Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kweli mkuu Yericko Nyerere ata mimi nampongeza sana ndugu Mohamed Said kwa kuibua changamoto hii ya kuitizama upya historia ya taifa letu lakini amefail kwa kiasi fulani kwa kua amekwisha chagua upande wa kuegemea hivyo ata kama ni data anatafuta atakua anatafuta zile zinazo suit ktk kile anachotaka kukipresent tu,ni kawaida kwa sisi binadamu ukishachagua upande ni lazima uutete kufa na kupona ata ikikubidi wakati mwingine kupotosha kwa makusudi ili lile lengo lako litimie.
 
Last edited by a moderator:

Sasa wewe andika Nyerere alitoka Magomeni akiwa na pesa mfukoni na hakukutana na Mshume. Na pia andika kuwa hotuba ile aliiandika Nyerere akiwa Pugu au vyovyote vile ujuavyo.

Kuna mtu alikulazimisha uyakubali aliyoyaandika Mohamed Said? aidha yakubali au usiyakubali, yaamini au usiyaamini, Mohamed Said kisha andika ajuavyo yeye. Wewe unaweza andika ujuavyo wewe kama unaona ya Mohamed Said hayakuingii. Mohamed Said kaona ya historia ya kivukoni hayamuingii akapekuwa makabrasha ya wazee wake na ya wengine wengi, akaja na kitabu kinachoeleza ajuavyo yeye wazee wake walivyopigania Uhuru.

Ulilazimishwa uamini? Unangoja nini kuandika unavyojuwa wewe kuwa ndio sahihi?
 

Kaka,
Mimi si mwandishi. Na si kila mtu ana kipawa cha uandishi. Lakini hilo halininyimi haki yangu ya kufichua upotoshaji. Tungekuwa sote waandishi nani angekuwa na nafasi ya kumsoma na kumkosoa mwenzake?
 
Mwalimu wetu Mohamed Said, wanafunzi wapo darsa wanasubiri kusoma.
 
Last edited by a moderator:
Kaka,
Mimi si mwandishi. Na si kila mtu ana kipawa cha uandishi. Lakini hilo halininyimi haki yangu ya kufichua upotoshaji. Tungekuwa sote waandishi nani angekuwa na nafasi ya kumsoma na kumkosoa mwenzake?

Sasa si uoneshe huo upotoshaji? wewe unapinga kuwa hivi si sawa lakini hicho kilicho sawa hukiandiki.

Mohamed Said ameshasema mara nyingi humu jamvini, ni wengi hawaamini kama haya kayaandika yeye. Wewe unaweza ukaamini unaweza usiamini, basi hata unachokijuwa ndio ukweli huwezi kukiandika kwa kuwa si mwandishi? mbona kupinga unaweza kuandika? Si lazima uandike kitabu kama Mohamed Said, hata mistari miwili mitatu ya kutuonesha ukweli unaoujuwa wewe inatosha, tutakuelewa.

Lakini leo unapinga kuwa huamini Mzee Nyerere aliweza kutoka Magomeni bila hata senti, sasa jiulize alikuwa na kazi ipi wakati huo ya kumuingizia pesa? ulitaka aibe? hakuwa mtu wa aina hiyo. Au unapinga kuandikiwa hotuba? leo hii duniani karibu Marais wote wana waandishi wao wa hotuba, nini cha ajabu? Fikiri!

Kama unaujuwa ukweli zaidi ya huo aliouandika Mohamed Said tujuze, si kupinga tu mradi upinge.
 

Zomba,
Kama wewe kweli unaamini Nyerere aliondoka Magomeni kwenda sokoni Kariakoo kuwanunulia watoto wake chakula huku hana hata senti tano mfukoni basi ama wewe ni mwendawazimu au Nyerere ndiye alikuwa na wazimu.
Na hotuba za Nyerere, hasa ile ya kwanza UN tunajua aliiandika mwenyewe. Kama TANU walimpa point of references na draft hilo ni jambo jengine ambalo Mohamed hakusema kabisa. Alitaka tuamini kuwa aliisoma kama kasuku huko UNO.
 

Hasira na kuitana wendawazimu inahusu nini? si uandike ukweli uujuavyo wewe. Hebu jikumbushe kidogo kuwa Mshume alishajitolea kabla ya siku hiyo;

Punguza ghadhab, utaona Mohamed Said anatowa kisa alichokihadithia Nyerere mwenyewe, sasa Mohamed Said atowe kitabu na Nyerere yuko hai amzulie? Nyerere huyu Nyerere? Fikiri!
 

Una matatizo mdogo wangu; historia ni historia hakuna cha ukweli au uongo. Ukisema uongo kuhusu historia hujaandika historia. Kwa hiyo kwenye historia ukweli peke yake husimama. Sasa tafsiri ya matukio mbalimbali ya historia ndio huwa ni mjadala. Alichofanya Mwalimu wenu hapa Mohammed Said ni kuweka tafsiri yake katika matukio ya historia. Ndio maana uandishi wake umejaa "inasemekana".. "iliaminiwa"... "ilisemwa"... nyingi mno. Wakati wowote hakuwa na ushahidi Mohammed anachomokea "Iliaminiwa" hata asipotaja na kina nani na kwanini...

Hatuhitaji kuandika kitabu kingine kwani historia ya Tanganyika imeandikwa kwa kirefu sana na watu wengi tayari - tatizo ni kuwa Mohammed Said peke yake ndio kajaribu kuiandika kwa kutumia prism ya udini. Matukio yote ya historia yetu (au karibu yote) ameyamulika kwa kutumia dini na hivyo mwanga huo wa dini umemfanya aone kila kitu kikiwa na dini hata kisichokuwa cha kidini.
 

Nimeyaandika haya baada ya Yericko kusema atawasiliana na nyie muandike kitabu cha uhuru.
 
Ndio maana kuna habari ambazo Mohamed hataki kuziongelea.
Mfano, ataongelea sana Nyerere kuishi kwa Sykes lakini hata jibu swali kuhusu mzozo wa umiliki wa Nyumba inayosemekana ilijengwa na Sykes.

Ameshindwa kukanusha yasijetokea yale ya Maryknoll na Mkutano mkuu wa AA 1946.

Mag3 ameuliza sana kuhusu Cecil Matola kilichofuata ni Mohamed kusema huyo alifariki mwaka 1939. Mohamed hakufanya utafiti kuhusu Cecil na jitihada zake kama kiongozi wa chama isipokuwa historia imeruka toka kwa Sykes kwenda kwa Sykes.

Mohamed antuambia role ya Mshume Kiyate( na tunaiheshimu sana) ni kubwa kuliko Cecil Matola.

Mohamed ameongelea kurasa nzima kuhusu Mwapachu na jinsi alivyotoka Makerere kiasi kwamba role ya Kyaruzi kama president wa TAA imekuwa kama haipo.

Ninarudia tena na tena Mohamed hajaweza kuthibitisha kuhusu sehemu kubwa ya historia na inabaki kuwa simulizi tamu la wahenga na malenga kama si ngano.

Mkuu Mkandara ameongelea vizuri sana jinsi wakoloni walivyotufanya tukawa hatujielewi na kwa bahati mabya miaka 50 baada ya wao kurudi makwao wametokea wakoloni wengine wanaotaka kutugawa kama wakoloni kwa kutumia dini.

Baada ya kusema hayo ''inasemekana'' Mkandara si mwislam safi kwasababu hakubaliani na maoni ya viongozi wa dini ya kiislam, naye pia amekuwa BAKWATA!
Hakubaliani na maoni ya msemaji wa waislam bwana Mohamed anayeeleza upande wa pili wa waislam

Hiyo ndiyo philosophy inayotumika kutisha watu!
 
hivi kama red maana yake ni hiyo blue, kwanini usingetumia hiyo red tu au blue tu?
dini yenu lazima ukitaja sentesi kwa lugha ya kiarabu lazima utafsili ndo utaeleweka?
Si anakusaidieni nyie msiojua Kiarabu!!
Kwani nyinyi mkiongea kisambaa kwa waswahili simnatoa tafsiri pia.
 
umejuaje kama wote humu hawajui kiarabu?

MM ubishi wako wakitoto!
Kwahio kama baadhi ya watu hapa wanajua kiarabu plus wewe zisitolewe tafsiri kwa Kiswahili kwa wale ambao hawajui kiarabu?
Haya tuseme wewe umegraduate darasa la kiarabu, je umewafundisha wote hapa kiarabu kufanya kila mtu asihitaji tafsiri.
 
Kaka yangu naona sasa hivi unajadili mpaka Like.
Kwa kweli Ritz kama umeweza kushabikia hayo ya zomba...! sina la kuongeza kwenye hilo...ila siku moja tusije kushtuka mtoto wa Sheikh Ponda akifuata nyayo za mtoto wa Salum Abdalla, naye akifanya utafiti aweze kuandika historia ya harakati za wazee wake katika mapambano ya kuupinga utawala wa Kikwete. Watoto wetu na wajukuu zetu nao watajikuta wakiikosoa hiyo histohisia kama tunavyokosoa histohisia ya Mohamed Said huku wajukuu wa Ritz na zomba nao wakimtetea mwalimu wao kama tunavyoshuhudia.

Ila wakati huo kutakuwa na tofauti, dhihaka na kejeli za wajukuu wenu hazitaelekezwa kwa Kikwete aliye madarakani akiiongoza serikali ya CCM bali zitajikita katika kuulaumu mfumo Kristo wakisahau kuwa shida na taabu walizozipata wananchi kutokana na uongozi dhaifu hazikuangalia dini ya mtu. Inasikitisha sana kuwa chuki zilizopandikizwa vichwani mwao kwa simulizi za barazani toka utotoni kutoka kwenye vinywa vya wazee wao, ndizo zilizowaongoza katika uandishi wao ingawa wenyewe watadai waliyoyaandika ndio ukweli.
 
Last edited by a moderator:

Samahani kama kutumia neno "mwendawazimu" ni ghadhab. Nilitaka kusisitiza kwamba haingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu kwamba Nyerere ataondoka Magomeni, achape mguu hadi Kariakoo kutafuta chakula cha wanae huku hana hata senti tano mfukoni. Ingeandikwa kwamba alikuwa amepungukiwa hela, ingeeleweka. Lakini kusema hakuwa na hela ni beyond imagination. Kuhusu hotuba, imo katika kitabu cha Nyerere, Freedom and Unity. Mohamed anao wajibu sasa wa kutuletea draft iliyoandikwa na Abdulwahid ili tulinganishe tuone ni maneno gani ya Abdulwahid ambayo Nyerere ali incorporate katika hotuba yake.
 
Siku zote huwezi ficha pembe la ng'ombe.

haya sasa yale yaliokuwa yamefichikana sasahivi yapo dhwahir shahir. Je umesikia yale ya kule Buseresere na katoro?
ndicho alichopanda kwa kificho JKN. sasa kipo hewani.
Udini wa Buseresere na Katoro umepandikizwa na Kikwete. Katuambia hapa hapa Mohamed jinsi Waislamu walivyokuwa wakinong'onezana misikitini katika uchaguzi wa 2010 wamchague muislamu mwenzao na siyo yule kasisi wa katoliki. Angekuwepo Nyerere upuuzi kama huu usingetokea. Lakini, but then, ulishatuambia kuwa huna akili kwa hiyo sishangai kwa kauli yako.
 

Jasusi,

Mimi singependa kulirejea suala la Mshume Kiyate na Nyerere.
Halina maana.

Pili suala la pale Kariakoo wana TANU kusaidia harakati kwa hali
na mali ni suala ambalo wala si letu sisi kukaa tukabisha kubwa
khasa ni kwa kuwa hayo yote yalikuwa mambo ya ikhsani.

Ila pale alikuwapo Abdu Sykes, Shariff Attas, Sharif Mbaya Mtu,
Shariff Mohamed na hawa ni watu waliokuwa karibu sana na TANU
na Nyerere.

Kuhusu ile document ni suala nyeti na wengi humu wameumizwa na
taarifa mpya za suala hili.

Kama nilivyoeleza chanzo cha document ile ni TAA Political Sub Committee
iliyoundwa mwaka 1950.

Document hii Abdulwahid Sykes kaitaja katika taarifa yake ya mwaka 1950
kwa wanachama wa TAA na akaeleza mchango wa Earle Seaton katika
kuiandika.

(Huyu Earl Seaton ndiye aliyeandika ''petition ya Wameru iliyosomwa na Japhet
Kirilo UNO katika Meru Land Case 1952).

Sasa document hii ya TAA Political Sub Committee ilizungumzwa katika kuunda
kwa TANU mwaka 1954.

Document hii imepotea haipo popote.

Maktaba ya CCM Dodoma hii document haipo wala Nyaraka za Taifa haionekani
ingawa jalada lipo lakini document imenyofolewa.

Nyaraka za Taifa jalada lipo document haipo na microfilm vilevile haipo.

Binafsi nimeandika makala iliyochapwa katika Africa Events kuhusu kupotea
kwa document za kihistoria.

Sina zaidi cha kuongeza kuhusu document hiyo na hotuba ya Nyerere UNO 1955.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…