zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Mohamed, sidhani neno uongo ni tusi.
Umesema wakristo walinong'onezana wasimpe mwislam tena. Ukishasema hayo tu maana yake ilikuwa ni siri yao hivyo haikusikika. Lakini zaidi ya hayo hatuwezi kutegemea maneno tu ya kusikia tu yasiyo na ushahidi. Huo utakuwa mwanzo wa kuwa na taifa la majungu. Kesho mwingine ataibuka na lake na hivyo kuchanganya umma. Kama una proof weka hapa ndio maana ya mnakasha.
Kitu cha kushangaza sana, malalamiko ya waislam ilikuwa dhidi ya CCM kwa uonevu wa miaka mingi ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wazee katika uongozi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa inasemwa hadi walipoamua kujiunga kwa wingi CUF ili kutafuta haki.
Sasa ilikuwaje tena wakanong'onezana misikitini wasimchague mkataoliki badala ya kunong'onezana wamchague Lipumba wa CUF
The whole story lacks connection for sober mind individuals na hii inatokana na ukweli kuwa kila kitu kipo fabircated.
Muhimu zaidi, je, kwa kunong'onezana iwe waislam au wakristo kuna aliye na afadhali sasa hivi? Inflation 20% wizi umekithiri na taifa lipo katika mzozo wa masuala ya kijamii, migomo n.k. nani anayefaidika kwa hilo.
Haiwezekani 2013 tukafikiri kwa kutumia majina na si vichwa vyetu! impossibe.
Niambie wapi udini katika Afrika umelata unafuu kwa kundi fulani!
Ukiijuwa sababu ya kiongozi wa nchi katika Afrika yenye serikali isiyo na dini kupewa uwenye heri na kutaka kupewa utakatifu utakuwa umeshapata jawabu.