Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Ni bahati mbaya ilioje kuwa wakati tunaendelea na huu mjadala tayari matunda ya uchochezi kama anavyokoleza huyu muongo waahed yanaanza kujitokeza. Kwa kuwa ameshindwa kujibu maswali kadhaa aliyoulizwa kwa nia ya kupata ukweli sasa tunaanza kumuumbua kwa hila zake za kupandikiza chuki kwa mgongo wa dini na kwa kutumia uongo.
Moja ya pendekezo lilitolewa na Abdu, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingi za kiafrika, lilikuwa ni TAU (Tanganyika African Union) na wazo lake lilishabihiana na Kenya ambao tayari walikuwa na KAU (Kenya African Union) Hapa ni wazi kuwa pendekezo lake halikuwa na ubunifu wowote lakini msomi Mwalimu, kwa muono wa kitaifa, akatambua mara moja kwamba ingawa TAU linaendana na vyama vingine Afrika, inakosa ule uzalendo wa kitaifa...hivyo akapendekeza neno National liongezwe kwenye TAU.
Wazo lake liliungwa mkono na wajumbe wote asilimia mia moja 100% na lililofuatia ni kwamba liwekwe wapi ndani ya neno TAU?Kulizuka mapendekezo mawili, TNAU (Tanzania National African Union) au TANU (Tanzania African National Union). Hapo ndipo Abdu akapendekeza TANU kwani inatamkika kirahisi kwa waswahili na wazo lake kuungwa mkono. Aliyekuwa anaongoza hiki kikao kilichoasisi TANU ni Raisi wake muasisi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hapa nawaachia wasomaji watoe uamuzi.
Kama unaongelea uasisi wa AA huu ni Uwongo namba moja...ukweli ni kuwa AA, haikuwa chama cha siasa bali club ya wafanyakazi Waafrika iliyoasisiwa na Gavana Cameroun wa serikali ya kikoloni ili kuwawezesha na wao wapate mahala pa kujumuika kama ilivyokuwa kwa Wazungu na Waasia.Anasema vyama vya siasa vinaanza kwenye fikra ya waasisi wake.
Uwongo namba mbili...mwanzoni viongozi wa AA waafrika na wasomi hawakuwa na pa kukutania hivyo ilibidi uzinduzi wake ufanyike nyumbani kwa Raisi Muasisi wa kwanza Cecil Matola, Myao msomi na mwalimu zao la shule ya Minaki, shule iliyokuwa na sifa ya pekee miaka hiyo.Kwa Abdu chama kilikuwa nyumbani kwao pale Kipata toka 1929.
Muongo mkubwa, uongo namba tatu...Baada ya muda mfupi Gavana Cameroun aliwapa nyumba aliyoijenga yeye mtaa wa New Street. Kuna utata mkubwa kuhusu namna ukoo wa Abdu ulivyokuja kumiliki hii nyumba na hapa namwomba Mohamed Said awe mwangalifu sana.Anapata fahamu baba yake anamchukua Mtaa wa Kariakoo na New Street siku ya Jumapili kwenye ujenzi wa ofisi ya African Association.
Kama mafaili yanasema nyumba ya mtaa wa New Street aliijenga Sykes, nashindwa kujua lengo la dai hilo ni nini. Naomba ikumbukwe kwamba mtu ambaye angeweza kukabidhiwa hiyo nyumba alikuwa Raisi wa AA, Cecil Matola lakini akaja kufariki mapema mwaka 1933...how convenient!Abdu kashuhudia haya kwa macho yake. Tuje kwenye mafaili ya Sykes.
Huu nao ni uongo usiokubalika, hakuna lolote hapo! Kama yapo mafaili nina hakika inazungumzia tu historia ya siasa Dar es Salaam na hasa mitaa ya Kipata, Gerezani na Kariakoo lakini si kama unavyotaka kuudanganya umma eti historia nzima...Tanganyika ilikuwa zaidi ya Dar es Salaam na hizo ni simulizi za mtaani alizokuwa anasimuliwa na wazee wake barazani kwa sababu wanazozijua wenyewe.Nyaraka ndani ya mafaili haya kwa hakika ndiyo yenye historia nzima ya siasa katika Tanganyika.
Huwezi na huthubutu kuyagusa kwa sababu yanakuumbua. Mathalani unadai TANU iliasisiwa na Abdu kama unavyodai pia AA iliasisiwa na Kleist lakini kati yao hakuna aliyekuwa na uwezo wala sifa za kuziongoza. Kwanza huko Burma walikutana waafrika kutoka sehemu mbali mbali za bara hili na African Association ya mwaka 1929 haikuihusu Tanganyika tu. Pili, harakati za kudai uhuru zilishika kasi miaka ishirini baadaye zikiongozwa na wasomi ...trust mchochezi mohamed kwa kupotosha ukweli! Yalikuwapo mapendekezo mengi ya jina la chama cha siasa kilichokuja kuasisiwa mwaka 1954.Hayo mengine siyagusi.