Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Jakaya alitunukia wale wazee 17 ambao historia ya kivukoni inawakubali. Sio akina Kiyate, Plantan, Amir,..., kumbe unamkubali Jakaya ee? Matunda ya mfumokristo huyo.

Mwanzo mzuri.

Chaguo la Mungu.
 
Cha ajabu sasa: Wakoloni hao wakamkatalia Abdu kwenda Makerere kwa sababu ya umri mdogo lakini katika umri huohuo wakamkubalia kujiunga na jeshi. Hayupo. Alishafariki tangu 1968. Atatuthibitishia nani haya Yarabi!

WC,

Kwa nini unajipa shida yote hiyo?
 
MM,

Ushanijua mie mtu wa porojo.
Sasa nini kinakushughulisha?

Mtaje huyo mwenyekiti wa kamati ya medali; watu wakamuhoji unasubiri hadi afariki??????.

Kuwa na hisani mzee wangu, wengne humu tu wajukuu kwako tusaidie tupate kuyajua haya.
 

Nguruvi3,

Tulia kisha andika kama msomi.
Nimekusoma sipendi unapoandika namna hii.

Lugha ya ''uongo,'' shutuma nk. nk. nk. hainogeshi
mjadala.

Ila nitakupa kidogo katika mambo haya ya siasa.
Kuna kitu kinaitwa ''changing horses mid stream.''

Ikiwa hujui hiyo ni kitu gani jishughulishe kusoma
kidogo na hiyo ambayo kwako ni ajabu itakuwa si
ajabu tena.

Waarabu wana msemo, ''Sababu huondoa ajabu.''
 
Mtaje huyo mwenyekiti wa kamati ya medali; watu wakamuhoji unasubiri hadi afariki??????.

Kuwa na hisani mzee wangu, wengne humu tu wajukuu kwako tusaidie tupate kuyajua haya.

 
Ngoja mie nikutajie ni John Malecela. Nenda kamuulize.
Mwaka 1985 John Malecela alikuwa mbali kabisa na Ikulu ya Mwalimu. Alikuja okolewa na Ali Hassan Mwinyi kwa kumteua kuwa RC, baadae balozi, kisha WaziriMkuu na Makamu wa Rais. Usijiingize kwenye majungu ya vijiwe vya Kariakoo.
 
Nguruvi3 Mimi ni kijana na kwa bahati nimeyaona pasi jicho la udini yanayoendelea nchi hii. Nakumbuka nikiwa sijafikisha umri wa kupiga kura mwaka 1995 nilikuwa nasikiliza na kufuatilia yale yaliyokuwa yanatokea kwenye uchaguzi ndani ya chama. Kwa kweli nilikuwa shabiki wa Kikwete tena kwa sababu tu alikuwa anaonekana kijana.

Sikumuona kuwa ni Muislam na hata miongoni mwetu walikuwepo wengi sana waliokuwa wanamtaka Kikwete au Salim japo hakuingia kwenye kinyang'anyiro. Na kumbuka hapo nilikuwa Musoma kwa akina Nyerere na hakuna niliyemuona akionyesha hisia za kidini. Rudi 2005 kwangu Salim ndio alikuwa chaguo na nafikiri wajumbe wengi tu wa NEC na mkutano mkuu walikuwa kwenye pande mbili kubwa za Salim na Kikwete...........humo wamo wakristo wengi tu na hawakuuona Uislam wa Kikwete/Salim.

Sasa hapo ndipo naposhangaa hivyo vyanzo vya MS ni vya aina gani. Na hapo huwa najiuliza:
Inawezekana wanaomwambia wanajua anapenda kusikiliza nini kwa hiyo wanampa ukweli uliopindishwa.

Au ni mtunzi mzuri wa ngano mwendelezo, unampa habari kidogo anaongezea nyama kwa wingi ili kufurahisha hadhira yake.

Au kuna mradi anoutumikia ambao unamtaka kujenga ovu lolote kuhusu Mwalimu/Ukristo kufurahisha wenye mradi.

Au ni njia rahisi ya kuwafanya Waislam wajione dhalili na kutofikiria kuweka mikakati ya kujikwamua ki-elimu ili yeye na wenzake wabaki "star" miongoni mwa wajinga!

Au ni chuki aliojengewa na yeye kuikuza kutokana na masimulizi na sasa anaweka "platform" ya kulipa kisasi.

Huwa siishi kujiuliza maswali napowasikia watu kama MS wakiweka jitihada ya kubomoa na kufarakanisha Taifa. Na kwa kweli ukimsoma katikati ya mstari utagundua kuna mwangwi wa wa moja ya maovu hapo juu. Na akishatia neno Uislam basiii wanyonge wake wananywea......Umpinge mtetezi wa "dini" thubutuuu.
 

P,

Nakujibu kwa heshima zote mdogo wangu.
Umenikumbusha nilikotoka mimi miaka mingi nyuma.

Endelea kusoma kuwa na akili ya udadisi mengi utajua.
 
Mohamed, sidhani neno uongo ni tusi.
Umesema wakristo walinong'onezana wasimpe mwislam tena. Ukishasema hayo tu maana yake ilikuwa ni siri yao hivyo haikusikika. Lakini zaidi ya hayo hatuwezi kutegemea maneno tu ya kusikia tu yasiyo na ushahidi. Huo utakuwa mwanzo wa kuwa na taifa la majungu. Kesho mwingine ataibuka na lake na hivyo kuchanganya umma. Kama una proof weka hapa ndio maana ya mnakasha.

Kitu cha kushangaza sana, malalamiko ya waislam ilikuwa dhidi ya CCM kwa uonevu wa miaka mingi ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wazee katika uongozi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa inasemwa hadi walipoamua kujiunga kwa wingi CUF ili kutafuta haki.
Sasa ilikuwaje tena wakanong'onezana misikitini wasimchague mkataoliki badala ya kunong'onezana wamchague Lipumba wa CUF

The whole story lacks connection for sober mind individuals na hii inatokana na ukweli kuwa kila kitu kipo fabircated.
Muhimu zaidi, je, kwa kunong'onezana iwe waislam au wakristo kuna aliye na afadhali sasa hivi? Inflation 20% wizi umekithiri na taifa lipo katika mzozo wa masuala ya kijamii, migomo n.k. nani anayefaidika kwa hilo.

Haiwezekani 2013 tukafikiri kwa kutumia majina na si vichwa vyetu! impossibe.
Niambie wapi udini katika Afrika umelata unafuu kwa kundi fulani!
 

Nanren,

Hatujapata kulala usingizi toka 1968 ukweli ulipotudhihirikia.

Ndiyo maana leo tupo hapa jamvini unasoma mengi yanakushangaza.

Jibu la haraka kutoka kwako ni ''uongo,'' ''hii haiwezi kuwa kweli,''
''huyu Mohamed ni mtu hatari nk. nk. nk.''

Watu wengi walipata mshtuko kwa mara ya kwanza waliposoma kitabu
changu.

Narudia kusema tena hapa mshtuko wa Prof. Haroub Othman.

Sikushangai wewe.

Lakini nakuambia yote niliyoandika ni kweli.
 
NYERERE huyu,ndio kaandikiwa hotuba na market master!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mohamed Said muogope GOD

Son...

Nimeeleza kisa cha hotuba hii si muda mrefu kuwa chanzo ni Political Sub
Committee ya TAA 1950 na wajumbe wake walikuwa hawa wafuatao:


  1. Sheikh Hassan bin Amir
  2. Abdulwahid Sykes
  3. Hamza Kibwana Mwapachu
  4. Dk. Vedasto Kyaruzi
  5. Steven Mhando
  6. Said Chaurembo
  7. John Rupia

Mshauri wa kamati hii alikuwa Earl Seaton.

Lakini naona unajisikia faraja kuweka kejeli kidogo.
Huna maswali kuhusu Seaton nk. nk.

Umevutiwa na ''Market Master.''

Si kitu nami nitakujibu.

Huo mshahara wa ''Market Master'' ndiyo uliokuwa ukifadhili TAA na TANU.
Zile ''lunch'' na ''diner'' pale nyumbani kwa Abdu Sykes Stanley Street
vyakula vilikuwa vinatoka katika ofisi ya ''Market Master.''

Hizi ''lunch'' na ''diner'' zikihudhuriwa na vigogo wa siasa wa wakti ule na
hapo ndipo palipokuwa ikipangwa mipango ya kuunda TANU na mbinu za
kumng'oa Mwingereza.

Aliyekuwa akipika hicho chakula na kuwahudumia waheshimiwa hawa alikuwa
mama yangu Bi Mwamvua biti Masha mke wa ''Market Master.''

Ikiwa wewe ni mwizi wa fadhila na ukaona huwezi kushukuru kwa ihsani
si kitu.

Kipi kitanishangaza mimi leo ikiwa hata cheo cha ''Market Master'' katika TAA
kilisahauliwa na medali kama mmoja wa waasisi wa taifa hili kaja kupewa baada
ya miaka 50?
 

TANU Supporters accompany Nyerere to the airport before his departure to deliver a speech UNO

Cha kuchekesha hapa anatajwa Nyerere peke yake wakati hawa wote wanajulikana majina yao.

Na wengine wamejitolea nguvu zao pamoja na mali lakini wametupwa nje ya historia ya TANU pamoja na uhuru.

Hao waswahili wanywa kahawa ndiyo waliomsindikiza Nyerere uwanja wa ndege kwenda UN.
 
Abdu ndie kila kitu kwenye kile kitabu chako. Kitabu kikijatengenezwa sinema ndie atakuwa "steringi". Ni vizuri watu tukamfahamu thoroughly.

WC,

Ukitaka awe kila kitu atakuwa kila kitu.

Lakini Abdu asingesikizwa na umma wa Dar es Salaam kama asingeungwa
mkono na Sheikh Hassan bin Amir na Baraza la Wazee wa TANU chini ya
Sheikh Suleiman Takadir.

Na wengine wengi pale New Street kama Idd Tosiri, Idd Faiz Mafongo na
wengineo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…