Duh..yote tisa lakini kwa stori tu.. mzee hujambo!! maana ukidhania hawezi kuja na simulizi la Marehemu basi anakuja nalo jingine.. sasa sijui anataka tuamini nini kwenye hili stori.. jamaa aliamua kufa kuliko kusoma ukweli?
Hata Nyerere ktk kusherehekea Birthday yake mwanzoni mwa mwaka 1999 alitamba kuwa ana uhakika wa kuishi mpaka miaka 100! ghafla tukamuona uwanja wa ndege akisindikizwa akiwa anafuraha kuelekea London kwa matibabu lakini alirudi akiwa maiti
Shekh Mohamed,
Huyu I ni nani?
ha ha ha,hapo ndipo ninapomfurahia mzee wetu.Tusubiri labda atakuja na simulizi nyingine
Mohamed Said
Samahani kwa kukirudisha nyuma. Hili suala la Abubakar Ulotu bado halijakaa vizuri kichwani kwangu. Kama ndiye yeye aliyeandika (japo umesema tusimwite "mwandishi") kitabu Cha Historia ya TANU ambayo hukuipenda, halafu ni yeye huyu huyu, akaja kuanzisha chama cha kiislam cha NRA mwaka 1995, ni kitu gani kilimbadilisha msimamo kutoka kwenye msimamo wake wa zamani? Ni baada ya kukutana na wewe?
Hiki kisa nimekileta baada ya Jasusi kumtaja Mzee Kitundu.
si ndio maana nimesema kwa stori hujambo? tatizo la stori zako ni hilo tu ni stori na inabidi tuzikubali hata kama akili zetu zinakataa ukweli wake au zinapotusukuma kuona hila au khiana iliyofichika ndani yake. Ujanja wako ambao ni wa tangu utoto ndio umekusaidia kuwavutia watu kukusikiliza bila kuwafanya wajue kuwa katika kila unachosema una lengo ndani yake - kuchochea mfarakano kati ya Wakristu na Waislamu wa Tanzania. Lengo lako liko wazi - Waislamu wawachukie Wakristu na wakipata nafasi wawatende kwani ndio wenye kuwadhulumu..
Maandishi yako yote yamejaa hii element of hatred.. kwako Dar-es-Salaam ilikuwa ni Waislamu, kwako wazee wako wenye kustahili heshima ni Waislamu, kwako wanaoudhulumiwa Tanzania ni Waislamu, kwako wenye hali ngumu ya elimu, afya na kwingine ni Waislamu. Macho yako kwa sababu ya chuki dhidi ya Ukristu na Wakristu hayakuruhusu kuangalia dhulma katika jamii nje ya Waislamu. Hujali nani anahujumiwa na mfumo wa utawala wa kifisadi - as a matter of fact - wewe utawala huu wa kifisadi ambao umetengenezwa na CCM (zao la tANU) haukusumbui sana.
Badala yake umetengeneza kama yule sanamu wa hadithi ya Sungura; wewe na wenzio mmezidi kumchapa vibao na kumtishia kuwa utamchapa na mguu.. hamjioni jinsi mnavyonasa tu..
I had crossed swords with Kimalando when we were transforming TAA into TANU when we at the headquarters backed Yusuf Olotu and other patriots and advised them to sideline him and register the new party.
Kimalando although was among founders of TANU in Dar es Salaam, once back in Moshi he refused to register the party in Kilimanjaro.
Reports reaching TANU headquarters were that Kimalando was collaborating with the colonial government to frustrate registration of the party.
He was ousted from the party and he joined UTP.
Kimalando was a seasoned politician having been in politics since the early days of the African Association.
Kimalando claimed to be among the founder members of the Association together with Sheikh Hussein Juma who was later to be Vice President of the United Tanganyika Party UTP, an opposition party formed by the British to oppose TANU.
Nadhani ushamjua huyo ''I.''
Hawa ndiyo wenye TANU yao waliosahauliwa hata kutajwa katika kitabu cha Kivukoni.
Hakika ahali yangu Mohamed Said wewe ni bahri ya historia na unamengi sana kama wanajamvi wangetulia ungetupa mengi zaidi.
Allah akubarik
MM,
Dunia zetu ni tofauti sana.
Nimesoma hapa kuwa ulikuwa CCM sasa uko CHADEMA.
Mimi wazee wangu ndiyo walioasisi AA kisha TANU.
Lazima tuone mambo kwa jicho tofauti sana.
Jasusi,
Katika wazee wako hapo Musoma mnae mtu kama Kleist
na mwanae Abdulwahid.
Watu wanaoweza kukupa historia yao ya harakati kuanzia
Wajerumani walipotia mguu Tanganyika hadi walipoingia
Waingereza?
Hapo Musoma mna Askofu aliyekuwa ndani ya TAA kisha
TANU kama Mufti Sheikh Hassan bin Amir.
Hapo Musoma mnao mfano wa Sheikh Mohamed Yusuf
Badi na mwanafunzi wake Yusuf Chembera wa Lindi
waloasisi TANU na kupambana na fitna za Kanisa Katoliki
lilokuwa linawatisha Wakristo wasijiunge na harakati za
kudai uhuru?
Sitaki nionekane nasimanga lakini ngoja nikuambie neno
langu la mwisho...
Hatungeweza sisi kuona historia hii ya wazee wetu inatupwa
nasi tukakaa kimya.
Hivi unajua kuwa siku ya Nyerere Day ndiyo Waislam nasi
huwaadhimisha mashujaa wetu?
Najua fika.
Hukuwa unajua.
Huu ndiyo ukweli.
Hivi ndivyo mambo yalivyo.
Unaona anavyosimulia tofauti kabisa... "we" is the operating word..
Mzee Said hata mimi wazee wangu ndio walikuwa waasisi wa AA na TANU hiyo hiyo.. so dunia zetu haziko tofauti sana. Tofauti ni kuwa wazee wako wewe ni wa dini moja tu...
Mohamed,
Hii dhana kwamba kanisa Katoliki lilikuwa linatisha wafuasi wake wasijiunge na harakati za kupigania uhuru unahitaji kuifanyia utafiti zaidi. Kwa nini nasema hivyo? Katika vitabu vyote nilivyosoma kuhusu harakati za uhuru Tanzania ni wewe peke yako unayedai kuwa Wakatoliki walikatazwa kujiunga na harakati za kupigania uhuru. Pili, kama hiyo ingekuwa ni kweli, Sivalon asingekuja na kitabu chake kuonyesha jinsi kanisa katoliki lilivyokuwa karibu na harakati za kupigania uhuru pamoja na ukaribu wake na Julius Nyerere. Kanisa ambalo ningekubali kuwa lilikataza wafuasi wake kujiunga na harakati za uhuru nadhani ni Anglican, kwa sababu hili ni dhehebu la Kiingereza. Kaka yangu mkubwa (marehemu) pamoja na Oscar Kambona na John Malecela walifukuzwa shule, kaka yangu akiwa mwanafunzi na Malecela na Kambona waalimu, pale Alliance Secondary School Dodoma mwaka 1954 baada ya wao kuhudhuria mkutano wa TANU. Mwaka 1974 nilisafiri pamoja na Samora Machel kwenye ndege ndogo ya serikali kwenda Musoma. Ilikuwa ni safari ya saa tatu. Mimi nilikaaa kiti cha nyuma na Machel alipoingia akakaa nyuma, mbele kuna Butiku na Braganza (huyu alikuwa Mreno akimshauri Machel, na walikufa pamoja kwenye ile ndege iliyotunguliwa na Afrika kusini.) Anyway, katika mazungumzo yetu nilibaini kuwa yeye pia alikuwa mkatoliki, lakini non practicing. Akaniambia hapa Tanzania, kanisa la Katoliki limejiweka upande wa wananchi wakati Msumbiji, kanisa katoliki lilikuwa bega kwa bega na Wareno kuwakandamiza waafrika. Kwa hiyo haiingii akilini kwamba kanisa ambalo liliwazuia wafuasi wake wasishiriki katika juhudi za uhuru hilo hilo litoe mchango kwa Nyerere kwenda UN 1955, mwaka mmoja tu baada ya kuundwa kwa TANU.
Mzee Said hata mimi wazee wangu ndio walikuwa waasisi wa AA na TANU hiyo hiyo.. so dunia zetu haziko tofauti sana. Tofauti ni kuwa wazee wako wewe ni wa dini moja tu...
MM,
Hapana.
Ungeuliza tu ''we'' ni nani ningekupa jibu.
We ni hawa:
- Julius Nyerere
- Abdulwahid Sykes
- Dossa Aziz
- John Rupia
- And others Dk. Michael Lugazi, Steven Mhando, Zuberi Mtemvu ...at TANU HQ New Street pamoja na Baraza la Wazee wa TANU.
MM,
Ningependa kupata majina yao ikiwa si mushkeli kwako.
Kituko kingine Mwanakijiji na Uislam au Waislam wapi na wapi jamani lini kwako Muislam hakawa na jema bahati nzuri mabandiko yako yapo mengi sana fikra zako kuhusu Waislam zipo wazi kabisa.