Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Samahani chama, ni vile tu imedaiwa na wanafunzi watiifu wa Mohamed Saidi kuwa yeyote asiyekubaliana na ngano anazozimwaga humu hafai kuitwa Muislaam!

Mbona kuna mengi ambayo sikubaliani na Mohamed Said hilo halinifanyi mimi nisiwe muislamu; imani yangu haitokani na mafundisho ya Mohamed Said, mimi ni muislamu kama kuna kitu ambacho sikielewi najua wapi pa kutafuta majibu; sina muda wa kujiingiza kwenye majibishano ya kidini; Mohamed Said anaongelea waislamu walionewa bahati mbaya mimi sipo kwenye kundi hilo na wala sitokani kwenye familia ya kifisadi ila naishukuru sana serikali ya Tanzania na sera za elimu za Mwalimu Nyerere ndizo zimenifikisha hapa kikubwa niliwasikiliza sana wazazi wangu wakati wananisisitiza kwenda shule nilikwenda na si mimi tu pamoja na wadogo zangu; nawapa ushauri wa bure msije mkachinjana kwa imani za kidini dini na siasa havijichanganyi msidanganye; wanaonufaika na vurugu hizo ni watu wachache sana ila wanatumia ujinga wa wengi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:

MM,

Labda unipe jibu.

Ilikuwaje historia hii niliyoandika mimi ikawa haifahamiki
na mashujaa hao niliowataja hadi leo hawajaadhimishwa?
 
Qur'an 2


6. Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini. ***


7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. ***


8. Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini. ***


9. Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui. ***


10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. ***


11. Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. ***

12. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui. ***


13. Na wanapo ambiwa: Aminini kama walivyo amini watu. Husema: Tuamini kama walivyo amini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu. ***


14. Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao na mashet'ani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi tunawadhihaki tu. ***


15. Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo. ***


16. Hao ndio walio nunua upotofu kwa uwongofu; lakini biashara yao haikupata tija, wala hawakuwa wenye kuongoka. ***


17. Mfano wao ni kama mfano wa aliye koka moto, na ulipo tanda mwangaza wake kote kote Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawawacha katika giza, hawaoni. ***


18. Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. ***
 

Nguruvi3,
Ndugu yangu kuna baadhi ya vitu kuhusu Waislam hujui bora uulize najua kama siku nyingi unakula chapati za samri na mbaazi za nazi.

Katika misikiti karibia yote hapa Dar es Salaa hakuna Masheikh waliosoma Pakistan nenda Mtoro unaousema nenda Kichangani Magomeni, Mtambani Kinondoni, Palestina Sinza, Idrisa Kariakoo, Madina Kariakoo, Qibratein Kariakoo, Makonde Kariakoo. Na mingineyo hakuna Masheikh waliosoma Pakistan.

Niulize Masheikh wetu wamesoma wapi takuambia.
 
Last edited by a moderator:

Jasusi,

Sina haja ya kusema mengi katika hayo ulosema ila nitakupa
moja tu.

Hiyo fikra kuwa TANU ilikuwa Nyerere ndiyo imefanya historia
ya uhuru iingie katika farka kubwa mpaka leo.

TANU haikuwa ya Nyerere peke yake.
Walikuwapo miamba walioisimamisha TANU hadi uhuru ukapatikana.

Mashujaa hawa nimewataja katika kitabu changu.
Hili na wewe halikupendezi.
 
Ritz nimecheka sana, nala chapati za kumimina!
Hujanitendea haki kwa jambo moja, mimi sijataja msikiti hata mmoja, kwahiyo usiniwekee maneno!

Katika orodha yako uliyoitaja umesahau Kheri, Kisutu, Manyema, Tambaza, Maamur, Lindi, Tungi n.k.
 

Nguruvi3,

Ikiwa atatokea Muislam dhalim.

Tutamshika mkono kumweleza kuwa
hivyo sivyo.
 
Ritz nimecheka sana, nala chapati za kumimina!
Hujanitendea haki kwa jambo moja, mimi sijataja msikiti hata mmoja, kwahiyo usiniwekee maneno!

Katika orodha yako uliyoitaja umesahau Kheri, Kisutu, Manyema, Tambaza, Maamur, Lindi, Tungi n.k.

Nashukuru kwa kuongezea majina ya Misikiti.

Haya tuendelee na munakasha.
 
Hapana. Umetaja baadhi tu ya mashujaa waliosimama kidete na Nyerere. Sijakusikia ukilalamika kuhusu kusahauliwa kwa wakina Phombeah, wakina Kyaruzi, wakina Kirlo, wakina Cecil, wakina Oscar, Kunambi kama unavyowalilia wakina Abdulwahid. Unachotaka kufanya ni kumfanya Julius na wenzake walikuwa wasindikizaji wakati ma sterling walikuwa waislamu wa Gerezani. Hilo hatutakubaliana kamwe maana hata pale hao ma sterling wako walipotaka kuanzisha kitu kilichosimamia uislamu peke yake walikanwa na jamii. Uhuru haukupiganiwa na dini yeyote bali ulipaganiwa na wafuasi wa dini hizo bila kujali dini zao, rangi zao, taifa lao, jinsia yao n.k.

Amandla.....
 
Nguruvi3,

Ikiwa atatokea Muislam dhalim.

Tutamshika mkono kumweleza kuwa
hivyo sivyo
.
Kama mnavyofanya kwa wakina Boko Haram? Al Shaabab? Al Qaeda?

Na hilo ndilo tatizo. Mtamshika mkono na kumnong'oneza wakati kinachotakiwa ni kumlaani kwa sauti kubwa, kumkana na kumuadhibu kama inawezekana. Hilo hauwezi kufanya hata siku moja maana dhana ya umma imekujaa.

Amandlaa......
 
Mashujaa na miamba wako hao walifanya kazi ipi? Kupeleka maharage na mchicha Magomeni kwa Mwalimu? Kuchangisha nauli ya kumpeleka Mwalimu UNO? Abdu aliwahi kufika hata hapo Morogoro kuitangaza TANU? Sheikh Amir alifika Bukoba na Lindi kuieneza TANU?

UHURU wa Tanganyika haukuwa na MIAMBA wala MASHUJAA kama tuliowashuhudia wale wa Kenya na MAUMAU yao. Unawakweza tu hawa wazee wako
 
Yapi sasa ya huko necta? Umedai NECTA haipasishi watoto wa Kiislamu..nimekuwekea ushahidi kuwa wapo watoto wa Kikristu wengi wanafeli na wapo wa Kiislamu wanafaulu..labda useme hawa watoto siyo Waislamu...
We Mzee wacha kutupoteza muda wetu kusoma pumba zako.Na ukiingia kwenye mjadala soma majibu kwanza kabla kurudia maswali yako.
Kule nimekujibu sababu ya waislamu kufaulu kwenye shule za kikristu.Hapa sasa Unamuuliza Mohamed suala lile lile.Elewa kwamba hapa huzungumzi na Mohamed pekee.
 
MM,

Labda unipe jibu.

Ilikuwaje historia hii niliyoandika mimi ikawa haifahamiki
na mashujaa hao niliowataja hadi leo hawajaadhimishwa?
Waadhimishwe kwa lipi? Kumpatia Mwalimu nauli akienda kwa miguu Kariakoo bila hata senti mfukoni?
 
Mohamed Said,
Nakusahihisha kuwa AA haikuasisiwa na uwaitao wazee wako, bali iliasisiwa na makafiri Sir D. Cameron na Cesil Matola akawa ndie rais wa kwanza,

Kumbuka na tambua kuwa AA haikuwa na lengo la kudai uhuru wala haki, bali kilikuwa chama cha starehe, (sehemu ya starehe ya weusi)

Kama utakumbuka kule nyuma nilikuambia kuwa vyama hivi AA,TAA, na TANU ni vyama vilivyokuwa na malengo tofauti ama filosofia tofauti,

Sasa nikikuuliza kuwa Klest Sykes aliingiaje AA na aliingia lini unaweza kuwa na majibu mseto kabisa.
 
Umesikia ya Padre aliyeuwawa kule Zanzibar leo asubuhi? Ipo dhulma inayozidi hii ya kutoa uhai wa mtu?
 
Dogo saana. Hata mimi leo kuna mtu nimemnunulia supu.

Wewe unasema huna dini halafu unataka kuwapangia wenye dini yao.

Waislam ndiyo wameamua kufanya ivyo hata kama jambo lenyewe ni dogo kama punje ya mchele.

WildCard mambo ya Waislam yanakukera sana.
 

Umesahihisha nini sasa hapa tuambie AA imeanzishwa lini na Matola alikuwa rais lini.

Kama AA kilikuwa chama cha starehe kwa watu weusi huyu mzungu Sir D Cameron kaingiaje kwenye chama cha starehe cha weusi.
 
Ndio sehemu ya porojo hizo; sijawahi kumtetea Kikwete kuwa namjua. Ndio tatizo la kutosoma mtu kaandika nini. Unaanza kuwa kama Mzee Said hapa kuandika historia kutoka kwenye hisia...
Hapa umekusudia kumtusi Mohamed lakini ukweli tusi linakurudia mwenyewe.Yaani wachapishaji na akina Ilife wote wamezungumzia na kuchapisha hisia tu.Nani utamdanganya na upuuzi wako huu.
InshaAllaha historia ya Tanzania iko mbioni kubadilika bila matakwa ya wanasiasa kutokana na historia ya Mohammed Said wewe bado unataka tuamini kuwa ni hisia tu.Wazee wetu shida zote zilizowapata na wenyewe kujieleza kwa kusononeka bado wewe unaita ni hisia.
Mzee Mwanakijiji kama uzee umekuzidi kaa kimya usijitukanishe.Fanya kama papa Benedict.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…