Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Ritz,
Ungemshauri asome kitabu cha Judith Listowel
"The Making of Tanganyika." Kitabu hiki kingempa
msingi mzuri.
Nimempa rejea moja ni kutoka "memoir" ya Kleist
semina paper aliandika Daisy Aisha Sykes 1968.
Daisy kasanifu lakini alichoandika ni kutokana na mkono
wa babu yake Kleist kuhusu maisha yake.
Kazi hii Daisy kaifanya chini ya usimamizi wa John Illife
mwalimu wake wa historia.
Daisy mimi ni dada yangu tumezungumza mengi kabla
ya mimi kuandika kitabu cha baba yake Abdu Sykes.
Mag hana akijuacho.
Mohamed Said,
Huyu
Mag3, huwezi tena kumshauri kitu chochote ndani ya kichwa chake kwenye "Brain Stem" kaishapafunga haitaji kusikia jambo jipya lolote kuhusu Wazee Wazalendo kutoka Dar es Salaam kama walipigania uhuru wa Tanganyika.
Bahati mbaya au nzuri huyu ndiyo gwiji wao wa historia wanaomuamini baadhi ya watu humu JF.
Wewe hauoni anafikia hatua ya kuchakachuwa maandishi hili wamuone kaandika ukweli.
Kanasa kwenye mtego wa Taa.
Last edited by a moderator: