo la Abubakar Mwilima?

Je ni kweli Mwalimu hakujibu kitu akabaki kumtazama tu Mwilima kama usemavyo majogoo watazamanavyo?
 
Nawashukuru Mods kwakuifanya kuwa thread maalumu, hilo litasaidia watanzania wengi kuujua uongo na uchonganishi wa huyu ndugu yetu Mohamed Said
 

sasa hizi porojo,,, wote waliokuambia sasa marehemu! hakuna hata mmoja tunayeweza kumuuliza.
 

Imani ndio nini? sisi Waislaam tuna nguzo za imaan. Jee wewe?
 
Zomba, huna hoja hapa, unapiga makelele kama mtoto tu, ona aibu, mtu mzima wa umri wako hata kama elimu ilikupita kando bado unanafasi ya kutumia uzoefu kujadiri hoja na sio ushabiki huu wa kipumbavu.

"lekebisha" basi ili tuanze kujadili mada kwa mujadala ulio fasaha. Usione haya wala yale.
 
zubeda, naomba mkumbushe na Biafra!
 
Last edited by a moderator:
Mohamed hebu watendee haki watu wanaotufuatilia hapa,

Hivi Mwalimu aahirishe kikao baada ya swali hilo la Abubakar Mwilima?

Je ni kweli Mwalimu hakujibu kitu akabaki kumtazama tu Mwilima kama usemavyo majogoo watazamanavyo?

Wewe si utuletee alivyojibu!
 
Nawashukuru Mods kwakuifanya kuwa thread maalumu, hilo litasaidia watanzania wengi kuujua uongo na uchonganishi wa huyu ndugu yetu Mohamed Said

Pia watapata kumjuwa Abdu Sykes, Kleist Sykes (senior), Iddi Mafongo, Mshume Kiate, Tosiri, Mashado Plantan< Mama Mluguru.

Udhalim wa Nyerere na Kanisa Katoliki.
 

Mohamed Said sijui mpaka lini utaendelea kupotosha ukweli kuhusu hili jambo, Nilishakueleza hili mjadala ule wa 2010/2011) na ukakiri huku ukiendelea kusisitiza eti msukumo mwingine ulitokana na hadithi zako. Haya narudia tena kukuelezea historia ya wazo la uandishi wa biografia ya Nyerere lilikujaje: This is an extract kutoka gazeti lile lile lilochapisha makala zako kwa wiki tatu mfululizo - The East African, October 26, 1999.



Bahati mbaya na Prof Othman akafariki pia.

Mzee Mohamed ni upotoshaji wa namna hii unaofanya baadhi ya members humu na watanzania kiujumla waone kwamba wewe una nia ovu, unataka kufitinisha jamii na kuleta mitafaruku isiyo na tija kwa "histohisia" , na lengo lako si jema hata kidogo. Unawezaje kuendelea kudanganya jamii mchana kweupee namna hiiii and not once Mohamed, not once. Sasa utaaminikaje na haya si mambo ya 1960's au enzi za African Association sijui 1930's. Kama nakumbuka vizuri MMM, Nguruvi na Mag3 walikubana utuambie kama umewahi kuwahoji Prof. Mohiddin na Ruhinda kuhusu uwepo wa hadithi zako kwenye maandalizi ya hiyo biographia jibu lake hujatoa mpaka leo. Halafu bila haya eti unasema yote uliyosema ni kweli!!!!
 
Ndio maana sisi wengine tunamwambia mchochezi Mohamed Said aache kujaza kurasa za JF na ngano na kujinukuu mwenyewe, ajibu maswali anayoulizwa lakini akiamua kuwa muongo ajue kutunza kumbukumbu.
 
Last edited by a moderator:



Brother MS.......maandishi uliyotoa hapo juu hayajibu maswali uliyoulizwa.......rudia kusoma swali la MMKJJ....


....na huo ndio MTEGO wa Brother MS...... uliowanasa vijana wengi....
 
Mohamed Said anatoa hoja based on some very wrong premise ambayo ni hatari katika ustawi wa taifa letu. Kwamba eti "waislamu ambao hawajafanikiwa ni kutokana na dhulma ya mfumo kristo na wakristo waliofanikiwa basi ni kutokana na kupendelewa na mfumo kristo. Hii ni premise ya aibu kabisa and makes u fail hata kabla safari haijaanza. Lakini ndugu yetu huyu na mashabiki wake kwao huo ndiyo ukweli. Je ni vipi kwa waislamu waliofanikiwa na wakristo walioshindwa na kukata tamaa?????????

Turudi nyuma kidogo, Mohamed katika kujenga hoja zake juu ya mfumo kristo amebase zaidi D'salaam kitu ambacho ni cha ajabu pia kwani taasisi dhulmati huwa ni nchi nzima hukuhitaji kwenda Johanesburg kuprove uwepo wa apartheid au DC kwenda kuuona utumwa.

Hoja ya waislamu kunyimwa elimu mifano mingi sana ameitolea kutokea Dar. Sasa twende nyuma kidogo mwanzoni mwa miaka ya 80. Nimechagua kipindi hiki kwani nilishuhudia nayotarajia kuyaandika. Kifupi Dar enzi zile elimu haikuwahi kupendwa na wala haikuwa ujanja. Shule ilikuwa ni kimbilio ya mijitu ya kuja ambayo ilikuwa haina namna nyingine zaidi ya kusoma ili ije mjini. That was the perception of the day. Wajanja enzi hizo walikuwa mabaharia, Ma Dj, wachezaji (Simba, Yanga, Pan), Wanamuziki wa dansi na Wafanyakazi wa Bandari (kama akina Mohamed Said mwenyewe). Shule haikuwa na nafasi, role models kwa vijana wadogo enzi hizo walikuwa akina Gerry Kotto, Kalikali, Seydou, Makochela etc. na si wasomi. Baadae walikuja wauza unga, clearing and forwarding agents etc. Perception hizi potofu kuhusu umuhimu wa elimu ziliathiri vijana wote waislamu kwa wakristo na zilienea mpaka mijini kwingine nchi nzima. I know some fools watarukia kwamba see "they are now blaming it on ubaharia, samba, yanga, dansi etc." lakini ukweli ndiyo huo kuhusu perception ya shule by then jiini.

Mwanzoni mwa miaka ya 80 kukaruhisiwa kuanzisha shule binafsi, ungetegemea nafasi hiii kutumiwa nchi nzima tena hasa kule kulikokuwa na shule chache za serikali. Lakini haikuwa hivyo shule binafsi zikashamiri kule kule kulikokuwa na shule nyingi za serikali Kilimanjaro, Mbeya, Kagera, Iringa Mwanza etc
na si Dar why? (Wateja wakuu wakiwa ni locals kutoka maeneo hayo zilikojengwa shule hizo binafsi) Kifupi ni kuwa Dar hakukuwa na local demand period. Maana hata hapa pia supply and demand rules. Lakini pia wazee wetu "wa kuja" hawakuiona Dara kama sehemu muafaka ya kusomesha watoto wao kutokana na shule kutothaminiwa. Dar ukichanganya na pwani kukawa na shule chache binafsi ukilinganisha na wilaya kama Moshi vijijini au Rungwe. Ikumbukwe kuwa hizi ni enzi "ukipasi" darasa la saba unafanyiwa sherehe nyumbani.

Ni sometimes mwanzoni miaka ya 90 ndio shule ikaanza kuonekana muhimu tena, "twisheni" kila mahali hadi "uswazi". Sera za soko huria zikapelekea influx ya uwekezaji mfano mabenki binafsi, makampuni ya sm yaliyokuja bidae, migodi, uchumi kukua. Na huu ndio ukawa mwisho wa umaarufu wa mabaharia, wachezaji, wafanyakazi wa bandari. It's just shule shule, shule. Sasa akina Mohamed badala ya kufanya utafiti wa kitaalamu na mikakati ya kujenga shule zaidi na nzuri, kuongeza vyuo, kupanua nafasi za ajira na kuhakikisha vijana wa kitanzania wanakuwa na bright future mbeleni wao wanatafuta wachawi kwa mgongo wa dini.

Ungetarajia basi kwa kuwa kuna hiyo alleged dhulma iliyo wazi basi akina MS wangemobilize taifa zima (Wakristo kwa Waislamu) tupambane na hiyo dhulma. Kama ilivyokuwa South Africa au US, wazungu wengi tu walikuwa wakizipinga serikali zao kwa mifumo ile dhalimu pamoja na wao kufaidika nayo. Unaweza kuwa mjinga kufikiri kuwa Mzee Said hajawahi kunavigate into those waters hell no!!!!!!!!!!Msisitizo kuwa mfumo kristo chini ya kanisa katoliki ulikuwa na lengo la kuwapendelea wao kuliko watu wengine ilikuwa ni careful move kuwafanya walutheri, wasabato, wahindu ect. wa-sympathize na hoja zake. Bahati nzuri na mbaya kwake hilo halijawezekana.

Kinachoshindikana hapa ni kuwa hiyo alleged dhulma kutoka mfumo kristo haijawa substantiated, wala kutolewa ushahidi usio na mashaka na haipo. That is why ni marehemu tu ndiyo wanaotumiwa na Mzee said kujengea hoja

Jingine ambalo hatuhitaji kulinyamazia ni hii tabia ya Tambo za Mohamed Said kujustfy Authority ya hoja zake. Hii ni staili ambayo amekuwa akiitumia sana kwenye majukwaa yake ya wale wanaomsikiliza tu. Mfano aliposema kitabu chake kipo mpaka library of congress, Mohamed Said hii kwake ni sifa mno na justification kwamba alichoandika ni facts tupu. Lakini kwa taarifa yake ni kuwa ndani ya library of congress kuna vitabu chungu nzima vya simulizi based on conspiracies, uzushi, hila etc. Mfano ni hivi hapa chini:

1. Obama's America : unmaking the American dream / Dinesh D'Souza.

2. Roots of Obama's rage / Dinesh D'Souza.

3. Demonic : how the liberal mob is endangering America / Ann Coulter.

4. Way things ought to be / Rush Limbaugh.

5. Real America : messages from the heart and heartland / by Glenn Beck.


Ndani ya hiyo Obama's America mwandishi amemtuhumu marehemu mama ya sitting president Obama kwamba alikuwa Malaya aliyependa kujirusha na wanaume wa thirld world. Sasa kwa wasikilizaji wa hadithi za Mohamed Said ni vema watambue kuwa maktaba hiyo ina vitabu mpaka vinavyomtukana raisi kwa uzushi ilhali MS anatumia uwepo wa kitabu chake mle kama authority.
Lakini pia kuna watanzania mfano Musiba, Hammie Rajab, Eric Shigongo etc. wana vitabu ndani ya Library of congress (Bofya hapa) na tumbukiza majina yao kwenye search utaviona. Hatujawasikia watanzania hawa wakitoa tambo kama hizi za MS.

Tukija kwenye suala zima la Nyerere kuwa alitaka aonekane yeye tu kama anavyotuhumu Mohamed Said hili ni kichekesho. Mwalimu by then na to the African politics of the day kama hii ingelikuwa hulka yake asingeshindwa kuuita UD university of Nyerere, same to the airport, port and all the major roads na wala isingeonekana kuwa jambo la ajabu. But hakuwa hivyo na historia yake itamsimamia.

Kiujumla sidhani kama kuna anayepinga hadithi za MS, kinachopinga ni kule kutaka ku-institutionalize hadithi hizo kuwa historia. Na pale anapoombwa ufafanuzi huchagua maswali ya kujibu, ukiombwa ushahidi aliyemwambia ni marehemu so and so. Mohamed said you just need to come clean juu ya agenda unaoipigania. Adios.

Hili ni bandiko langu la mwisho kwenye mjadala huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…