Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nisahihi kabisa, labda kwakuongezea tu nikuwa tutawajumuisha watanzania wenzetu akina Mohamed Said, Ritz, Zomba, Boko Haram, Kichwangumu nk!

Sisi mpaka sasa tuna Maalim Mohamed Said tuna Dr. Hamza Njozi ambae kitabu chake Nkapa kakipiga marufuku lakini kinasomwa kwa sana tu, bado tunatoa nao. Nyinyi kusanyikeni wote na mje na kitabu chenu, tena naona mnachelewa, mwaka wa kumi na tano huu kitabu cha Mohamed Said kinatamba.

Na kuna vingine vinashuka hivi karibuni, kaeni chonjo.
 
Sisi waswahili wauza kahawa wenye akili za madrasa tutakichafua kitabu chenu.

waswahili sisi tangu lini mambo haya?

wataanza kutumia kikristo (kiingereza) ambacho sisi hatujui mpaka tutumie google translate
 
waswahili sisi tangu lini mambo haya?

wataanza kutumia kikristo (kiingereza) ambacho sisi hatujui mpaka tutumie google translate

Huo ubaguzi ndio unaoliangamiza taifa leo!

Kwanini mnapenda usisi na unyinyi katika Taifa hili ambalo wazazi wetu walifanya kazi kubwa sana kutuweka pamoja?
 
Alamat'l Munafik Thalatha. Alama za mnafik ni tatu. Jee, unazijuwa?
hivi kama red maana yake ni hiyo blue, kwanini usingetumia hiyo red tu au blue tu?
dini yenu lazima ukitaja sentesi kwa lugha ya kiarabu lazima utafsili ndo utaeleweka?
 
hivi kama red maana yake ni hiyo blue, kwanini usingetumia hiyo red tu au blue tu?
dini yenu lazima ukitaja sentesi kwa lugha ya kiarabu lazima utafsili ndo utaeleweka?

Jibu swali. Wacha porojo.
 
Zomba,
Si kila mtu ana kipaji cha uandishi. Mohamed kajaliwa kipaji hicho. Lakini kwa sababu Mohamed kaandika kitabu akijikita zaidi kwa michango ya Waislamu, hakuna sababu yangu mimi kuandika kitabu cha michango ya Wakristo. Lakini wakati huo huo tunayo haki, kama wasomaji, wa kupinga yote anayosema Mohamed kwa sababu kwa kanuni za uandishi, yeye ameegemea zaidi upande mmoja tu, kwa kuzingatia simulizi za wazee wake. Kuna vitabu vingi tu vimeandikwa ambavyo ni more balanced, na tumevisoma na ndiyo sababu tuko hapa kumwonyesha Mohamed ni wapi amepindisha na ni wapi anapotosha kwa malengo yake.
 
Hiyo vita ndio hatuwezi kuongopeana kabisa uwadanganye hawa vijana waliozaliwa miaka ya '70 kuelekea '80. Uongo mzuri ni kama wa mzee Mohamed aliouficha kwenye kanzu na barghashia za wazee wake wa Kariakoo.
WC unajua ukiamini masimulizi ni rahisi sana kupotezwa. Simulizi zima la vita vya Kagera limelenga katika kumtuhumu Nyerere na udini dhidi ya Idd Amin ambaye hata Waganda wanaishukuru sana Tanzania hadi leo.

Hao wanaoamini vita ya Kagera hawajui kuwa kulikuwa na mtafaruku mkubwa 1973 uliosuluhishwa na Marehemu Haile Selasi wa Ethiopia. Hawaelewi kuwa Mwanza ilishawahi kushambuliwa kwa mabomu.
Uktaka kumpata Mtanzania basi tunga jambo halafu chomeka harufu ya udini kila mmoja ataingia kichwa kichwa.

Tatizo la taifa letu ni watu kutopenda kutafuta elimu kwa kujisomea. Kila jambo limekuwa ''mission town'' hata elimu watu wanaifanya hivyo
 

Nakaa kisha nainamisha kichwa kushoto natafakari sana, kisha najiuliza hivi wanaounga ngano za Mohamed Said wanaunga kwakusimamia ukweli wa historia au wanasimamia ukweli wa imani zao?

Kwanini imani iwalazimishe waukane ukweli na kuziabudu ngano hizo?


Kweli napata tabu sana kichwani mwangu, sijui niamue kuwaweka kundi gani hawa watanzania wenzangu?!

Sijui niwasaidieje, nazidi kuwaombea kwa Jah awape ufahamu na waifahamu kweli nayo kweli iwaweke huru!
 

Mpaka sasa hamjafanikiwa. Hapo sasa.
 
Hamtachafua, kwanini unapenda kusema chenu ama chetu?

Kitabu kitakuwa cha watanzania wote mimi, wewe na wale!

Acha ubora mimi ndugu!

Wazee wa Kariakoo na Gerezani waliopigania Uhuru watakuwemo katika kitabu chenu?
 
Mohamed, Mag3 ameelezea kuhusu mzozo wa nyumba uliomhusisha D.Cameron.
Katika maelezo yako unaelezea ujenzi wa nyumba hiyo tu.
Bado hoja haijajibiwa kwa ukweli kuwa hujakanusha kuwepo kwa mzozo.

Labda tuulize tena, Je, ni kweli kulikuwa na mzozo wa Nyumba iwe hiyo au iwayo kama alivyosema Mag3?
 

Jiulize wewe unaepinga unachokipinga ni nini? Mshume? Tossiri? Dossa? Mashado? Bi Titi? Mtemvu? Kandoro? Tambaza? Ramia? Stanley Street? Mzee Shebe? Takadiri? TANU? TAA? AA? Burma? New Street? Jammiatul Islamiya? Rupia? Kambona? Nyerere? Mama Mluguru? Ali Sykes? Abbas Sykes, Abdulwahid Sykes? Magomeni? Tewa? EAMWS?

Nini haswa unachokipinga?

Unajuwa kuwa Nyerere alikuwa anapiga fegi?
 

Nyinyi si mnajuwa historia, mnamuuliza Mohamed Said kwanini? si muandike mjuavyo nyinyi?

Uwepo mgogoro usiwepo mgogoro, hiyo nyumba ipo haipo? inahusu nini?
 
Mpaka sasa hamjafanikiwa. Hapo sasa.

Inategemeana na maana ya kufanikiwa. Hivi ni kweli Nyerere alitoka Magomeni kwenda Kariakoo bila hata senti mfukoni?
Hivi ni kweli Nyerere alisoma hotuba UN kama kasuku aliyeandikiwa na Abdulwahid Sykes na kwenye kitabu chake akaiandika in the first person? Hiyo ni mifano michache tu ufanisi wetu wa kuumbua upotoshaji wa Sheikh Mohamed.
 

Ikiwa mnajuwa maana ya matusi ni kwamba ni hatua ya mwiisho saaaana katika maoambano ya aina yeyote kwa ivo mwoneeni huruma ndugu yetu alichobakiza cha kumsaidia kwa akili yake ni matusi na sio yeye tu jaribun kufuatilia mjadala mzima kyna watu wanasiraha yao kuu matusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…