Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


WC,

Medali zile alitunuku Nyerere mwenyewe na kuna mambo wewe
huyajui.

Mwenyekiti wa Kamati ile ya Medali yu hai ingawa sasa hivi
amestaafu.

Alimuuliza mbona watu fulani hawamo?

Nakupa changamoto tafuta jina la mwenyekiti huyi na uwajuvye
wanajamvi.

Ukilijua jina hilo kuna mengi utayapata.
 
Naamini hotuba hiyo hainamaana kwako tu kwakuwa inavuruga malengo yako, lakini usiwasemee waislamu wa Tanzania kuwa haina maana,
 
Angalia uongo huo uliotukuka ulivyo. Waislam wepi hao wanaomlaani Mwalimu? Abdulwahid akanyimwa kwenda Makerere at the of 17! Alifikaje hiyo standard 10 katika umri huo mdogo? Mtu wa standard 10 anamwandikia hotuba mtu mwenye M.A ya Edimburgh! Kweli?
 


Yericko,

Kwangu mie si lazima kusikiliza ile hotuba kwani nishaisikia.

Ili wewe udhihirishe kuwa mimi ni muongo ni lazima, ni muhimu
sana tena sana kabisa utuwekee clip jamvini tuisikilize.

Hivi ndivyo nilivyoandika katika kitabu changu, ''The Life and
Times of Abdulwahid Sykes...'':

Nyerere himself has never talked about this election
or how he came to lead the Party in Dar es Salaam.

The nearest he got to reflect on Abdulwahid was in
the farewell speech to Elders of Dar es Salaam, and
unfortunately his memory failed him as he could
not recall what post Abdulwahid was occupying
when he (Nyerere) joined TAA in 1952.
 

Iko wapi hiyo hotuba? si ulisema utaileta mara ooh, wanataka pesa tukakupa offer kuwa wewe sema tu pesa ngapi sisi tutakulipia, mpaka sasa umeshindwa. Umebandika maandiko yako unayodai kuwa ni hotuba, nayo pia hayajaonesha ni wapi Mohamed Said alipofanya uchochezi wala dhihaka. Sana sana hayo mabandiko uliyoweka yanakusuta wewe mwenyewe, hujaona palipoandikwa kuwa hata jina la TANU walikuja nalo kina Sykes kutoka walipokuwa Burma?

Ukipeleka mahala shutuma inatakiwa utoe na ushahidi, huna mpaka sasa huo ushahidi na shutuma zako kwa lugha ya kitaalam ni "futile".

Unalo? kaa upate darsa kutoka kwa Mohamed Said ujuwe hii nchi imetoka wapi.
 
Hapa ni JF. Weka jina la huyo Mwenyekiti. Mimi siwezi kulipata. Vinginevyo, hii nayo ni "ngano" ya kawaida ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yako yasiyo na ushahidi kwa Mwalimu.
 
Ina maana ipi baada ya kuiuwa nchi kwa miaka 24 mfululizo?
Laanatullah zomba. Mwalimu kaacha nchi bikra kabisa hii. Mnachinjana wenyewe sasa hivi badala ya kuchinja ng'ombe na mbuzi.
 
Last edited by a moderator:
Angalia uongo huo uliotukuka ulivyo. Waislam wepi hao wanaomlaani Mwalimu? Abdulwahid akanyimwa kwenda Makerere at the of 17! Alifikaje hiyo standard 10 katika umri huo mdogo? Mtu wa standard 10 anamwandikia hotuba mtu mwenye M.A ya Edimburgh! Kweli?

WC,

Mimi siwezi kusema uongo.

Ni haki yako kushangaa vipi alimaliza darasa la 10 katika
umri mdogo kama ule.

Mimi nimeshangazwa na mengi ya marehemu Abdu Sykes.

Moja wapo ni kuona shajara zake (diaries) alizokuwa akiziandika
kwa hati mkato wakati wa kuunda TANU kati ya 1950 - 1954.

Hilo la kusema darasa la kumi kuandika hotuba nadhani unaandika
hivyo kwa kukosa kujua wakati ule elimu ilikuwa ya kiwango gani.

Jitulize na soma utajua.
Usifanye haraka ya kuandika ikiwa huna elimu ya kile unachokiandika.

Nakuombeni msome vizuri post zangu ninapozungumzia haya mambo
ambayo nyingi yanakuchomeni nyoyo zenu.

Hii document asili yake ni TAA Political Sub Commitee iliyoundwa mwaka
1950.

Wajumbe wa Kamati hii ni hawa wafuatao:


  1. Mufti Sheikh Hassan bin Amir
  2. Abdulwahid Sykes
  3. Dk. Vedasto Kyaruzi
  4. Hamza Mwapachu
  5. Said Chaurembo
  6. John Rupia
  7. Steven Mhando

Kamati hii ilikuwa na mwanasheria wake Earle Seaton.

Ukipenda unaweza kumtia Seaton kama mjumbe wa nane wa TAA Political
Subcommittee.

Seaton aliisaidia sana TAA katika mawasiliano yake na serikali ya kikoloni.

Seaton ndiyo aliandika ile petition ya Meru Citizens Union kwenda UNO katika
ule mgogoro wa Meru Land Case mwaka 1952.

Abdu Sykes ndiye aliyemleta Seaton TAA.
Walikuwa marafiki wa muda mrefu.

Katika kitabu changu nimeandika maneno haya:

The author was for the first time informed of the existence
of this document by one of Mwapachu's children, Juma Volter
Mwapachu.

He was informed that Mwapachu took great pridein having
participated in the drafting of this document.

In her book Listowel mentioned this document and its historical
significance to the political history of Tanganyika.

But it was Pratt who analysed the document in detail.

The document was first consulted by Pratt in 1959 in a file of the
Committee on ‘Constitutional Development Report/and Despatches
to the Secretary of State' no. 1146-6, Dar es Salaam Secretariat Library.

Although this file is available at the Tanzania National Archives, the
document is missing.

The author was informed that a microfilm of the document was available
but that too could not be traced.

For more information on loss of historical documents see M. Said,
‘In Praise of Ancestors Revisited' in Africa Events, London March,
1989, pp. 50-51.
 

Kwa hiyo WildCard ni uongo Nyerere akutoa Medali Ikulu.
 
Hapa ni JF. Weka jina la huyo Mwenyekiti. Mimi siwezi kulipata. Vinginevyo, hii nayo ni "ngano" ya kawaida ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yako yasiyo na ushahidi kwa Mwalimu.

WC,

Mimi kama ninavyosema.
Siko humu kufanya ubishi.

Kwani ikiwa JF ndiyo nini?
Ndiyo iniondolee muruwa wangu?

Niko hapa kueleza yale niyajuayo.

Ikiwa toka awali sikutaka kuweka jina
la Mwenyekiti wa Kamati ya Medali ni
kwa kuwa nilikuwa na sababu.
 
Laanatullah zomba. Mwalimu kaacha nchi bikra kabisa hii. Mnachinjana wenyewe sasa hivi badala ya kuchinja ng'ombe na mbuzi.

Kwi kwi kwi teh teh teh, unajionesha upeo wako. Wala huwa sitatizwi na hayo, unajuwa kuwa kwetu Kariakoo?
 

WC,

Hayo maneno unasema wewe.

Maandishi yangu yako wazi peupe yanasomwa
kwingi.

Una haki ya kuamini upendavyo.
 
Laanatullah zomba. Mwalimu kaacha nchi bikra kabisa hii. Mnachinjana wenyewe sasa hivi badala ya kuchinja ng'ombe na mbuzi.

Wewe kweli ndio mjinga eti unalaani waulize wenye kuujua uislamu kama mtu analaaniwa kirahisi hivyo kungekuwa na fimbo ya kumcharaza mtu viboko ningeanza na wewe, Nchi bikra ndio watu wanunue sukari kwa foleni tv tukaangalie kwa jirani mimi nakumbuka kombe la dunia tulikuwa tunaenda kuangalia kenya huyu baba ahhh si mpatii picha!!!!!!!!!!!!
 

Huyo wala asikushughulishe, darsa limemuingia na sasa anapingana na nafsi yake.
 
Mzee wangu Mohamed Said umesema mwenyewe Abdulwahid Sykes kamaliza std 10.Hivi unajua Mwl kipindi hicho tayari alikuwa na MA na alikuwa na uwezo mkubwa kumzidi A Sykes sasa unapotundanganya hata makabrashi (hotuba) Mwl kaandikiwa huoni huko ni kukidhalilisha kitabu chako.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo WildCard ni uongo Nyerere akutoa Medali Ikulu.
Kutoa medali kitu kingine na kuandaa orodha ya watakaopewa hizo medali suala jingine. Jamani, tujifunze jinsi serikali na vyombo vyake vinavyofanyakazi. Nikuulize swali moja Ritz: Ni Jakaya Kikwete aliyemkatalia dhamana Sheikh Ponda? Kwa nini yooote yaliyofanyika wakati wa Mwalimu lawama zooote anabebeshwa yeye?
 

Hujaiona na kuisoma hiyo hotuba hapo juu ya rangi ya bluu?

Ajabu unauliza hiyo hotuba lakini unauliza swali linalotoka ndani ya hotuba hiyohiyo,

Kwakukujbu swali lako, naomba nikuulize swali:

Mtoto huzaliwa ndipo apewe jina au hupewa jina kabla ya kuzaliwa?

Ukijibu, ndilo jibu la swali lako mkuu!
 
Achana kabisa na habari za kuokoteza vijiweni. Hauna ushahidi juu ya hili la mwenyekiti wa kamati ya medali. Ni aibu kwa mtu mzima kama wewe. Lolote linalosemwa vibaya kumhusu Mwalimu hii ni habari kubwa kwako. Wanaokufahamu wanajua unataka uambiwe nini kumhusu Mwalimu. Wanajua unachotaka ukisikie kwa Mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…