Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Unajua maana ya kuja na data?

Kuja na data maana yake ni kuja na vielelezo visaidizi nje ya wewe mtuhumiwa/muhusika!

Sasa lieleze jukwaa hili ni data zipi ambazo Mohamed Said amekuja nazo hapa kujibu hoja zetu nje ya aliyoyaandika yeye mwenyewe na kibaya zaidi ni kuwa data hizo ndizo tunazozipinga hapa!
 
heshima ingetakiwa ianzie kwake kama yeye alishindwa kuwapa kipaumbele waliompokea hayo ndio matokeo yake
Ndio tofauti ya mtazamo na fikra tengefu za Mwalimu Nyerere na wazee wenu na sasa nyinyi mmeriithishwa,

Mwalimu aliwaona watanzania wote ni sawa, ilifikia kipindi akakataa kuitwa MTUKUFU na badala yake aitwe NDUGU,

Hilo la usawa kwa wote nyinyi mlitaka awape kipaumbe kwakuwa eti mlishiriki ukombozi??? Haahaaa polenini sana, acheni Nyerere aitwe mtakatifu, kwani kazi aliyoifanya kutuweka sawa ni kubwa mno na haimithiriki hata kwa chembe ya haradari!

Wabaguzi hawana nafasi hata yakumkaribia Muumba tu!

Nikiwauliza kipaumbele hicho mlitaka kiweje, bila shaka mtakosa jibu la kuuaminisha umma wa Watanzania!
 
Mimi nilidhani mjadala tumeshaufunga baada ya kuweka mambo kadha wazi na Bw. Said hajayakanusha.

a. Hakufuata kanuni za uandishi wa historia (historical method) katika kujaribu kusimilia "historia"

b. Katika hilo la (a) alichagua vyanzo vyenye kukubaliana na nadharia yake na hivyo kutafuta ushahidi wa yale yanayoendana na hisia zake. Lolote lililopingana na hisia hizo aliliweka pembeni.

c. Ametegemea ushahidi wa watu rafiki tu na wa karibu kama ushahidi pekee wa msingi huku ushahidi wa vyanzo vyenye kuweza kujua zaidi akiviacha pembeni.

d. Vyanzo vile ambavyo ameweza kuvinukuu karibu vingi tayari vimetangulia mbele ya haki. Hakuna mahali popote ambapo amewarekodi hao anaodai aliwasikia ili watu wengine waweze kupima ukweli wa wanachodaiwa kusema (mfano mzuri ni nukuu yake kuhusu Ditopile akielezea suala la Mshume Kiyate)

e. Madai yake yake kuwa yeye ndiye amekuwa wa kwanza kuwataja 'wazee wake' hadharani na kuhusika kwao kwenye harakati za uhuru yamethibitika kuwa si ya kweli kwani wapo wengi waliowataja kabla yake; John Illife na August Nimtz ni mfano tu ambao waliutaja kwa usahihi kabisa mchango wa wazee wa Kiislamu katika harakati za Uhuru - bila kujaribu kumfanya Nyerere duni ili wapande kwenye mabega yake.


KUtokana na hayo yote a-e ni wazi kuwa soma maandishi ya Bw. Said at your own risk lakini ukiwa na open mind kuelewa kuwa unachosoma siyo historia bali ni HISTOHIA - yaani historia inaposimuliwa chini ya mwanga wa hisia za msimulizi.
 
heshima ingetakiwa ianzie kwake kama yeye alishindwa kuwapa kipaumbele waliompokea hayo ndio matokeo yake

Ulitaka awape kipaumbele gani? Hivi unajua ni wazee wangapi wa Jijini Dar amb ao walipewa kipaumbele katika serikali (na watoto wao) kulinganisha na wazee wengine? Ulitaka afanye nini awajengee chumba Ikulu?
 
Ulitaka awape kipaumbele gani? Hivi unajua ni wazee wangapi wa Jijini Dar amb ao walipewa kipaumbele katika serikali (na watoto wao) kulinganisha na wazee wengine? Ulitaka afanye nini awajengee chumba Ikulu?

Haaahaa daaah nimecheka sana!

Mimi nadhani kitendo cha Mwalimu kukwepa jaribio lao la kumpa mke wa kimanyema huenda liliwauzi pia hawa ndugu zetu! (Ngano)
 

Unataka Mohamed Said ajibu hoja gani tena wakati wewe ndiyo umeanzisha huu uzi kuwa Mohamed Said ni mchochezi wewe ndiyo unatakiwa uthibitishe uchochezi wake.

Bila Mohamed Said wewe usingejua kama John Hatch kutoka chama cha Labour cha Uingereza alifanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja kuunga mkono ukombozi wa watu weusi watu 20,000 walihudhuria huo mkutano Ally Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani, pembeni yupo Oscar Kambona na Denis Phombeah. Nyerere alikuwa yupo Musoma.

Bila Mohamed Said ungewajua hawa Schneider Plantan, Liwali Yustino, I. C. Chopra. Charles Philips, Robert Makange, Arthur Lewis.

Hebu na wewe tupe data na facts ambazo unazo kutoka AA, TAA, TANU.
 
Kaka yangu Jasusi,

Hakuna asiyefahamu umahiri wa Mwalimu katika hotuba hata kama haijaandikwa. zomba hataki kuelewa kwa makusudi tu. Muulize kama aliwahi kuona au kusoma kokote hotuba ya Abdulwahid Sykes. Elimu ya Mwalimu na Abdu ilikuwa tofauti kama kichuguu na mlima Kilimanjaro. Mwalimu kwa jeuri yake na kujiamini alikokuwa nako asingeweza kuandikiwa hotuba na mtu kama Abdu ambaye hata elimu yake Mzee Mohamed Said haiongelei sana zaidi ya kumsifia kuwa alikuwa na akili sana! Hotuba hii ninayoinukuu hapa chini aliitoa mwaka 1995 kwenye Mkutano Mkuu wa CCM ambao hatimaye ulimteua Mkapa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Hakuwa ameiandika popote:

"Ukabila bado upo. Kwa hiyo, ukabila lazima uendelee kupigwa vita. Hapana kukaa na kusema "Tanzania hatuna ukabila". Hapana. Watu hatujawa Watanzania bado. Kwa hiyo, lazima tuendelee kuupiga vita. Na watu wana udini dini. Kuna watu kabisa wanatamani nchi hii iwe ya Kikristu, wajinga. Kuna watu wanatamani nchi iwe ya Kiislamu, wajinga. Natumia neno zuri wajinga, sisemi wapumbavu. Wajinga.

Tunataka rais wetu, akiwa Mkristu, ajue hatumchagui kwa sababu ya Ukristo wake. Akiwa Muislam, ajue hatukumchagua kwa sababu ya Uislam wake. Hatumchagui awe rais wa Wakristu wala awe wa Waislam, na tunataka hilo alikubali kwa dhati na alisimamie na ndiye kiongozi wetu. Alisimamie kwa dhati bila woga, ndiye kiongozi wetu.Katika nchi changa namna hii, ambayo watu haraka sana hukimbilia ukabila, haraka sana hukimbilia udini, tunataka kiongozi awe imara kabisa katika mambo haya." Niishie hapo kunukuu na ni mshukuru MSOMAJI RAIA wa Raia Mwema ya leo.
 

Mjadala haujafungwa kama wewe umechoka au unakereka na michango ya Mohamed Said unaweza kukaa pembeni kuna umati wa Watanzania wanafuatilia huu mjadala.
 


Hapo unajiona umeandika sana,si ndiyo?
Too bad because we can clearly feel your emotions on this,well you can call it whataever you wish,but those who are independent thinkers and anti-religious people like you have already understood the reality,

pia,i am warning,usijaribu kuzisemea hisia za watu na kutolea conclusion,kama wewe umeamua kuziona ni histohisia na kukubali kwa dhati ya moyo wako basi fanya hivyo na uamini hivyo moyon mwako,na usijaribu sasa kuja na kusema ya kwamba mass kubwa ya watu waamini hivo,usiwashikie watu akili zao,kila mtu ana akili zake na ana uwezo wa kupima upi ni ukweli na upi ni uzandiki,Mohamed Said hajamshikia mtu kabora hapa..
 
Ulitaka awape kipaumbele gani? Hivi unajua ni wazee wangapi wa Jijini Dar amb ao walipewa kipaumbele katika serikali (na watoto wao) kulinganisha na wazee wengine? Ulitaka afanye nini awajengee chumba Ikulu?


Punguza hasira,Calm down,hakuna unaerushiana ngumi hapo,usije kuvunja keyboard za laptop yako bure..!
Hivi kabla hujaandika ulifikiri kidogo ukakasi wa maandish haya?kwa hakika yanaelezea kwa ndani kabisa uhalisia wa chuki na uzandiki uliojificha deep inside your heart,hii ni mbaya sana hasa kwa watu wenye ufaham wa kuzisoma hisia za mtu kama sisi,unasikitisha sana kwa kweli.
 
Mjadala haujafungwa kama wewe umechoka au unakereka na michango ya Mohamed Said unaweza kukaa pembeni kuna umati wa Watanzania wanafuatilia huu mjadala.

Ritz,

Hawa ndugu zetu ni watu wa kuonewa huruma kwa maana
wanakikimbilia chombo kinachozama.

Walimleta Martin Kayamba na kumtaka awe shujaa wao.
Kwa kweli mimi nilitingisha kichwa kwa masikitiko na huruma.

Najiuliza hivi hawa wanamjua huyu Martin Kayamba?

Wewe ukawaambia huyu bwana umaarufu wake ulikuwa kufuga
kuku pale Muheza.

Mimi nikawaeleza wenzake walikuwa wanamuonaje - kibaraka
wa Waingereza aliyependa kujikomba kwa bwana.

Siku nyingi nikijua kuwa hawa ndugu zetu hii historia ya Tanganyika
hawaijui lakini kinachowasukuma kuitetea ni ule mshtuko uliowapiga
baada ya kusoma yale waliyokuwa wamefichwa kwa miaka mingi.
 
Ulitaka awape kipaumbele gani? Hivi unajua ni wazee wangapi wa Jijini Dar amb ao walipewa kipaumbele katika serikali (na watoto wao) kulinganisha na wazee wengine? Ulitaka afanye nini awajengee chumba Ikulu?

Tarehe 27 Aprili, 1985 Nyerere akijulikana kama Baba wa Taifa katika sherehe kubwa Ikulu alitoa Medali 3,979 kwa Watanzania waliochangia maendeleo ya Taifa letu.

Katika waliopewa Medali alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo peke yake.

Sasa wewe Mwanakijiji hebu jiulize hawa wazee wengine wa Dar es Salaam waliyomsaidia katika harakati za uhuru siyo wazalendo.

Hapo juu kwenye hotuba yake mwenyewe anakiri walimsaidia sana na walianzisha TANU lakini hata mmoja aliyempa Medali.
 

Too bad,kumbe Mwanakijiji upeo wake wa kufikiri upo chini kias kile?
I can not believe..
 
Angalau nakufahamu kidogo Mzee Mohamed. Mtu ambaye hakuwa upande wa wazee wako huyo lazima alikuwa kibaraka wa wakoloni. Mtu ambaye alikuwa upande wa Mwalimu, hata kama ni Muislam mwenzako kama akina Rashid Kawawa, huyo naye ni kibaraka wa mfumokristo! Mtu wa ajabu sana mzee wewe ambaye unadhani uko sahihi wakati wote.
 
Hivi kweli Rais wa NCHI anaweza kuhangaika kujua nani apate medali? Awape medali hata waliompelekea maharage na dagaa kule Magomeni? Masuala ya medali hayaandaliwi na ofisi ya Rais jamani. Nchi haiendeshwi hivi. Hata familia zetu sio kilakitu ni baba.
 

Mohamed Said kaja na kitabu, wewe umekuja na shutuma, wewe ndio ulitakiwa ulete ushahidi wa tuhuma zako, umeshasahau hii mada imeanzishwa na nani na kwa nini?
 

Ushahidi wa uchochezi wake nimeuweka hapo juu ya mada kuu wenye rangi ya bluu ambao ni hotuba stahiki ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere inayopingana moja kwa moja na madai ya Mohamed Said kwa kila neno mfano, Mohamed alisema Mwalimu alisema hakumbuki Abdul alikuwa na cheo gani, lakini Hotuba hiyo imetufichulia ukweli kuwa Mwalimu alisema wazi kuwa Abdul alikuwa Katibu wa TAA!

Je unataka ushahidi gani kudhihirisha uongo na uchochezi wa Mohamed Said?
 
Mohamed Said kaja na kitabu, wewe umekuja na shutuma, wewe ndio ulitakiwa ulete ushahidi wa tuhuma zako, umeshasahau hii mada imeanzishwa na nani na kwa nini?

Ndugu yangu pembuka basi,

Kitabu alichokuja nacho ndicho ninachokipinga na nimekuja na vielelezo mbadala kama vile Hotuba ya baba wa Taifa, na historia ya usharika wa kanisa katika Ukombozi wa Tanganyika ambavyo kwako na wenzio vilikuwa vigeni kabisa!
 

WC,

Unasema sijzungumzia elimu ya Abdulwahid Sykes.

Nitaanza na elimu ya baba yake, Kleist Sykes pamoja na ndugu zake wengine aliolelewanao:


[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ''Kleist was enrolled in a German school which was located at the Ocean Road Hospital where he learnt German, typing and shorthand, a rare and precious skills for an African to acquire at that time.

In the household of Affendi Plantan, Kleist was raised with Affande Plantan’s own children, Schneider Abdillah, Ramadhani Mashado and Thomas Sauti a child of a distant relative.

All these children received a good education which enabled them to become important personalities in Dar es Salaam.

Mashado Plantan was employed as a policeman with the title of ‘English-Speaking Policeman’ and later became editor of his own newspapers. His first paper was Dunia.

During the Second World War he founded a newspaper Zuhra.
This was TAA's mouth piece and later TANU and Nyerere's.Thomas Sauti became a school teacher, Schneider was a farmer and later in his life joined Sheikh Hassan bin Amir to became secretary of Daawat Islamiyya (Muslim Call).

Kleist beat them all. He excelled more than his brothers.

He became a man of ideas and a founder of various organisations.

But above all Kleist left a legacy.

His name would come to be associated with the struggle of the people of Tanganyika against colonial oppression.''

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sasa tuje kwa Abdulwahid Sykes:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ''Abdulwahid-the name means the ‘servant of one and only’ meaning Allah-was the grandson of Sykes Mbuwane, a lone wanderer who laid down his life in Tangayika, serving the Germans.

In school Abdulwahid was always on top of his class.

After completing his lower primary education at Al Jamiatul Muslim School he was selected to join Dar es Salaam Government School where he was taught by Mwalimu Mdachi Sharifu.

Sharifu was the President of Tanganyika Territory African Civil Services Association (TTACSA).

Abdulwahid completed standard ten, did his qualifying examination for Makerere College and passed.

On considering his father’s political background, the colonial government refused to recommend Abdulwahid for Makerere entrance on the pretext that the candidate was under age.

Abdulwahid was at that time seventeen years old.

He was considered underage to pursue studies at Makerere but old enough to be conscripted into the King’s African Rifles (KAR).
''[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sasa kwa hali ilivyo leo hotuba ya Nyerere haina maana yoyote kwa Waislam.

Mwaka huo 1995 wakati Nyerere anatoa hotuba hiyo mimi nilialikwa na Muzdalifa
kuhutubia mkusanyiko wa Waislam Mnazi Mmoja katika kuadhimishwa mwaka mpya wa Kiislam.

Katika hotuba yangu ile ndiye kwa mara ya kwanza niliposikia jambo ambao si kuwa lilinishtua
bali niliona kama niko kwenye ndoto.

Hili jambo sipendi kulisema na ni katika mambo yanayosikitisha sana.

Hivi unajua ukilitaja jina la Nyerere Waislam wanamlaani?
Wanasema, ''Laanatullah.''

Siku ile mwaka 1995 ndiyo kwa mara ya kwanza niliposikia Waislam wanamlaani Nyerere.

Hapa ndipo tulipoifikisha nchi yetu.
Haitotusaidia sisi kujifanya mambo yote ni shwari.

Hata kama utaweka hotuba elfu za Nyerere hakuna Muislam atakezipatiliza.
 
Mohamed Said kaja na kitabu, wewe umekuja na shutuma, wewe ndio ulitakiwa ulete ushahidi wa tuhuma zako, umeshasahau hii mada imeanzishwa na nani na kwa nini?
Ajabu sana..!
badala ya mleta shutuma kuja na hoja za kupinga,yeye anadai hoja za kuthibitishiwa shutuma zake,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…